Je, kuna tofauti ya IQ za Watanzania kutokana na dini zao? Kuna dini wanapasi sana, wanafeli sana, huwa wanabaguliwa na kudhulumiwa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,501
113,610
Wanabodi,

Kuna msemo wa kizungu usemao, "numbers don't lie" yaani numbers, haziongopi!.

Japo mimi nilipokuwa primary School nilikuwa mzuri wa hesabu, sekondari nikakutana na Additional mathematics, nilikuwa mzuri wa algebra, ila nilipoamua kufanya HGL A-Level, somo la hesabu nilipata C, sambamba na Chemistry, Physics, na Biology, zote nilipiga C!, lakini naomba kukiri, japo mimi sio mzuri kivile kwenye takwimu, lakini mtu akileta mada na kuivisha data za kimaghumashi, nina uwezo wa kubaini!.

Huko nyuma, tuliwahi kupishana na Mkuu Maalim Mohamed Said kwenye takwimu zake za idadi ya Wabunge Wakristo na Waislamu, ndani ya Bunge la JMT. Yeye alisema idadi ya wabunge Waislamu ni asilimia 6%, hii maana yake wabunge Wakristo ni asilimia 94%!, nilimbishia nikasema ni urongo!. Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!.

Ubishi huo ulianzia huku Mohamed Said: TANU kilikuwa chama cha Kiislam, hili hakuna mtu anayeweza kulipinga

Baada ya kumpinga with data estimates only kwa kutumia sampling ya wabunge wa Zanzibar tuu ndani ya Bunge la JMT ambao wote ni Waislamu, idadi hiyo ni over and above hiyo 6%! ile video ya urongo, iliondolewe kule YouTube!.

Sasa angalia takwimu hizi za matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mujibu wa Mkuu Maalim Mohamed Said
Unasema shule za Wakristo zimetaifishwa ili Waislam wasome.
Inaelekea hujui yaliyokuwa ndani ya Wizara ya Elimu na NECTA.

Angalia mfano huu na haya yamekuwa yakitendeka bila hofu:

Ninayo ripoti ya mwaka huu.

Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu.

Asilimia 29 ni wengine. Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21.

Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.

Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79. Katika asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, aseme kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.''

Lakini huwa tunazungumza na wengi ndani ya serikali ambao wanajua kuwa hili ni tatizo ambalo ni muhali mkubwa kwa serikali kukiri kuwa ndani ya serikali kumekuwa na dhulma hizi.
Kwenye takwimu hizi

Mkuu Maalim Mohamed Said ametoa hoja ya msingi sana na ameuliza
1. ama Waislamu wajinga
2. ama akili yao haifanyi kazi,
3. ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu,
4. ama kuna kitu.
5. Kisha akamuomba Waziri anayehusika, ajitokeze na aseme kwa hali ilivyo kama Waislamu wameumbwa wajinga.''
6. Mwisho ndipo kwenye hoja za bandiko hili, Maalim Mohamed Said amesema "huwa tunazungumza na wengi ndani ya serikali ambao wanajua kuwa hili ni tatizo ambalo ni muhali mkubwa kwa serikali kukiri kuwa ndani ya serikali kumekuwa na dhulma hizi"
Conclusion yake ni kuwa matokeo hayo kwa Waislamu ni wanafanyiwa dhulma, serikali wanajua kuhusu dhulma hiyo ila ni muhali kwa serikali kukiri kuhusu Waislamu kufanyiwa dhulma, hapa kwenye dhulma mimi ndipo nataka tuanze napo!.

Hatua ya kwanza ni authentication ya hizi data, kanuni ya kutoa data zozote ni lazima utaje source!, nauliza jee hizi data ni kweli Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71% ni Waislamu na dini nyingine zote ni asilimia 29%?.

Hizi data za asilimia za idadi ya watu wa dini fulani, zinapatikaje maana kwenye sensa ya watu na makazi, hakuna hojaji ya dini?!, sasa mtu utajuaje idadi ya Wakristo na Waislamu kwenye mtihani wa darasa la 7?!. Naomba mtu asiibuke na kuniambia wametumia kigezo cha majina ya Kiislamu na Kikristu!.

Katika hiyo asilimia 71 % ya Waislamu waliofanya mtihani huo wa darasa la 7, waliofaulu kwenda sekondari ni asilimia 21% tuu, hii maana yake kati ya Waislamu waliofanya mtihani wa darasa la 7, waliopasi kwenda sekondari ni asilimia 21% ya wale asilimia 71% Waislamu, na kati ya wale Wakristu asilimia 29% waliopasi kuingia sekondari ni asilimia 79%. Hii ni kweli?!.

