Shalom
JF-Expert Member
- Jun 17, 2007
- 1,315
- 128
Hii ni ishara tosha kwamba JF kuna propaganda watu tunalishwa. Kwa kelele za hapa JF mimi niliamini kabisa CHADEMA wanashinda Busanda.
Ina maana taarifa nyingi tulizokuwa tunaletewa zilikuwa za uongo au za upande mmoja. Pale CHADEMA wanapofanya vizuri habari zake tulikuwa tunaletewa, kule wanakofanya vibaya habari zinafichwa. Hiyo ni propanda sawa tu na TV ya serikali au magazeti ya RA au vyombo vya habari vya Mengi.
Inabidi JF tuwe zaidi ya mambo tunayoyapinga.
Nimeshangaa mkuu Pasco ambaye mimi huwa namwamini kutokana na maandishi yake mbalimbali, ghafla kapotea si ajabu baada ya kuona CCM wanaanza kushinda.
Hapa JF hakuna wapiga kura, lazima tuhakikishe tunapeana habari za ukweli mtupu. Kuja kumwaga propaganda JF haitusaidii kabisa badala yake mnaishia kuumiza mioyo ya wapenzi wenu ambao wanajenga hope kumbe hakuna kitu.
Kama kilichokuwa kinaandikwa kilikuwa sahihi basi kuna mawili, either CCM wameiba kura au wale watu waliokuwa kwenye hiyo mikutano walikuwa mamluki kutoka sehemu nyingine na hawakuwa wapiga kura.
Si uje wewe utoe habari vizuri unapenda kupewa tu. Dawa kama unaona kuna tatizo basi jitahidi ulitatue sio kuomba jirani akutatulie