CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Kwa kweli Busanda aliekoa jahazi ni Magufuli pekee heshima kwake tafadhali.....woooote waliotangulia wanaijua hilo...hata helikopta yao haikufua dafu kwa Magu,kazi ianze tena Biharamulo.....Chadema jipangeni upya acheni unafiki.....
 
kweli wasukuma hawaoni umasikini.....siku wakijua kwamba kura yao kwa sisiemu ndo inawafanya wawe masikini, basi chama dume kiatanguka..... wananunuliwa kirahisi mno, wanawake ni chumvi ya mawe , wanaume gogno, vijana soda na ahadi hewa....mpaka miaka miatano tena!!!!

Acha matusi wewe ,Tuambie wewe unayeona umasikini mbunge wako ni nani?
 
Kulingana na historia ya nchi yetu kisisasa na ninavyoona matokeo haya ya Busanda, ninaendelea kuamini imani kuwa Tanzania bado ni sikio la kufa.

Tatizo walilonao wapinzani kwa kiasi kikubwa ni wao kwa wao,kwa mfano uchaguzi wa 2005 kanda ya ziwa ilikuwa ni cuf ikiminyana na ccm,sasa ni chadema,ila inamaanisha kuwa wale waliokuwa wanachama wa cuf ndio wameipa nguvu chadema,ccm iko pale pale kwa kiasi kikubwa,wapiga kura bado si bado si wengi kama inavyotakiwa,hata hivyo chadema wamepiga hatua kutoka kura 3,000's za mwaka 2005 hadi 21,000's za mwaka huu,ni hatua. Ila tatizo kubwa ni mapandikizi ama uwezo wa ccm kuwachanganya wapinzani....Mambo ambayo yanaonekana ni madogo madogo lakini yana cost kwasababu ni vita ya kisaikolojia.

Uchaguzi wa mwaka 2005 wa urais ni wananchi milioni 11 tu ndio waliopiga kura,yani wananchi milioni 11 kati ya wananchi zaidi ya milioni 40, sasa hao milioni 30 wako wapi na wanafanya nini?

Nawapa hongera kwa kazi mliofanya chadema,si wakati wa kukata tamaa,ni wakati wa kuweka mkakati na kuhakikisha hao wananchi milioni 30 wanapatikana at least milini 10 more,ni changamoto.

Huko vijijini ni lazima muanze kujikita,huko kila mtu anamjua mwenzake,na kwa hivyo kuwepo na namna ya kujiunga kwenye shghuli za kijamii kwani watanzania wanadhani siasa ni maneno tu na ndio maana ccm inashinda kwa maneno,kama chadema imeshinda mjini basi hao waliopiga kura ndio wawaeleweshe wenzao waliowaacha huko vijijini kwasababu huko mijini pia asilimia kubwa ni wahamiaji kutoka vijijini na wengi wameacha ndugu jamaa na marafiki.

Seriousness kuhusiana na vita ya ufisadi bado haina kipaumbele,ni vita inayohitaji sio tu kuwa funded,bali kupewa uzito mithili ya mapambano ya uhuru,ama gonjwa la ukimwi nk Nilishatoa ushauri kama huu hapo nyuma.
 
- Kwa hiyo kumbe tulitabiri vizuri kwamba CCM itashinda, pamoja na zomea zomea ya vijana wasiowapiga kura toka Tarime!

- Naomba niwape Chadema tathimini ndogo sana ya siasa zetu, bado ni siasa za majina na sio sera wala records, wananchi wetu bado wanaamini in names, ukabila, undugu na udini mpaka tutakapopita haya as a nation itaendelea kuwa hivi hivi, najua CCM imeshinda maana nimemuona Muungwana, akiwa na furaha sana tena sana, sio kama ambavyo amekua siku za nyuma, ambapo alikuwa mkali na very depressed!

- Haya uchaguzi umeisha sasa wananchi turudi kuwa ndugu moja, taifa mbele tusigawane maana utengano ni udhaifu.

Respect.

FMEs!
 
