CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

Kavunja kamati ya kampeni rasmi.Pengine hajasema alivyokereka na kuomba kila sent kwa prince kwa kipindi chote cha kampeni.Halafu leo ndio najikuta akitakiwa jikomba NEC wakati teammates wake wakichuku nafasi NEC.
Kusema ukweli hata mimi nashangazwa sana,hivi mkuu unadhani ni kitu gani watakachofanya?Inawezekana Kinana yupo kwenye kambi ya tofauti na mtoto wa JK na FL?Maana mtu alikuwa kwenye kampeni ya mzee wake halafu wamletee mizengwe?inaonekana haziivi kwasababu hiyo.Yani amemeneji kampeni ya mzee wao,lakini wao wanapita bila kupingwa na yeye zengwe!

Halafu kumbe alikuwa akichukuwa pesa kutoka kwa mtoto wa JK?Duuh!No wonder amesema hayo.

Nakubaliana na wengine kuwa there is something going on kwasababu Nape analeta habari za kutokugombea,lakini hasemi hayo ya barua,sasa uko aliko,natamani Kinana azime simu yake maana watakuwa wanamtafuta halafu utashangaa barua inadraftiwa upya,ama hata kusema haikuwepo,sasa hata Nape hataki kusema maneno hayo ya Kinana kama alimsikia akiyazungumza ama ameyaona kwenye barua.

Hivi mkuu huyu Kinana yupo kundi gani kati ya hayo ya kina EL vs Sitta na wengineo?Pia kundi la mtoto wa JK ni lipi?
 
Mbona hili mmefanya mapema hivi kuja kukanusha?! I can sense the sign of RED FLAG! Nafahamu wazi kwamba udhaifu mkubwa wa CCM ni ama kupuuza moja kwa moja au kuchelewa kuchukua hatua za kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya chama hususani zinazotolewa hapa JF! Au ndo tuseme Idara ya Uenezi imezaliwa upya na kwa kasi mpya?! Hata hivyo msisahau kwamba, mashahidi wa tuhuma za Richmond, including Dr. Msabaha ndani ya kiapo alisema vingine na nje ya kiapo "akawang'ata sikio" kwamba mzigo ni wa bwana mkubwa na yeye anatolewa kafara tu....so, inawezekana kabisa Kinana kwenye barua ameandika kwamba anang'atuka kupisha damu changa na nje ya barua akawang'ata watu sikio kwamba hawezi kuendelea na siasa uchwara!
absolutely you are the great thinker.....
 
Hivi Kinana amejiuzulu ama kung'atuka kitu gani?Alikuwa ana madaraka gani ndani ya chama hadi usawa huu?Msaada tutani tafadhali.





bml1.jpg


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda
(kushoto), Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa, Waziri wa Kilimo Profesa
Jumanne Maghembe na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Mhe Samuel
Sitta baada ya kumalizika kwa mkutano maalumu wa Baraza la Mawaziri
pamoja na Manaibu Mawaziri na Makatibu wakuu alipokutana nao Alhamisi
Septemba 8, 2012 katika ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu jijini Dar es
salaam.

5996140674267894691-4795733563052290545


View attachment 65850

Ukisoma hizi pics..ndio utaona jinsi CCM ni chama cha hovyo.Na ukiwa na kumbukumbu ya magazeti kipindi cha myuma utaona jinsi uswahiba wa msomali na the first family unalivyosuasua.Sijui ile Saigon ya pale Arusha mtaa wa Pangani hadi Bondeni ita react vipi?game limekwisha bao wamepigwa.Hakuna tena umuhimu wao,kwani hakuna tena haja ya kuahidi wala kutimiza.
 
Me naomba hiyo barua iwekwe hapa ndani najuwa watu wanayo.......

Achana na barua hiyo wakati uthibitisho ni huu hapa wa Nape. Ukiona Vuvuzela anahaha kuzima ukweli ujue mambo mazito kweli kweli huko mjengoni.

avatar11941_3.gif


icon1.png
Uzushi dhidi ya Kinana kutogombea unasikitisha!

