Kuanzia ale Yeriko alipojiunga na dini ya kipuuzi hakika nimemdharau sana
Dini ya kipuuzi ndo dini gani mkuu??
Kuanzia ale Yeriko alipojiunga na dini ya kipuuzi hakika nimemdharau sana
Kwako kubadilisha mfumo wa kuongoza serikali au chama sio mambo ya sera na madaraka yako kwa raisi kama ulivyokiri mwenyewe? Mtendaji mkuu wa serikali anatenda kwa maagizo ya aliye juu yake ambae ni raisi. Hivyo hivyo kwa mtendaji mkuu wa kampuni au shirika anaongoza kwa maagizo ya bodi na anawajibikwa kwao.Kama nitakuwa sahihi waziri mkuu wa sasa alishindwa kumwajibisha hata kumsimamisha tu kazi waziri alietakiwa kuwajibishwa na bunge. Nini kilitokea wote tunakumbuka waziri mkuu aliliahidi bunge kuwa ataongea na raisi aliekuwa ziarani A. kusini na kusikitika kwa kutokuwa na madaraka hayo. Pia wengi watakumbuka Lowassa akiwa wazri mkuu baada ya kugundua mapungufu ya richmond na kuwa hawawezi kuliletea taifa umeme alimpigia simu raisi akiwa nje ya nchi na kumweleza dhamira yake kuufuta mkataba wa serikali na richmond baada ya kubaini hawana utaalam, mtaji na hata ofisi nchini. Alieleza Lowassa mwenyewe kwenye kikao cha chama cha kamati kuu kuwa alijibiwa awaache hadi arudi nchini na aliporudi hakufanya maamuzi yoyote. Hiyo yote inaonyesha pamoja na utendaji wa shufhuli zote za serikali waziri mkuu hana nguvu ya kubadilisha lolote bali aliemteua. Nadhani sasa umeelewa vya kutosha na hutaniquote tena kwa jambo hili hili.
Na Saed Kubenea MAWAZIRI watatu katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wanatarajiwa kujiuzulu wakati wowote kutokana na kashfa ya mkataba wa Richmond, MwanaHALISI limedokezwa. Taarifa za kuaminika kutoka serikalini na ndani ya Bunge zinasema mawaziri hao watatu wanatajiuzulu katika kipindi cha mkutano huu wa Bunge. Tayari mmoja wa mawaziri anapitapita miongoni mwa wabunge mjini Dodoma akilalama kuwa ameponzwa na Waziri Mkuu Edward Lowassa. Haijafahamika ni kwa msingi gani. Ndiyo wapo mawaziri watakaojiuzulu wakati wowote kuanzia sasa. Sifahamu ni lini, lakini ni katika mkutano huu wa Bunge, kimeeleza chanzo cha habari cha gazeti hili. Chanzo hicho kimesema, Inawezekana wakajiuzulu kabla ya ripoti ya Dk. Mwakyembe (Dk. Harisson Mwakyembe), kuwasilishwa bungeni, au baada ya kuwasilishwa na kujadiliwa. Lakini uhakika ni kwamba watajiuzulu. Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu mkataba katiya serikali na kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond, inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano wa sasa wa bunge. Taarifa zinasema kujiuzulu kwa mawaziri hao kunafuatia shinikizo kubwa lililotokea ndani ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Imeelezwa kuwa baadhi ya wajumbe wa CC, walikuja juu, wakitaja majina na kushinikiza kwamba wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi unaohusu Richmond waachie ofisi za umma na bila mjadala. Imefahamika kwamba wajumbe waliokuwa wakishinikiza waliongozwa na Abdulrahaman Kinana na makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela. Taarifa zinasema walishinikiza kwamba rais Kikwete awaondoe mawaziri wake iwapo hawatakubali kujiuzulu kwa hiari. Mjadala ulikuwa mkali. Rais alikubaliana na hoja za wajumbe. Alisema kila anayetuhumiwa ni vema akaondoka, kabla hajaondolewa, alisema mjumbe mmoja wa CC, akimnukuu Kikwete. Mawaziri wawili wanaotajwa kuwa na uwezekano wa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mtangulizi wake katika wizara hiyohiyo, Dk. Ibrahim Msabaha. MwanaHALISI halikuweza kupata mara moja jina la waziri wa tatu anayetakiwa kujiuzulu. Dk. Msabaha ambaye sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki, anasulubiwa kutokana na mkataba huo kusainiwa wakati wa utawala wake. Dk. Msabaha aliondolewa katika wizara hiyo Oktoba 2006 katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri. Karamagi amebanwa ajiuzulu kutokana na tuhuma kwamba aliongeza mkataba wa kampuni ya Dowans, bila kumshirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini. Dowans