CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

This i plain truth, emotion huwa hazizuii jambo kutokea! kuna wakati huwa watu wakisema ukweli wanatukanwa humu na kuonwa mafisadi au wajinga!
Chadema kama vyama vingine , tafadhali msisubiri dakika za majeruhi ili muonekane kwa wananchi, wananchi wanatakiwa wawa -'feel' nyie.

Kaeni chini, jipangeni, vita inaendelea, kazi mliyonayo ni kuingia katika vinywa na mawazo ya raia wa kawaida! hii itawezekana kama tu mtaamua kubadilisha chama kutoka chama na kuwa ni sehemu ya watu kupata faraja, matumaini, toka ngazi ya kaya mpaka ya taifa!

Kwenye injili tunatumia technique ya nyumba kwa nyumba!, kwenye misiba, harusi n.k let people see you , let them feel you! watumieni watu wenu, mkifanya hivi kwa miezi sita tu, mwakani mnaweza kuleta maajabu!

kukaa na kusubiri kutumia helkopta ''gia kubwa' haitasaidia.JIKITENI VIJIJINI KUANZIA SASA, PIA KUPIGA KELELE KAMA 'OPERATION SANGARA PIA HAKUTAWASAIDIA!!! INAONGEZA MAADUI ZENU KUONGEZA STRATEGY!

Kama tukitaka mambo yatokee then we do not need kelele, silent maana simba mwenda pole ...
 
This i plain truth, emotion huwa hazizuii jambo kutokea! kuna wakati huwa watu wakisema ukweli wanatukanwa humu na kuonwa mafisadi au wajinga!

Chadema kama vyama vingine , tafadhali msisubiri dakika za majeruhi ili muonekane kwa wananchi, wananchi wanatakiwa wawa -'feel' nyie.

- Wapunguze propaganda huku JF, na kutuletea tathmini zenye ukweli labda tunaweza kuwasaidia ushauri, badala ya matusi na ubabe huku tunajua wazi kuwa wanashindwa, huko Biharamulo wawasaidie TLP maana wana mzizi mzito sana huko.

Respect.

FMEs!
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali vijijini bado wamelala, mimi ni Msukuma niliyezaliwa na kukulia mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi literacy level ilivyo kubwa kimenisikitisha na kunihuzunisha. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika na hizo kura imebidi wapigiwe.
Hii ignorance level CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani Wasukumu, ili tumethibitisha ujinga, sisi sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, tumelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwafanya mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini. Pia kuna sisi tunaoichagua CCM kwa sababu hakuna mbadala. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa.
Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika.2010 will never be the same, japo sio anguko kuu la CCM, but the going gets tough na mabadiliko yanakuja.

Wenzetu ilio mbali, Geita isikieni hivyo hivyo, ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!. Nyumba za nyasi ni nyingi kuliko nyumba za bati!.
Watoto wanasura za kutilisha huruma, Wakinamama sura za kukatisha tamaa, kinababa sura za mashaka, dada poa Geita buku, buku mbili, ukitoa dala anataja kuhamia! Unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu unaweza kulia
Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na Geita Gold Mine, upande mwingine Bulyanhulu, upande mwingine Buzwagi, upande mwingine Kahama Gold Mine, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo wameambiwa ni kazi nzuri ya CCM na bado mnawachagua kuyaendeleza kisa
wasukuma ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.
Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....

Pasco.

Lawama za ndugu zako wa vijijini kutokuwa na elimu hata wewe unahusika,umechangia kwa kiasi kikubwa wao kuwa wajinga, ni watu wachache au mmoja huleta mabadiliko kwenye jamii yake.

kama kweli ni kwenu basi unajitukana mwenyewe.ushauri tengeneza sasa mikakati ya kuwainua jamaa zako usisubiri kundi la kampeni ya Chadema liende ndio nawe uende.fungua NGO ya kuleta maendeleo huko mtafanya Mengi ya maana ,kuliko hata angepatikana mbunge kupitia Chadema au Cuf.kuna watu wengi wa Mwanza wamefanikiwa ukiwa mkweli watakusaidia,upinzani kwa kiasi kikubwa umeanzia Mwanza vijijini na shinyanga kwa kina Cheyo na Danhi Makanga.

watu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro wanajipanga wenyewe kabla ya kusubiri serikali iwaletee maendeleo.ukiwa unaishi Dar basi unachukua jamaa wa kijijini kwako waje kusoma.Wapemba na wakinga wameinuana kwenye biashara kwa utaratibu huo.

