CCM ni cha Waislamu: Haya Madai Si Ya Kupuuza

Inawezekana kuna ukweli fulani kwa maneno yako ila hilo la uislama kuwa rangi sijui. lakini nimesikia pia waislam wakisema kuwa ccm ni chama cha wakritstu, ccm=christian church of Tanzania na kwamba Nyerere alipogundua kuwa waislam ni wengi kwenye TANU akaunda ccm na kuweka alama ya mslaba kwa kisingizio cha jembe na nyundo.Unasemaje hapo jerusalem

Umeonesha ujinga kupita maelezo! Yaani unaona jembe na nyundo unasema msalaba?? wapi na wapi...hiyo ni alama ya Wafanyakazi na Wakulima full stop!

Mawazo mengine sijui mnayatoa wapi ambayo hayana mantiki!! kha!
 
Unajuwa kwenye maisha ya mwanadamu huwa anazaliwa na mwisho wake ni kufa, sasa kama CCM ni chama cha waislam basi waislam wajuwe kuwa wanafikia mwisho wao katika jukwaa la siasa. maana ni imani yangu kuwa wameshindwa kuleta maendeleo kwa taifa la tanzania kila siku maisha ya mwananchi yanazidi kushuka kutokana na uongozi mbaya wa CCM.
sasa basi kinachotakiwa ni kuunda mbinu mpya za kukabiliana na maisha magumu ya Mtanzania wa leo na siku za usoni.
 
Huu ni unafiki na uletaji fitina na ningeshauri watu wapendao maadili na amani wajitenge na huu uongo. Alie towa hoja mara ya kwanza ya kuunganisha TANU ans ASP alikuawa mwalimu Nyerere ambae ni mkristo. Naomba mwana JF alie na wakati atutolee takwimu za wabunge na mawaziri tokea 1977 ilipoundwa CCM aonyeshe wangapi walikua Waislamu na wangapi wakristo - penye ukweli - uongo hubainika.
 
inawezekana kuna ukweli fulani kwa maneno yako ila hilo la uislama kuwa rangi sijui. Lakini nimesikia pia waislam wakisema kuwa ccm ni chama cha wakritstu, ccm=christian church of tanzania na kwamba nyerere alipogundua kuwa waislam ni wengi kwenye tanu akaunda ccm na kuweka alama ya mslaba kwa kisingizio cha jembe na nyundo.unasemaje hapo jerusalem

[red highlight]
ma great thinkers hawaongeagi pumba, nadhani hili kamwambie mkeo au mmeo.
 
Binafsi ninavyofahamu ni kuwa CCM si chama cha waislamu ila kuna viongozi wa juu wa sasa wa chama na serikali (ambao ni waislamu) wanaamini kuwa kuna watu fulani ndani ya uislamu walichangia sana wao kuwa madarakani na kutamani kutimiza yale yote wayatakayo kama njia ya kulipa fadhila. Hawa viongozi ndio wanafanya CCM kionekane kuwa chama cha waislamu.

Nyerere na serikali yake mtakumbuka walikuwa ni wapinzani wakubwa wa udini na ukabila. Mtaona namna ambavyo upinzani wao wa udini na ukabila ulivyokuwa chanzo kikuu cha amani nchini. Hivi vyumba viwili vikifunguliwa na kuachwa wazi bila usimamizi thabiti ndani ya chama na serikali, then tutegemee mipasuko ambayo madhara yake tunayajua sote.

Natumai ni sahihi, lakini naamini kuwa kuna waislamu wakorofi na watulivu; the same applies kwa dini zingine. Watu hawa huwa wanaisumbua sana nchi na kujifanya wao ndio wamewaweka viongozi wa juu madarakani, matokeo yake kuishia kuwaghasi na matakwa kibao kushinda hata wahisani na wafadhili.

JK amka na uwageuke wanaokudanganya na kujifanya kukuweka madarakani kisha usimamie katiba na misingi mikuu iliyotufanya tuwe nchi ya umoja na amani. Kuna wakristo, wapagani, waislamu watulivu na dini zingine kibao ambao walipambana kukuweka madarakani, usikubali kudanganywa na kuwasaliti watu hawa na kuwaona si lolote katika juhudi za kukurudisha state house. Usikubali kufavor dini fulani na kuigeuza serikali kuwa ya kidini (sina maoni zaidi juu ya chama chenu, mkichakachue muwezavyo but tuachieni nchi yenye amani, umoja na utulivu).
 
Upotofu umefikishwa vizuri kwa wapotevu...

Mmejitahidi kujenga hoja za kuvutia na kuvuta wengi kati mawazo mabovu...

Kwakuwa ASP AU TANU Si baba au mama wa tulio wengi basi tumseme tutakavyo mwanae CCM au CUF AU Chadema kwani kwa hayo hakuna afaye wala aponaye bali ni udhanifu tu...

Utawala wa kidunia upo na utakwepo, ukichukia hiki yupo apendaye kile ni mtazamo tu...

Tuendeleze hoja tuachane na viroja...

Tuendelee kuota lakini tusilazimishe ziso na ukweli ati tuweze kuwachota...

Alo na macho haambiwi tazama na iwapo muziki haueleweki msijelazimisha watu kwa midundo...

Huo ni mtazamo na mawazo yangu dhaifu...

Jazakha llahu kheri...

Tuko Pamoja...
 
Back
Top Bottom