Kwa kweli Busanda aliekoa jahazi ni Magufuli pekee heshima kwake tafadhali.....woooote waliotangulia wanaijua hilo...hata helikopta yao haikufua dafu kwa Magu,kazi ianze tena Biharamulo.....Chadema jipangeni upya acheni unafiki.....

- CCM ina viongozi wengi wakali na wachache wabovu, as opposed na Chadema, wananchi hawawezi kuwapa uongozi Dr. Slaa, Zitto (CCM), Ndesamburo, Mbowe, Lissu, na Mwanakijiji tu, mnahitaji safu kubwa na nzito kidogo kuliko hawa tu,

- Yaani eti Manu wasingeshinda bila Ronaldo, ebo! sasa unafikiri kwa nini walimsajili na kumlipa mahela yote hayo, ya Maghufuli ni kama sizitaki mbichi hizi!

Respect.

FMEs!

Uchaguzi mdogo Magogoni: Matokeo
Invisible
user_offline.gif
Today, 04:50 AM
Jumla ya wapiga kura waliojiandikisha ni 5,494 na zilizopigwa ni 4,917.

Matokeo:

CCM: 2,874

CUF: 1,974

SAU: 22

Zilizobaki (47?) zimeharibika.
__________________
Ficha upumbavu wako usiifiche hekima yako!

- Sasa na huku nako Magogoni, alienda Magufuli au?

FMEs!

Tatizo walilonao wapinzani kwa kiasi kikubwa ni wao kwa wao,kwa mfano uchaguzi wa 2005 kanda ya ziwa ilikuwa ni cuf ikiminyana na ccm,sasa ni chadema,ila inamaanisha kuwa wale waliokuwa wanachama wa cuf ndio wameipa nguvu chadema,ccm iko pale pale kwa kiasi kikubwa,wapiga kura bado si bado si wengi kama inavyotakiwa,hata hivyo chadema wamepiga hatua kutoka kura 3,000's za mwaka 2005 hadi 21,000's za mwaka huu,ni hatua. Ila tatizo kubwa ni mapandikizi ama uwezo wa ccm kuwachanganya wapinzani....Mambo ambayo yanaonekana ni madogo madogo lakini yana cost kwasababu ni vita ya kisaikolojia.

Uchaguzi wa mwaka 2005 wa urais ni wananchi milioni 11 tu ndio waliopiga kura,yani wananchi milioni 11 kati ya wananchi zaidi ya milioni 40, sasa hao milioni 30 wako wapi na wanafanya nini?

Nawapa hongera kwa kazi mliofanya chadema,si wakati wa kukata tamaa,ni wakati wa kuweka mkakati na kuhakikisha hao wananchi milioni 30 wanapatikana at least milini 10 more,ni changamoto.

Huko vijijini ni lazima muanze kujikita,huko kila mtu anamjua mwenzake,na kwa hivyo kuwepo na namna ya kujiunga kwenye shghuli za kijamii kwani watanzania wanadhani siasa ni maneno tu na ndio maana ccm inashinda kwa maneno,kama chadema imeshinda mjini basi hao waliopiga kura ndio wawaeleweshe wenzao waliowaacha huko vijijini kwasababu huko mijini pia asilimia kubwa ni wahamiaji kutoka vijijini na wengi wameacha ndugu jamaa na marafiki.

Seriousness kuhusiana na vita ya ufisadi bado haina kipaumbele,ni vita inayohitaji sio tu kuwa funded,bali kupewa uzito mithili ya mapambano ya uhuru,ama gonjwa la ukimwi nk Nilishatoa ushauri kama huu hapo nyuma.

Asilimia 80% kwa kila familia ya mtanzania ni watoto Kwa mantiki hiyo hao milioni 30 ni watoto ambao hawawezi kupiga kura
 
Kulingana na historia ya nchi yetu kisisasa na ninavyoona matokeo haya ya Busanda, ninaendelea kuamini imani kuwa Tanzania bado ni sikio la kufa.

Tanzania sio sikio la kufa. Katika mikakati yote ya propaganda inayotumiwa na CCM kuna hoja moja ambayo Vyama vingine vya siasa havijaweza kuijibu CCM na hii hoja itaiweka CCM madarakani for unseen years unless wapinzani waje na altenative strategy ya kuipangua.