Kingine usibabaike na helkopta iliyokwenda siku tatu kabla ya uchaguzi ilitakiwa MBOWE awepo huko kipindi cha kujiandikisha kupiga kura,sio siku tatu kabla ya uchaguzi.kama mtu amevutiwa na sera zako hawezi kujiandikisha kwani siku za undikishaji zimekwisha.

Mrema alikuwa anapata watu wengi 1995 kwenye mikutano yake lakini sio wapiga kura,watu wakiona kuna mkusanyiko hata wakupigwa risasi kwa watanzania wanajazana.

Busanda kama ni kijijini ikija Helkopta wanakijiji wanafuata helkopta sio chama wala sera ni kama imekuja sinema au wanatizama mpira.

MkamaP amekujibu kuwa kuwa mjini sio uelevu, ukitizama jiji la Dar-es salaam maeneo ya waliokwenda shule hayana ushawishi wa upinzani ni maeneo ya wasiosoma kama MBAGALA ndiko utaona upinzani una nguvu kama vurugu alizopata mkuu wa mkoa bwana Lukuvi toka kwa mwenyekiti wa serikali za mitaa wa CUF.
MBAGALA ikiwa jimbo la Kigamboni ilitoa mbunge pekee wa upinzani Frank Magoba kwa tiketi ya CUF.

Zitto Kabwe jimbo lake ni la kijijini kuliko Geita au Busanda,marehemu Kabuye mbunge wa TLP yeye anawakilisha Bukoba vijijini,Tlp wameshawahi kushika Kilimanjaro vijiji, unaweza kusema watu wa Bukoba na Kilimanjaro wamesoma lakini kwa Zitto KABWE ni kijijini na kunawasio soma wengi.

mfano wa wazi ni kisiwa cha Pemba majimbo yote ya Pemba hakuna CCM na huko hakuna shule nyingi au umjini,wapemba wengi wanaonekana ni washamba kwa waunguja.

Vyama vya siasa vinatakiwa muda kama huu kuwa bukoba vijijini kuanza kujitambulisha,hawafanyi hivyo kwa vile hawana PLAN na hawataki kupoteza pesa zao wanasubiri bado wiki mbili ndio wanapita.

wewe kama mpenzi wa chadema chukua mfano wa MBEYA VIJIJINI ambako Chadema na CUF vilipata wafuasi wengi kule ni MBEYA VIJIJINI sio mjini CUF walipata karibu kura elfu kumi na kitu wakaweka upinzani mkubwa kwa ccm, jee baada ya uchaguzi ule kuna chadema au Cuf wamekwenda tena? au kuna mkakati wa kuona kuwa eneo lile ni rahisi kupatikana kunatakiwa plan ya kurudi mara kwa mara?

hivi kura mlizozipata BUSANDA mtazipoteza kwani hamtakwenda tena hadi uchaguzi wa mwakani mtapiga kampeni ya siku moja,huwezi kushinda.

elewa kuwa 2010 sio rahisi chadema kupata kura zaidi ya hizo kwani MBOWE,ZITTO,SLAA na wengine watakuwa hawana muda wa kukesha kwa wiki kadhaa kwani wao watakuwa na shughuli kwenye majimbo yao.inasikitisha Pasco huna utaratibu wa kuwapitia watu wa kijijini kwenu hadi umekwenda kikazi au kikampeni.

ukianza wewe wenzako watafuata,fanya fund raising ya kujenga shule moja kwenu tutasaidiana hapa hapa JF.kuwaletea maendeleo watu wako sio lazima uwe mbunge,wapo wabunge wanaojua wajibu wao kama MKONO na Ndesamburo kwa wapiga kura wao.
 