Uamuzi wa Kinana kutogombea umepokewa kwa hisia tofauti lakini kuna watu wanajaribu kupotosha ....ETI NI KUACHANA NA SIASA UCHWARA...!!!!! hii hapa chini ndio sehemu ya maneno yake binafsi juu ya uamuzi wake huu....

"SIJAGOMBEA KWAKUWA MIAKA 25 YA KUSHIRIKI KATIKA KAMATI KUU NADHANI INATOSHA NA NI VIZURI KUNG'ATUKA. NAAMINI KUNA WANACCM WENGI WAZURI WENYE SIFA NA UWEZO WA KUONGOZA CHAMA. UONGOZI NI KUPOKEZANA VIJITI NA NI WAKATI WANGU KUKABIDHI WENGINE KIJITI HIKI"


Sasa wanaosema eti siasa uchwara wanayatoa wapi........ Uzushi mwingine ni wa ajabu sana..

##nakuomba mods msiunganishe hii thread na ile ya uzushi tafadhali!
 
Kusema ukweli hata mimi nashangazwa sana,hivi mkuu unadhani ni kitu gani watakachofanya?Inawezekana Kinana yupo kwenye kambi ya tofauti na mtoto wa JK na FL?Maana mtu alikuwa kwenye kampeni ya mzee wake halafu wamletee mizengwe?inaonekana haziivi kwasababu hiyo.Yani amemeneji kampeni ya mzee wao,lakini wao wanapita bila kupingwa na yeye zengwe!

Halafu kumbe alikuwa akichukuwa pesa kutoka kwa mtoto wa JK?Duuh!No wonder amesema hayo.

Nakubaliana na wengine kuwa there is something going on kwasababu Nape analeta habari za kutokugombea,lakini hasemi hayo ya barua,sasa uko aliko,natamani Kinana azime simu yake maana watakuwa wanamtafuta halafu utashangaa barua inadraftiwa upya,ama hata kusema haikuwepo,sasa hata Nape hataki kusema maneno hayo ya Kinana kama alimsikia akiyazungumza ama ameyaona kwenye barua.

Hivi mkuu huyu Kinana yupo kundi gani kati ya hayo ya kina EL vs Sitta na wengineo?Pia kundi la mtoto wa JK ni lipi?

Soon developing story itanenepa kwa haraka sana.Ndani ya NEC waliopigika ni wengi ,roho zinawauma hawawezi vumilia JF ndio pekee inaweza kuwa last hope.Wakipata chance kidogo tuu hata ya kwenda msalani simu zao zitatuma kitu, km si baada ya kusikia mgazeti ya kesho yanavyowaumiza wengine roho na kuwapa kiburi wengine,basi itakuw ani ile tabia yao ya kutaka jifanya kuwa uongozi bora ni kujua matukio.
 
Kulikuwa na maneno ya mitaani kuwa baada ya kampeni aliahidiwa kupewa kiwanja pale kamata alichokifanya yadi ya kampuni (sijui yake) ya Usafirishaji.

Udaku unajuza zaidi kuwa baadhi ya fungu la pesa halikumfikia baada ya wamiliki wa chama kulidaka likiwa hewani, na alipojaribu kudai kwa mwenye jamuhuri aliambiwa awaone haohao wamiliki wa chama, inatajwa kuwa alinuna sana na sasa kama vile yametimia tu.

Huu ni udaku kutoka kwa nzi aliyekaribu na Mzee Kinana.
 
Kuna juhudi kubwa sana za kuficha kile kinachoendelea ndani ya chama. Juzi tu Sitta katamka kwamba chama inabidi kizaliwe upya. Chama hakiwezi kuzaliwa upya wakati kuna makundi chungu nzima yanayopingana huku kila kundi likiwa na mtu wake ambaye kundi lingependa aingie kweye kinyang'anyiro cha 2015. Hali ni mbaya sana na pesa za mafisadi zinafanya kazi usiku na mchana katika makundi hayo ili kuhakikisha kundi lao wanashika hatamu ndani ya chama na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri kuelekea uchaguzi wa 2015. Mficha ugonjwa kifo kitamuumbua...jitihada zao za kuyaficha yale yanayojiri ndani ya chama chao kamwe hazitafanikiwa.

