Sinkala
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 1,773
- 688
Matokeo gani, ya darasa la saba au Form Four? 😀matokeo yametoka?
Matokeo gani, ya darasa la saba au Form Four? 😀matokeo yametoka?
Kwa hujui matokeo yanayosubiriwa?Matokeo gani, ya darasa la saba au Form Four? 😀
Issue sio wapinzani wapi tumewachagua, wala sina maana kuchagua upinzani ndio kuamka, ama kuichagua CCM ndio kulala usingizi.
Nimesema mimi pia naichagua CCM kwa sababu sijaona mbadala. Wapinzani hawachaguliwi kwa sababu hawajaonyesha wanaweza, nimehudhuria kampeni ya Chadema nikathibitisha wameonyesha wanaweza na wakasema wanaweza watu wa mijini wakawasikia wakawakubali wakawachagua. Watu wa vijijini, wamewasikia, au hawakuwaelewa, au hawakuwakubali wakawapiga chini. Kwa nilichosikia na kuona, ndipo nikakubali ndugu zangu bado wamelala.
Mimi ni pro-democracy siichukii CCM wala sishabikii Chadema, bali natamani tupate heathy opposition kama Democrat na Republican Us na Labor na Conservative UK.
Ili tupate demokrasia ya kweli ndani ya bunge.
Maadamu wapinzani wameanza kuonyesha wanaweza, wananchi wapatiwe civic education ya elimu ya demokrasia, waamke wachague vyama kwa sababu sio kwa mazoea.
2010 maeneo yenye literacy level ya hali ya juu na hali ya kiuchumi yenye ehueni, ushindi wa CCM sio walkover wapinzani watachance, sehemu zenye low literacy level na umasikini wa kutupa ni CCM tuu kwa sababu uelewa ni mdogo ndio maana nasisitiza elimu ya uamsho.
Msimamizi wa Uchaguzi ameamua kusitisha zoezi la majumuisho, amekwenda kuwaandikia barua nyingine CUF, UDP na Chadema, kuwatahadharisha zoezi litaanza bila uwepo wao.
CCM waliopo, wametaka zoezi la majumuisho lianze kwa utaratibu wa asiyekuwepo na lake halipo.
Wamesisitiza utumike utaratibu kama wa kwenye mechi za mpira, hata kama timu haijafika uwanjani, muda ikiwadia kipenga cha kuanza mechi kinapulizwa kikifuatiwa na vipenga vitatu vya kipenga cha mwisho, mpira umekwisha, aliyekuwepo ndiye mshindi.
Vyama vilivyoshindwa vinataka kutuletea mchezo wa kitoto kususia kuhesabu kura ili wasisaini fomu za matokeo ili wakimbilie mahakamani kutaka kubatilisha uchaguzi huu ambao kampeni zake zilitawaliwa na kila aina ya uvunjaji waa sheria ambazo ushahidi ukipelekwa mahakamani, uchaguzi unabatilishwa.
Ikumbukwe kuwa kipindi kilichobakia cha Bunge lililopo ni kifupi, hakuna chaguzi ndogo nyingine yoyote zaidi ya Biharamulo. Ni fainali tuu 2010.
Mlio karibu na kina Zitto, Mzee Invicible, mwambie rafiki yako aje kura zihesabiwe na wakubali matokeo. Nilijipanga kuondoka Busanda milango ya saa 5 ili niwahi feri ya saa 8 na kuishia zangu
Hiki kitendo cha hivi vyama kitapelekea matokeo kuchelewa na mimi nitaondoka bila kumalizia matokeo rasmi.
Ka-nzi ka Mwanakijiji kama unanisikia nakuomba uendeleze nitakapoishia ili JF tuendelee kutamba we arre the first to know.
Ile live ya TBC-1 kumbe siyo kwa ajili ya CCM, bali ni kutangazwa kwa live kwa matokeo. Hivyo kaeni mkao wa kula na TBC-1 Mkongwe aliyebobea na asiyeegemea upande wowote, Richard Leo atawavurumishia matokeo live from Geita.
Kweli kabisa hapa umeongea kisagarani. ndiyo maana walimchagua mnyika kuwa mbunge wao ubungo!
FMES, Wasukuma pamoja na umasikini wetu, we are not that cheap!. Sisi ni masikini jeuri, tuko tayari kufa njaa kuliko kuendekeza njaa. Naamini huyo mwananchi anauza uhuru wake kwa shibe ya siku moja sio Msukuma.
- Busanda sikujui lakini ninawaamini wananchi wa huko kwamba wanajua what is better kwao, nimewahi ksuema hivi hapa JF, kwamba niliwahi kukutana na mwamanchi mmoja aliyeniambia hivi yeye ana njaa kijijini mgombea ubunge anakuja na kumpa kilo tano za mchele, akasema eti ataacha kumpigia kura kwa sababu ya maneno ya huku JF no way,
- Busanda CCM wameshinda kwa sababu wananchi wameamini zaidi kuliko wengine wote, sasa labda uwasaidie mawazo Chadema, lakini sio kuwatukana wananchi wa Busanda, hata mikoa ya Kaskazini yote ni CCM tu hamna lolote, viongozi wote wa upinzani ni CCM tu.