Watanzania wanaiamini CCM katika swala la Usalama and CCM they know this so they use fearmongering strategy kuhakikisha kwamba that strategy inaendelea kufanya kazi.

Maeneneo kama ya Mwanza Vijijini Vyama vingine vinaitwa ni vya majingiri(Majambazi) which is very hard to unregister from wapiga kura hasa hasa watu wazima na wazee.

Pili CCM vijijini is a substitute ya Government kwenye sehemu nyingi ambazo hazina watendaji wa serikali. Migogoro mingi sehemu ambazo hazina mahakama ya mwanzo huishia na kuktaturiwa CCM au hata sehemu zenye mahaka ya Mwanzo kesi hufika makama ya mwanzo baada ya kushindikana katika ofisi za ccm which give the party a very powerfull grassroot postion.

Tatu wapinzani kushinda it will depend with demographic shifts , it will take another 10-15 years kwa kizazi cha nyerere kupotea na kupoteza ushawishi kwenye siasa zetu na ndipo wapinzani wanaweza kuitoa CCM as long as Kizazi cha nyerere bado kina influence na siasa za Tanzania kuitoa CCM ni ngumu sana. Ndio maana mtu kama malecela akisamama watu wa kizazi cha nyerere they can identify with him and trust him easly.

Nne kuna njia nyingine ya kuitoka CCM madarakani kwa kipindi kifupi zaidi ya 10-15 years na hii kwa vijana wote smart and ambao wako kwa ajili ya reform and they beleive in clean politics tuingie CCM na tukisafishe Chama ndani,itakuwa kazi ngumu na itasababisha chama kugawanyika , mafisadi hawezi kukubali therefore watatoka ndani ya Chama and this will be a start of pure politics in Tanzania na watu wataanza kushindana kwa policy na perfomamnce and therefore Vyama vya upinzani kama vitakuwa na policy bora kuliko CCM that time wataweza kuitoa CCM madarakani.
 
Kwa mara nyingine tena, Chama cha Mapinduzi kimeonesha uwezo wake wa kushinda kura kwa mkakati (strategy). Wapinzani somo hili bado hawajalimudu. Huwezi kushinda uchaguzi kwa kuhutubia. Mara zote kwenye chaguzi aidha nguvu zinatumika au mkakati.

Katika hili CCM bado wana ujuzi na uzoefu wa muda mrefu.

Wakati huo huo hata hivyo tutambue pia kuwa Chadema imeonesha nguvu kubwa huko, tatizo ni je watajenga kutoka hao 21,000? Nitaandika ukosoaji wangu wa wazi baadaye.

Ushindi ni ushindi, CCM imejistahilisha ushindi kwa kujua nini cha kufanya. Kuzomea, kushangilia, kukimbilia helikopta kamwe hakushinda uchaguzi; ni mkakati tu na zaidi ya yote kujiandikisha.

Hili la kujiandikisha nalo ni jambo jingine ambalo linaathiri sana chaguzi hizi; binafsi ningeona ni vyema sana panapotokea uchaguzi mdogo, basi muda wa kujiandikisha kupiga kura nao uongezwe na wananchi wapya wapewe nafasi ya kujiandikisha.

CCM inastahili pongezi zote!
 
- Analysis nzito sana, ila kuna moja tu halisema nalo ni unafiki wa viongozi wa upinzani, kujifanya wako kule kumbe wako CCM kilichowashinda kusimamisha mgombea mmoja ni nini kama sio ushiriki wao wa kisiri ndani ya CCM?

- CCM wana fimbo moja nayo ni mfarakano wa upinzani, CCM wana miaka 50 zaidi au 100, mkuu elewa hao kina Malecela wanasaidia ana angalau kuwepo na some decency kwenye hizi chaguzi, can you imagine kina Nchimbi ndio wanaosimamia uchaguzi on their own hivi kweli unafikiri kutakuwa na haki au heshima japo kidogo kama sasa, subiri uje uone wao watanunua tu hizi chaguzi na kuchapa viboko wananchi mpaka upinzani.

Respect.

