CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Kwa sasa CCM ndio mzizi wa matatizo ya Watanzania. it's time kuing'oa CCM by other means...ballot box can't work now.

Tatizo sio CCM, Tatizo ni ukiritimba wa CCM.....watanzania wakiweza kuondoa ukiritimba huo na huku vyama mbadala vikikuwa na kujijenga kiasasi na kiufuasi ni wazi hali itabadilika ingawa pengine isiwe ile hali wanayoitaka watanzania....

Ili tuendelee ama hata kujinasua katika mwenendo huu wa kuzama kwa taifa letu tunahitaji zaidi ya kuondokana na CCM, tunahitaji mbadala wa kweli wa CCM...hadi sasa nasikitika kusema bado tatujaweza kuonyeshwa mbadala wa kweli wa CCM...ama hatujaweza kutikeleza wajibu wetu wa kujenga mbadala wa kweli ambao watanzania wataweza kuupa imani yao.

Na mnapo hubiri hizo other means nawashauri kwenda kutembelea MBAGALA kujua what realy other mean mean...

omarilyas
 
Mtafute Ka-inzi na utabiri wake...:D Leo mnalala nalo tu donge la koo! CCM kidedea
Mh. Zitto, Benson Kigaila, Dr. Slaa, Mbowe. Na nani vile... Dada Asha Abdallah.
Nawaomba sana msijekuwakatisha tamaa wapenzi waliowapigia kura! Waambie kura mlizopata hazijatosha tu 2010 zitatosha. Naomba msirudi Dar Kabla ya kuwashukuru wananchi wa Busanda.
There is a STRONG mesg kwa CC0
 
Wameshinda kwa bao la mkono!
At last nimempata Zitto, kakiri CCM wameshinda. Yeah, kwa wapenda kuona mabadiliko inaweza kuwakera au kuwauma, lakini jiulizeni kabla ya uchaguzi upinzani katika jimbo hilo ulikuwa katika hali gani? Nadhani kuna maendeleo makubwa. Suala si kuondoa CCM kabisa, suala ni kuonesha kuwa kunahitajika mabadiliko haraka iwezekanavyo! Mabadiliko ya kuwasaidia wananchi
 
Kwa sasa CCM ndio mzizi wa matatizo ya Watanzania. Kibunango kama wapinga hili, nitakuongeza katika orodha ya Mengi....Upinzani ukishindwa Busanda, it's time kuing'oa CCM by other means...ballot box can't work now.
Soma hapo Chini

Kwa ufupi,

CCM wameshinda... Am out
Nina kila sababu ya kwenda kupata ze laga jioni ya leo... Panapo majaliwa Ka-inzi atatuletea habari ya kukubali ama kukata rufaa.

Kwa sasa Hongera sana CCM, juhudi zenu za dhati katika kutumikia wananchi zinaonyeshwa kwa ushindi huu muhimu. Zaidi ni kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuondoa kero zao za kila siku.

Hongera sana Mh. Mbunge mchaguliwa.

Shukrani kwa wote ambao wamewezesha kupatikana kwa matokeo haya hapa JF
 
Nadhani tunaweza kuendelea kuanzia hapo, tutafika tu, hata hiyo jamii ya vijijini itafikiwa. Mabadiliko siyo kitu cha mara moja ni process. Tusikate tamaa, tukaze mwendo, safari ni ndefu, lakini anguko la hawa jamaa haliko mbali sana!!! Kuna mwanga mbele.
 
At last nimempata Zitto, kakiri CCM wameshinda. Yeah, kwa wapenda kuona mabadiliko inaweza kuwakera au kuwauma, lakini jiulizeni kabla ya uchaguzi upinzani katika jimbo hilo ulikuwa katika hali gani? Nadhani kuna maendeleo makubwa. Suala si kuondoa CCM kabisa, suala ni kuonesha kuwa kunahitajika mabadiliko haraka iwezekanavyo! Mabadiliko ya kuwasaidia wananchi

Tatizo la CHADEMA
wanafikiri wananchi wote ndio wafuasi wa JF,kumbe JF ngoma karibu zote ziko nje?
Waulizeni CHADEMA ofsi zao ktk jimbo hilo zipo ngapi? mambo ya zima moto hayo,wakishindwa huko watakuja kusema wameibiwa kura
 
Anyway, sio safari mbaya, next time tutafika kileleni. Kuna haja tu ya kujifunza zaidi baada ya matokeo kama haya. Mapungufu makubwa yalikuwa upande upi, na shria na taratibu jinsi ambavyo zinaathri demokrasia.

