CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

bml1.jpg


Duh! Hii picha imeniacha hoi...ningekuwa Waziri wa Fedha nikitoka hapo nafanya kama alivyofanya Kinana!​

Na huyo mwenye lips kama Diamond ndio nani vile? teh teh teh...siasa zimekuwa nzuri kweli siku hizi
 
Inachotufanya tuamini kuwa Mzee Kinana ameachana na nyadhifa zote serikalini ni kuhepuka siasa uchwara nikwamba, CCM tunamuhitaji Mzee Kinana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote. Katika wanachama viongozi wasio na makundi ya wazi (anayeweza kuunganisha makundi yote) yeye ni mmoja wapo kati ya wachache sana. Nafikiri kasi ya mgawanyiko wa makundi imemshinda na kumuacha pekeyake. Hilo la chama kuendeshwa kifamilia ni sababu mojawapi ndogo sana ambayo ingeweza kutolewa maamuzi makini. Bilashaka kuna mengi yamejificha na tutakuja kuyajua tu, kuanzia uozo unaoendelea UVCCM hadi kwenye NEC achilia mbali udhaifu wa serikali unavyotutia aibu.
 
Mshitueni na Pius Msekwa naye apumzike. Kinana msalimie sana Mzee Makamba huko mapumzikoni ingawa yeye alitumia ile staili inayotaka kuzoeleka ndani ya CCM ya kata mti panda mti.
 
Hizi ni nafasi za kugombea na kuchaguliwa. Kinana hakuwa na haja ya kututangazia. Angekaa kimya tu asichukue fomu basi. U-NEC wa CCM unaonekana kuwa zaidi ya UBUNGE? Boresheni democrasia ndani ya CCM ili tuone nafasi za juu kabisa ndani ya chama hiki zikigombewa badala ya mtindo wa sasa wa kumpata Mwenyekiti, Makamu wake wawili, Katibu Mkuu, Wajumbe wa CC, Sekretariet, ambako kote huko watu wanateuana tu.

Mkuu maneno ya busara sana. Hakua na haja ya kutangazia umma. Kwani alipochukua form ya kugombea aliitangazia umma?

Mzee naye kwa siasa uchwara!! CCM yote siasa Uchwara tu
 
Bora Kinana ujipumzikie tuuu,ule maisha kwa kuwa umeshakusanya vya kutosha,isije ikakupata aibu kuelekea 2015 kwani kasi hii ya kutaka mabadiliko huiwezi.Pia wazee wote CCM wanatakuwa kuiga mfano wako!.
 
naomba muongozo hapa

kwa yote aliyoifanyia ccm miaka takriban 25 ndani ya chama .... ni nini stahiki ya A. Kinana katika medani ya siasa .... kung'atuka au kujiuzulu au jambo ambalo halisemwi ambalo ndiyo sahihi kabisa ... kustaafu

farewell A.Kinana
 
Kinana ameachana na siasa uchwara za CCM

Kama kweli Kinana amejiuzulu basi ccm kutakua na pengo kubwa kwa yeye kiukweli amekua msaada mkubwa sana kwa jk,namheshimu sana mzee yule kwa kuwa ana akili nyingi sana tofauti na wengi wanavyofikiria na pia alikua kinara katika kuiondoa ccm mikoni mwa Rostam na Lowassa,naamini kuiondoka kwake kutalipa nafasi genge la lowassa kuanza kujiimarisha tena ndani ya vikao vya ccm,tatizo la jk ubishi,aking'ang'ania jambo na kuliingiza kichwani ni ngumu kulitoa,niliwahi kuzungumza na kinana kuelekea uchaguzi mkuu nikambana kuhusu yeye kama meneja kumruhusu mgombea wake kwenda igunga na monduli na kuinua mikono ya wagombea ubunge wa majimbo yao kama ilikua sahihi,alichonijibu ni kwamba jk ni mbishi,yeye binafsi alimshauri waachane na hao wagombea kwa kuwa hata kama wasipoenda wao wenyewe wanazo nguvu kubwa za kushinda hayo majimbo hivyo wajiepushe nao kwani kwenda kuwapigia kampeni kutadhoofisha kampeni za urais kwani wananchi hawatawaelewa na kama anaona ni lazima kwenda basi bora aende mgombea mwenza Dr.Bilal na timu yake,lakini jk ni mbishi na akaendaq mbali zaidi mzee kinana kwa kudai kwamba inavyoonekana jamaa anataka kuwarudisha hao mafisadi kwenye serikali yake ijayo kama atashinda,huyo ndio kinana ninaemfahamu,na tuliongea mengi sana siku hiyo pale Best bite Namanga yeye na januari makamba wakitoka kuzungumza na reginald mengi kuhusu moja ya gazeti lake kuonekana linabase zaidi kwa Dr Slaa na kumgonga Jk!
 
