CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

Siasa uchwara au siasa safi, sasa inatosha inabidi wazee wapishe wengine nao wachukue nafasi.

Binafsi naamini mzee Kinana ameona wanakoenda hali sio hali. Maana juzi juzi alishaanza kuumbuliwa kwenye biashara zake...

Pesa tamu, kati ya pesa na siasa bora pesa.

Umefanya vyema Mzee Kinana
 
kwa role aliyoplay na mafanikio ya A. Kinana ndani ya ccm ninategemea sitegemei exit yake iwe shaghala bhagala namna hii .... I sound abnormalities ..... kuna ukweli mwingi sana unafichwa .... nikiunganisha dots jinsi nape alivyokimbia haraka humu jf na kukanusha 'contents' za thread ya Kinana kun'gatuka (kukanusha kinana kung'atuka) na nape kuwa mkakati wa kuzuia siri za vikao na habari za ndani za chama tutegemee a lot of uncovered stories underneath
 
Meneja wa Kampeni ya Rais Kikwete ya Urais Bw. Abdulrahman Kinana ametajwa kuwa ndiyo mhusika mkuu katika kashfa kubwa kabisa ya kwanza ya ufisadi mkubwa wa raslimali za Tanzania ya Loliondo mwanzoni mwa miaka ya sitini. Ni yeye inadaiwa kuwa aliyeshiriki kwa kina katika mazungumzo ya kuikaribisha kampuni ya OBC toka UAE.

Kwa wale ambao hawako katika ujuaji wa wahusika wa Loliondo, kimsingi ni watu wale wale ambao walijitokeza tena katika kashfa ya Dowans na yale ya Yaeda Chini.

Kwa ufupi inatajwa kwamba Kinana ni miongoni mwa wahusika wakubwa wa kashfa mbalimbali za ufisadi wa maliasili nchini. Meneja mwingine wa kampeni ya Kikwete ya 2005 ni Bw. Rostam Aziz.

Kinana na Loliondo
 
kwa role aliyoplay na mafanikio ya A. Kinana ndani ya ccm ninategemea sitegemei exit yake iwe shaghala bhagala namna hii .... I sound abnormalities ..... kuna ukweli mungu sana unafichwa .... nikiunganisha dots jinsi nape alivyokimbia haraka humu jf na kukanusha 'contents' za thread ya Kijana kun'gatuka (kukanusha kinana kung'atuka) na nape kuwa mkakati wa kuzuia siri za vikao na habari za ndani za chama tutegemee a lot of uncovered stories underneath

Unakumbuka Waziri wa maliasili alivyoanza kazi kwa kasi?
Unakumbuka makampuni ya Mzee Kinana recently yamewekwa kwenye spotlight?
More to come..
 
JK alisema Watanzania wana viwanda vya kuzalisha uongo, natamani angeenda mbali zaidi kuwa viwanda vyenyewe havijasajiliwa BRELA, havilipi kodi TRA na mbaya zaidi havichagui vema huduma na bidhaa zao za uongo zinazozalishwa ili kujua kama zitauzika ama zitaWATIA hasara ya mwili

Ha haaa, kwa hiyo mpaka leo hujakubali kwamba kan'gatuka! Au tomaso!
 
Kupitia kampuni yake ya TRANS AFRICAN LOGISTICS LTD (TALL) ambayo ni bandari ya nchi kavu maeneo ya Kamata, amekuwa akichelewesha mizigo ya wateja kwa makusudi kwa kisingizio cha system ya Ascuda kusumbua ili tu aweze kutoza storage charges kwa wateja.

Haiingii akilini kila siku ascuda iwe inasumbua kwenye yard ya mzee Kinana tu wakati bandari kavu nyingine zikitoa mizigo kama kawaida.

Tunawaomba wahusika kama TAKUKURU, vyombo vya habari, TRA waingilie kati kuokoa bandari yetu ya Dar kwa sababu kuna idadi kubwa ya wateja wanaokimbia na kwenda bandari za Wavis, Maputo na Durban.