Last edited:
mojawapo ya kitu kilichonishangaza ni kuwa dakika za mwisho Chadema waliweza kupata wanafunzi hata kutoka Nyegezi (St. Augustine) pale kuwa mawakala wa kusimamia kura.. well.. I could use them in a different way. Ngoja tuwasikie maelezo yao kama yatabakia kuibebesha lawama CCM au wanajua makosa waliyoyafanya.
 
Nichukue fursa hii kukipongeza CCM,wameonesha namna gani uzoefu na mtandao wa mashina mijini na vijijini unasaidia hata katika wakati mgumu...

Ushindi huu unatokana na umoja uliooneshwa ndani ya chama .....haasa baada ya kuweka kando umtandawo na kurejesha nguvu za kichama ...kazi iliyofanywa na John malecela ,anne, Na nguvu kubwa aliyoleta John magufuli ...wakati wa lala salama si ya kubeza hata kidogo...

ZAIDI tuwapongeze CHADEMA na kuzidi kuwatia moyo...HAWAJASHINDWA ..huu ni ushindi kwenye safari ndefu...watanzania tunahitaji chama kama chadema...hili hata mwalimu nyerere alilioona na alitabiri wakati huo chadema hawakuwa hata na mbunge mmoja kuwa CHADEMA kitakuja kuwa chama mbadala ....inakuwa kweli!!!......shime chadema wasikate tamaa walk up and walk head straight to biharamulo...kwaani mnapanda mbegu za uamsho kwa watanzania!!

CUF ...hawakunifurahisha saana hasa kwa kushindwa pale magogoni...kwani tofauti ya kura 1,000 kwa zanziba ni kubwa sana....na ukizingatia nguvu za CUF pale...lakini pia wajipange kwani wete patakuwa na uchaguzi soon na ccm wanataka kuwa surprise pemba!!!!

Wapinzani kwa ujumla wamenisikitisha kwa namna wanavyopingana...silaha kuu ya ccm...haswa unapokuta wote badala ya kushambulia adui yao mkuu ccm...wanatumia muda mrefu kuishmbulia CHADEMA....Sijui wanamaanisha niini!!!
 
hijab sio uadilifu wa moyo bana! au unadhani ufichapo mwili ndo kuficha tabia? au wadhani yule ni kobe kupewa gamba gumu ati kisa ni mpole? mwizi ni mwizi 2
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali vijijini bado wamelala, mimi ni Msukuma niliyezaliwa na kukulia mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi literacy level ilivyo kubwa kimenisikitisha na kunihuzunisha. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika na hizo kura imebidi wapigiwe.
Hii ignorance level CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani Wasukumu, ili tumethibitisha ujinga, sisi sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, tumelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwafanya mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini. Pia kuna sisi tunaoichagua CCM kwa sababu hakuna mbadala. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa.
Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika.2010 will never be the same, japo sio anguko kuu la CCM, but the going gets tough na mabadiliko yanakuja.

Wenzetu mlio mbali, Geita isikieni hivyo hivyo, ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!. Nyumba za nyasi ni nyingi kuliko nyumba za bati!.
Watoto wanasura za kutilisha huruma, Wakinamama sura za kukatisha tamaa, kinababa sura za mashaka, dada poa Geita buku, buku mbili, ukitoa dala anataja kuhamia! Unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu unaweza kulia
Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na Geita Gold Mine, upande mwingine Bulyanhulu, upande mwingine Buzwagi, upande mwingine Kahama Gold Mine, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo wameambiwa ni kazi nzuri ya CCM na bado mnawachagua kuyaendeleza kisa
wasukuma ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.

Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....