Kila nikirudia rudia kuisoma kwa makini hii thread naona ni useless na ni irrelevant topic, cha msingi Kinana hatokuwepo tena kwenye lile jumba la Mizwengwe White House, hizi lugha zingine ni mapambio tu ya Nape Nnauye.

Labda tu nasubili Nape aipeleke JF Mahakamani kwa kuandika habari za barabarani, maana siku hizi huyu bwana amewaagiza waandishi wa Habari wa Tanzania wawe wanacopy habari kutoka kwake na kwenda kuzipaste kwenye Magazeti yao.

Waandishi wa habari wa Tanzania ni dhaifu sana mpaka kufikia kuwekewa masharti namna ya kureport habari na mtu Kilaza kama Nape na mpaka leo wapo kimya, ni kitendo kinachofedhehesha sana.
 
Kuna watu humu kwa ushabiki viziwi wa chama wako radhi hata kugeuza maana ya mada ili tu habari iwaridhishe wao!,acheni ushabiki wa kutoa habari zenye favour upande mnaoutaka nyie!,aya nan aliepata kuiona iyo barua alieiandika kinana,na maneno alieyasema!!,mnakera na ushabiki kondoo wenu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ninachofahamu mimi ni kwamba, Kinana yupo katika kundi la wale wanaotaka akina EL& CO Ltd waondolewe kwenye uongozi wa juu wa chama. Tofauti ya Kinana na watu kama akina Sitta ni majukwaa ya kauli zao. Kinana amekuwa akitumia vikao halali vya chama wakati akina Sitta hata ukiwaalika kufungua shule ya chekechea; watatoa msimamo wao huko!

Sina shaka kwamba msimamo wa Kinana na Nape unawiana ingawaje tofauti yao ni ile ile iliyopo kati ya Kinana na Sitta! Jambo ambalo nashindwa kuanganisha dots ni tofaut kati ya Kinana na Nape ingawaje nahisi wanatofautiana katika namna ya uwasilishaji hoja.....tusisahau, Kinana ni kizazi kilichotokana na zama za chama kufuata maadili(usiniulize wht abt Sitta) so lazima awe anakerwa na staili za uendeshaji chama za akina Nape!! Hilo moja!

Lakini vilevile naamini Kinana alitarajia uchaguzi huu wa ndani wa CCM ungekuwa ndio mwisho wa akina EL.....sina shaka ameona ndoto zake zinaelekea kupeperuka kwa kuona nguvu ya akina EL inavyopasua anga za uchaguzi huo. Si ajabu KInana ameona harakati za wazi wazi za kuhakikisha akina EL wanabaki na kuchukua nafasi za juu kwenye chama!! Hapa kuna vita, kati akina Lowassa pamoja na Kinana.

Tusisahau miezi michache iliyopita tulijuzwa ufisadi wa Kinana humu jamvini.....nahisi huo ulikuwa ndio mwanzo wa vita hii!! Mwanzo wa kumtia adabu ili aache kuwasakama akina Lowassa!
Strong Point,kinana amekua akionekana mwiba kwa lowassa na genge lake,na mwenyewe amekua akisema mara kadhaa yeye hamuogopi mtu kwa kuwa hategemei kuwa waziri wala mkuu wa mkoa balia anataka kufanya biashara zake na ni yeye ambae amekua akiwasema kina lowassa waziwazi kwenye vikao vya chama kwamba wao ndio tatizo na kama wakiachwa watakiua chama,lakini mwenyekiti amekua akionekana kuwa mzito kufuata ushauri wa kinana.
 
