CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

CCM imeshinda kwa kura zaid ya 29,000 dhidi ya kura zaidi ya 22,000 za Chadema katika uchaguzi mdogo wa Busanda. Tume inatarajiwa kutangaza matokeo wakati wowote leo

Mbona hizi data zako zimekaa kipolitiki zaidi??? Waliopiga kura ni wangapi?
 
Makada/Wabunge wa Chadema wameshakubali kushindwa. Nasi tukubali matokeo. Tugange yajayo. Au mnataka waanze kuchoma ofisi za uchaguzi kama Kibondo?
 
This is strange! kama ni kweli magazeti yalitoa updates za jana usiku Mtanzania inasema CCM walikuwa wanaongoza kwa kura zaidi ya 30,000 na Chadema kura 21,000. Sina shida na kura za Chadema . lakini hizi za CCM iweje zipungue! vinginevyo ama magazeti hayasemi kweli au mwanajamvi hana updates!
 
- The simple truth ni Upinzani hawakuwapa wananchi wa Busanda sababu za kutoichagua CCM.

FMEs!
No sababu kutoichagua CCM, waliwapa na CCM ikatoa sababu za kuachiwa iendelee, Wanabusanda wakakubaliana na sababu za CCM, wakawapa ridhaa yao.
 
Kama Busanda ingeshinda Chadema ingelikuwa ni mara ya kwanza jimbo lolote la uchaguzi katika mkoa wa Mwanza kuangukia upande wa upinzani.Kama Watanzania wengi tulivyo na tunavyoamini CCM ndiyo baba na mama yetu.

Ni sehemu chache sana ambazo zinaweza zikachagua chama cha upinzani kwa hoja yoyote ile.CCM ni kama imani ya kidini inavyojengeka kwa muumini si rahisi kuiacha bila mbadala unaoridhisha.

Hakuna wa kulaumu kuhusu hali hii ila Mwalimu Nyerere.Alitutawala kifikra na kulifanya taifa kufuata sera za kijamaa zilizodumaza akili za watu.Alipokubali mfumo wa vyama vingi angejiondoa CCM na kuwa Baba wa Taifa wa kweli wa Tanzania,hali isingekuwa kama ilivyo sasa.Kasumba ya mwalimu haijaondoka na haitaondoka hivi karibuni.

Vyama vyetu vya upinzani vina sera nzuri na vina viongozi shupavu,lakini matatizo ya Watanzania ni makubwa mno kuliko tunavyoweza kudhani.Hatujaanza kuondokana na kasumba ya Nyerere na kwa ujumla umma wetu bado kabisa unaishi katika fikra za enzi za Mwalimu kukiwa na mabadilko kidogo sana.Tuna kazi kubwa sana ya kuubadili mfumo uliopo lakini akili zetu bado bado hazijakaa sawa.

Kuna mmoja wetu alilaumu kwamba Wasukuma wana matatizo ya kutoelewa na katoa mifano kadhaa lakini amejisahau kuwa si Wasukuma pekee.Ukiangalia idadi ya viti vya wabuge wa upinzani nchi nzima utaweza kung'amua kuwa akili za Watanzania hazijawa tayari.Tunahitaji mageuzi ya akili za watu kuziondoa kwenye upumbavu wa kulelewa na mawazo ya Mwalimu na kupigania katiba mpya,demokrasia ya kweli na haki za kiraia.Bado safari ni ndefu ndugu zangu.

Iwapo hamtaki kubadilka basi CCM itaendelea kutawala hadi mwisho wa karne.
 
...cant believe hawa taleban wameshinda Busanda,yaani na ufisadi wote huu wameshinda? mungu atusaidie tuu maana
 
Naamini demokrasia ya kweli Tanzania bado na tutaendelea kusubili sana mtu anatishiwa ukikipigia cha upinzani utakiona cha moto hapa kijijini.
Mnaunga mkono naona mnaridhika kabisa na utawala wa CCM lakini kesho msirudi tena hapa mkaanza kulalamika ooh wameweka nguzo umeme mpaka leo bado.
 