Ni wazo zuri kwa chadema kuwashukuru wananchi kwa ushindi huu walioufikia ukilinganisha na kura za kipindi kilichopita.

Hii inaonyesha sawia kabisa kuwa kukiwa na uwanja tambarare vyama kama CHADEMA vinafursa ya kubadilisha upepo na kufanya watanzania waweze kusikika tofauti na ilivyo sasa kwa bunge la ccm pekee.

Mungu ibariki Tanzania na wote wapenda mabadiliko ya kweli.
 
Tatizo la CHADEMA
wanafikiri wananchi wote ndio wafuasi wa JF,kumbe JF ngoma karibu zote ziko nje?
Waulizeni CHADEMA ofsi zao ktk jimbo hilo zipo ngapi? mambo ya zima moto hayo,wakishindwa huko watakuja kusema wameibiwa kura
MkamaP,

JF haina udugu na chama chochote cha siasa. Ndo maana kuna Kibunango, Mwiba na Mnyika. Tunatazama pande mbili za shilingi.
 
Nadhani tunaweza kuendelea kuanzia hapo, tutafika tu, hata hiyo jamii ya vijijini itafikiwa. Mabadiliko siyo kitu cha mara moja ni process. Tusikate tamaa, tukaze mwendo, safari ni ndefu, lakini anguko la hawa jamaa haliko mbali sana!!! Kuna mwanga mbele.

Hakuna cha kufika hapo NCCR mwaka 1995 ilikuwa chachu kuliko leo 2010 CHADEMA. Huwezi kusema watu ndio wanaanza kuamka wakati 1995 tuliona wabunge wengi wa upinzani.Kusema hivyo nikujaribu kujidaganya tu.
 
At last nimempata Zitto, kakiri CCM wameshinda. Yeah, kwa wapenda kuona mabadiliko inaweza kuwakera au kuwauma, lakini jiulizeni kabla ya uchaguzi upinzani katika jimbo hilo ulikuwa katika hali gani? Nadhani kuna maendeleo makubwa. Suala si kuondoa CCM kabisa, suala ni kuonesha kuwa kunahitajika mabadiliko haraka iwezekanavyo! Mabadiliko ya kuwasaidia wananchi

Kweli sasa nimekubali kuwa nchi hii ina laana, du! itabidi nifanye mpango wa kuishia na kwenda kutafuta nchi ya ahadi na kuhakikisha navuta ndugu zangu wote ili nisikumbuke tena huku Misri!

Wtu wengine wanafanya mzaa lakini inauma sana siwezi kuendelea kuwa shuhuda wa
-Vifo vya Albino
-Vifo vya kina mama wajawazito kati ya 1000 , 150 hufa
- Bila rushwa hamna maisha
-Watoto wenye umri chini ya miaka mitano
-kila mtu anataka kuwahi barabarani basi ukiwa mstaarabu kila siku unachelewa kazini
- approval za mabenki yetu zote zinatoka kenya au SA
- maji kama zahabu
 
Tatizo la CHADEMA
wanafikiri wananchi wote ndio wafuasi wa JF,kumbe JF ngoma karibu zote ziko nje?
Waulizeni CHADEMA ofsi zao ktk jimbo hilo zipo ngapi? mambo ya zima moto hayo,wakishindwa huko watakuja kusema wameibiwa kura

Naona unaanza kutokuwa realistic, huwezi kutegemea CHADEMA kuwa na ofisi kila sehemu nchi hii ghafla kama unavyodhani. Hapo baadaye sawa, tatizo lililopo kwa sasa ni kila mmoja kudhani kuwa kazi ya kuikomboa hii nchi ipo mikononi mwa CHADEMA,nadhani si sahihi.
Hii ni nchi yetu sote, kuanza kuwalaumu wao kama chama ni kosa, tuipiganie sote. Watu fulani wanafanya kadri ya uwezo wao kujaribu kuleta mabadiliko, kuna kundi linafanya kila namna kupinga hayo mabadiliko na kutetea UFISADI na looting. Ni vita unayowapigania watu ambao hata wenyewe hawaelewi kuwa unawapigania. Mpenda mabadiliko yeyote aliyechoshwa na utawala huu ni lazima afanye jambo, hata kama ni kwa kuwashawishi ndugu zako popote walipo waachane na hilo chama lao inaweza kuwa ni hatua ya kuanzia. Nimeanza na babu yangu, ameelewa somo, japo umri umeenda wewe umeanza na nani?
 