Naam, wengi tunaweza kabisa kuangusha kilio cha masikitiko. Kusikitika huku ni kuhusu ushindi mwingine kwa Chama Cha Mafisadi, chama ambacho ni chanzo cha matatizo yetu chungu nzima kama nchi. Pamoja na rasilimali chungu nzima tulizojaliwa na Mungu, misaada na mikopo toka nchi wafadhili, mabank mbali mbali ya dunia na mashirika ya kimataifa, bado asilimia kubwa ya Watanzania wanaishi katika ufukara wa kutisha huku viongozi wachache na wapambe wao mapapa wa mafisadi wakijilimbikizia utajiri uliokithiri huku wakiishi maisha ya kifahari kama wale wacheza sinema wa Hollywood na kuwa na majumba ya kifahari katika nchi mbali mbali Ulimwenguni, wakati Watanzania wengi hawajui hata mlo mmoja watupata wapi. Mungu inusuru nchi yetu na janga la kuongozwa na CCM.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Nichukue fursa hii kukipongeza CCM,wameonesha namna gani uzoefu na mtandao wa mashina mijini na vijijini unasaidia hata katika wakati mgumu...

Ushindi huu unatokana na umoja uliooneshwa ndani ya chama .....haasa baada ya kuweka kando umtandawo na kurejesha nguvu za kichama ...kazi iliyofanywa na John malecela ,anne, Na nguvu kubwa aliyoleta John magufuli ...wakati wa lala salama si ya kubeza hata kidogo...

ZAIDI tuwapongeze CHADEMA na kuzidi kuwatia moyo...HAWAJASHINDWA ..huu ni ushindi kwenye safari ndefu...watanzania tunahitaji chama kama chadema...hili hata mwalimu nyerere alilioona na alitabiri wakati huo chadema hawakuwa hata na mbunge mmoja kuwa CHADEMA kitakuja kuwa chama mbadala ....inakuwa kweli!!!......shime chadema wasikate tamaa walk up and walk head straight to biharamulo...kwaani mnapanda mbegu za uamsho kwa watanzania!!

CUF ...hawakunifurahisha saana hasa kwa kushindwa pale magogoni...kwani tofauti ya kura 1,000 kwa zanziba ni kubwa sana....na ukizingatia nguvu za CUF pale...lakini pia wajipange kwani wete patakuwa na uchaguzi soon na ccm wanataka kuwa surprise pemba!!!!

Wapinzani kwa ujumla wamenisikitisha kwa namna wanavyopingana...silaha kuu ya ccm...haswa unapokuta wote badala ya kushambulia adui yao mkuu ccm...wanatumia muda mrefu kuishmbulia CHADEMA....Sijui wanamaanisha niini!!!

- Mkuu PM umesikika sana tena kwa masikio makubwa sana, leo nilipomuona Muungwana aliniambia "..safari hakukuwa na dosari kaka, ushindi saafi...", sasa kwa haya maneno yako nimeamini kwamba finally CCM imeshinda bila mizengwe wala kuiba kura, wewe na Mkulu Mwanakijiji mkikubali, basi inatosha, maneno yako mengi hapo juu ni siasa nzito sana zinazojali masilahi ya taifa.

- Ni kweli bila Chadema, CCM na serikali yake wangekuwa ni usingizi mzito, lakini mpaka kuwaleta wote huko Busanda, tena kwa kuwakimbiza mafisadi na mtandao, basi Chadema mbarikiwe sana na Mungu aibariki Tanzania.

Respect.

FMES!
 
Nilishawahi kusema huko nyuma ya kuwa Watanzania awajui uwiano kati ya siasa na maisha yao kila siku. That is all I can say...
 
Hizi sifa za kuwa na nguvu kwenye mashina ni ccm na policy yake juu ya maendeleo ya nchi?? au ni historical?? Mwalimu na kundi lake tangu enzi za tanu walifanya haya mambo...
It has taken them over 40yrs to establish this??...hongera chadema kwa kuwasha moto even at all odds and history not on your side!!
 
Heshima kwenu wakuu wangu.