Wanajamvi,

Kwanini Nape amekuja kwa kasi? Jibu ni kuwa vikao vya chama vinaendelea na habari hizi kuvuja JF zinaufikia umma kwa haraka sana. Kitakachotokea ni wale wenye hati hati ndani ya chama kujipanga kabla ya kumalizika vikao.
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.

Kitendo cha Kinana kusema hayo aliyoyasema kinaashiria ujio wa jambo zito. Anaweza kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia baada ya kutathmini hali ya chama na mustakabali, au anaweza kuwa amefanya hivyo ili ku-set tone kwa maamuzi yanayoonekana kuwa mazito na yenye madhara 'repercussions'.

Kwahiyo msibabaike sana ujio wa Nape ni katika mkakati wa 'pre-emptive strategy' hasa baada ya JF-Leak.
Nisomeni vizuri, Jumatano na Alhamisi zitakuwa siku zenye habari nyingi za kisiasa, siku zitakazoonyesha hatima ya CCM na wale waliokubali kubeba jeneza na kibao cha R.I.P.

Nasema R.I.P kwasababu damage ya chama ni kubwa sana kiasi kwamba kinachohitajika ni injini mpya na si bodi.
Hilo halitatokea katika makundi yaliyopo na kuparaganyika ni jambo la kwanza hata kama litafunikwa na maneno 'tumeingia wamoja tumotoka wamoja'. Underneath there is a big rift for the part to stand tall as it used to be.
 
Habari sio za ukweli (take from me )
Bila kuweka source inakuwa tabu.
Halafu kuna watu wanajadili!!!
Jf sasa ni kijiwe cha porojo...Mods ondoen huu ujinga hakuna ukweli wowote
habar walakin!
Hizi hbari sio za kweli anatupima huyu aliyeleta hii thread. aweke source kama kweli
I'll be the last person to believe this!
Ngumu kumeza
thread yangu kuhusu kuwasahihisha chadema imefutwa mda sio mrefu...hapa zinaletwa porojo za bavicha zitawekwa hadi sticky...alafu ndio mnataka tuwaachie nchi na upendeleo wenu wa kichaga.
Kinana huyuhuyu aliekua meneja kampeni wa jk 2010 leo atangaze kujiuzuru tena na kashfa kwa familia ya jk.. Huu ni uongo uliochacha.!!
Pumba hizi...Peleka Lumumba sio hapa
Asante sana AL sadat, hivyo ndivyo JF ilivyoweza kujijengea heshima na umaarufu...yaani kuwa source ya breaking news kabla ya wengine kudandia. Tatizo ni kwamba hivi sasa kuna watu, kama hao hapo juu, wamedandia JF bila kufanya hata kautafiti kadogo kujua kwa nini JF ni JF...ona sasa wanavyoumbuka! Habari ikiletwa JF, jiulize mara mbili kabla ya kuirukia kama walivyofanya hawa jamaa zetu hapo juu...JF iko pote hadi vyumbani mwenu! Wasio na akili wanafikia hata kuihusisha Chadema na hizi kukuru kakara za kunyang'anyana tonge mdomoni ndani ya chama cha walafi, manyang'au yanaanza kutafunana yenyewe kwa yenyewe, aibu yao...na bado!
 
nguruvi,kumbe hilo la kurudi kwa kupitia ukatibu lilishazungumzwa?
CHADEMA, mafisadi waichanganya CCM
Mwandishi Wetu

