CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

CCM yaitisha Kamati Kuu kwa dharura

jaman ccm mtatutoa roho watanzania mbona ving'ang'anizi hivyo jaman miaka 53 bado mna hamu ya kuliongoza tena Taifa la tanzania mmmh labda mturudishie aliye kuwa Gavana wa benk kuu ndugu Daudi balali ndipo tutawapa madarakani
 
....

"Urais Tanzania, kuanzia 25/10/2015, iwe mchana au usiku, iwe kiangazi au masika, iwe mawingu au jua kali, Dr Slaa chini ya UKAWA ndie rais wa wote, wema na wabaya".

OVER !!
 
Ikitokea Padre,Dr Slaa kawa Rais wa Tz nitakuwa wa kwanza kuhama Tanzania.

Mandla.
 
Kamati kuu ya ccm baada ya sintofahamu ya siku mbili, imebadili ghafla eneo la kufanyia mkutano wao kutoka Dodoma na kwenda Ikulu Dar,

Hali hiyo inafuatia taarifa za intelijensia kuwa Lowasa na Timu yake tayari wameweka kambi Dodoma wakijiandaa kwa maandamano na kuvamia ukumbi kama shinikizo la kuzuia jina la mlalaheri Lowasa kwa pepo ya mabwege lisikatwe.

Kwahatua hii tegemea maamuzi mazito au ya kipuuzi leo, Wajumbe wamegeuza tayari Kuja dar na kikao kitafanyika Leo usiku ikulu dar.

Timu Lowasa mnaarifiwa kuwa nendeni mkaandamanie Ikulu ya magogoni ili muone hasira ya kibanga wa ubara.


"Urais Tanzania, kuanzia 25/10/2015, iwe mchana au usiku, iwe kiangazi au masika, iwe mawingu au jua kali, Dr Slaa chini ya UKAWA ndie rais wa wote, wema na wabaya".
bado tunasubiri mchakato wa UKAWA Dr.Slaa umeamua mwenyewe chumbani?
 
Kila la kheri JK ktk kuwatafutia watanzania kiongozi bora

Yap inataiwa afumbe macho aweke ushkaji pembeni afanye maamuzi kwa maslah ya taifa na si kumfurahisha mtu au kulipa fadhira
 
Hakatwi mtu maan yake nini, wote 40, watakwenda IKULU? Na Lowassa wenu mmechanganyikiwa

Kati ya hao 40 wenye nia ya kweli ni wawili tu wengine mmewaweka Kama magalasa ya kusema mbona flani kakatwa hajalalamika.

Lowassa ni mmoja ya walioingia gentlemen agreement na vasco da gama mwaka 1995/2005.
 
Sijui kama M/Kiti wangu huyu anajua nafasi yake ka m/kiti ilivyo. Mwl. Alikuwa anatoa tamko zito kwanza ndo kikao. Hilo tamko atakalolitoa litatokea wapi? Kama wauza unga liowajua majina na namba zao 2005 alipoingia madarakani, leo ni more than 8 yrs anasherehekea sikukuu ya wauza unga duniani na kuwahakikishia kuwa hawatakaa wauawe Tz bali waendelee kusherehekea sikukuu yao kwani watafungwa tuu. Hilo ndo tamko zito??
Msiogope, kama ni kweli tungetamani amseme huyo mwali wa ccm ni nani sio bla bla. Jambo likiwa siri saana hata likifunuliwa halina ladha tena. Atamke leo kuwa Maccm yatampata wapi huyo mgombea safi asiyesafishwa na dodoki. Ila kwenye orodha hatuja mwona mtu huyo mtia nia bali tumewaona wavunja nia tuu
 
Kamati kuu ya CCM inayotarajiwa kukutana leo jioni jijini Dar es Salaam itatoa ujumbe mzito kwa wasaka urais wa CCM.

Rais Kikwete anayetarajiwa kuongoza kikao hicho, mbali na teuzi mbalimbali zitakazofanyika, pia Kikwete ameonyesha kukerwa na baadhi ya mwenendo ya wasaka urais wa CCM wakiwemo January Makamba, Edward Lowassa na Benard Membe ambapo anatarajiwa kutoa ujumbe mzito kwao.

Kiwete ameonyesha kustushwa na mwenendo wao wa kupiga kampeni waziwazi huku akisema kuwa "kamati kuu haitothubutu kuwapitisha wafanya mazingaombwe"
asitudanganya wakati anajua kuhusu richmond,epa,escrow,naye ni fisadi tu
 
Back
Top Bottom