ndiyo iliyonunua mkataba wa Richmond ambapo kama ilivyokuwa kwa dada yake (Richmond), ilishindwa kukamilisha kazi kwa wakati. Wakati mawaziri wanajiandaa kujiuzulu kwa shinikizo, mmoja wa wabunge wa zamani katika CCM anasema kunaweza kuibuka mgogoro mkubwa iwapo mawaziri hao watakataa kushinikizwa na kutaka waondoke na waliokuwa wakiwatuma. MwanaHALISI inazo taarifa kwamba kuna malalamiko mengi miongoni mwa watuhumiwa ambao wanadai kuwa walikuwa wakipokea amri kutoka juu katika kutekeleza mkataba wa serikali na Richmond. Iwapo watakuwa jasiri na kumtaja huyo aliyeko juu na ambaye alikuwa akiwaamuru au kuwaelekeza, basi watakuwa wamepona na yeye atalazimika kujiuzulu kwa aibu kubwa, kimeeleza chanzo cha gazeti hili. Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkataba kati ya serikali na Richmond ulisainiwa bila kufuata taratibu, ikiwamo kutofikishwa katika kikao cha makatibu wakuu (AMTC). Kikao hicho kinachokuwa chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, ndicho chenye jukumu la kujadili jambo lolote ambalo litatakiwa kufikishwa katika Baraza la Mawaziri. Kutokana na hali hiyo, mkataba wa Richmond haukifikishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri, ambacho mwenyekiti wake ni rais wa Jamhuri. Vyanzo vyetu vya habari vinasema, mkataba kati ya serikali na Richmond ulijadiliwa na Dk. Msabaha kama waziri mwenye dhamana ya umeme, Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na Waziri Mkuu Lowassa. Mkataba haukufikishwa katika kamati ya makatibu wakuu. Wala haukufikishwa katika Baraza la Mawaziri, waziri mmoja mwandamizi ndani ya serikali aliliambia MwanaHALISI. Alisema, Wakati mkataba unasainiwa, rais Jakaya Kikwete alikuwa ziarani Marekani. Aliporudi nchini akakuta tayari kila kitu kimevurugika. Ndipo alipoamua kufuatilia ili kujua ukweli wa suala hili. Bunge katika kikao chake kilichopita, liliunda Kamati teule kuchunguza mkataba kati ya serikali na kampuni Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na mbunge wa Kyera (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe. Taarifa za ndani ya kamati zinasema, pamoja na mambo mengine, Kamati imeridhika kwamba Richmond haikuwa kampuni yenye hadhi, uwezo, wala heshima ya kupewa kazi iliyoomba. Inaelezwa kwamba, Kamati ya Bunge, imeridhika kwamba Richmond nchini Marekani, ni kampuni inayojishughulisha na vifaa vya ofisini, wakati nchini Tanzania inajishughulisha na utoaji huduma za intaneti. Mjadala wa Richmond tayari umepamba moto kila pembe ya nchi, huku wabunge wakingangana kutaka kuwatoa macho wote wanaohusika. Kama mjadala utakuwa umekwenda kwa usawa, hakuna mwenye uhakika wa kubaki. Hata Lowassa, anaweza kungoka, alisema mbunge mmoja wa CCM. Katika hali inayoashiria kwamba mambo yameiva, mwishoni mwa wiki iliyopita, wabunge waligomea semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu muswada wa Sheria ya Umeme na Biashara ya Mafuta ya Petroli. Kwa kauli moja wabunge walishinikiza kwanza waletewe ripoti ya Richmond ili waijadili kabla ya kupitisha mswada huo. Aidha, wabunge walisikika wakisema kwamba hawana imani na uongozi wa wizara hiyo na Tanesco kwa vile vimejaa uchafu, na kwamba hawawezi kujadili mambo mengine hadi wahusika wajisafishe. Zile za jana (Jumapili iliyopita) zilikuwa salamu za rasharasha. Kazi kamili inakuja wakati wa kuwasilisha hoja. Safari hii hatutaki tena kutumiwa kama mihuri, alisema mbunge mwingine wa CCM, ambaye alitaka jina lake lisitajwe gazetini. Kujiuzulu kwa mawaziri kutapunguza shinikizo la wanachama wa CCM kwa viongozi wakuu wa chama hicho, hasa rais Kikwete ambaye amekuwa akituhumiwa kulinda mawaziri wake walioboronga. Naye mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akizungumzia mvutano kati ya wabunge wa CCM na mawaziri wao, alisema kwamba kama Karamagi anasoma nyakati alipaswa kujiuzulu mapema. Kama kujiuzulu, alitakiwa ajiuzulu tangu siku ya semina. Sura za wabunge zilionyesha wazi kuwa hawamtaki, alisema Dk. Slaa.
