CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Tatizo la vyama vyetu vya upinzani vinahhirikiana kwa maneno lakini inapofikia kupractice kwa vitendo ni F.Nimekerwa sana na vyama vya upinzani kuwa na mgombea zaidi ya mmoja kama wangeshirikiana wangweza kuiangusha CCM.Naomba waanze kujifunza kutokana na hili la BUSANDA
 
Mapolisi walikuwa wamepotea Mwanza na Mara....kwa shughuli ya usalama wa CCM huko Busanda.Ilikuwa amani kwa wengi hasa daladala.

Sasa tunategemea warudi tuanze ufisadi barabarani.
 
ahsante makalangilo kwa kulielewa hilo.. ni kweli watanzania tumefanya ccm kama ndo damu yetu, lakini wasukuma wamezidi kwani nadahani wanaamini hata pumzi yetu tulionayo watanzania inamilikiwa na ccm...mwanza, shinyanga, tabora nk wakonyuma kwa kila idara lakini sisiem inapeta tu.... magu ni wilaya moja wapo tanzania zenye mapato makubwa na idadi ya watu wengi lakini haina shule ya a level ni sisiem inapeta... mbaya kuliko na wasomi wa kizazi kipya wamelijua hili nao wameamua kuwa wenzao...nchimbi, dc magese, ngeleja wote hawana jipya ufisadi mtu

Tanzania will never develop until ccm is out of power
 
Mapolisi walikuwa wamepotea Mwanza na Mara....kwa shughuli ya usalama wa CCM huko Busanda.Ilikuwa amani kwa wengi hasa daladala.

Sasa tunategemea warudi tuanze ufisadi barabarani.


Walishakula posho zao za siku kadhaa hivyo mtarajie kupumzika kwa siku kadhaa mpaka pale mifuko yao itakapopwaya
 
Pia kuna haja ya kutofautisha chaguzi ndogo na uchaguzi mkuu. Ni kawaida sehemu mbalimbali vyama vya upinzani hufanya vizuri kwenye chaguzi ndogo maana ni rahisi kuweka resources zote pamoja. Uchaguzi mkuu utakuwa tofauti, itabidi kila mtu ajifungie kwake akitetea jimbo lake.

Nilichojifunza kwenye chaguzi za vijijini ni kwamba viongozi wa vijiji na kata husaidia sana kuleta ushindi. Chama kinachokuwa na viongozi wengi wa namna hiyo, huwa vinashinda kwenye majimbo husika. Ukisikia wizi wa kura ni hao viongozi ndio wanafanikisha. Ndio maana ni ngumu sana CCM kushinda Pemba kwasababu hawana viongozi wa kuwasaidia kule matawini na hata wakipanga kuiba mbinu zao zinajulikana.

Upinzani mujitahidi sana kushinda viti vingi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwaka huu. Hao ndio watu wanaofanya chama kishinde au kishindwe huko wilayani. Nafikiri hata Tarime ilikuwa hivyo hivyo, CHADEMA wana viongozi wengi kule hivyo ujumbe wao ulikuwa unafika kwa wananchi kirahisi.

Wilayani kuna watu wengi hawana kazi za kufanya, kukiwa na mkusanyiko wowote, wao wanajazana hapo kujifurahisha. Mikutano ya nje mara nyingi inadanganya maana unaweza kufikiri una watu wengi, kumbe wengine wamekuja kuangalii sanaa za wanasiasa. Kampeni za mlango kwa mlango ni muhimu mno.

CHADEMA mmejitahidi lakini kujitahidi hakutoshi, inatakiwa kushinda. Inabidi kuboresha mapungufu mbalimbali ambayo wengi hapa wameyaongelea. Pia jaribuni sana kutumia weaknesses mbalimbali za CCM. Kwa mfano kuwavuta haraka wale wanaoshindwa kwa mizengwe kwenye chaguzi za CCM maana wengi wanakuwa na watu wa kutosha. Mimi nimemsifu malecela kwasababu kitendo cha kumrudisha yule jamaa aliyeshindwa kwenye kampeni za CCM naamini kimewasaidia. Viongozi wengine wangedharau na kumwacha nje ya kampeni.