Haya ndo yanayoitwa siasa uchwara aka siasa chafu. Sasa hapa kampuni na Asycuda system na Kinana wapi kwa wapi!! Asycuda ni issue ya TRA sio kampuni ya Kinana.

Bora umejiuzulu mzee..
 
[h=1]Sakata la nyara za Serikali: Kada wa Kikwete lawamani[/h]
maalum.jpg

Na Mwandishi wetu - Imechapwa 08 September 2009

kinana_1.jpg



KAMPUNI ya uwakala iliyosafirisha kontena lililokuwa na meno ya tembo ambayo yalikamatwa nchini Vietnam, inamilikiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, Abdulrahman Kinana, imefahamika.
Taarifa zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo inayoitwa Sharaf Shipping Company iliyosajiliwa Dar es Salaam.
Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussen anamiliki hisa 2,500 zenye thamani ya shilingi 1,000 kila moja.
Kwamujibu wa taarifa za usajili, wamiliki wote wawili, Kinana na Rahma wanapatikana kwa S.L.P 10910, Kiwanja Na. 403 Mtaa wa Tosamaganga, Msasani Peninsular, Dar es Salaam.
Nyaraka zilizopo katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Makampuni na Biashara (BRELA), zinaonyesha kuwa kampuni ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati Na. 47221.
Sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali zilizosafirishwa na kampuni ya Sharaf Shipping Agency liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza na mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.
Hati ya kusafirisha makontena hayo mawili yaliyokuwa yamesheheni pembe za ndovu ilisainiwa na mfanyakazi mwenye asili ya India wa kampuni hiyo Samir Hemani.
Nyaraka zote zilionyesha kuwa kilichokuwa ndani ni plastiki zilizorudufiwa, wakati baada ya makontena kukamatwa, walikuta yamesheheni pembe za ndovu.
Taarifa zinasema kibali cha kusafirishwa kontena hilo kilisainiwa 13 Novemba 2008 na Meneja wa Fedha na Utawala wa Kampuni hiyo.
Wakati Hemani anasaini nyaraka hizo, kibali chake cha kuishi nchini tayari kilikuwa kimeshaisha. Kibali cha Hemani kiliisha 7 Mei 2008.
Makontena yalikamtwa nchini China yakisafirishwa kwenda Hong Kong.
Akichangia makadirio ya bajeti ya wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2009/2010, Kilango alisema utafiti wake umeonyesha kuwa makontena hayo yalipitia bandari ya Dar es Salaam na nyaraka zinaonyesha ndani kulikuwa na plastiki.
Kilango alisema nchi zinazoongoza kwa kupokea nyara kutoka Tanzania ni Phillipines, China, Singapore na Hong Kong.
Kutokana na kutopatikana kwa Kinana juzi kuzungumzia suala hilo, haikufahamika iwapo kampuni ya spika huyo wa zamani wa Afrika Mashariki au yeye mwenyewe, walijua kilichokuwamo katika makontena hayo.
Lakini afisa mwandamizi katika wizara ya Viwanda na Biashara alisema kazi ya kukagua kilichomo kwenye kontena linalosafirishwa si ya wakala wa meli kwani wenye mamlaka na idhini ya kufanya hivyo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Alisema wanaowajibika kusitisha mzigo kusafirishwa pindi wanapoutilia mashaka ni TRA.
"TRA ndio wanakagua na baada ya kujiridhisha kama kilichomo ndani ndicho kilichotamkwa kwenye nyaraka na ni halali, ndipo wanaweka muhuri (seal) wa mwisho," alisema afisa huyo.
"Ukitamka kwa mfano, kuwa katika nyaraka ndani ya kontena kuna matairi 40 ya magari, lazima TRA wafungue na kukagua kuona kama kweli yako matairi 40 au kitu kingine. Baada ya hapo wanaweka seal; sasa kuna kila sababu ya kujenga mashaka," alieleza.
Alisema, "Wakala wa meli kazi yake ni kusafirisha mzigo wa mteja wake. Hata mteja akija na kontena tupu na kusema anataka liende nchi fulani, kazi yake ni kulipeleka kunakohusika na si kuhoji kilichomo."
Alifafanua kuwa watu muhimu wa kuhojiwa na ambao wanaweza kuwa wanajua mchezo wote, kama upo, ni wafanyakazi wa TRA.
Hadi juzi Jumatatu hakukuwa na taarifa zozote za maofisa wa TRA kuhojiwa kuhusiana na sakata hilo.