Nimesoma breaking news za uchaguzi wa Busanda page 1 - 18, Kimsingi nawapongeza sana wachangiaji wote kwa kazi nzuri mlioifanya. JF naiamini sana, nadhani kwa TZ ni blog inayoongoza kwa ufanisi na ubora kuliko zote

Katika kupitia kwangu hiyo breaking news nilijikuta nashawishika kufanya tathmini ya huo ushindi wa CCM na impact yake kwa JF. (zinaweza zikawa si athari za moja kwa moja (direct effects) ila nimeshawishika nizitaje kwa kifupi kama ifuatavyo.

1. Ushindi huo imepelekea members (JF) wengine WARUSHIANE MATUSI, hii ni negative effect kwa sababu inaadhiri mahusiano na mshikamano. Nakiri hapa ni lazima TUSHIKAMANE LAKINI SI LAZIMA TUAFIKIANE na kwa sababu hiyo haihalalishi kutukanana.

2. Members tumepigana vijembe, hili ni kwangu halina athari aweza nikasema changamoto yake ni fifty fifty. Naamani halina negative effects wala positive effects.

3. Utani, nimeona utani umeibuka, hii ni nzuri sana mana utani unaimarisha mahusiano na ndani yake SMS inakuwa sent and delivered.

4. HEKIMA, BUSARA NA UKOMAVU WA KIMAWAZO, nimejifunza hayo kwa baadhi ya members, mfano baadhi walitukanwa ama walipigwa vijembe lakini wao wakageuza kuwa utani. NIMEFURAHISHWA SANA NAO, nadhani walistahili kupewa uzee wa mahakama maana hiyo ni busara, hekima na ukomavu wa kimawazo kwani hawakujibu kwa tusi amma vijembe. HILO NAWATHIBITISHIA KUWA NAMI NIMELIKOPI NA NIMELIPEST KWENYE MEDULA OBALANGATA.
Naamini inadumisha umoja, mshikamano na kuheshimiana.

I believe in UNITY WITHOUT UNIFORMITY.

HITIMISHO.

Kila mahali penye watu zaidi ya mmoja ni lazima pawe na tamaduni ilyokubalika, kanuni na VALUES. Maana yake bila kujali itikadi zetu, imani zetu, tamaduni zetu na tabia zetu we need to be abide with our JF culture, values and norms.

Mwenye komenti juu ya tathmini na koments zangu naomba amwage hapa JF.
 
Nichukue fursa hii kukipongeza CCM,wameonesha namna gani uzoefu na mtandao wa mashina mijini na vijijini unasaidia hata katika wakati mgumu...

Ushindi huu unatokana na umoja uliooneshwa ndani ya chama .....haasa baada ya kuweka kando umtandawo na kurejesha nguvu za kichama ...kazi iliyofanywa na John malecela ,anne, Na nguvu kubwa aliyoleta John magufuli ...wakati wa lala salama si ya kubeza hata kidogo...

ZAIDI tuwapongeze CHADEMA na kuzidi kuwatia moyo...HAWAJASHINDWA ..huu ni ushindi kwenye safari ndefu...watanzania tunahitaji chama kama chadema...hili hata mwalimu nyerere alilioona na alitabiri wakati huo chadema hawakuwa hata na mbunge mmoja kuwa CHADEMA kitakuja kuwa chama mbadala ....inakuwa kweli!!!......shime chadema wasikate tamaa walk up and walk head straight to biharamulo...kwaani mnapanda mbegu za uamsho kwa watanzania!!

CUF ...hawakunifurahisha saana hasa kwa kushindwa pale magogoni...kwani tofauti ya kura 1,000 kwa zanziba ni kubwa sana....na ukizingatia nguvu za CUF pale...lakini pia wajipange kwani wete patakuwa na uchaguzi soon na ccm wanataka kuwa surprise pemba!!!!

Wapinzani kwa ujumla wamenisikitisha kwa namna wanavyopingana...silaha kuu ya ccm...haswa unapokuta wote badala ya kushambulia adui yao mkuu ccm...wanatumia muda mrefu kuishambulia CHADEMA....Sijui wanamaanisha niini!!]!