Watu kama Dr. Slaa, Zitto, Mnyika, Kitila na wengine wachache wana uwezo, lakini namba bado ni ndogo. Wavuteni watu wengine wengi hata hapa JF ili wakasaidie kusukuma gurudumu la chama hapo 2010. Mkiweza kuwashawishi, kuna watu wengi hapa JF wanaweza kukubali kugombea kupitia CHADEMA.
 
ahsante makalangilo kwa kulielewa hilo.. ni kweli watanzania tumefanya ccm kama ndo damu yetu, lakini wasukuma wamezidi kwani nadahani wanaamini hata pumzi yetu tulionayo watanzania inamilikiwa na ccm...mwanza, shinyanga, tabora nk wakonyuma kwa kila idara lakini sisiem inapeta tu.... magu ni wilaya moja wapo tanzania zenye mapato makubwa na idadi ya watu wengi lakini haina shule ya a level ni sisiem inapeta... mbaya kuliko na wasomi wa kizazi kipya wamelijua hili nao wameamua kuwa wenzao...nchimbi, dc magese, ngeleja wote hawana jipya ufisadi mtu

Tanzania will never develop until ccm is out of power

Mimi nadhani hayo ni matusi kwa Wasukuma.

Badala yake tutizame wapinzani wameshindwa wapi?

Lazima tukubaliane kua CCM bado wana mtandao mkali sana vijijini kwenye wapiga kura wengi.

Hoja ni vipi kufika kwenye wapiga kura wengi.

Tatizo la CHADEMA limejirudia tena, kwa maoni yangu tatizo ni kama la Tunduru.

CHADEMA wanahadaika sana na utitiri wa watu katika mikutano yao ya mijini,wanapaswa kujua miongoni mwao hawakujiandikisha,wakulima wamekuja kuuza mazao yao,vibaka n.k

Zipo taarifa kua CHADEMA ilipanga watu wa kuzomea mikutano ya CCM,pia iliarifiwa kuwa Kamanda Zitto aliamuru watu wavae manati,hivi ni baadhi ya vitu vinavyo viza kampeni za wapinzani.

CCM walipogundua kua CHADEMA wana wanazi wengi mijini hasa kata ya katoro,wakaamua kubadili mbinu kwenda vijijini kama walivyofanya Tunduru,matokeo yake ni kama haya.

Wapinzani wanapswa kua wamoja na kufanya kampeni zao kisayansi,vinginevyo tutaendelea kutukana makabila ya watu wakati wapinzani wenyewe hawako makini.
 
Hakuna wa kulaumu kuhusu hali hii ila Mwalimu Nyerere.

Nakubaliana na hoja zako lakini sidhani Mwalimu ni mchawi wa kila tatizo. Wasukuma wanaongoza kwa mauaji ya vikongwe na ablino, ni fikra za Mwalimu hizo? Mimi nadhani ustaarabu ulichelewa tu kuingia Sukumaland, kuchelewa kwa shule na dini kupenya katika eneo hilo pia kumechelewesha mengi.

Wenzetu bado wana 'hangover' ya utawala wa Waingereza ya 'Uwagawe ili Uwatawale'. Wamegawanyika sana hata wabunge hawaelewani wao kwa wao ingawa wote ni wa CCM.Ukumbuke kuwa Sukumaland ndiyo inayotuamulia nani awe Rais wa nchi hii kutokana na kuwa na wapiga kura wengi.
 
Matokeo ya uchaguzi huu yanadhihirisha kuwa ili upinzani uweze kushinda viti vingi zaidi vya ubunge, kazi ya ziada inahitajika. Si sahihi kudhani/kushutumu wananchi kwa kufanya uamuzi wao wa kidemokrasia katika kuamua nani awe mwakilishi wao. Wameamua kuipa CCM nafasi hiyo, na hiyo ni haki yao na ni sahihi kabisa. Ni sahihi pia kama wangeamua mgombea mwingine yeyote kuwa mwakilishi wao Bungeni. Wao ndio wanaojua wanachokitaka, na wamechagua wanachokitaka.

Wapinzani na hasa CHADEMA ni vyema wakafahamu kuwa, kura walizopata zimetokana na kazi nzuri waliyofanya Busanda. Wanabidi kufahamu kuwa 2010, kura hizo zinaweza kuongezeka ama kupungua, kutokana na jinsi watakavyoamua kuzilinda na/au kuziongeza.