Tatizo la CHADEMA
wanafikiri wananchi wote ndio wafuasi wa JF,kumbe JF ngoma karibu zote ziko nje? Waulizeni CHADEMA ofsi zao ktk jimbo hilo zipo ngapi? mambo ya zima moto hayo,wakishindwa huko watakuja kusema wameibiwa kura

You make me sick!
 
Binafsi kwa matokeo haya bado naona tumeshinda pamoja na kwamba Magesa haendi bungeni. Hakuna mtu atakayebisha kuwa operasheni sangara imefanya kazi, na kwamba CHADEMA really is becoming an alternative party and a government in waiting. Siku za CCM zinahesabika, sio chadema walioamua hivi ni wananchi wenyewe.

Hili pia ni jibu kwa tafiti tata za REDET. Sasa wajiulize hizi data ambazo wamekuwa wakitoa zikionyesha kwamba CCM bado wanakubalika sana hasa vijijini hao research assistants wao huwa wanazitoa wapi? Hawa ma-RAs wa REDET wanaendaga field kweli au hujaza dodoso wenyewe?

Na mwisho hili liwe ni jibu kwa ndugu zetu CUF kwamba wananchi wameshaamua kuwa huku bara mbadala wa CCM ni CHADEMA. Wakiendelea kulifumbua macho hili wananchi watawaweka katika kapu moja na CCM na athari zake hazitaishia bara, bali zitateremka hadi visiwani.
 
Ni bahati mbaya lakini ni muhimu niseme CCM ndiyo inaweza kujifunza zaidi kwenye uchaguzi kama huu zaidi ya CHADEMA.
Ushauri: acheni upuuzi wa vita vyenu vya mtu kwa mtu vya mafisadi.
Operation Sangara ndio ya maana. Hasa wewe Dr. Slaa unamaliza airtime ya wapinzani kwa vita vyako visivyokuwa na miguu wala kichwa.
 
Hii ni ishara tosha kwamba JF kuna propaganda watu tunalishwa. Kwa kelele za hapa JF mimi niliamini kabisa CHADEMA wanashinda Busanda.

Ina maana taarifa nyingi tulizokuwa tunaletewa zilikuwa za uongo au za upande mmoja. Pale CHADEMA wanapofanya vizuri habari zake tulikuwa tunaletewa, kule wanakofanya vibaya habari zinafichwa. Hiyo ni propanda sawa tu na TV ya serikali au magazeti ya RA au vyombo vya habari vya Mengi.

Inabidi JF tuwe zaidi ya mambo tunayoyapinga.

Nimeshangaa mkuu Pasco ambaye mimi huwa namwamini kutokana na maandishi yake mbalimbali, ghafla kapotea si ajabu baada ya kuona CCM wanaanza kushinda.

Hapa JF hakuna wapiga kura, lazima tuhakikishe tunapeana habari za ukweli mtupu. Kuja kumwaga propaganda JF haitusaidii kabisa badala yake mnaishia kuumiza mioyo ya wapenzi wenu ambao wanajenga hope kumbe hakuna kitu.

Kama kilichokuwa kinaandikwa kilikuwa sahihi basi kuna mawili, either CCM wameiba kura au wale watu waliokuwa kwenye hiyo mikutano walikuwa mamluki kutoka sehemu nyingine na hawakuwa wapiga kura.
 
Hakuna cha kufika hapo NCCR mwaka 1995 ilikuwa chachu kuliko leo 2010 CHADEMA. Huwezi kusema watu ndio wanaanza kuamka wakati 1995 tuliona wabunge wengi wa upinzani.Kusema hivyo nikujaribu kujidaganya tu.

So what is your point here bwana mkubwa? Kukua kwa chadema kunakukera au namna gani? Sijakupata kabisa unachojaribu kusema!
 
CCM inabidi walisifu sana trekta, bila ya Malecela huu uchaguzi wangebwagwa tena.

Msekwa hana uwezo wa kuongoza kampeni za CCM, kazi imemshinda na kama JK anajua kusoma alama inabidi amwondoe.

Nilifikiri trekta limezeeka lakini kwa hili nafikiri yule mzee ni asset kwa CCM.
 
Back
Top Bottom