CCM ivunjike tu

CCM ivunjike tu

Tatizo kubwa sana nilionalo mimi Watz wengi sana mnafananisha CCM na KANU na kwamba kilichotokea kwa KANU basi kitatokea CCM hilo haliwezekani!
CCM SIYO KANU!
Mazingira ni tofauti kabisa, Kenya na TZ tuko tofauti sana na sababu kubwa ni hii!
Kenya siasa ni Mtu na ndio maana KANU ilivunjika kwa maana Wananchi wanafwata Mtu, hapa kwetu siyo hivyo Siasa siyo Mtu bali ni Chama hivyo leo hii Mtu yoyote yule maarufu CCM pmj na Lowasa mwenyewe kama akitoka CCM hakuna atakayemfwata na huo ndio utakuwa mwisho wake!

Na hii ni kwa sababu hakuna kitu ambacho kitamfanya Mtz awe tayari kufa kwa ajili ya binadamu mwingine tofauti na Kenya au nchi nyingine wana siasa za Ukabila hivyo kama kwa mf. Raila akiwa KANU basi wajaluo wanaona wana muwakilishi KANU hivyo kama akitoka ni rahisi kufanya propaganda na kuwadanganya Wajaluo kwamba anaonewa na Wakikuyu na hivyo Wajaluo wote wanafwata kwa maana wanaona kama wanatea Kabila lao vivyo hivyo kwa Wakikuyu au sijui Kalenjili sasa hilo TZ halipo hivyo Lowasa akitoka kesho CCM ambacho ni chama Dola watamtumia TAKUKURU watamtafungulia mashitaka na watamfunga kabla ya Uchaguzi na HAKUNA kitu yeye (Lowasa) au wafuasi wake watafanya sana sana wataingia brn. mara moja Serikali watapiga risasi wawili watatu na wengine hawataona umuhimu wa kufa kwa ajili yake kwa maana hakuna bond ya aidha Ukabila au udini zaidi ya siasa hivyo hakuna aliye tayari kufa kwa ajili tu ya siasa hiyo ndiyo tofauti!

Ukitaka kuielewa CCM angalia Chama cha kikomunisti cha Uchina au Komunisti ya Urusi hivyo ndivyo vyama ambavyo CCM imefwata muundo wake na siyo KANU, hivyo na Urusi hakuna mwenye uwezo wa kuitoa Chama cha Putini madarakani hata iweje labda ije Vita Kubwa sana lkn siyo kwa Kura na sababu ni moja tu kama ilivyo CCM ni Chama Dola!

Kumbuka ukubwa wa madaraka ya Raisi wa JMT ambaye ndiye Mkubwa wa CCM, Kikwete ana uwezo wa kuahirisha uchaguzi na hakuna kitu Mtz yoyote yule anaweza kufanya, anaweza kubuni tu kwa kutumia Usalama wa Taifa hali ya hatari na kila kitu kwisha, anaweza kukifuta CHADEMA kesho na hakuna kitu CHADEMA watafanya zaidi ya kwenda kulia kwa Wazungu ili waikemee CCM, hivyo yoyote yule kwenye makundi ya CCM analijua hilo, kwani Amrani kombe yuko wapi si alipigwa risasi live na hakuna kitu Mtu alifanya?

Haya ndio mambo (Katiba Mpya) ambayo Upinzani walipaswa kupigania kwenye katiba Mpya, Madaraka ya raisi, kofia mbili lkn wapi walikuwa busy kudai haki ya Mtz Bara kuishi Zanzibar akina Tundu Lisu wakaishi kumtukana Nyerere na kusifiwa kwenye Majukwaa lkn mambo ya muhimu wakayapuuzia, hivyo CCM itabakia Madarakani hata Miaka 50 ijayo labda nguvu za nje ziingilie na hilo kutokea ni lazima Wazungu waone maslahi yao yako hatarini!

Barbarossa wewe unaamini katika kutishia watu. Amin usiamini CCM inaendakuvunjika. Utakuja kubaini baada ya 12 July 2015. Wakina Mkama walituharibia Chama na operation zao za kijinga ambazo hazikufua dafu.

CHADEMA nako kuna shida ni mkusanyiko wa watu kutoka kanda Fulani. Hawa watakuwa wabaya kuliko CCM. Hawa wana ishara za siri hata watia nia katika jumbo au kata waCDM ni hao hao kwa wingi wao. Wameshahamasishana wajianfikishe lengo likiwa moja tu................inchi.

Kwa kila kitu,,..............
 
2-en-1116938c9f89284a9bf4058caef47ad7.jpg

Kuvunjika kwake kumechelewa; kulipaswa kutokea tangu Kikao cha Butiama. Na labda ingevunjika hata kabla ya uchaguzi wa 2010. Ilichelewa kwa sababu bado hakukuwa na watu waliokuwa tayari kuimegua. Sasa hivi watu hao wapo, sababu zipo na inaonekana kuvunjika huku safari hii hakuepukiki - iwe kabla ya Uchaguzi au baada ya uchaguzi (itakapopoteza kiti cha Urais).