Yeah, lakini kipindi cha kutoka magazetini hakina update yoyote, kwani wanasoma magazeti haya haya ya leo yaliyokuwa na latest news za jana usiku. Tunataka update za sasa si tena kwa lengo la kujua nani kashinda, ila sasa kwa ajili ya analysis. Ikumbukwe mwaka 2005 CCM walipata asilimia 79, CHADEMA asilimia 4 na CUF asilimia 16. Sasa hapa tunasubiri asilimia za kura mwaka huu ili kuangalia trend inaendaje. Roughly inaonyesha CCM itakuwa imepata about 55% na CHADEMA 38% na the rest wamegawana CUF na UDP (nimesema roughly kutokana na matokeo ya awali). Hata hivyo tusubiri matokeo rasmi tuangalie trend.

Wananchi tusikate tamaa, kwa jimbo ambalo hawakuwahi kuwa na joto kali la upinzani kwa CCM, kupata asilimia 38, ni ushindi tosha. Message sent and delivered. Nasikia zimepelekwa nguzo za umeme kama sehemu ya kampeni. Zamani, baada ya ushindi huo ungekuwa ndiyo mwisho wa umeme kama ahadi za barabara zilivyo, lakini kwa upinzani huu lazima hizo ahadi zitekelezwe vinginevyo 2010 CCM watakuwa na kazi kubwa zaidi.
Tatizo lingine ni idadi ya waliopiga kura. Waliandikishwa 135,000 lakini hadi sasa inaonekana waliopiga kura ni zaidi kidogo ya 50,000. Hii ni karibu 40%. Kwa uchaguzi uliokuwa na joto kama hili turnout ingekuwa angalau 70%. Hapa nina wasiwasi na wapiga kura hewa hasa wakati wa uchaguzi mkuu. Inawezekana kwa chaguzi hizi ndogo, vituo hewa vinadhibitiwa kwani viongozi wana concentrate katika eneo dogo, tofauti na uchaguzi mkuu. Naomba chadema mfuatilie kituo hadi kituo kujua exactly idadi ya wasiopiga kura. Mnaweza kukuta kituo kizima hakikupiga kura, au katika baadhi ya vituo walijitokeza watu wengi sana laikini kwa kuwepo na wapiga kura hewa, bado hao wengi wanakuwa wachache kiasilimia.
 
Huyo mama inaonekana ni mwizi mwizi yeye kafuata nini huko wakati watoto wanakaa chini hawana madawati? hawana walimu wa kutosha kwenye mashule huyo ni mwizi tu hawezi kutu convice kuwa sio mmoja wa mafisadi wa wizi wa kura.
 
Wanajamvi, nimechemsha, natakiwa Busisi saa 7 safari saa 8 hivyo nimeondoka bila matokeo. Angalieni TBC watayarusha live
Samahanini sana, Asanteni.
 
Kwa mujibu wa Bwn Mollel, ambaye ni msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Busanda,akihojiwa na tbc leo saa moja asbh alisema matokeo yaliyokuwa yanasubiriwa ni ya kata moja inakuwaje hayajapatikana,au kuna umbali gani.ninawasiwasi kuna mapishi yanayoendelea huko.
 
Asante Mnozya, nimefurahishwa na tathmini yako. Uzuri wa hapa ni uhuru wa kutoa mawazo bila kuogopa. Vyama vya siasa vimatakiwa kujifunza hapa JF na kuiga kulioko kuwatisha wanachama/viongozi wanaotoa maoni yao.
 