Mkuu Nape, kwanza asante kujitokeza mapema kuujibu ule uzushi!, lakini kusema tuu ni uzushi hakutoshi!. Ile thread unayoiita ya uzushi, inazungumzia barua Kinana aliyoiandika!, wewe unazungumzia maneno Kinana aliyoyatamka, hivyo ni vitu viwili tofauti!.

Sasa ili kanusho lako liwe na maana, tungeshukuru kama ungetufafanulie
  1. Jee Kinana ameandika barua?.
  2. Kwenye barua hayo uliyoyasema wewe ndiyo yaliyomo kwenye hiyo barua?.
  3. Kama ameandika barua, na hayo uliyoyasema ni matamshi ya mdomo, then ile thread still stands mpaka uthibitishe hata kwenye barua, yale hayapo!.
  4. Mode, Nape akithibitisha ule ni uzushi, then funge ile thread na kumpatia muanzisha thread haki yake!.
  5. Nape, tunakushauri, karibu tena na tena sio tuu kukanusha thread za uzushi, bali pia jitokeza kujibu baadhi ya hoja valid kuhusu CCM!.
Asante.

Pasco.
Pasco,
Umeniangusha kidogo. Hizi ni nafasi za kuchukua fomu na kugombea. Aandike barua ya nini wakati muda wake wa ujumbe wa NEC unaisha mwaka huu? Kinana wala hakuwa na haja ya kuutangaza uamuzi wake huu. Ujumbe wa NEC ya CCM una umuhimu gani enzi hizi za vyama vingi? Hata hii "reaction" ya Nape haikuhitajika sana. Mtu ambaye ndani ya CCM akitangaza kutogombea ikawa ni habari kubwa ni Mwenyekiti wao tu ingawa naye hajazi fomu kugombea nafasi hii.
 
source mwananchiKinana ang’atuka CCM Monday, 24 September 2012 08:02Kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman KinanaNI BADA YA KUWA MJUMBE NEC, KAMATI KUU KWA MIAKA 25, AZUNGUMZIA UCHAGUZI 2015, HATIMA YAKE BAADA YA SIASAMwandishi WetuKADA maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahaman Kinana ametangaza kung’atuka rasmi katika siasa baada ya kukitumia chama chake kwa miaka 25 akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Kamati Kuu (CC) na Kamati ya Maadili.Kinana ambaye amekuwa Meneja wa Kampeni za mgombea urais wa CCM tangu mwaka 1995 ulipoanza uchaguzi wa vyama vingi, alisema kwamba baada ya kutumikia chama katika nyadhifa za juu kwa robo karne sasa, ameamua kupumzika ili kuwaachia vijana waendelee kukijenga chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika.“Nimekuwa Mjumbe wa NEC kwa miaka 25, bila shaka muda huu unatosha, kwani wanaCCM wamenipa heshima ya kuwa katika vikao vya juu vya chama kwa robo karne. Sasa ni wakati wa kung’atuka, nimetoa mchango kwa kadri nilivyoweza katika vikao mbalimbali na katika shughuli nyingi,” alisema.Alisema anaamini kuachana kwake na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchaguzi wa 2015.“Uongozi ni kupokezana vijiti. Wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza. Nawashukuru wanaCCM na viongozi kwa heshima waliyonipa wakati wote huu,” alisema Kinana ambaye alikuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Benjamin Mkapa kwa vipindi viwili na Rais Jakaya Kikwete kwa vipindi viwili vya uchaguzi.Kinana alisema anajivunia kufanya kazi na marais wote wa Tanzania kuanzia Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais Kikwete kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.”Ushauri wangu katika vikao umekuwa ukiheshimika sana. Nimekuwa nikiheshimiwa na uongozi wote wa CCM na hata wapinzani nao tunaheshimiana. Nimesimamia kampeni za kistaarabu na ambazo zimeleta ushindi mkubwa kwa CCM tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi,” alisema.Kinana ambaye pia alikuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), ameshauri vijana ndani ya CCM watangulize masilahi ya taifa mbele na wasikilize wananchi.Ni muhimu washikamane, wabuni mikakati ya kusaidia kukuza uchumi kwa haraka zaidi na kuendeleza umoja na undugu wetu,” alisema.Ushauri wa viongozi wapya CCMKinana alishauri viongozi wapya ambao wanatarajiwa kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe.“Ni matumaini yangu kuwa watakaopata uongozi wataona upungufu na watasahihisha makosa yangu,” alisema.Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa 2015, Kinana aliwaasa viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urais bali washughulikie kero za wananchi.“Bado tuna kazi kubwa ya kutekeleza Ilani. Tusiwasumbue Watanzania kuwa ni nani anafaa kuwa Rais bali tushughulikie matatizo yao. Kwa sasa ajenda ya CCM ni kutekeleza ahadi zetu katika sekta zote siyo kutafuta nani atakuwa Rais 2015," alisema na kuongeza: "Hata wapinzani wawaeleze Watanzania yale ambao wamedhamiria kutekeleza. Kueleza upungufu wa CCM ni mtaji mdogo kwa wapinzani, ajenda kubwa ni watafanya nini? Hapa bado wana kazi kubwa. Wanapoona upungufu wasisite kutusema,”Kinana ambaye ana shahada ya uzamili katika utawala na masuala ya sera kutoka Chuo Kikuu cha Harvad nchini Marekani, alisema anatarajia kufundisha na kusoma Shahada ya Uzamivu (PhD) katika moja ya vyuo vikuu vya hapa nchini.“Baada ya kustaafu kuna mambo mawili ambayo natarajia kufanya. La kwanza ni kuona kama naweza kufundisha. Pili kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu,” alisema.Mbali na nyadhifa zilizotajwa huko juu, Kinana ametumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa muda mrefu na kupanda cheo hadi kufikia Kanali.Amewahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Arusha Mjini.Nape alisema Kinana ni miongoni mwa wanasiasa waadilifu wa CCM ambao wamekitumikia chama kwa muda mrefu na kwa uaminifu wa hali ya juu.Ni kweli hajagombea, lakini kutokugombea kwake hakujafungwa milango kwa CCM kumtumia au kutumia uzoefu wake pale watakapomhitaji.Alisema "Kwa mfano Mwenyekiti wa CCM ana nafasi alizopewa kikatiba kuteua wajumbe wa NEC, huwezi kujua anaweza akamwona anafaa na akamteua,"
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nape on a serious note Kinana deep moyoni mwake anakerwa na jinsi CCM inavyoendeshwa. Naona ameamua kungatuka ili asiwe sehemu huo ubovu.