Meguka!

MMM
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, this can only happen if wishes were horses!.
Hii hoja yako ya CCM kuvunjika, hukuianza leo, nakukumbuka toka enzi za
[h=3]Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!
[/h]
baadaye ukatupatia somo kuhusu [h=3] CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!
[/h] [h=3] Mambo 7 ambayo CCM ikifanya yaweza kujiokoa;
[/h]

Mimi naendelea kusisitiza kuwa humu jf tuna watu wa aina tatu, tuna wishful thinkers, tuna day dreamers, na tuna ma realists!. Ma wishful thinkers na ma day dreamers ndio wengi zaidi humu na siku zote waki shout sauti zao husikika sana, lakini tupo sisi ma realist, ambao ni wachache na sauti zetu ni ndogo, kazi ya wishful thinkers ni kutoa mawazo yao yenye kuonyesha wishesh zao, ili tuu kufurahisha genge, lakini siku zote hawasemi how hizo wishes zitatimia, they only wish!, ndio maana nikasema haya yatamimia only if wishes were horses maana beggars would ride!, sisi ma realist humu kazi yetu ni kuusema ukweli halisi jinsi ile ulivyo, no matter ni mchungu kiasi gani kumeza, ila huo ndio ukweli halisi, kuwa upinzani wa Tanzania, ni upinzani nyoro nyoro, hakuna chama chochote hata UKAWA kina nguvu ya kuondoa CCM madarakani kwa sababu kiukweli kabisa tena ukweli mchungu, kwa Tanzania bado hatuna mbadala wa CCM!, mnaobisha bisheni tuu ili kujifurahisha na kujifariji lakini ukweli ndio huo!.

Tanzania bara hatuna anye credible opposition yenye uwezo wa kuishinda CCM, not Chadema not UKAWA, hivyo wale wote wenye matumaini kuwa UKAWA wanaweza kuishinda CCM na kuingia ikulu keshokutwa, wote ni wishful thinkers and day dreamers!. The only hope kwa opposition kushinda nchi hii ni kama CCM itameguka!, na ili CCM imeguke ni endapo itamkataa Lowassa, kisha huyo Lowassa amege kundi lake na kuhamia nalo opposition, then agombee urais, hapo ndio the only chance kwa opposition kukanyaga ikulu yetu ya Magogoni chini ya hapo hakuna kitu!.

Chadema kama Chadema, hakuna kitu kabisa mule!. Kwa wale wenye nafasi, hebu pitieni uzi huu wa Mkuu Mchambuzi
muusome kwa makini uliandikwa lini?, nini kilisemwa?, leo ni lini?, na nini kimefanywa?!, halafu tukiwaambia humu Chadema ni empty, watu mnaishia kutunyooshea vidole kuwa sisi ni magamba!.
Tangu 2010 sisi tumesema humu,
[h=3]CCM Imechokwa: CHADEMA Haijajipanga!,
[/h][h=3]CHADEMA: Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na Hamtajipanga!.
[/h][h=3]CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015!.
[/h][h=3]Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!...Only if
[/h]Tubishane kwa hoja na sio kwa wishful thinking only!.

Pasco.
 
Baada ya kututetea wananchi ndio wanatunyonya kupitia biashara zao kama mafuta. Haya mlieishabikia au kuichagua CCM wote chamoto tunakiona
 
Imekuwa kama watoto wadogo,eti Lowasa anatishia wenzie akikatwa atamleta Dr.Balali,sasa hicho ni chama ama ni genge la wavuta bangi nibangue

Huko sawa kabisa. Kimsingi hiki siyo chama bali kundi la vibaka kama alivyosema Makongoro Nyerere. Wanagombania nafasi ili waweze kuiba na ndiyo maana wanaanza kutishiana namna hiyo. Kwamba sisi wote ni wezi sasa nipishe mimi ukikataa nasema madudu yako kwa watu.
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.

we unachekesha sana eti huwezi kuongozwa na fisadi.. inaonyesha wewe hujitambui... hapo ulipo hujui kama unaongozwa na serikali ya wasanii mafisadi vibaka yani unajiona kama unatendewa haki kumbe unamegwa tu bila kujijua.
huyo unaesema ni fisadi ndio mpe mwanao akulelee uone kama akishindwa ndio ni rahisi kumchukulia hatua
 
Let it go, we are tired of robbers, thieves, power mongers, corruption, uncouthness, burglars, terrorists, murderers, slaughterers etc just to name a few characters of what they are.
Katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu tuombe sana Mwenyezi Mungu atuepushe na jitu hili linalotunyonya damu ili afya zetu ziweze kuimarika.
 