Kwa mtazamo wangu, wapinzani wanatakiwa kufanya yafuatayo ili kujihakikishia ushindi katika chaguzi zifuatazo;

1. Wahakikishe wanakuwa na matawi mengi vijijini: Wananchi wa vijijini hawana kitu kinachoweza kuwafanya waamini kuwa wapinzani wanaweza kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji. Bila vyama vya upinzani kuwa na presence kubwa vijijini, chaguzi mbalimbali zitaendelea kuwashangaza.

2. Wahakikishe kuwa, sera zao zinalenga katika kujibu matatizo ya hali halisi ya wananchi wanaotarajia kuwaomba kura. Sera ziwekwe bayana, na ziwe zinazokubalika. Kubainisha mapungufu bila kutoa suluhu ya matatizo, haimaanishi kuwa matatizo hayo yatakwisha endapo wapinzani watachaguliwa. Inabidi kutoa utatuzi wa matatizo hayo na kubainisha jinsi ambavyo sera za CCM haziwezi kuyatatua bali wao pekee ndio wenye uwezo huo.

3. Wahakikishe kuwa mikakati ya ushindi ni endelevu. Wasiweke jitihada za ushindi wakati inapotokea nafasi ya uchaguzi tu. Inabidi hata kipindi ambacho hakuna uchaguzi, kuwe na tathmini zinazoweza kuwafanya wajue idadi ya kura wanazoweza kupata endapo uchaguzi utafanyika, na ubunifu wa mbinu za kuziongeza kura hizo (kata hadi kata). Tathmini hizo ziwe za ukweli na zinazoendelea kubadilika siku hadi siku, wiki hadi wiki, mwezi hadi mwezi na hata mwaka hadi mwaka.

4. Wajue mbinu zinazotumiwa na wapinzani wao. Waangalie nguvu za kila chama katika eneo husika, na watafute mbinu za kuweza kuzishinda nguvu za wapinzani wao kila mara. Wajue pia udhaifu wa wapinzani wao na kuutumia bila subira katika kujenga nguvu zao. Wakati huo huo, wanatakiwa wajue nguvu ya baadhi ya wananchi wenye kukubalika katika maeneo husika, na hao watumike kuongeza nguvu zao.

5. Kampeni ni njia ya kuomba kuchaguliwa au kujenga kukubalika kwa wananchi. Upinzani unatakiwa kujua jinsi ya kuongea na wananchi ili waweze kukubalika kwao. Mbinu za ubabe, matusi au kashfa haziwezi kusaidia kuongeza kukubalika kwa chama chochote. Wananchi huogopa na pia huchukizwa na vyama vinavyotumia nguvu nyingi, dharau na maneno yasiyoonyesha nidhamu katika kuomba kura.

CCM imeshinda Busanda, na CCM inaweza kushinda sehemu nyingine nyingi zaidi endapo upinzani utaendelea kutojifunza kutokana na matokeo katika majimbo kama haya (Busanda, Tarime). Kila uchaguzi ni lazima uzae somo kwa wanasiasa wanaokusudia kupata ushindi kwa vyama vyao.

Kama upinzani ni kushinda chaguzi tu basi hapo unayosema nayakubali maana niwatu kupata nafasi za uongozi tu na hii kwangu inaonyesha dalili ya selfish attitude. Kazi ya upinzani nikuleta awareness ku create checks and balance etc etc. Wapinzani wamefanya kazi kubwa sana kwa kuwa force CCM kupeleka hata angalau nguzo za umeme Busanda; think of kama chama kingekuwa kimeshika hatamu what could have been the out come? Nawapa hongera wapinzania kwa kusimama katika zamu yao naomba wasife moyo uongozi si lazima uwepo kwenye nafasi hata ukiweza kuinfluence maamuzi to the welfare of many people inatosha.... Keep it up.
Hata kwa viongozi wakuu wa chama na serikali kuwepo Busanda at a particular time ni mchango tosha wa upinzani kwa watu wa Busanda kwani wameona baadhi ya matatizo na kwakujua kesho yaja wata act accordingly. Hongera pia kwa mzee wangu Malecela kwa mapenzi mazito ya chama chake hata pamoja na kutokuwa na nafasi yeyote ya juu ya uongozi kitaifa bado alikubali kubeba jukumu la kuletea ushindi chama chake... it shows how commited is to his party keep it up mzee na mimi kama mpenda upinzani ntaeendelea kukipinga chama chako ili kuleta chachu ya maendeleo kwa watanzania na kuleta democracy ya kweli kati yetu sisi raia wa nchi hii.
 