Toleo la 253
8 Aug 2012


ccm_253.jpg



  • Kasi ya CHADEMA kisiasa mwiba, vijisenti vya mafisadi vurugu tupu
  • Sasa wawakumbuka Kinana, Mangula
    BAADHI ya wana CCM wanafikiria kuwatosa Katibu Mkuu Wilson Mukama na Makamu Mwenyekiti Bara Pius Msekwa ili kuwaingiza Abdulrahman Kinana na Philip Mangula kukabili tishio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imefahamika.
    Endapo mpango huo utafanikiwa unalenga pia kupambana na makundi ya kifisadi ndani ya chama hicho ukiunda safu mpya ndani ya chama kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
    Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari, ingawa CCM inachagua viongozi wake kwa kuzingatia kanuni na taratibu zake, lakini inaelezwa kuwa, kasi na mikakati ya CHADEMA kwa namna fulani ni kati ya vigezo vinavyotumika kujenga hoja, pamoja na mambo mengine, dhidi ya mtandao wa mafisadi ndani ya CCM.
    Lakini wakati vigezo kadhaa vikitumika kwa chama hicho kikongwe kujinusuru angalau na taswira chafu mbele ya umma, mtandao wa kundi la wasio wadilifu ambao wamepewa jina la mafisadi nao umekwishapanga safu yake na kinachoendelea sasa ni kuzidi kupenyeza fedha ili watu hao washinde nyadhifa mbalimbali za uongozi.
    Taarifa zinafichua kuwa, sasa kuna kambi ya wazalendo na kambi ya mafisadi ndani ya chama hicho katika wakati huu wa mchuano wa kupata uongozi mpya.
    Hali hiyo ya mpambano kuelekea kilele cha uchaguzi wa CCM imegusa viongozi kadhaa, kuanzia wale wanaotajwa kukosa uadilifu na hata baadhi ya viongozi wa sasa, kila mmoja akichambuliwa kwa kadiri ya mwenendo wake na akipimwa kwa kuzingatia vigezo kadhaa, ikiwamo kasi ya kisiasa nje ya chama hicho, kasi ambayo bila shaka, inahusisha CHADEMA.

Nafasi ya Katibu Mkuu
Katika nafasi hii, inaelezwa kuwa kundi la wazalendo bado linaendelea kumshawishi Mwenyekiti wa Kampeni za mgombea urais wa CCM, mwaka 1995, 2005 na 2010 na mlezi wa chama hicho kwa Mkoa wa Dar es Salaam, Kinana, ateuliwe kushika wadhifa wa Katibu Mkuu wa CCM.
Hata hivyo, inadaiwa ya kuwa Kinana bado hana majibu ya moja kwa moja ya kukataa au kukubali majukumu hayo.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kama Kinana atakubali uteuzi huo ataweza kuwaunganisha wanaCCM wenye kutaka chama hicho kurejea katika misingi yake. Lakini pia kama atakubali, anatajwa kuweza kuweka masharti kadhaa yanayoweza kutafsiriwa kuwa ni magumu kutekelezwa na viongozi wengine wa chama hicho.
Kwa muda mrefu, Kinana amekuwa akitajwa kupingana na viongozi wa chama hicho wanaozongwa na kashfa, akiwa ni kati ya wanaoshinikiza baadhi ya viongozi wenye tuhuma ama kujiondoa au kuondolewa ndani ya chama hicho.
Ushawishi kwa Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM unatokana na kile kinachoelezwa na baadhi ya wanaCCM kwamba, Katibu Mkuu wa sasa, Wilson Mukama, licha ya kuteuliwa mahsusi kushika wadhifa huo ili kutekeleza kile kilichopata kupendekezwa na kamati aliyoiongoza kuhusu mabadiliko ndani ya CCM, hajafanya vizuri sana katika kusimamia mabadiliko hayo.
Katika mapendekezo ya Kamati ya Mukama, msemo maarufu wa kujivua gamba uliibuka lakini usimamizi wake umekuwa ukikosa msukumo uliostahili.
Baadhi ya wanaCCM wanasema, Mukama alipaswa kuonyesha msimamo katika utekelezaji wa kile alichokiamini na kilichopendekezwa na kamati yake na kama baadhi ya viongozi wenzake wa juu walikuwa wakimkwamisha, basi alipaswa kujiuzulu.
Licha ya Mukama kuonekana kutakiwa kustaafu na Kinana kushawishiwa kuchukua nafasi hiyo, kundi la wanaCCM walioko katika tuhuma za ufisadi linatajwa kuhakikisha hapati nafasi hiyo.
Inaaminika kuwa Kinana ni kikwazo kwa kundi hilo na hasa kutokana na msimamo wake wa kupinga matumizi ya fedha katika uchaguzi wa chama hicho, sambamba na tabia ya kulindana miongoni mwa viongozi serikalini.
Mikakati inatajwa kufanywa kumchafua Kinana, ikiwa ni pamoja na kuhusisha baadhi ya vyombo vya habari nchini. Mikakati hiyo imepangwa kutekelezwa kabla ya Novemba, mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti CCM
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, wito sasa unatolewa kwa Pius Msekwa anayeshikilia nafasi hiyo kwa sasa astaafu.
Msekwa amekuwa katika nyadhifa kuanzia wakati wa TANU, ambako baada ya chama hicho kujibadili kuwa CCM akawa Katibu Mkuu Mtendaji wa chama hicho kilichoshiriki harakati za Uhuru wa iliyokuwa Tanganyika.
Msekwa anatajwa kutomudu kasi ya sasa ya ushindani wa kisiasa nchini inayochochewa kwa namna fulani na CHADEMA. Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa kundi la wazalendo ndani ya CCM linaendeleza ushawishi ili nafasi hiyo ichukuliwe na aliyepata kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Mangula.
Mangula anasifiwa katika kubuni na kusimamia mikakati ya kisiasa, akiwa na uwezo mkubwa wa kusimamia bila kutetereka kanuni za chama hicho, ambazo hakuna sehemu zinazopoeleza kuhusu viongozi watuhumiwa wa ufisadi kutetewa na chama.
Bado haijulikani utayari wa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, ambaye ni yeye ndiye anayepaswa kuamini katika utendaji wa Mangula ili hatimaye mwanasiasa huyo aliyemwachia ‘kijiti' cha Katibu Mkuu CCM, Yusuf Makamba, apewe nafasi hiyo ya makamu mwenyekiti.