Kama hizi data za Maalim Mohamed Said ni data za kweli, then kuna shida mahali!, kuna tatizo!, linalohitaji critical analysis kulibaini na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu kulitatua tatizo hilo!. Watanzania ni watu wamoja, haiwezekani tujione wamoja kumbe kuna wenzetu wanafanyiwa dhulma kubwa ya kihivi, huku kuna watu ndani ya serikali yetu wanafanya dhulma hii!, huku kuna watu ndani ya serikali yetu wanajua kuhusu dhulma hii, wanaiona dhulma hii na wanainyamazia!. Nashauri kama ni kweli kuna dhulma hii, tuifanyie utafiti wa kina na tukiibaini kwa kuithibisha kwa tafiti, tusiinyamazie, tuikomeshe!.

Huko nyuma niliwahi kuuliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Pia nikauliza Je, kuna uhusiano kati ya IQ, Dini ya mtu na Longevity? Naomba kuwatumia Marais wa Tanzania kama Sampling

Na nikauliza tena Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?

Na nikauliza tena na tena Je, kuna uhusiano kati ya IQ ya mtu na kabila lake, umasikini wake au kimo chake?

Kote huko nilikokuwa nauliza, nilipata upinzani mkubwa kwa kunyooshewa vidole vya udini!.

Nashauri ili kukata mzizi wa fitna kuwa kuna jamii inadhulumiwa systematically kwasababu ya dini yao, tufanye utafiti wa Idadi ya Waislamu na Wakristu kwenye maeneo yafuatayo

1. Kiwango cha umasikini kati ya Wakristo na Waislamu
2. Idadi ya wafanyabiashara Wakristo na Waislamu
3. Idadi ya matajiri Wakristo na Waislamu
4. Auandikishaji wa darasa la kwanza, primary school dropout na Ufaulu wa darasa la Saba wa Wakristo na Waislamu
5. Kujinga na sekondari, dropouts na Ufaulu wa kidato cha 4 wa Wakristo na Waislamu
6. Udahili post secondary education na elimu ya juu kwa Wakristo na Waislamu
7. Asilimia wenye astashahada kati ya Wakristo na Waislamu
8. Asilimia ya wenye Stashahada kati ya Wakristo na Waislamu
9. Asilimia ya wenye Shahada kati ya Wakristo na Waislamu
10. Asilimia ya Shahada za uzamili kati ya Wakristo na Waislamu
11. Asilimia za Shahada za uzamivu kati ya Wakristo na Waislamu
12. Idadi wafungwa, mahabusu na uhalifu kwa Wakristo na Waislamu
13. Idadi ya joblessness kwa Wakristo na Waislamu
14. Idadi ya wale dada zetu wanaofanya ile biashara ya usiku ya kuuza naniliu kati ya Wakristo na Waislamu
15. Idadi ya wife materials na husbands material kati ya Wakristo na Waislamu
16. Idadi ya kuoa na kuolewa, na waoaji na waolewaji kati ya Wakristo na Waislamu
17. Utulivu kwenye ndoa kati ya Wakristo na Waislamu
18. Idadi ya broken homes kati ya Wakristo na Waislamu
19. Idadi ya single mothers kati ya Wakristo na Waislamu
20. Wanaume wanaotekeza watoto kati ya Wakristo na Waislamu

Amini usiamini, matokeo ya tafiti hizi, kwanza yata surprise wengi, na hapa sasa ndipo nitafungua jicho la kuangazia tatizo, na japo matokeo hayo yata surprise wengi, lakini hizo data zitatusaidia kubaini kuwa tuna tatizo kwenye jamii yetu, hivyo tuanze kuchukua hatua kulitatua, vinginevyo, wachochezi wa udini, watakuwa wanaendelea kutulisha matango pori kuwa kuna dini wanapendelewa na kuna dini wanabaguliwa, kumbe the actual fact ni kuna wenzetu wanashida, wana matatizo, wanahitaji msaada na tuwasaidie, tusaidiane!.

Paskali
 
naam sasa mmeanza kuelewa kwamba falsafa ya dini ndiyo inayoleta maendeleo na utu wa binadamu, mfumo unaotawala Dunia leo hii ni western christianity hivyo yoyote ambaye hafwati christianity ( western) way of life hawezi kuendelea.

na ndio maana nchi zinafwata uislamu afrika ni shida tupu kuanzia somalia, chad, maurtania na kwingineko pakistani, irani au hata yemeni.

hata tanzagiza, jiulize kwa nini awamu ya 4 na sada hivi wanazima umeme? tumeishi for 5 years bila ya shida ya umeme, tanesco ile ile inayozima umeme leo hii ndiyo iliyowasha umeme bila ya shida 2015/20, swali ni kwamba kwa nini?

tusiogope maswali magumu tujiulize ili tuweze kusonga mbele labda tutapata suluhisho lkn ukweli ni kwamba uislamu at least wa tanzagiza haufundishi partriotism na hard work ushahidi upo kila mahali hapa tanzagiza kuanzia perfomance za watoto shuleni mpaka maofisini, angalia akina kunde walivyoifanya tanesco yetu walikuuta vizuri leo kila kitu destroyed …
 
Mkuu Pascal

Kindergarten & Montessori au niseme elimu ya awali ..