FMEs!
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali vijijini bado wamelala, mimi ni Msukuma niliyezaliwa na kukulia mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi literacy level ilivyo kubwa kimenisikitisha na kunihuzunisha. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika na hizo kura imebidi wapigiwe.
Hii ignorance level CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani Wasukumu, ili tumethibitisha ujinga, sisi sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, tumelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwafanya mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini. Pia kuna sisi tunaoichagua CCM kwa sababu hakuna mbadala. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa.
Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika.2010 will never be the same, japo sio anguko kuu la CCM, but the going gets tough na mabadiliko yanakuja.

Wenzetu ilio mbali, Geita isikieni hivyo hivyo, ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!. Nyumba za nyasi ni nyingi kuliko nyumba za bati!.
Watoto wanasura za kutilisha huruma, Wakinamama sura za kukatisha tamaa, kinababa sura za mashaka, dada poa Geita buku, buku mbili, ukitoa dala anataja kuhamia! Unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu unaweza kulia
Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na Geita Gold Mine, upande mwingine Bulyanhulu, upande mwingine Buzwagi, upande mwingine Kahama Gold Mine, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo wameambiwa ni kazi nzuri ya CCM na bado mnawachagua kuyaendeleza kisa
wasukuma ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.
Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....
 
Kwa mara nyingine tena, Chama cha Mapinduzi kimeonesha uwezo wake wa kushinda kura kwa mkakati (strategy). Wapinzani somo hili bado hawajalimudu. Huwezi kushinda uchaguzi kwa kuhutubia. Mara zote kwenye chaguzi aidha nguvu zinatumika au mkakati.

Katika hili CCM bado wana ujuzi na uzoefu wa muda mrefu.

Wakati huo huo hata hivyo tutambue pia kuwa Chadema imeonesha nguvu kubwa huko, tatizo ni je watajenga kutoka hao 21,000? Nitaandika ukosoaji wangu wa wazi baadaye.

Ushindi ni ushindi, CCM imejistahilisha ushindi kwa kujua nini cha kufanya. Kuzomea, kushangilia, kukimbilia helikopta kamwe hakushinda uchaguzi; ni mkakati tu na zaidi ya yote kujiandikisha.

Hili la kujiandikisha nalo ni jambo jingine ambalo linaathiri sana chaguzi hizi; binafsi ningeona ni vyema sana panapotokea uchaguzi mdogo, basi muda wa kujiandikisha kupiga kura nao uongezwe na wananchi wapya wapewe nafasi ya kujiandikisha.

CCM inastahili pongezi zote!

- Mkuu Mwanakijiji, huu wako ni mfano wa kuigwa, hizi ndio siasa tunazozihitaji Tanzania, ni leo tu mke wangu alikuwa ananiambia kwamba hizi siasa zenu za Forums ni za kitoto sana, kwa sababu mbona kina Lowassa na Mama Kilango wanatwangana mawe kwenye siasa, lakini bado wanaelewana kama wananchi, nyinyi huku forums mbona ni chuki tu na wivu mtupu, na majina ya bandia! Nikamwambia hii ni jungle!

- Sasa hivi nimemuonyesha hii comment yako, na amekubali kwamba kumbe kuna wengine humu ni wastaarabu kama viongozi wetu, saafi sana mkuu maana wewe kichwa ukikubali, basi wenzangu na miye yaani mkia ni kufuata tu!

Respect.

FMEs!
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali vijijini bado wamelala, mimi ni Msukuma niliyezaliwa na kukulia mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi literacy level ilivyo kubwa kimenisikitisha na kunihuzunisha. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika na hizo kura imebidi wapigiwe.
Hii ignorance level CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani Wasukumu, ili tumethibitisha ujinga, sisi sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, tumelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwafanya mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini. Pia kuna sisi tunaoichagua CCM kwa sababu hakuna mbadala. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa.
Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika.2010 will never be the same, japo sio anguko kuu la CCM, but the going gets tough na mabadiliko yanakuja.