PM, hili ndiyo tatizo kubwa la vyama vya upinzani na sijui kwa nini hawalioni miaka nenda miaka rudi. Wako radhi watumie nguvu zao nyingi kuishambulia CHADEMA badala ya kuishambulia CCM. Na sijui kwanini vyama vya upinzani hawataki kusikia wito uliotolewa kwao na Watanzania mbali mbali ndani na nje ya nchi wa umuhimu mkubwa wa vyama hivyo kuungana na hatimaye kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kupambana na CCM katika kila kona ya nchi. Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga pia aliwapa nasaha kwamba ili kuishinda CCM inabidi waunganishe nguvu na kuunda chama kimoja lakini ushauri ule wala hawakuufanyia kazi. Ubinafsi wa vyama vya upinzani utaisadia CCM kushinda katika chaguzi nyingi zijazo mpaka hapo Wapinzani watakapoamka na kuuweka pembeni ubinafsi huo.
 
I hate politiks...nawaonea huruma watu wa BUSANDA!.....

nimejifunza never underestimate the power of Ignorant pipo especially when they are in large groups...they are bad enough in smaller gatherings. CHADEMA waendelee na kuelimisha jamaa wa vijijini kufatilia ahadi za waomba kura...umeme uje BUSANDA vinginevyo 2010 waulizie....Pamoja na kushindwa ni hatua kubwa nawapongeza bado nimeshindwa fungua champagne yangu!
 
PM, hili ndiyo tatizo kubwa la vyama vya upinzani na sijui kwa nini hawalioni miaka nenda miaka rudi. Wako radhi watumie nguvu zao nyingi kuishambulia CHADEMA badala ya kuishambulia CCM. Na sijui kwanini vyama vya upinzani hawataki kusikia wito uliotolewa kwao na Watanzania mbali mbali ndani na nje ya nchi wa umuhimu mkubwa wa vyama hivyo kuungana na hatimaye kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kupambana na CCM katika kila kona ya nchi. Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga pia aliwapa nasaha kwamba ili kuishinda CCM inabidi waunganishe nguvu na kuunda chama kimoja lakini ushauri ule wala hawakuufanyia kazi. Ubinafsi wa vyama vya upinzani utaisadia CCM kushinda katika chaguzi nyingi zijazo mpaka hapo Wapinzani watakapoamka na kuuweka pembeni ubinafsi huo.

BAK siasa za bongo ni ajira na mwajiri mkuu ni CCM, sasa wasipofanya hivyo watakosa ujira. Vyama vingi vinamamluki walio kwenye payroll ya UWT
 
Ushindi ni ushindi tuu, 'The Winner Takes it All, the looser standing small' ni wimbo wa ABBA.
Lazima tuipongeze CCM kwa ushindi wa kishindo.
Nimehudhuria kampeni na kushuhudia upigaji kura. aminini msiamini, CCM imeshinda sio kwasababu inapendwa sana, bali vijijini bado wamelala, mimi ni Msukuma niliyezaliwa na kukulia mjini. Kitendo na kurudi vijijini na kushuhudia jinsi literacy level ilivyo kubwa kimenisikitisha na kunihuzunisha. Asilimia kubwa ya ndugu zangu hawajui kusoma wala kuandika na hizo kura imebidi wapigiwe.
Hii ignorance level CCM wameitumia to their advantage. Siwatukani Wasukumu, ili tumethibitisha ujinga, sisi sio watu wa fujo ila sio siri Wasukuma wa vijijini, tumelala mno!.

Inahitajika civic education ya ukweli kuwafanya mamilioni ya Watanzania wanaoichagua CCM bila kujua wanachagua nini. Pia kuna sisi tunaoichagua CCM kwa sababu hakuna mbadala. Baada ya kuhudhuria kampeni za Chadema jana pale Katoro, nikasema kama CCM itashinda, basi wanaKatoro ni vichaa au wamelogwa.
Chadema imethibitisha inaweza kuwa chama mbadala, Watanzania waliolala wanazidi kuamka na wale wajinga wanazidi kuelimika.2010 will never be the same, japo sio anguko kuu la CCM, but the going gets tough na mabadiliko yanakuja.

