CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

Jinga sana wewe, Sijawahi kula hata senti tano ya CCM, ila nasukumwa na mapenzi binafsi kwa chama pamoja na ukweli kuwa CCM ndio chama makini kuliko vyote TANZANIA, licha ya mapungufu madogo madogo yanayojitokeza hapa na pale! Ila CCM haina Mbadala kwa sasa, Wengine ni wasaga sumu tu!

unamsifia nini sasa? mtu mwenyewe hata ukimuita kwenye mdahalo na january makamba anamtoa jasho hadi la unyayo
 
Kamati kuu ya CCM inayotarajiwa kukutana leo jioni jijini Dar es Salaam itatoa ujumbe mzito kwa wasaka urais wa CCM.

Rais Kikwete anayetarajiwa kuongoza kikao hicho, mbali na teuzi mbalimbali zitakazofanyika, pia Kikwete ameonyesha kukerwa na baadhi ya mwenendo ya wasaka urais wa CCM wakiwemo January Makamba, Edward Lowassa na Benard Membe ambapo anatarajiwa kutoa ujumbe mzito kwao.

Kiwete ameonyesha kustushwa na mwenendo wao wa kupiga kampeni waziwazi huku akisema kuwa "kamati kuu haitothubutu kuwapitisha wafanya mazingaombwe"

Kikwete haogopwi na mtu yoyote CCM..anashtuka nini wakati yeye mwenyewe aliingia kwa mtindo huo huo..anapanic kwa sababu tutusa lake membe limejichanganya linakeaha mwitongo kupiga magoti kwenye kaburi la nyerere kuomba mizimu
 
Cheki miCHADEMA inavyopenda kushadadia vita, hivi vita ni sera yenu? Maana Dr. Slaa aliposhindwa urais na JK mwaka 2010 alisema nchi haitatawalika lakini mwisho wa siku ameaibika kwani nchi inatawalika ipasavyo. Shame on you!

Hivi unajinadi kabisa nchi inatawalika..... una matatizo si bure!
 
yeriko nyerere katika kiwango chake cha uongo,hongera majibu mtayapata october ndanganyaneni sana hapo ufipa ccm kwa sasa wapo kwenye pre campani wakisharuhusiwa kuanza campani yenyewe watakua walishamaliza game
 
..."Urais Tanzania, kuanzia 25/10/2015, iwe mchana au usiku, iwe kiangazi au masika, iwe mawingu au jua kali, Dr Slaa chini ya UKAWA ndie rais wa wote....
UPDATES:
Yericko, hata kama CHADEMA inawaundermine members wengine wote wa UKAWA, huna haja ya kuandika kitu kama hiki hali ukijua wazi hakuna kikao chochote cha UKAWA kilichokaa na kubariki jina la Dr. Slaa. Ni mambo kama haya yanayoleta sintofahamu ndani ya UKAWA.
 
unamsifia nini sasa? mtu mwenyewe hata ukimuita kwenye mdahalo na january makamba anamtoa jasho hadi la unyayo
Kwahiyo kwa upeo wako, mtu yeyote anayeshiriki midahalo anafaa kukuongoza wewe na wenzio katika Urais?
 
hakuna kitu nachotamani kama hiki

lowasa akatwe na kamati kuu


baada ya kukatwa ahame ccm na wapambe wake woote


akishahama ccm kiparanganyike


kuanzia hapo tusiwe na chama tawala kibabe tena kama ca ccm

kuanzia hapo chama chochote cha upinzani kichukue nchi na kuanzia hapo tuwe tunabadilisha chama kinachotawala kama kenya

kila chama kikiingia madarakani kiwe macho kwani muda wowote kinaweza pigwa chini.


natamani ccm itoke madarakani

mkuu watanzania wote wapenda demokrasia wanaomba mungu yatokee hayo..
 
Jirani na mzee wetu wa awamu nne tengeneza historia na kudumisha heshima yako kwa maamuzi sahihi na yatakayoikomboa Tanzania mikononi mwa wanyanganyi. Amen

Adumishe heshima gan wakati kula yake ni moja tu kaka?,Edo ni kimbunga aisee!
 