Respect.
FMES!
FMES, Wasukuma pamoja na umasikini wetu, we are not that cheap!. Sisi ni masikini jeuri, tuko tayari kufa njaa kuliko kuendekeza njaa. Naamini huyo mwananchi anauza uhuru wake kwa shibe ya siku moja sio Msukuma.
Ni kweli CCM imeshinda kwa sababu wananchi wamewaamini. Kwa upande wangu siwatukani lakini ignorance ya ndugu zangu inachangia, Wasukuma sio watu wa makuu, tangu enzi za almasi walichezea bao na wazungu wakawapa gololi kubadili kwa Almasi.
Geita is filthy rich ana wananchi wanaogelea kwenye stinking poverty. Hivi kweli hiki ndio wanachokitaka Wanabusanda, no, hawajua watakacho, hawajui utajiri wao, demokrasia kwao siyo issue, wanachohitaji ni kuelimishwa elimu ya uraia, kueleweshwa wao wana nini, na kuamka usingizini kudai haki zao.
Nimekaa Dodoma vijijin enzi hizo, its the same scanerio na Busanda, hakuna maji, hakuna umeme, hakuna chochote simply nothing. Kuoga ni luxury. Siwashangai Kinamatonya wakiwa ombaomba kwa sababu some of them hawana altenative. In Dodoma there is nothing sio Geita, why watu wawe masikini kama watu wa Dodoma ama Singida?.
Please dont take it personal its just a scanerio.
CCM itachaguliwa Milele, Kidumu Chama Cha Mapinduzi!.
Mkuu Pasco,kabla hujaondoka uwanjani hebu tufafanulie katika hiyo redMsimamizi wa Uchaguzi ameamua kusitisha zoezi la majumuisho, amekwenda kuwaandikia barua nyingine CUF, UDP na Chadema, kuwatahadharisha zoezi litaanza bila uwepo wao.
CCM waliopo, wametaka zoezi la majumuisho lianze kwa utaratibu wa asiyekuwepo na lake halipo.
Wamesisitiza utumike utaratibu kama wa kwenye mechi za mpira, hata kama timu haijafika uwanjani, muda ikiwadia kipenga cha kuanza mechi kinapulizwa kikifuatiwa na vipenga vitatu vya kipenga cha mwisho, mpira umekwisha, aliyekuwepo ndiye mshindi.
Vyama vilivyoshindwa vinataka kutuletea mchezo wa kitoto kususia kuhesabu kura ili wasisaini fomu za matokeo ili wakimbilie mahakamani kutaka kubatilisha uchaguzi huu ambao kampeni zake zilitawaliwa na kila aina ya uvunjaji waa sheria ambazo ushahidi ukipelekwa mahakamani, uchaguzi unabatilishwa.
Ikumbukwe kuwa kipindi kilichobakia cha Bunge lililopo ni kifupi, hakuna chaguzi ndogo nyingine yoyote zaidi ya Biharamulo. Ni fainali tuu 2010.
Mlio karibu na kina Zitto, Mzee Invicible, mwambie rafiki yako aje kura zihesabiwe na wakubali matokeo. Nilijipanga kuondoka Busanda milango ya saa 5 ili niwahi feri ya saa 8 na kuishia zangu
Hiki kitendo cha hivi vyama kitapelekea matokeo kuchelewa na mimi nitaondoka bila kumalizia matokeo rasmi.
Ka-nzi ka Mwanakijiji kama unanisikia nakuomba uendeleze nitakapoishia ili JF tuendelee kutamba we arre the first to know.
Ile live ya TBC-1 kumbe siyo kwa ajili ya CCM, bali ni kutangazwa kwa live kwa matokeo. Hivyo kaeni mkao wa kula na TBC-1 Mkongwe aliyebobea na asiyeegemea upande wowote, Richard Leo atawavurumishia matokeo live from Geita.
Yeah, lakini kipindi cha kutoka magazetini hakina update yoyote, kwani wanasoma magazeti haya haya ya leo yaliyokuwa na latest news za jana usiku. Tunataka update za sasa si tena kwa lengo la kujua nani kashinda, ila sasa kwa ajili ya analysis. Ikumbukwe mwaka 2005 CCM walipata asilimia 79, CHADEMA asilimia 4 na CUF asilimia 16. Sasa hapa tunasubiri asilimia za kura mwaka huu ili kuangalia trend inaendaje. Roughly inaonyesha CCM itakuwa imepata about 55% na CHADEMA 38% na the rest wamegawana CUF na UDP (nimesema roughly kutokana na matokeo ya awali). Hata hivyo tusubiri matokeo rasmi tuangalie trend.nimesikia kupitia kipindi cha toka magazetini kuwa CCM wako mbele kwa kula 9000, na vimebaki vituo vitatu tu, tena vya vijijini! ni wazi ccm wameibuka kidedea tena!!
Matokea ya uchaguzi jimbo la Busanda