Nilitegemea angejiuzuru mara tuu baada ya uchaguzi wa 2010 bse kuna mambo yeye kama yeye yalikuwa yanamkera. Ila nampongeza ni zamu ya damu changa sasa kushika hatamu za chama

Anakerwa haswa na NAPE alivyogeuza CCM ni cham cha kisanii zaidi
 
Mjumbe wa Almashauri kuu na kamati kuu ya CCM captain Abdulharaman kianana amejiuzulu nafasi zote alizonazo ndani ya ccm kwa madai ya kuachana na siasa uchwara.

Kinana amedai kuachana na siasa uchwara zinazoendeshwa na Nape Nnauye akishirikiana na Chilagati na january makamba.

ktk barua yake ya kujiuzulu kinana pia ametaja kutofurahishwa najinsi jk na familia yakea inavyoendesha chama'' chama ni taasisi hauwezi ukaendesha chama kwa kutumia familia baba , mama na mtoto ,nimefanya kazi chini ya Nyerere ,mwinyi na mkapa hatukushirikisha familia zao''


Tatizo ni kwamba hivi sasa kuna watu, kama hao hapo juu, wamedandia JF bila kufanya hata kautafiti kadogo kujua kwa nini JF ni JF...ona sasa wanavyoumbuka!

Mag3 nakushukuru sana kwa kuwaweka hawa wadandiaji wote pamoja maana huwa nakereka sana pale mtu asiyejua anapojifanya anajua zaidi. Wanabisha kuwa ni uongo wakati huo ukweli hawausemi.
Mkuu Mwana Mpotevu na Mag3 mi naomba uthibitisho kwenye red tu hapo juu. Ukinithibitishia baaaaaas sitakuwa na tatizo na nyie otherwise hizi ni Porojo tena yawezekana zimepikwa na wafuasi wa EL
 
Mkuu uwe unasoma thread nyingine kabla ya kupost.
 
Back
Top Bottom