CCM kama wanakithamini chama chao hali iliyojitokeza Busanda siyo ya kushangilia hata kidogo. Inaonyesha dhahiri kabisa ule MTAJI wa AMANI NA UTULIVU umeshaanza kupungua nguvu na kama hawatakuwa wabunifu na kusoma nyakati basi chama hiki kitapata wakati mgumu sana huko mbeleni wa kutetea uwepo wake. Kwa matokeo haya tusemeje, wananchi wameamka na kujua haki zao ndio maana wapinzani wamepata kura nyingi? Au ni kampeni za wapinzani na ahadi za kuwaletea maendeleo?

-Kama ni wananchi wameamka na kujua haki zao za msingi, basi tuhesabu ushindi maana rungu mwananchi alilotumia kuipunguzia CCM kura ni hilohilo litakalotumika kwa vyama vingine endapo havitakidhi matakwa yao kimaendeleo.

-Endapo watakuwa wamefanya hivyo kwa sababu tu ya chopa na ahadi tamu tamu za kufanyiwa mambo mazuri, basi safari ya maendeleo ya taifa la Tanzania bado ndefu maana aina hiyo hiyo ya AHADI ndiyo inayotumiwa na CCM ambayo sasa TUMEICHOKA!
 
Kama Busanda ingeshinda Chadema ingelikuwa ni mara ya kwanza jimbo lolote la uchaguzi katika mkoa wa Mwanza kuangukia upande wa upinzani.Kama Watanzania wengi tulivyo na tunavyoamini CCM ndiyo baba na mama yetu.

Ni sehemu chache sana ambazo zinaweza zikachagua chama cha upinzani kwa hoja yoyote ile.CCM ni kama imani ya kidini inavyojengeka kwa muumini si rahisi kuiacha bila mbadala unaoridhisha.

Hakuna wa kulaumu kuhusu hali hii ila Mwalimu Nyerere.Alitutawala kifikra na kulifanya taifa kufuata sera za kijamaa zilizodumaza akili za watu.Alipokubali mfumo wa vyama vingi angejiondoa CCM na kuwa Baba wa Taifa wa kweli wa Tanzania,hali isingekuwa kama ilivyo sasa.Kasumba ya mwalimu haijaondoka na haitaondoka hivi karibuni.

Vyama vyetu vya upinzani vina sera nzuri na vina viongozi shupavu,lakini matatizo ya Watanzania ni makubwa mno kuliko tunavyoweza kudhani.Hatujaanza kuondokana na kasumba ya Nyerere na kwa ujumla umma wetu bado kabisa unaishi katika fikra za enzi za Mwalimu kukiwa na mabadilko kidogo sana.Tuna kazi kubwa sana ya kuubadili mfumo uliopo lakini akili zetu bado bado hazijakaa sawa.

Kuna mmoja wetu alilaumu kwamba Wasukuma wana matatizo ya kutoelewa na katoa mifano kadhaa lakini amejisahau kuwa si Wasukuma pekee.Ukiangalia idadi ya viti vya wabuge wa upinzani nchi nzima utaweza kung'amua kuwa akili za Watanzania hazijawa tayari.Tunahitaji mageuzi ya akili za watu kuziondoa kwenye upumbavu wa kulelewa na mawazo ya Mwalimu na kupigania katiba mpya,demokrasia ya kweli na haki za kiraia.Bado safari ni ndefu ndugu zangu.

Iwapo hamtaki kubadilka basi CCM itaendelea kutawala hadi mwisho wa karne.
 
Turn up ya wapiga kura kuwa chini ya 50% ya waliojiandikisha ni dalili tosha kuwa huenda raia bado hawaelewi umuhimu wa kupiga kura, ama kuogopa vitisho, ama kwa kununuliwa ili wasifike vituoni. Itatuchukua muda kufikia democrasia ya kweli!
 