Naelewa sana kuwa alikuwa sehemu ya serikali iliyoshindwa na hata ya nyuma yake.Labda wewe na ukada wako ndio huelewi kuwa tatizo la nchi hii ni mfumo wa uongozi wa serikali na chama chako kinachoongoza. Nae alikuwa waziri mkuu tu tena awamu hii ya nne angeweza kushauri na sio kubadilisha lolote.Sasa anakuja kama kiongozi wa nchi na atafutilia mbali mfumo huu unaokumbatia wezi na kutoa maamuzi kwa wakati muafaka.Nadhani nimekuongezea uelewa fulani tofauti na unavyonifikiria kuwa mimi ni -----.

ww kweli hamnazo atawezaje kuwafuatilia mbali wezi wakati yy ni sehemu yao???
RA,Karamagi,Chenge na wengine wengi hivi atawezaje kuwatokomezea mbali watu ambao ndio behind the scene Directors wa kila anachofanya
Karamagi huyuhuyu aliesaini mkataba wa kuiza Buzwagi akiwa hotelini leo hii anatuchagulia Rais na Mbulula kama ww unashangilia???
 
kikwete ukiondoa hayo majambazi ccm tutakukumbuka daima maana baada ya nyerere wewe urakuwa mwenyikiti wa pili kwa heshima,mungu akusaidie
 
1,kikwete
2, comred mangula
3, nape
tusaidie kuwaondoa wanaotumia kichaka cha ccm kutafua uongozi kumbe sio wanacm haiwezekani mtu anajifanya ni mwamba zaidi ya taasisi,hata ndani ya familia mtoto akijifanya anaakili kuriko baba unafukuza, ukimuacha basi wewe baba unamapungufu
 
Waziri Mkuu ndio kiongozi mkuu wa serikali, Raisi mbwembwe tu.., mambo yote ya kiutendaji siku hadi siku yanaishia kwa PM, Raisi ana-deal na mambo ya kisera tu. Sasa kama PM kaboronga, kashindwa kushauri, hawezi kuja kudai kuwa ana kipya. Kwani hana ushawishi, na hawezi kuongoza, kama unashindwa kumshawishi mtu mmoja awe na sera sahihi, unaweza vipi shauri mamilioni kufuata sera zako?

Kama alishindwa kama Mtendaji mkuu wa serikali kufanya hizi porojo anazodai sasa hivi sidhani kama ana kipya.

Kwako kubadilisha mfumo wa kuongoza serikali au chama sio mambo ya sera na madaraka yako kwa raisi kama ulivyokiri mwenyewe? Mtendaji mkuu wa serikali anatenda kwa maagizo ya aliye juu yake ambae ni raisi. Hivyo hivyo kwa mtendaji mkuu wa kampuni au shirika anaongoza kwa maagizo ya bodi na anawajibikwa kwao.Kama nitakuwa sahihi waziri mkuu wa sasa alishindwa kumwajibisha hata kumsimamisha tu kazi waziri alietakiwa kuwajibishwa na bunge. Nini kilitokea wote tunakumbuka waziri mkuu aliliahidi bunge kuwa ataongea na raisi aliekuwa ziarani A. kusini na kusikitika kwa kutokuwa na madaraka hayo. Pia wengi watakumbuka Lowassa akiwa wazri mkuu baada ya kugundua mapungufu ya richmond na kuwa hawawezi kuliletea taifa umeme alimpigia simu raisi akiwa nje ya nchi na kumweleza dhamira yake kuufuta mkataba wa serikali na richmond baada ya kubaini hawana utaalam, mtaji na hata ofisi nchini. Alieleza Lowassa mwenyewe kwenye kikao cha chama cha kamati kuu kuwa alijibiwa awaache hadi arudi nchini na aliporudi hakufanya maamuzi yoyote. Hiyo yote inaonyesha pamoja na utendaji wa shufhuli zote za serikali waziri mkuu hana nguvu ya kubadilisha lolote bali aliemteua. Nadhani sasa umeelewa vya kutosha na hutaniquote tena kwa jambo hili hili.
 