Source:Sakata la nyara za Serikali: Kada wa Kikwete lawamani | Gazeti la MwanaHalisi
 
Kwanini NAPE awe msemaji mkuu hata kwa yale maamuzi binafsi yaliyomo kwenye mioyo ya wanachama?
 
Ukitaka kufahamu kuwa hili neno 'kupokezana vijiti' linawekwa tu ili kujibu hoja hata kama halina mantiki fikiria haya:
F.Sumaye na E.Lowassa wamefikia katika uongozi wa juu kitaifa (mawaziri wakuu), wamepata fursa ya kufanya yale waliyoyafikiria kwa taifa iwe kwa njia nzuri au mbaya. Hivi kuna sababu gani ya wao kugombea NEC, kwanini wakiwa wameshatoa vijiti wanarudi upande wa pili kulilia vijiti vile vile?

Pili, jiulize muda wa kupokezana vijiti ni miaka mingapi? Kama tutakubali Kinana anatoa kijiti basi wote akina Nape na wengine nao watatumia miaka 25 kama base line. Jiulize kupokezana vijiti kunatokea mtu akiwa katika utumishi wa chama kwa miaka mingapi, na nafasi gani zinazotumika kutoa vijiti?

Fikiria kuwa ndani ya NEC na CC ya sasa kuna watu wangapi wametumikia kwa miaka zaidi ya 15 hadi 20.
The bottom line, ni kigezo gani linatumika kusema huyu kajiuzulu, huyu kakimbia siasa uchwara,huyu katoa kijiti, huyu kaogopa chama kufia mikononi mwake n.k.

Are these guys teaming up for 2015? Just curiosity because I think some guys, though in secret like doing things strategically.
 
Very big show is coming! Mama Joniiiii, coke and porpcon please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli! Ila nataka niamini, maneno aliyoyatoa ametumia busara na uzalendo zaidi ya kuonyesha hisia halisia ndani ya nyoyo zake Kama bado anazo!

Nape, asante kwa kutudhihirishia Yale yaliypkuwa yanatuzonga ndani mwetu! Huwezi ukafanya utawala aw Jamhuri ukawa wa kifamilia! Tanzania has never been a monarchy and shall never be! This is notwithstanding the emerging practice of politician offsprings, the kind of Napes taking over their dads roles in politics!

Mkuu hapo kwenye red ni kweli kwa Tanzania kwa maana ya Serikali lakini kwa CCM inawezekana ndo maana mke watoto pamoja na baba wanapita bila kupingwa kwa kisingizio kwamba hakuna aliyejitokeza kupambana nao.
 
Mimi napenda hiyo moto yako "Kigamboni na Tanzania kwanza" iwapo tu ingekuwa ni ya vitendo. Kuna thread imeanzishwa kuhusu utendaji wako jimboni Kigamboni hasa Mbagala tunasubiri majibu
 
Hizi ni nafasi za kugombea na kuchaguliwa. Kinana hakuwa na haja ya kututangazia. Angekaa kimya tu asichukue fomu basi. U-NEC wa CCM unaonekana kuwa zaidi ya UBUNGE? Boresheni democrasia ndani ya CCM ili tuone nafasi za juu kabisa ndani ya chama hiki zikigombewa badala ya mtindo wa sasa wa kumpata Mwenyekiti, Makamu wake wawili, Katibu Mkuu, Wajumbe wa CC, Sekretariet, ambako kote huko watu wanateuana tu.
 
Back
Top Bottom