Matokeo ya uchaguzi huu yanadhihirisha kuwa ili upinzani uweze kushinda viti vingi zaidi vya ubunge, kazi ya ziada inahitajika. Si sahihi kudhani/kushutumu wananchi kwa kufanya uamuzi wao wa kidemokrasia katika kuamua nani awe mwakilishi wao. Wameamua kuipa CCM nafasi hiyo, na hiyo ni haki yao na ni sahihi kabisa. Ni sahihi pia kama wangeamua mgombea mwingine yeyote kuwa mwakilishi wao Bungeni. Wao ndio wanaojua wanachokitaka, na wamechagua wanachokitaka.

Wapinzani na hasa CHADEMA ni vyema wakafahamu kuwa, kura walizopata zimetokana na kazi nzuri waliyofanya Busanda. Wanabidi kufahamu kuwa 2010, kura hizo zinaweza kuongezeka ama kupungua, kutokana na jinsi watakavyoamua kuzilinda na/au kuziongeza.

Kwa mtazamo wangu, wapinzani wanatakiwa kufanya yafuatayo ili kujihakikishia ushindi katika chaguzi zifuatazo;

1. Wahakikishe wanakuwa na matawi mengi vijijini: Wananchi wa vijijini hawana kitu kinachoweza kuwafanya waamini kuwa wapinzani wanaweza kuwaletea mabadiliko wanayoyahitaji. Bila vyama vya upinzani kuwa na presence kubwa vijijini, chaguzi mbalimbali zitaendelea kuwashangaza.

2. Wahakikishe kuwa, sera zao zinalenga katika kujibu matatizo ya hali halisi ya wananchi wanaotarajia kuwaomba kura. Sera ziwekwe bayana, na ziwe zinazokubalika. Kubainisha mapungufu bila kutoa suluhu ya matatizo, haimaanishi kuwa matatizo hayo yatakwisha endapo wapinzani watachaguliwa. Inabidi kutoa utatuzi wa matatizo hayo na kubainisha jinsi ambavyo sera za CCM haziwezi kuyatatua bali wao pekee ndio wenye uwezo huo.

3. Wahakikishe kuwa mikakati ya ushindi ni endelevu. Wasiweke jitihada za ushindi wakati inapotokea nafasi ya uchaguzi tu. Inabidi hata kipindi ambacho hakuna uchaguzi, kuwe na tathmini zinazoweza kuwafanya wajue idadi ya kura wanazoweza kupata endapo uchaguzi utafanyika, na ubunifu wa mbinu za kuziongeza kura hizo (kata hadi kata). Tathmini hizo ziwe za ukweli na zinazoendelea kubadilika siku hadi siku, wiki hadi wiki, mwezi hadi mwezi na hata mwaka hadi mwaka.

4. Wajue mbinu zinazotumiwa na wapinzani wao. Waangalie nguvu za kila chama katika eneo husika, na watafute mbinu za kuweza kuzishinda nguvu za wapinzani wao kila mara. Wajue pia udhaifu wa wapinzani wao na kuutumia bila subira katika kujenga nguvu zao. Wakati huo huo, wanatakiwa wajue nguvu ya baadhi ya wananchi wenye kukubalika katika maeneo husika, na hao watumike kuongeza nguvu zao.

5. Kampeni ni njia ya kuomba kuchaguliwa au kujenga kukubalika kwa wananchi. Upinzani unatakiwa kujua jinsi ya kuongea na wananchi ili waweze kukubalika kwao. Mbinu za ubabe, matusi au kashfa haziwezi kusaidia kuongeza kukubalika kwa chama chochote. Wananchi huogopa na pia huchukizwa na vyama vinavyotumia nguvu nyingi, dharau na maneno yasiyoonyesha nidhamu katika kuomba kura.

CCM imeshinda Busanda, na CCM inaweza kushinda sehemu nyingine nyingi zaidi endapo upinzani utaendelea kutojifunza kutokana na matokeo katika majimbo kama haya (Busanda, Tarime). Kila uchaguzi ni lazima uzae somo kwa wanasiasa wanaokusudia kupata ushindi kwa vyama vyao.
 
Back
Top Bottom