CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!


Posted by Mzee Mwanakijiji:
``Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.``

- Utabiri maana yake ni moja tu nayo ni prediction, inaweza kuwa ukweli au uongo, lakini haina maana ya ukweli kwa 100%, ukweli huwa unaitwa the truth na sio utabiri au prediction.

- Utabiri ni utabiri tu na sio anything else, hauwezi kuchukuliwa serious hata siku moja.

Respect.

FMES!
 
PM, hili ndiyo tatizo kubwa la vyama vya upinzani na sijui kwa nini hawalioni miaka nenda miaka rudi. Wako radhi watumie nguvu zao nyingi kuishambulia CHADEMA badala ya kuishambulia CCM. Na sijui kwanini vyama vya upinzani hawataki kusikia wito uliotolewa kwao na Watanzania mbali mbali ndani na nje ya nchi wa umuhimu mkubwa wa vyama hivyo kuungana na hatimaye kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kupambana na CCM katika kila kona ya nchi. Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga pia aliwapa nasaha kwamba ili kuishinda CCM inabidi waunganishe nguvu na kuunda chama kimoja lakini ushauri ule wala hawakuufanyia kazi. Ubinafsi wa vyama vya upinzani utaisadia CCM kushinda katika chaguzi nyingi zijazo mpaka hapo Wapinzani watakapoamka na kuuweka pembeni ubinafsi huo.

- Mkuu Bubu too late, tayari CCM imeshinda Busanda na Magogoni , na watashinda tena Biharamulo mpaka upinzani watakapojifunza kwamba uchaguzi wa jimbo huko mikoani huwa hauamuliwi na JF, bali wananchi wa jimbo, nguvu nyingi zinapotezwa hapa badala ya huko majimboni, haya ndio matokeo yake!

FMES!
 
hata mie mwana CCM mzee....tupongezane...lakini wakuu wanamtandano wenzangu tukumbukane kwenye kugawana vyeo......FMES,kibunango sasa nguvu tuzihamishie biharamulo.....
Huko Biharamulo ni kuweka rekodi nyingine kali zaidi, kabla ya 2010 na onyo kwa wengine wote wenye ndoto za Alinacha
 
FMES mimi kinachoniuma sio CCM kushinda uchaguzi , kinachoniuma ni jinsi wananchi wa hilo jimbo walivyorubuniwa. Inasikitisha kwamba katika karne ya 21 hawa ndugu zetu hawana umeme na wanaishi katika maisha duni sana.

FMES hebu nieleze CCM imewafanyia nini cha maana hawa watu wa huko Busanda ? Inaniuma sana kwani hawa watu walikuwa na nafasi ya kusend strong message kwa chama tawala lakini wameshindwa. Mimi ndio maana naiheshimu sana mikoa ya kaskazini ...
 
- Mkuu Bubu too late, tayari CCM imeshinda Busanda na Magogoni , na watashinda tena Biharamulo mpaka upinzani watakapojifunza kwamba uchaguzi wa jimbo huko mikoani huwa hauamuliwi na JF, bali wananchi wa jimbo, nguvu nyingi zinapotezwa hapa badala ya huko majimboni, haya ndio matokeo yake!

FMES!

Mkuu FMES, hivi wapinzani wanadhani chaguzi ndani ya Tanzania huamuliwa JF tangu lini!? Na ni kiongozi gani wa upinzani wa CHADEMA, CUF au vyama vingine aliyetamka kwamba chaguzi ndani ya Tanzania huamuliwa JF? Alitoa kauli hiyo lini na wapi? Na hizo nguvu wanazozipoteza JF wanazipoteza kivipi!? Wanafanya nini hapa JF kinachosababisha wapoteze nguvu hizo?
 
FMES mimi kinachoniuma sio CCM kushinda uchaguzi , kinachoniuma ni jinsi wananchi wa hilo jimbo walivyorubuniwa. Inasikitisha kwamba katika karne ya 21 hawa ndugu zetu hawana umeme na wanaishi katika maisha duni sana.

FMES hebu nieleze CCM imewafanyia nini cha maana hawa watu wa huko Busanda ? Inaniuma sana kwani hawa watu walikuwa na nafasi ya kusend strong message kwa chama tawala lakini wameshindwa. Mimi ndio maana naiheshimu sana mikoa ya kaskazini ...

- Busanda sikujui lakini ninawaamini wananchi wa huko kwamba wanajua what is better kwao, nimewahi ksuema hivi hapa JF, kwamba niliwahi kukutana na mwamanchi mmoja aliyeniambia hivi yeye ana njaa kijijini mgombea ubunge anakuja na kumpa kilo tano za mchele, akasema eti ataacha kumpigia kura kwa sababu ya maneno ya huku JF no way,

- Busanda CCM wameshinda kwa sababu wananchi wameamini zaidi kuliko wengine wote, sasa labda uwasaidie mawazo Chadema, lakini sio kuwatukana wananchi wa Busanda, hata mikoa ya Kaskazini yote ni CCM tu hamna lolote, viongozi wote wa upinzani ni CCM tu.

Respect.

FMES!
 