Kabla sijasahau, soma summary ya kilichotokea RICHMONDI, tazama list ya watuhumiwa(Karamagi), halafu tazama list ya wapambe wa Lowassa(kuna Karamagi). Kama hujajiona bw*ge basi una matatizo ya akili.
MKATAMBUGA: Sakata la Richmond: LOWASSA KITANZINI
Kwa bidii mnazo na wengine wote wanaonishambulia eti namuunga mkono Lowassa na pia nawashabikia mafisadi.Hakuna popote nilipofanya hivyo zaidi ya kuwaeleza madaraka aliyo nayo waziri mkuu na kwamba wote hamuelewi kuwa yote haya yanasababishwa na mfumo unaoiongoza serikali na chama kinachoiongoza. Hivi kuna mtia nia yeyote anaewania uraisi aliekuwepo serikalini na hata waliopo ambae hajatoa ahadi kwa wananchi kuwa akichaguliwa ataboresha uchumi wa nchi na hata wa raia mmoja mmoja. Kwamba atarudisha viwanda na hata kutoa elimu ya bure kwa wanafunzi na kupunguza deni la taifa. Hivi mnafikiri atayatekelezaje haya chini ya mfumo uliopo kwenye chama chake.Kwamba wote hao walikuwepo serikalini na hawakuweza kubadilisha lolote maswali kama hayo angeulizwa raisi ambae amewahi kuongoza nchi hii na kurudi tena kuwania nafasi hiyo. Nani asiejua mamlaka aliyo nayo waziri serikalini.Anaweza tu kushauri ila hana uwezo wa kubadili mfumo zaidi ya raisi aliepo madarakani na wakati huo huo akiwa m/kiti wa chama wa taifa.Ni nani anaejua kama wanashauri lakini hawasikilizwi?. Ni kwamba wanaelewa kwa nafasi ya uraisi inawezekana kubadilisha mfumo huu unaokumbatia ufisadi wa hela za serikali na rasilimali zetu kiasi wanashindwa hata kuwawajibisha na kuishia kuwaambia wengine walipe wanachodaiwa na hawatafikishwa mbele ya sheria.Kwamba ukiwakamata taifa litaingia kwenye matatizo. Yote haya yanatendeka kutokana na mfumo m-baya baada ya kuua azimio la Arusha. Watalirudisha na ndio maana ya ahadi hizi wanazotoa. Sasa kama hampendi hivyo wapeni ukawa kura waongoze taifa hili.
Kufanyia mikutano ya CCM ndani ya Ikulu ni sahihi? Nadhani tuna sheria inayozuia watumishi wa umma kusijihusisha na mambo ya vyama. Itakuwaje kwa watumishi wa Ikulu watakaokuwa wanahudumia mkutano huo?
Kufanyia mikutano ya CCM ndani ya Ikulu ni sahihi? Nadhani tuna sheria inayozuia watumishi wa umma kusijihusisha na mambo ya vyama. Itakuwaje kwa watumishi wa Ikulu watakaokuwa wanahudumia mkutano huo?