Itikadi na Uenezi
Katika nafasi hii ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, ambayo kwa sasa inashikiliwa na Nape Nnauye, vyanzo vyetu vya habari vinaeleza kuwa kati ya wanaopendekezwa kuchukua nafasi hii kutoka katika makundi ya kisiasa ndani ya CCM ni pamoja na William Ngeleja au Martin Shigela.
Nape anatajwa kuendelea kutetewa na wazalendo ndani ya chama hicho lakini wanaompinga wanadai ni kijana mwenye msimamo usiowafurahisha baadhi ya watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.
Kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi, msimamo ambao ni mtaji mbele ya vijana na Watanzania kwa ujumla, inaaminika kwamba Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema na aliyepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini, kabla ya kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri miezi kadhaa iliyopita, na Shigela ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM, wachukue nafasi ya Nape.
Hata hivyo, tofauti na Nape ambaye bado hajawa na rekodi ya kuzorota kisiasa na hasa katika usimamizi na ufuatiliaji, ikiwa ni pamoja na kukabili wimbi la siasa nje ya chama chake, Shigela anatajwa kushindwa kuinua Umoja wa Vijana wa CCM.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanaCCM kadhaa ambao hawakutaka kuandikwa majina yao gazetini, Shigela akiwa mtendaji mkuu wa UVCCM anatajwa kuwa ameufanya umoja huo kutokuwa tishio la kisiasa kwa vyama vya upinzani na hata yeye binafsi, si mwanasiasa mwenye umahiri unaotishia vyama vingine kisiasa.
Kwa Shigela kupewa nafasi hiyo ya Katibu wa Itikadi na Uenezi, inaelezwa kuwa ni sawa kuzorotesha idara ya itikadi na uenezi ya chama hicho.
Shigela kwa baadhi ya wanaCCM anatajwa kutokuwa mbunifu na inadaiwa UVCCM kwa sasa inaomba hata fedha kwa ajili ya kugharimia mikutano na semina zake licha ya kuwa na vitega uchumi kadhaa.
Kwa namna fulani, Ngeleja naye anatajwa kuwa ni sawa na kijana ambaye uteuzi wake utadhoofisha idara hiyo, ikiaminika kwamba, ameondolewa serikalini kutokana na jamii kumtazama kwa jicho la kutokuwa mchapa kazi.

Katibu wa Uchumi na Fedha
Nafasi hii kwa sasa inashikiliwa na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mwigulu anatajwa kutofanya kazi yake ya masuala ya uchumi vizuri lakini akionyesha umahiri katika uwanja wa siasa za moja kwa moja, akipata kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge, Igunga, mkoani Tabora kwa mafanikio ingawa katika kampeni za ubunge Arumeru Mashariki, alianguka.
Bado idara yake ya uchumi inakabiliwa na changamoto nyingi, chama chake kikiwa hakijabuni vyanzo vipya vya mapato, huku matumizi ya ruzuku yakizidi kupanuka, hasa baada ya chama hicho kuanzisha mikoa mipya ya kisiasa. Hata hivyo, Mwigulu anatajwa kutokuwa na madhara kwa mtandao wa mafisadi ndani ya CCM.