Kama CCM wameshinda basi sina budi kuwapa hongera kwani inaonesha wapiga kura wengi wa busanda (kama kweli) walikubaliana na sera sera za ahadi zisizotekelezeka. Hongera sisemu kwa ushindi
 
Kama CCM wameshinda basi sina budi kuwapa hongera kwani inaonesha wapiga kura wengi wa busanda (kama kweli) walikubaliana na sera sera za ahadi zisizotekelezeka. Hongera sisemu kwa ushindi


CCM wameshinda lakini naamini somo lenyewe wamelipata ingawa sina hakika kama wamelielewa. Kutoka kushika hatamu hadi kuzomewa wazi wazi ni "Mapunduzi ya fikra". Watu wasikate tamaa, chombo kinakaribia pwani! Tutafika salama tu.
 
Ufisadi wa ccm utamalizika mpaka waTz wote tutakapoamua kama kufa na tufe.... tumesikia busanda wakala wa Cuf hakuruhusiwa kuingia hali ya kuwa amekamilisha taratibu zote na barua ya tume anayo na chedema walivodhulumiwa..

Magogoni kuna watu walikuwa wanakusanya shahada za wapiga kura baada ya kutoka katika chumba cha kupiga kura, wengine wamonekana na shahada 3 mkononi wakakimbia wasipigwe picha,kama hiyo haitoshi wakati wa kuhesabu kura ilikuwa usiku UMEME UKAZIMWA... Yapo matukio ya kabla uchaguzi nayo ni mengi tu...

SASA KWA HALI HII TUTAWEZA KUIONDOA CCM WAKATI NA JESHI LOTE LIPO KUHAKIKISHA CCM INABAKI MADARAKANI KWA GHARAMA YOYOTE,IKIWA KUUWA,KUPIGA,KUTESA,KUNYANYASA NA MENGINEO NA YOTE YAMETOKEA HAYO ???

 
Watanzania tuliochoswa na utawala wa sasa ambao umedumu kwa miaka 47, na mpaka sasa haturidhiki tulipofikia, tunajihisi nchi inaenda mwendo wa kinyonga kama sio imesimama kabisa.

Pamoja na maoni yote yaliyotolewa humu..tusiwaachie hii kazi wapinzani peke yao. MIMI NA WEWE tumechoswa,
MIMI NA WEWE tunataka mabadiliko. Je MIMI NA WEWE tufanye nini?


Nasisitiza haya matokeo yanaonyesha vijijini sio kwamba wamelala, ila wanatakiwa kuamshwa. Hii kujaribu kuwaamsha inapokaribia uchaguzi inaonekana haisaidii sana.
Wengi wameshauri wapinzani wafungue matawi vijijini ambako bado wanaamini CCM ndio BABA, ndio MAMA, ndio MILELE. Hili ni wazo zuri sana...ianzie hapo.


Lakini na SISI PIA tujitolee kwa hali na mali kuwaelimisha wananchi tusiseme tu "UPINZANI UNATAKIWA KUFANYA HIVI NA VILE ILI WASHINDE", tujiulize MIMI NA WEWE tufanye nini??
Tuwaelimishe wananchi waepukane na dhana potofu kuwa UKICHAGUA UPINZANI AMANI ITATOWEKA. Tuwaelimishe nia na madhumuni ni kuiweka hii nchi ili ianze kutembea towards maendeleo kwa mwendo unaoridhisha.


So MIMI NA WEWE, tujumuike kwa vitendo, SEHEMU YEYOTE, WAKATI WOWOTE NA MAHALI POPOTE tunapokuwa. Hata TUKIjikuta vijijini kwa ajili ya kazi. Tutumie hiyo opportunity kuwaelimisha wananchi wenzetu...na nina imani mwishowe tutashinda.
Statistics za jumla ya kura za CHADEMA katika hilo jimbo zinaridhisha, hawajapata ushindi lakini %wise wameimprove toka 2005..so hii inatia moyo. Inaonekana sasa wananchi wanaamka, sasa tusiwaache walale kusubiria 2010. Tuendelee kuwapa dozi za chachu ya mabadiliko.
Tujitahidi hata kama JK akishinda uraisi 2010, tuhakikishe idadi ya wapinzani bungeni inaongezeka.