Najifunza Geography, Arithmetics (Mathematics),A little philosophy (Religion) . Literature/Poetry kidogo (Arts)

Mohamed anakwenda Chuo ..

Anajifunza Kiarabu alphabets ..

Alif , Be ....
Toka ameanza kuweza kutembea vizuri miaka mi3,4 Mpaka 7 Kweli kweli utamlinganisha na Mimi?
 
naam sasa mmeanza kuelewa kwamba falsafa ya dini ndiyo inayoleta maendeleo na utu wa binadamu, mfumo unaotawala Dunia leo hii ni western christianity hivyo yoyote ambaye hafwati christianity ( western) way of life hawezi kuendelea.

na ndio maana nchi zinafwata uislamu afrika ni shida tupu kuanzia somalia, chad, maurtania na kwingineko pakistani, irani au hata yemeni.

hata tanzagiza utaona awamu ya uislamu hakuna umeme shida na matatizo kila kona akiingia padri mambo yananyooka ndani ya mwaka tu.
Kuna Imani Fulani wanasema kuwa wao wapo mwaka 1400 na sio 2024
 
naam sasa mmeanza kuelewa kwamba falsafa ya dini ndiyo inayoleta maendeleo na utu wa binadamu, mfumo unaotawala Dunia leo hii ni western christianity hivyo yoyote ambaye hafwati christianity ( western) way of life hawezi kuendelea.

na ndio maana nchi zinafwata uislamu afrika ni shida tupu kuanzia somalia, chad, maurtania na kwingineko pakistani, irani au hata yemeni.

hata tanzagiza, jiulize kwa nini awamu ya 4 na sada hivi wanazima umeme? tumeishi for 5 years bila ya shida ya umeme, tanesco ile ile inayozima umeme leo hii ndiyo iliyowasha umeme bila ya shida 2015/20, swali ni kwamba kwa nini?

tusuiogope maswali magumu tujiulize ili tuweze kusonga mbele labda tutapata suluhisho lkn ukweli ni kwamba uislamu at least wa tanzagiza haufundishi partriotism na hard work …
China ? Japan ?
 
Umesahau picha. Hii hapa.

IMG-20240128-WA0024.jpg
 
Sijaona kama kuna haja ya kujadili kuhusua dini...kwa vile taifa ni moja ,mambo ambayo hayana mpango.

Mwisho wa siku kila mtu anatafuta ugali wake ,takwimu hazina maana kwa asilimia zote ...Shule niliyomaliza enzi zetu alifaulu mkristo mmoja tu basi tena amebadili dini miaka kadhaa aliolewa na muislamu namkumbuka mpaka leo ...Pia ule mkoa ulikuwa na waislamu wengi ila haina haja ya kupata takwimu kwa wote...
 
IQ is malleable na inategemea na culture (utamaduni) wa sehemu mtoto anayoishi.. baadhi ya dini zinakuja na tamaduni zake.wenzetu wazungu na wengineo waliweza kutenganisha dini na tamaduni,na wakatengeneza tamaduni nyingine japo walimega kidogo vitu kutoka kwenye dini kama morals ex. Mambo ya wizi,uzinzi,ulevi wakaongeza na vitu ;na iliwachukua karne na karne kufikia huku waliko.

Evolution ya culture inachukua muda mrefu na inatofautiana from one country to another..miaka ya 90 ungemwambia mwarabu wa Saudia amruhusu mkewe aendeshe gari ,ungepigwa lakini sasa hivi wanafanya hivyo japo Marekani walpitia hili in late 19th century (women's sufferage)..

Kwahiyo tukirudi kwenye suala la IQ,, usiangalie dini,angalia vizuri wale unaohisi Wana IQ Kubwa, utakuta regardless wametoka dini gani,Kuna pattern kwenye maisha yao zinafanana.and that is culture..
 
wanafwata western christian economic system, wajapani waliendelea kwa sababu walikwenda kujifunza Europe na USA how to run a country btw. Japan ni part of the western world kuna sababu kwa nini iko hivyo, china mpaka leo hii anafanya copy & paste ya western christian economic system …
Western christian economic system 🤡

Taifa gani linajiendesha kiuchumi kama China katika ulimwengu wa kimagharibi ?
 
Una point, lakini wapo watakaoona wamenyanyapaliwa hapa.

Vijana wa mudi wengi ni wauza ngada, wanatumia muda mwingi madrasa kukarili majuzuu, wanapuuza elimu ya kitaasisi inayopimwa na taasisi za mitihani.

Wanaposhindwa kutetea hoja zao, utasikia elimu dunia haina maana.

Ngoja waje tuwasikie, wazee wa vipedo.
 
Back
Top Bottom