Naibu Katibu Mkuu-Bara
Nafasi hii inashikiiwa na John Chiligati ambaye ni mbunge. Chiligati anatajwa kutokuwa mzigo katika safu ya uongozi wa chama hicho. Ni mwanasiasa mzoefu ambaye hata hivyo, wanaCCM wenzake wanamtafasiri kama anayeanza kuachwa nyuma na changamoto za kisiasa nchini, hususan na mazingira ya kisiasa nje ya CCM. Anatajwa kuwa mzito katika kuamua, kinyume na hali halisi katika siasa za wakati huu.

Katibu wa Mambo ya Nje
Nafasi hii inashikiliwa na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba, ambaye kutokana na uteuzi wake wa kuwa Naibu Waziri na kwa kuzingatia taratibu mpya za CCM, hatapaswa kurejeshwa katika nafasi yake hii ya chama.
Katika uongozi wake ndani ya CCM, Januari anatajwa kutokuwa na misimamo yenye kueleweka, hakuwa akieleweka kuwa anaamini katika nini. Mazingira hayo ya kutokueleweka yanamhusisha na sifa zisizohitajika katika kutafuta viongozi wanaoweza kuipigania imani ya chama hicho kwa hali na mali.
Ukiondoa udhaifu huo kwa kiongozi kutojulikana unasimamia nini, Januari anatajwa kupanua shughuli za Idara yake ya Mambo ya Nje, jambo ambalo linatajwa kupaswa kuendelezwa na atakayeshika nafasi hiyo baadaye mwaka huu.
BTW kuna wale watetezi wakubwa wa magamba humu ambao siwaoni kabisa,nadhani ni wahusika wakuu kwenye hivyo vikao,sitaki kuwataja majina,lakini siwaoni kabisa.
 
Katika picture ni rahisi kuona mwenyekiti na rais alivyo kila kitu katik CCM.mkuu wa kaya alikuwa anataka chapa mtu ngumi..6 yuko mbali kama mtoto anayeshudia mama yae akiliwa na simba usiku na hajui pa kukimbilia(6 hafai ktk matatizo kam ailibyo kwa malecela), pinda kwa nafasi yake alipaswa kuwa kama Putin na kuchukua control hapo,ila kawa kama Medvedev, huyu mpare prof Maghembe..si rahisi kujua alipo kwani anasubiri atoke hapo akawatukane wapare wote kuwa ni wajinga na hawajasoma.Waziri mhusika kama anajitetea asikilizwe kabla ya kichapo, au tishio la kupigwa nje.I like JF members kwa kuchukua pics
 