Tunachoomba vyama vya upinzani, wahakikishe wanateua wagombea wenye NIA na MALENGO ya kumkomboa mwananchi maskini.
UMASKINI jamani sio mzuri, unatiisha huruma kwa kweli. Halafu mbaya zaidi kwa asilimia kubwa ni umaskini wa kujitakia kwa sababu ya UTAWALA MBOVU.

Nasisitiza, hata ikibidi kuvichangia kimapato vyama vya upinzani iwe CHADEMA ama CUF kama tunaridhia wasifu wa mgombea na tusaidie pia tusiwaachie peke yako.
KAMA TUMECHOKA, NA SISI TUWASAIDIE WAPINZANI KWA VITENDO.
 
Ka nzi ka kijiji kametua Busanda tangu jana, na taarifa za matokeo ya uchaguzi zimeanza kutiririka sasa hivi. Kura zimemalizwa karibu masaa matatu yaliyopita.

a. Chadema kama ilivyotabiriwa inaelekea kuchukua ushindi eneo la Katoro (mjini) kwa ushindi wa tsunami. Hata hivyo ngoma yote inaonekana kuwa iko kijijini. Utabiri wangu wa Chadema kushinda jimbo zima kati ya asilimia 50-55 bado unasimama.

b. Naibu waziri mmoja (Mwantuma Mahiza) na diwani wadaiwa kukutwa na shahada ambazo hazijatumika na haieleweki kwanini amekutwa nazo. Chanzo kingine kinasema ni karatasi zilizokwishapigiwa kura ingawa chanzo cha awali is more authoritative (non-partisan).



will keep u updated every half hour..
Mbona kimya sana mkuu imeshapita zaidi ya masaa mawili bila updates! Tupe hizo news mapema sana maana ukimya wako watupa wasiwasi mkuu! Vip upo pamoja nasi au?
 
MISSKITIM...
Take 5 baba but it would be better ingekua hiyo post yako ungeifanya thread mpya kabisa tuchangie kama SISI ( MIMI NA WEWE ) tunatakiwa tufanye nini kuamsha wananchi na kusaidia vyama vya upinzani...
 
Mapolisi walikuwa wamepotea Mwanza na Mara....kwa shughuli ya usalama wa CCM huko Busanda.Ilikuwa amani kwa wengi hasa daladala.

Sasa tunategemea warudi tuanze ufisadi barabarani.



Alnadaby hawa polisi lengo kama ilikuwa ni kuleta amani Busanda!!!! But lengo kuu na la kupangwa ni kuwa polisi hao na wengine toka sehemu .... walikuwa ni miongoni mwa wapiga kura wa Busanda!!! Zile shahada zilizokusanywa kabla ya uchaguzi zilitumika zote jana!!!! Sasa 2010 ndiyo inakuja, wanajeshi na polisi wanaanza kuandaliwa sasa, likizo za dharura kwa askari jeshi/polisi ziko nyingi siku chache kabla ya uchaguzi na wanarudi vituo vya kazi mara baada ya uchaguzi, na wengine wanatumwa zile sehemu ambazo kuna stiff competition ili wakadhibiti!!! SSSSSMMMMMM tu wajanja mno!!!


Hatutegemei mabadiliko yoyote kiutendaji wa serikali hii kwa wabunge wote walioshinda (huko Zanzibar na Busanda), hakuna kitu hapo.
 
wakuu heshima kwenu.
Nadhani kuna umuhimu wa kuwa na tathimini ya kweli bila kufarijiana kitoto juu ya kushindwa kwa upinzani katika uchaguzi huu ndipo kunaweza leta mabadiliko kidogo, vinginevyo itakuwa ni kufurahishana tu janvini.
Ukweli ni kuwa Mzee Malecela alisema...ndege hazishindi vita bali askari wa nchi kavu ndio huteka na kushinda vita, wakampuuza wapinzani, sasa kipigo kimewashukia kila mtu anakuja na sababu yake.
Mara zote ndugu zangu wapinzani wanasahau kuwa kuna mkakati muhimu baada ya kufunga kampeni saa kumi na mbili jioni siku ya mwisho wa kampeni. Hapo ndipo upinzani hupigwa mabao yote.
Ukiona CCM imeshindwa mahali ujue anayeongoza kampeni hizo aliiga kampeni za upinzani za kupiga kelele na kama mwandishi wa barua kwa yeyote anayehusika badala ya kuandika specific address.
Ushauriç imedhihirisha ni ngumu mno kwa upinzani kushinda kwa s
 
Back
Top Bottom