Wenzetu ilio mbali, Geita isikieni hivyo hivyo, ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!. Nyumba za nyasi ni nyingi kuliko nyumba za bati!.
Watoto wanasura za kutilisha huruma, Wakinamama sura za kukatisha tamaa, kinababa sura za mashaka, dada poa Geita buku, buku mbili, ukitoa dala anataja kuhamia! Unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu unaweza kulia
Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na Geita Gold Mine, upande mwingine Bulyanhulu, upande mwingine Buzwagi, upande mwingine Kahama Gold Mine, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo wameambiwa ni kazi nzuri ya CCM na bado mnawachagua kuyaendeleza kisa
wasukuma ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.
Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....

- The simple truth ni Upinzani hawakuwapa wananchi wa Busanda sababu za kutoichagua CCM.

Wamjini kama wewe mlioamka na mnaojuwa kusoma hadi mko ma profesa ni mbunge gani wa upinzani mmemchagua.
Mimi nafikiri unapotoa shutuma kama kijijini kumelala lazima utoe reference point kwamba wamjini na tunaojuwa kusoma na kujipigia kura wenyewe tumefanya hivi .
Naomba unipe takwimu kidogo tu tangu upinzani umeanza ni sehemu ipi kati ya mjini na kijijini ambao wamewahia angalau kujaribu wapinzani kwa rate kubwa?
 
Mimi nionavyo
Tatizo la Tanzania wala si mjini wala kijijini tabia zetu ni moja ya kwamba hatukubali kukubali matokeo na kujirekebisha kutokana na matokeo na ya kwamba lazima kufail kwangu ni sababu ya jirani .Huu ni ujinga kabisa.

Pili Tatizo letu nionavyo bado hatujakubali kuwa matajiri ama wote tuwe middle class tunaonelea umasikini ni size yetu na si utajiri.Mfano ukipromoka kifedha kutoka hali nzuri hadi mbaya watanzania wengi watafurahi ni wachache mno watakaosikitika ,Hii tabia ya wote wa mjini na vijijini.

Tatu Tunapenda sifa na umarufuu usio na sababu utasikia amejipatia umarufaa kisiasa.
 
Kwa mara nyingine tena, Chama cha Mapinduzi kimeonesha uwezo wake wa kushinda kura kwa mkakati (strategy). Wapinzani somo hili bado hawajalimudu. Huwezi kushinda uchaguzi kwa kuhutubia. Mara zote kwenye chaguzi aidha nguvu zinatumika au mkakati.

Katika hili CCM bado wana ujuzi na uzoefu wa muda mrefu.

Wakati huo huo hata hivyo tutambue pia kuwa Chadema imeonesha nguvu kubwa huko, tatizo ni je watajenga kutoka hao 21,000? Nitaandika ukosoaji wangu wa wazi baadaye.

Ushindi ni ushindi, CCM imejistahilisha ushindi kwa kujua nini cha kufanya. Kuzomea, kushangilia, kukimbilia helikopta kamwe hakushinda uchaguzi; ni mkakati tu na zaidi ya yote kujiandikisha.

Hili la kujiandikisha nalo ni jambo jingine ambalo linaathiri sana chaguzi hizi; binafsi ningeona ni vyema sana panapotokea uchaguzi mdogo, basi muda wa kujiandikisha kupiga kura nao uongezwe na wananchi wapya wapewe nafasi ya kujiandikisha.

CCM inastahili pongezi zote!
Mwanzo nilisema CCM itashinda, nikaja Busanda nikashuhudia CCM imeshindwa, matokeo yametoka CCM imeshinda.
Naungana nawe kuipongeza CCM, pia nazikubali tathmini zako. Yametimia yale uliyoyasema kuhusu ushindi kwa CCM. Hongera CCM, Hongera Mzee Mwanakijiji.!.
 
Kwa mujibu wa tovuti ya chadema kuhusiana na uchaguzi wa ubunge jimbo la Busanda 2005, sijaweza kuona alizopata mgombea wa ccm plus total votes,lakini kuna hatua,mgombea wao alipata kura zifuatazo...

Busanda alisimamishwa ISMAIL, Manyanya Chalahani kura 3,1070 ambazo ni asilimia .351%

Mushi,
Hizi namba kwenye red hazijakaa vizuri waweza kuziweka sawa? Au ulimaanisha 3,107 = .351 %?
 