Mimi ni chadem lakini Slaa sio presidential material kabisa mara mia asimamishwe makaidi au Dovutwa

hahaha naona unamgogoro na nafs yako...moyon unakir kwenye mwandiko unajisahaulisha....dr.slaa ndio habar ya mjin mkuu taka usitake
 
Sasa anakuja kama kiongozi wa nchi na atafutilia mbali mfumo huu unaokumbatia wezi na kutoa maamuzi kwa wakati muafaka..

Bila shaka u kipofu, yaan timu ya Lowassa,Chenge,Karamagi, na Rostam iende kupambana na wizi?mambo mengine mtumiage na akili.


Uchaguzi upo mbele yako, pindi hao watu wakichukua serikali basi gesi yetu imeenda.Itakula kwetu mazima na wajukuu wetu watalia kwa upumbavu wetu..

Ni mtu mpumbavu tu ndiye atakayeweza kuipa timu ya wezi eti ikalinde na kusimamia pesa na rasilimali zetu.
 
Kwako kubadilisha mfumo wa kuongoza serikali au chama sio mambo ya sera na madaraka yako kwa raisi kama ulivyokiri mwenyewe? Mtendaji mkuu wa serikali anatenda kwa maagizo ya aliye juu yake ambae ni raisi. Hivyo hivyo kwa mtendaji mkuu wa kampuni au shirika anaongoza kwa maagizo ya bodi na anawajibikwa kwao.Kama nitakuwa sahihi waziri mkuu wa sasa alishindwa kumwajibisha hata kumsimamisha tu kazi waziri alietakiwa kuwajibishwa na bunge. Nini kilitokea wote tunakumbuka waziri mkuu aliliahidi bunge kuwa ataongea na raisi aliekuwa ziarani A. kusini na kusikitika kwa kutokuwa na madaraka hayo. Pia wengi watakumbuka Lowassa akiwa wazri mkuu baada ya kugundua mapungufu ya richmond na kuwa hawawezi kuliletea taifa umeme alimpigia simu raisi akiwa nje ya nchi na kumweleza dhamira yake kuufuta mkataba wa serikali na richmond baada ya kubaini hawana utaalam, mtaji na hata ofisi nchini. Alieleza Lowassa mwenyewe kwenye kikao cha chama cha kamati kuu kuwa alijibiwa awaache hadi arudi nchini na aliporudi hakufanya maamuzi yoyote. Hiyo yote inaonyesha pamoja na utendaji wa shufhuli zote za serikali waziri mkuu hana nguvu ya kubadilisha lolote bali aliemteua. Nadhani sasa umeelewa vya kutosha na hutaniquote tena kwa jambo hili hili.


Ndugu punguza kutetea watu wasioteteeka, utaonekana hamnazo.

Hayo ya richmond, yalishajadiliwa humu kwa mapana na marefu mwaka 2007, bahati mbaya kwako wengine tulikuwepo humu na tunakumbuka kila kilichotokea.

Huyo rafiki yako Lowassa, kupitia wapiga dili wenzake ndio walituletea kampuni hewa, isiyokuwa hata na ofisi, iliyokuwa inalipwa milioni 150 kwa SIKU,bila kutengeneza umeme wowote, haikuwa hata na mtambo mmoja.Msabaha alipewa amri ya kubadilisha taratibu za manunuzi na rafiki yako Lowassa, na huyo jamaa yako unayemtetea, kwa miaka aliona kinachoendelea, kajiuzulu baada ya tumwe kuundwa na yeye kupatikana na hatia, JK kama kawaida yake alimpa simple altimatum, jiuzulu au nikufukuze.

Kujaribu kutuaminisha kuwa yeye ndio alianzisha uchunguzi ni vichekesho vya mwaka, Richmondi ilifukuliwa na wapinzani walioshinikiza Serikali iunde TUME. msifanye watu wasahaulifu.

Lowassa ni kati ya viongozi wala rushwa maarufu kuliko wote Tanzania, hiyo sio siri, kujaribu kumsafisha huyu ni sawa na kujaribu kuipeleka Taifa Stars kombe la dunia. inabidi ujiandae kweli kweli, na probability ya kufeli ni 0.999
 
Back
Top Bottom