Wenzetu ilio mbali, Geita isikieni hivyo hivyo, ndio wilaya yenye utajiri mkubwa wa dhahabu kuliko wilaya zote. Kwa kifupi ndio wilaya tajiri zaidi Tanzania mzima, lakini watu wake ni masikini wakutupwa!. Nyumba za nyasi ni nyingi kuliko nyumba za bati!.
Watoto wanasura za kutilisha huruma, Wakinamama sura za kukatisha tamaa, kinababa sura za mashaka, dada poa Geita buku, buku mbili, ukitoa dala anataja kuhamia! Unagusa tuu, kwisha hata hujasema!, kama ni kwenu unaweza kulia
Hiyo ndiyo Geita iliyozungukwa na Geita Gold Mine, upande mwingine Bulyanhulu, upande mwingine Buzwagi, upande mwingine Kahama Gold Mine, hivi kuna sababu kweli ya Geita kuzama kwenye lindi la Umasikini?. Yote hayo wameambiwa ni kazi nzuri ya CCM na bado mnawachagua kuyaendeleza kisa
wasukuma ni masikini jeuri, umasikini ni jadi yetu, utajiri hatuujui and you can never miss something you have never had.
Wasukuma bado wamelala, wakiamka, walioamka watalala 2010!.
Naomba nikatishie hapa nisije ishia kulia bure...
Kidumu Chama Cha Mapinduzi ....

Ndiyo msimila, hapa naona umemwaga nondo na nakubali kwamba kweli watanzania wengi wa vijijini si wasukuma pekee yao wanahitaji civic education ili kuwaepusha na wimbi la umasikini.
Sisi wachache tuliopata bahati ya kuona uchafu na uozo wa CCM tunajukumu kubwa sana la kuwaelisha wenzetu wengi ambao bado wako katika giza nene.
 
- Mkuu PM umesikika sana tena kwa masikio makubwa sana, leo nilipomuona Muungwana aliniambia "..safari hakukuwa na dosari kaka, ushindi saafi...", sasa kwa haya maneno yako nimeamini kwamba finally CCM imeshinda bila mizengwe wala kuiba kura, wewe na Mkulu Mwanakijiji mkikubali, basi inatosha, maneno yako mengi hapo juu ni siasa nzito sana zinazojali masilahi ya taifa.

- Ni kweli bila Chadema, CCM na serikali yake wangekuwa ni usingizi mzito, lakini mpaka kuwaleta wote huko Busanda, tena kwa kuwakimbiza mafisadi na mtandao, basi Chadema mbarikiwe sana na Mungu aibariki Tanzania.

Respect.

FMES!

Huko nyuma nilisema kuwa CCM wanaonekana kuwa wana mipang mizuri ya ushindi, wanaweza ku-analyze pbs na namna ya kutatua na wanweka wazi jinsi gani ya kuwasahwishi wananchi (kutokana na minutes za kikao warak uliowekwa hapa JF)............naona matunda ya strategies zao yanaonekana...........well sipendi lakini ukweli ndio huo hongera CCM
 
Kwa mara nyingine tena, Chama cha Mapinduzi kimeonesha uwezo wake wa kushinda kura kwa mkakati (strategy). Wapinzani somo hili bado hawajalimudu. Huwezi kushinda uchaguzi kwa kuhutubia. Mara zote kwenye chaguzi aidha nguvu zinatumika au mkakati.

Katika hili CCM bado wana ujuzi na uzoefu wa muda mrefu.

Wakati huo huo hata hivyo tutambue pia kuwa Chadema imeonesha nguvu kubwa huko, tatizo ni je watajenga kutoka hao 21,000? Nitaandika ukosoaji wangu wa wazi baadaye.