- Chadema waache ubabe na matusi, haya sio maadili yetu wananchi wa Tanzania , halafu ukiifanyia CCM ubabe unategemea watakulipa nini kama sio ubabe uliokubuhu, halafu wajiangalie tena maana wengi wao ni CCM.

FMEs!
 
Wamjini kama wewe mlioamka na mnaojuwa kusoma hadi mko ma profesa ni mbunge gani wa upinzani mmemchagua.
Mimi nafikiri unapotoa shutuma kama kijijini kumelala lazima utoe reference point kwamba wamjini na tunaojuwa kusoma na kujipigia kura wenyewe tumefanya hivi .
Naomba unipe takwimu kidogo tu tangu upinzani umeanza ni sehemu ipi kati ya mjini na kijijini ambao wamewahia angalau kujaribu wapinzani kwa rate kubwa?
Issue sio wapinzani wapi tumewachagua, wala sina maana kuchagua upinzani ndio kuamka, ama kuichagua CCM ndio kulala usingizi.
Nimesema mimi pia naichagua CCM kwa sababu sijaona mbadala. Wapinzani hawachaguliwi kwa sababu hawajaonyesha wanaweza, nimehudhuria kampeni ya Chadema nikathibitisha wameonyesha wanaweza na wakasema wanaweza watu wa mijini wakawasikia wakawakubali wakawachagua. Watu wa vijijini, wamewasikia, au hawakuwaelewa, au hawakuwakubali wakawapiga chini. Kwa nilichosikia na kuona, ndipo nikakubali ndugu zangu bado wamelala.
Mimi ni pro-democracy siichukii CCM wala sishabikii Chadema, bali natamani tupate heathy opposition kama Democrat na Republican Us na Labor na Conservative UK.
Ili tupate demokrasia ya kweli ndani ya bunge.
Maadamu wapinzani wameanza kuonyesha wanaweza, wananchi wapatiwe civic education ya elimu ya demokrasia, waamke wachague vyama kwa sababu sio kwa mazoea.
2010 maeneo yenye literacy level ya hali ya juu na hali ya kiuchumi yenye ehueni, ushindi wa CCM sio walkover wapinzani watachance, sehemu zenye low literacy level na umasikini wa kutupa ni CCM tuu kwa sababu uelewa ni mdogo ndio maana nasisitiza elimu ya uamsho.
 
Poleni sana wakuu, binafsi nisingependa kuiona CCM inashinda kwa asilimia zaidi ya 60 hapo 2010. Hata kama watashinda basi iwe kwa majority ndogo sana ili wasiliburuze bunge tena.

Uchaguzi mkuu utakuwa tofauti sana maana upinzani hawatakuwa na resources za kupambana na CCM nchi nzima. Hizi chaguzi ndogo ni nafasi nzuri ya upinzani kuchukua majimbo na kujiimarisha.

Jitahidini kufika huko vijijini na kujiimarisha badala ya kuhangaika na hao vijana wazomeaji walioko mjini. Hao sio wapiga kura, wakipewa pesa kidogo wanauza shahada zao za kupigia kura.

Pia hawa wapiga debe hapa JF wanawadanganyeni bure maana wapiga kura walio wengi hata hawajui kama kuja JF. Njia nzuri iwe kwa vijana kuja hapa JF kupata mbinu mpya na kisha kuelekea vijijini kuwahamasisha wananchi walio wengi.

Kule Biharamulo CHADEMA waungeni mkono TLP ili angalau muonyeshe mnaweza kushirikiana na wenzenu.

Kama alivyoandika Mwanakijiji, hii mikutano mikubwa mikubwa japo inasaidia lakini sio substitute ya kampeni za mlango kwa mlango, kitanda kwa kitanda. Ni muhimu kuwa na watu kule chini ambao wanauwezo wa kuendesha kampeni za nyumba kwa nyumba.

Kwenye hili jimbo la uchaguzi mimi nilishaamini kabisa CHADEMA wameshinda, labda nilibugizwa mno na propaganda za JF.
 
Back
Top Bottom