Mh. tujipe muda kuna mengi nyuma ya pazia, tafakari there is something behind the screne
kung'atuka nakubali lakini mimi zaidi naona huyu mzee ameogopa songombingo ya 2015. Maana 2010 alionekana kuzidiwa sana na akawa analaumu watu wengine ovyo. Hivyo ameamua kujificha la sivyo jamaa wakichukua nchi lazima wa kwanza kumkumbuka ni campaign manager ambaye atatoa maneno ya ovyo wakati wa campaign. Na yeye kihistoria ni Msomali ingekuwa rahisi jamaa kumtarget mara baada ya CCM kudondoka 2015. Nina uhakika beyond the reasonable doubt kuwa CCM haitoshinda tena.
\
Ni mawazo yangu tu
Huu uchafu peleka Michuzi Blog, na magazeti ya Shigongo
Hiki ndicho chama tunachoambiwa kina hazina ya viongozi na ina Jumuiya ya Umoja wa Vijana kama tanuru la kupika viongozi, lakini bado katibu wa Propaganda wa chama hicho hicho anatamani Mwenyekiti atumie mamlaka yake kumteuwa tena Kinana huyu huyu ambaye kwa hiyari yake amesema inatosha!! yangu macho.
Ni kweli hajagombea, lakini kutokugombea kwake hakujafungwa milango kwa CCM kumtumia au kutumia uzoefu wake pale watakapomhitaji.
Alisema "Kwa mfano Mwenyekiti wa CCM ana nafasi alizopewa kikatiba kuteua wajumbe wa NEC, huwezi kujua anaweza akamwona anafaa na akamteua,"
Hata mimi chuki za kuendeleza usomali kwa Bashe sikuzipenda,ni bora ameliona ilo la ndugu yake kunyanyaswa.Halafu kuna watu wanajadili!!!
mnatafuta kitu ambacho hakipo na wala hakijawahi kuwepo!ingepatikana hiyo barua ya kinana ndiyo ingekuwa vizuri zaidi.
Barua ya nini? Amesema hatagombea U-NEC wa CCM uchaguzi ujao. Hajajiuzulu nafasi hiyo kwa sasa. Aandike barua akieleza nini hasa, kwamba hatagombea! Kwani ni lazima?Ingepatikana hiyo barua ya Kinana ndiyo ingekuwa vizuri zaidi.
Wajumbe wa NEC ya sasa ya CCM wako zaidi ya 200. Kwa nini kung'atuka kwa Kinana kuwe habari kubwa namna hii?! Nimeyashangaa hata magazeti ya leo habari hizi ziko kurasa za mbele na zingine ni habari kubwa ya leo. Ule umeneja wake wa kampeni za Mkapa na baadae Kikwete ndio umempa umaarufu huu?
Namfahamu kidogo Kinana. Mara ya kwanza nilimwona mwaka 1985 akiwa PEO makao makuu ya Brigedi ya JWTZ pale Tabora. Alikuja kambini kwetu Msange JKT kumfanyia kampeni Mzee AH Mwinyi achaguliwe kuwa Rais wa JMT. Kwenye ziara hiyo aliongozana na bosi wake Kanali Gidion Mwasomola.Unamjua KINANA au humjui?......
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/12529-abdulrahman-kinana-who-is-he.html
Mkuu mimi hata kuiangalia naiogopa manake hapo mkulu alikuwa kama zidane harufu ya kumpiga kichwa ilikuwa inakaribia.
Nape si uutenge tu huo mzigo wote wa barua ya babu Kinana hapa watanzania tuuchambue wenyewe?? au ni nyaraka ya serikali?? anyways, hata wewe huwezi kuaminika kwa hiyo mistari yako uliyoiweka hapo.
ILA ANGALAU TUMEJUA KUWA KINANA KAAMUA KUKAA KANDO, IWE KWA KHERI AU KWA SHARI. Halafu Nape, haya maneno ya siasa uchwara ndani ya CCM mbona ni ya kawaida sana, kilichokufanya uje haraka haraka kui-neutralize ile thread iliyotangulia ni nini??
MBONA ROSTAM ALIZICHANA SIASA UCHWARA ZA ccm LIVE, NA WEWE BINAFSI UKANYWEA NA HUKUTOA TAMKO?? duh!! Nape bhana una matatizo sana.