Asante sana AL sadat, hivyo ndivyo JF ilivyoweza kujijengea heshima na umaarufu...yaani kuwa source ya breaking news kabla ya wengine kudandia. Tatizo ni kwamba hivi sasa kuna watu, kama hao hapo juu, wamedandia JF bila kufanya hata kautafiti kadogo kujua kwa nini JF ni JF...ona sasa wanavyoumbuka! Habari ikiletwa JF, jiulize mara mbili kabla ya kuirukia kama walivyofanya hawa jamaa zetu hapo juu...JF iko pote hadi vyumbani mwenu! Wasio na akili wanafikia hata kuihusisha Chadema na hizi kukuru kakara za kunyang'anyana tonge mdomoni ndani ya chama cha walafi, manyang'au yanaanza kutafunana yenyewe kwa yenyewe, aibu yao...na bado!
Mag3 nakushukuru sana kwa kuwaweka hawa wadandiaji wote pamoja maana huwa nakereka sana pale mtu asiyejua anapojifanya anajua zaidi. Wanabisha kuwa ni uongo wakati huo ukweli hawausemi. Inabidi watu wafikirie kabla ya ku-judge na kudai source. kwani alyeweka uzi sio source? By the way, sources wengine huwa hawatamkwi, siwezi kusema nimeambiwa na Jack Zoka (mfano tu). hapa sasa wameambuulia kuvuna aibu baada ya Nape kuthibitisha. Shame on them all.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Pasco,huna tena haja ya kunijibu kuhusu Kinana na EL,samahani kwa usumbufu...
Licha ya Mukama kuonekana kutakiwa kustaafu na Kinana kushawishiwa kuchukua nafasi hiyo, kundi la wanaCCM walioko katika tuhuma za ufisadi linatajwa kuhakikisha hapati nafasi hiyo.
Inaaminika kuwa Kinana ni kikwazo kwa kundi hilo na hasa kutokana na msimamo wake wa kupinga matumizi ya fedha katika uchaguzi wa chama hicho, sambamba na tabia ya kulindana miongoni mwa viongozi serikalini.
Mikakati inatajwa kufanywa kumchafua Kinana, ikiwa ni pamoja na kuhusisha baadhi ya vyombo vya habari nchini. Mikakati hiyo imepangwa kutekelezwa kabla ya Novemba, mwaka huu.
BTW JK na EL ni kweli hawakukutana barabarani.Jamaa style yake huwa inanishangaza sana,ndo maana alikuwa akiunda kamati na tume za uchunguzi,alikuwa akiwachanganya mafisadi na wale wanaowapigia kelele,so go figure.Ila hayo yana mwisho kwasababu unafiki una mwisho,kuna siku utaumbuka tu,kwa mfano hivi sasa yani nasubiri nione wataplay game gani tena.Ndo ile maneno ya presha inapanda,presha inashuka ina make sense hapa.
 
Mkuu Nape, kwanza asante kujitokeza mapema kuujibu ule uzushi!, lakini kusema tuu ni uzushi hakutoshi!. Ile thread unayoiita ya uzushi, inazungumzia barua Kinana aliyoiandika!, wewe unazungumzia maneno Kinana aliyoyatamka, hivyo ni vitu viwili tofauti!.

Sasa ili kanusho lako liwe na maana, tungeshukuru kama ungetufafanulie
  1. Jee Kinana ameandika barua?.
  2. Kwenye barua hayo uliyoyasema wewe ndiyo yaliyomo kwenye hiyo barua?.
  3. Kama ameandika barua, na hayo uliyoyasema ni matamshi ya mdomo, then ile thread still stands mpaka uthibitishe hata kwenye barua, yale hayapo!.
  4. Mode, Nape akithibitisha ule ni uzushi, then funge ile thread na kumpatia muanzisha thread haki yake!.
  5. Nape, tunakushauri, karibu tena na tena sio tuu kukanusha thread za uzushi, bali pia jitokeza kujibu baadhi ya hoja valid kuhusu CCM!.
Asante.

Pasco.
can we put the link to that thread ya uzushi? li mambo yaende vizuri bin mswano
 
Mag3 nakushukuru sana kwa kuwaweka hawa wadandiaji wote pamoja maana huwa nakereka sana pale mtu asiyejua anapojifanya anajua zaidi. Wanabisha kuwa ni uongo wakati huo ukweli hawausemi. Inabidi watu wafikirie kabla ya ku-judge na kudai source. kwani alyeweka uzi sio source? By the way, sources wengine huwa hawatamkwi, siwezi kusema nimeambiwa na Jack Zoka (mfano tu). hapa sasa wameambuulia kuvuna aibu baada ya Nape kuthibitisha. Shame on them all.

AL sadat
Mwana Mpotevu
Ieleweke kuwa watu hatubishi, kinachotakiwa katika uandishi mtu jitahidi kueleza source ya habari iwe kama ni kama mojapo ya:
  • Tetesi toka mjengoni
  • Mhusika toka mjengoni katipa tip
  • Habari zilizovuja toka mjengoni
  • Taarifa toka kwa Nape
  • Nukuru kutoka chombo cha habari
  • Nk.
Hata kama chanzo kamili hakija kamilika inatupa fursa ya kuijadili huku tukiwa na tumaini fulani kuwa habari itakuja kamilika lakini tunaweza kujadili.