This is a Blessing in disguise kwa CHADEMA. Waangalie wapi panahitaji marekebisho zaidi kwa ajili ya mwakani ambapo kutakuwa na majimbo mengi zaidi ya kunyakua. Kuteleza si kuanguka.
 
Naona hii thread inakamuelekeo kalekale ka watu kudhani matokeo yao ya kisiasa ni muhimu kuliko mustakabali wa wapigakura wenyewe. Nways, binafsi siamini kuwa siasa ni suluhisho la matatizo ya kijamii. Hivyo basi indeleeni na thread yenu halafu mwishoni mnipe majibu ni vipi wa Busanda watapata maji au umeme kwa kupitia mbunge..lol
 
Wapinzani aka wazee wa magigambo.
Muuache upuuzi wa kutafuta urais naomba mufanye uchunguzi mujue majimbo gani mtasimamisha wagombea mahiri. Tunataka mtoe wabunge wa kuchaguliwa wasiopungua 100 mwaka 2010.
Musione tatizo kuachiana majimbo na sio lazima kusimamisha wagombea kila jimbo hata pale ambapo mnajua hamuwezi kushinda au hamkuwahi hata kuwa na tawi la chama.
 
Kwa hali hii naamini kabisa CHADEMA wameshinda kwani karibu nusu ya kura zote ilizopata CCM ni wizi mtupu.
 
... Chadema kama ilivyotabiriwa inaelekea kuchukua ushindi eneo la Katoro (mjini) kwa ushindi wa tsunami. Hata hivyo ngoma yote inaonekana kuwa iko kijijini. Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.
...
Yale majigambo ya Chadema kuongoza, kushinda kwa asilimia 50-55 yako wapi?
Sidhani kama mtu anapotabiri ndo maana yake anafanya majigambo !! Kama utabiri ndio majigambo, basi nadhani Sheikh Yahya anaongoza kwa majigambo Tanzania!!
 
Lakini pamoja na hayo CHADEMA imeweza kuitikisa ngome ya CCM, maana wasukuma na CCM ni balaa.
 
Mkuu FMES,

Heshima Mbele,

Umeongea maneno mazito sana,na ndiyo maana kama utakumbuka Mkuchika alisema magazeti yataandika sana kuhusiana na CHADEMa il wananchi wa kule hawatapata nafsai y a kusoma(which is bad) ila ni moja ya Propaganda .

Mwanzoni kabisa nilitoa maoni kuwa awa jamaa wanatakiwa waunganishe nguvu pamoja kama wapinzani,wakaona ushauri wa kijinga kisa unatoka kwa mwana CCM.Ila wameshindwa kwa kuwa CHADEMa siku zote imejiona ni bora kuliko chama kingine na hii ni tabia ya viongozi waliopo ndani ya CHADEMA.

Nadhani kwa sas watakuwa wamejifunza nini maana ya kuungana na kuwa kitu kimoja.Huko Zanzibar nilijua tu coz mtu kuwa CCM au CUF ni kama DIni yako!

Kuhusu Tarime,CCM wangewe kutumia Mbinu walizotumia Busanda ila Tariiem kulikuwa na ugomvi baina yao(CCM kwa CCM) na pia tatizo lingine ni wale Mungiki ambao walitishia kuchoma vituo vya mafuta kama CHADEMA isingeshinda,Serikali ikaamua ni bora tuwape tu!

Pesa za Helikopta zimepotea Bure na kama mkishindw akuungana Basi mjue Upinzani kusinda sehemu kubwa ya Tanzania Ni Vigumu sana.Mzee Mwanakijiji utrabiri wako ni sawa na Nguvu za Giza katika hili.Haukuona Mbali na haukujua ulisemalo na zaidi ya yote wewe siyo mtu wa Busanda hivyo si miongoni mwao,siyo Mpiga kura na Ndiyo CCM imeshinda sababu ya Ujinga WA WAPINZANIA NA TABIA YAO YA uBINAFSI...SHAME!

UNGANENI!
 
CCM imeshinda sababu ya Ujinga WA WAPINZANIA NA TABIA YAO YA uBINAFSI...SHAME!

Hii kauli si sahihi.

Walioshindwa uchaguzi ni wana-Busanda wenyewe na huo ndio ukweli. Tusikwepekwepeshe mpira golini wajameni. The next thing fot them is to suffer the consequences, or rather to continue to suffer..lol
 
Kuhusu Tarime,CCM wangewe kutumia Mbinu walizotumia Busanda ila Tariiem kulikuwa na ugomvi baina yao(CCM kwa CCM) na pia tatizo lingine ni wale Mungiki ambao walitishia kuchoma vituo vya mafuta kama CHADEMA isingeshinda,Serikali ikaamua ni bora tuwape tu!
I didn't know before kuwa serikali ndio huwa inaamua nani apewe jimbo gani na nani asipewe!! Mkuu Gembe tupe utaratibu wa kuomba jimbo serikalini, kwani kule kwetu Kwela kuna mbunge huwa hatumtaki lakini kila uchaguzi anashinda yeye, maybe tukiiomba serikali itaamua kutupa tunayemtaka
 
Back
Top Bottom