Kufanyia mikutano ya CCM ndani ya Ikulu ni sahihi? Nadhani tuna sheria inayozuia watumishi wa umma kusijihusisha na mambo ya vyama. Itakuwaje kwa watumishi wa Ikulu watakaokuwa wanahudumia mkutano huo?
Yaani kuna mijitu ikishapewa tu pesa inajitoa ufahamu kabisaaaa!! iko tayari kufanya lolote ilimradi kumfurahisha fisadi wao
Tatizo lako hujui wapi pa kusimamia. Mkataba wa Richmond yeye ndie aliyeujadili na washakaji zake wakina Karamagi, leo hii unajifanya hana madaraka?Mifano yako ya pinda ni kwa presidential appointees, haina uhusiano na ukuu wa serikali alionao pinda. PM ndio bosi wa shughuli zote za serikali bungeni, yeye ndie alfa na ulela wa makosa yoote ya serikali kwenye utendaji.
Ndugu yako nasikia leo karopoka miezi 6 inatosha kumaliza foleni Dar, amesahau kuwa alikuwa PM kwa miaka 2!!and the best he came up with ni kuifanya alihassan mwinyi road kuwa na ratiba za ajabu ajabu jioni na asubuhi kwa kuongeza nusu lane upande mmoja.
Mie sijawahi kumtetea kiongozi wa CCM pale asipostahili, na kusema ukweli wa kilichotokea Richmond, hakumaanishi JK ndio msafi kivile, kwani at the end of the day yeye ndio alimteua mshkaji wake ili watuibie vizuri. UNAFKI nisioutaka mie ni huyu huyu mwizi aliyetuibia richmond kurudi kwa gia ya kufikiri wote tuna kumbukumbu fupi na kuanza uongo ili apewe kura. THAT i will not tolerate ndio maana nakuelimisha, ili ukimpigia kura usije kulalamika hapa kwa kuchagua hovyo.
Huko Ukawa shida iko kuwa nako kumejaa hot heads wasio na proper qualifications wala plan. NI MWEZI wa 3 sasa hakuna la maana linalosikika kutoka kwa watangaza sera wa UKAWA, zaidi ya kubishana mgawanyo wa majimbo tuu. Mtu pekee anayezunguka kusema atafanya nini ni Zitto, ambaye hana tumaini hata robo la kuchaguliwa kuongoza. hivyo CCM hovyo, Upinzani Shaghalabagala.
Nami nilikuvuta makusudi nizidi kuujua undani wako na kinachokusumbua. Sasa nimekuelewa unasumbuliwa na ukabila wala sio uongozi bora. Pili nimejifunza kuwa uelewa wako ni mdogo sana kuchangia jukwaa hili. Umejifanya huelewi somo kwa kuwa sikumpendekeza Zitto kwenye mabandiko yangu yote. Sasa kama hata wewe huuoni uwezekano wa ndugu yako kuchaguliwa/kupendekezwa kuliongoza taifa hili nifanyeje zaidi ya kukushauri kupeleka kilio kwenu? Huo ubunge wenyewe una hakika atatoboa Kigoma mjini? Sina nilichojifunza kwenye ngonjera zako na hata ukiniquote sikujibu na majukwaa ya mipasho sitembelei huko.
Sikuilewa post yako; ya kwangu iko wazi kabisa kuwa si sahihi kwa chama cha siasa kufanyia shughui zao Ikulu, ni kama ambavyo chama cha siasa hakiwezi kufanyia mambo yake WizaraniSasa usahihi unaouthibitisha hapa uko wapi kama tunayo sheria inayowakataza watumishi wa umma kujihusisha na mambo ya siasa? Mimi nikidhani ungesema sio sahihi mikutano hiyo kufanyika ikulu kwa kuwa ni ya taifa na sio ya chama. Hata ikatokea wakaondolewa madarakani watarudi Lumumba na ikulu kubakia ya taifa. Kama kweli ipo sheria inayowaruhusu kufanyia mikutano yao ya chama ikulu ni muda sasa ikarekebishwa.Ni mikutano ya kiserikali tu inayoruhusiwa huko. Au haya ndio madhara ya kiongozi wa chama kuwa pia kiongozi wa nchi kwa kubadiliaha tu kofia.