Habari hii ilivyoletwa haikuwa kamili hasa kuelezea wapi alikopata taarifa hizo ingawa habari yenye ina mvuto sana.
Tunapojaribu kuelezea hayo ni kwa nia njema ya kuelimishana, nafasi nyingine anapoleta habari iwe kamili au breaking news walao iwe na information za source.

That's all what we'r talking about.

Tujitahidi kuipa Jamii Forums hadhi stahiki kama moja ya source kubwa ya habari hapa nchini.
 
Ndugu Pasco,huna tena haja ya kunijibu kuhusu Kinana na EL,samahani kwa usumbufu...

BTW JK na EL ni kweli hawakukutana barabarani.Jamaa style yake huwa inanishangaza sana,ndo maana alikuwa akiunda kamati na tume za uchunguzi,alikuwa akiwachanganya mafisadi na wale wanaowapigia kelele,so go figure.Ila hayo yana mwisho kwasababu unafiki una mwisho,kuna siku utaumbuka tu,kwa mfano hivi sasa yani nasubiri nione wataplay game gani tena.Ndo ile maneno ya pesha inapanda,presha inashuka ina make sense hapa.
dot..zitaanza ungana vyema na baadaye watu wanaanza eliminate unnecessary links na kubakiwa na bigger picture with no blur.Nape akirudi anakuta majibu ya mbele ya hiyo single yake.Itambidi arudi tena studio kutengeneza nyingine ya fastafasta.Atakuwa behind the schedule kwa muda wote wa shughuli ndani ya CCM.
 
Mag3 nakushukuru sana kwa kuwaweka hawa wadandiaji wote pamoja maana huwa nakereka sana pale mtu asiyejua anapojifanya anajua zaidi. Wanabisha kuwa ni uongo wakati huo ukweli hawausemi. Inabidi watu wafikirie kabla ya ku-judge na kudai source. kwani alyeweka uzi sio source? By the way, sources wengine huwa hawatamkwi, siwezi kusema nimeambiwa na Jack Zoka (mfano tu). hapa sasa wameambuulia kuvuna aibu baada ya Nape kuthibitisha. Shame on them all.

Ieleweke kuwa watu hatubishi, kinachotakiwa katika uandishi mtu jitahidi kueleza source ya habari iwe kama ni kama mojapo ya:
  • Tetesi toka mjengoni
  • Mhusika toka mjengoni katipa tip
  • Habari zilizovuja toka mjengoni
  • Taarifa toka kwa Nape
  • Nukuru kutoka chombo cha habari
  • Nk.
Hata kama chanzo kamili hakija kamilika inatupa fursa ya kuijadili huku tukiwa na tumaini fulani kuwa habari itakuja kamilika lakini tunaweza kujadili.

Habari hii ilivyoletwa haikuwa kamili hasa kuelezea wapi alikopata taarifa hizo ingawa habari yenye ina mvuto sana.
Tunapojaribu kuelezea hayo ni kwa nia njema ya kuelimishana, nafasi nyingine anapoleta habari iwe kamili au breaking news walao iwe na information za source.

That's all what we'r talking about.

:msela:Tujitahidi kuijengea hadhi yake JF kama source ya kuaminika katika vyombo vya habari:msela:
 
Achana na barua hiyo wakati uthibitisho ni huu hapa wa Nape. Ukiona Vuvuzela anahaha kuzima ukweli ujue mambo mazito kweli kweli huko mjengoni.

Yeah mkuu wangu nimekupata vizuri sana, na kweli nimeona jamaa ameingia humu ndani straight na kuja kutetea hoja, na siku zote huwa anatetea ujinga huyu mtu, me nataka waendelee kuvurugana tu ndio vizuri.
 
Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.

Kutokana na chama chenu kilivojaa hila, uwongo, mbinu chafu, wizi, ufisadi u-kolimba nk chochote kinachosemwa na makada wenu hakuna anayeamini ni cha kweli au kinatoka rohoni!Kifupi CCM imekosa credibility mbele ya umma, mfano hata wewe mwenyewe bungeni mishipa ilikutoka ukipigania swala la kigamboni hadi ukafukuzwa nje ya bunge leo hii upo unaitetea ccm hiyohiyo!!shame on you sijui wewe doctor wa nn??
 
Back
Top Bottom