Ushindi ni ushindi, CCM imejistahilisha ushindi kwa kujua nini cha kufanya. Kuzomea, kushangilia, kukimbilia helikopta kamwe hakushinda uchaguzi; ni mkakati tu na zaidi ya yote kujiandikisha.

Hili la kujiandikisha nalo ni jambo jingine ambalo linaathiri sana chaguzi hizi; binafsi ningeona ni vyema sana panapotokea uchaguzi mdogo, basi muda wa kujiandikisha kupiga kura nao uongezwe na wananchi wapya wapewe nafasi ya kujiandikisha.

CCM inastahili pongezi zote!

Badala ya kutoa hilo somo nadhani tuandikie wachambuzi mlivyosoma vibaya alama na kutabiri makosa.

Sasa hivi wewe huna mamlaka, huna kuaminika, kutupa mhadhara wa udhaifu wa CHADEMA na uimara wa CCM, milinganyo ya nani kamzidi nani mbinu. Ungeyajua hayo yote usingesema CHADEMA watashinda.

Posted by Mzee Mwanakijiji:
``Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.``
 
Kosa walilofanya wanabodi wengi ni ku-underestimate ujinga wa watu wa Busanda. Hivi kweli inamake sense after what all they have been through , they are still electing CCM . These people are living in the 16 century ;no power, poor education system for their kids but still they are embracing CCM. This is totally insane na ndio maana nasema hivi watu wa kwenye hii forum wanarepresent 0.0001 ya mawazo ya watanzania. Ndugu zetu wengi bado wamelala inabidi wapewe elimu ya uraia kabla ya kuruhusiwa kupiga kura. Kama tungekuwa na watu asilimia 30, wenye mawazo kama ya JF , trust me CCM would have been eliminated longtime ago.
 
Last edited:
kuing'oa CCM madarakani lazima kazi ya ziada ifanyike, bila hivyo tutakuwa tunalalamika kila siku na hali ya Taifa inazidi kuangamia.
Tatizo kuna baadhi ya watu huko vijijini hata hawajui kama kuna vyama vya siasa, wao wanajua chama cha Nyerere (CCM). Viongozi toka vyama vya siasa inabidi wafanye juhudi ya hali ya juu kufikia kijiji hadi kijiji ili baadhi ya watu watoke na imani kwamba kuna chama kimoja tu CCM. Labda hizi juhudi zikifanyika ndipo hapo vyama vya upinzani viweze kushinda Urais miaka hiyo ijayo.
 
Kosa walilofanya wanabodi wengi ni ku-underestimate ujinga wa watu wa Busanda. Hivi kweli inamake sense after what all they have been through , they are still electing CCM . These people are living in the 16 century ;no power, poor education system for their kids but still they are embracing CCM. This is totally insane na ndio maana nasema hivi watu wa kwenye hii forum wanarepresent 0.0001 ya mawazo ya watanzania. Ndugu zetu wengi bado wamelala inabidi wapewe elimu ya uraia kabla ya kuruhusiwa kupiga kura. Kama tungekuwa na watu asilimia 30, wenye mawazo kama ya JF , trust me CCM would have been eliminated longtime ago.

- Pole pole mkuu, wananchi wamezungumza kwa kutumia kura zao through the ballot, kama Democracy inavyotaka, hakukuwa na wizi wa kura wala matatizo katika huu uchaguzi, wewe na mimi hatuishi Busanda, sasa kuwatukana wananchi wa Busanda kwa sababu ya fantansies za JF, wakati wao ndio wanaoijua hali yao ya maisha sio ustaarabu,

- Hivi ni kwa nini usikubali ukweli kwamba umedanganywa na propaganda za JF, kwamba Chadema itashinda kumbe ni uongo wa mchana na matokeo ndio haya yako wazi, kwamba wananchi wa Busanda wanataka kuongozwa na CCM, washambulie Chadema kwa kutowapa wananchi wa Busanda sababu ya kutoichagua CCM.

Respect.

FMES!
 
Back
Top Bottom