Ccm wanakosea kitu kimoja ukweli wananchi wamekichoka hicho chama hata kukisikia tu walichotakiwa kufanya ni kuunda chama kingine kipya
 
Tatizo Upinzani kuna watu MashaAlllah kuongea tu wamejaliwa , lakini mapaka sasa hakuna Chama hata kimoja huko upinzani kipo tayari kuendesha hii nchi... wao kwa wao ndani ya vyama wana migogoro, vyama vimejikita katika mikoa na wilayani tu! CCM ina mizizi vijijini ....
CCM haikubaliki kwa jamii, na wao wanajua hilo, huwa nachafukwa kweli kweli wanaposema wanakubalika kwa jamii. Hii sio kweli hata kidogo. Kama wanakubalika kweli kama wanavyoaminisha watu, wafanye uchaguzi ulio huru na wa haki. Waunde tume huru ya uchaguzi yenye kutenda haki tuone. Kuwe kuna uandikishwaji wa kina wa wapiga kura, pia Kuwe na mchakato wa wazi wa kuwapata washindi tuone, pia ccm wasitumie police na usalama wa taifa, tuone. Hawa watu wanaishi kwa hila, mpaka mungu awafarakanishe ndo kutatokea mabadiliko. Watu waovu, wanaotoa kafara kwenye ajali za mabasi na kuua maalbino ili washinde uchaguzi. Kila uovu una mwisho wake
 
Brother, we are living in the crazy world!!! While you are praying bad for Lowassa, other folks somewhere are praying good for him!

It's like this, a woman may look so ugly in your eyes, but that same woman may look vey beautiful in the eyes of another man!

So remember to make the provisions as the unlikely thing may happen!!!
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.
 
Kama fisadi ni moja tu ndani ya CCM, kama mikwara yote ya watangazania 42 inasababibishwa na mtu moja tu, kama katika idadi ya wananchama wanaodaiwa kuwa milioni tano (sic!) fisadi na mwizi ni mtu moja tu, kama kwa watangazania wote 42 ni mtu moja tu anayedhani chama ni cha kwake na kama, kama...duh! Heri hiki chama kivunjike vipande vipande kila moja abebe fito zake.

Fikiria mtu moja...EPA yeye, Richmond yeye, Kagoda yeye, Meremeta yeye, mauaji ya tembo yeye, kutoroshwa kwa twiga yeye, Escrow yeye, utawala dhaifu yeye, mauaji ya Albino yeye, ufujaji kwenye halmashauri yeye, madawa ya kulevya yeye, Katiba mbovu yeye, kero za Muungano yeye, ukosefu wa madawa hospitalini yeye, uhaba wa madawati yeye, kufeli katika masomo yeye, polisi kuua watu yeye, TISS kuwang'oa wananchi kucha na meno yeye, wanajeshi kuwapiga raia yeye, kuzurura nje kwa Raisi yeye na, na...

Bavaria, je unakubaliana na Mzee Mwanakijiji kuwa kama ni kuvunjika ni heri CCM ivunjike haraka taifa lipate nafuu kwa kuondokana na yote niliyoyataja hapo juu?
Kama inawezekana mtu mmoja akawa nado chanzo cha matatizo ya watu milion 50 basi huyo mtu lazima awe na akili nyingi sana. Mimi sikubali kwamba Lowasa ndo mtu anayeweza kuchukuwa mali za watanzania wote peke yake. Ila kama kaweza basi aendelee na awe rais.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, with due respect, this can only happen if wishes were horses!.
Hii hoja yako ya CCM kuvunjika, hukuianza leo, nakukumbuka toka enzi za
Kuanguka kwa CCM - Unabii Utatimia!

baadaye ukatupatia somo kuhusu CCM kumeguka ni muhimu kwa Taifa!

Mambo 7 ambayo CCM ikifanya yaweza kujiokoa;

Mimi naendelea kusisitiza kuwa humu jf tuna watu wa aina tatu, tuna wishful thinkers, tuna day dreamers, na tuna ma realists!. Ma wishful thinkers na ma day dreamers ndio wengi zaidi humu na siku zote waki shout sauti zao husikika sana, lakini tupo sisi ma realist, ambao ni wachache na sauti zetu ni ndogo, kazi ya wishful thinkers ni kutoa mawazo yao yenye kuonyesha wishesh zao, ili tuu kufurahisha genge, lakini siku zote hawasemi how hizo wishes zitatimia, they only wish!, ndio maana nikasema haya yatamimia only if wishes were horses maana beggars would ride!, sisi ma realist humu kazi yetu ni kuusema ukweli halisi jinsi ile ulivyo, no matter ni mchungu kiasi gani kumeza, ila huo ndio ukweli halisi, kuwa upinzani wa Tanzania, ni upinzani nyoro nyoro, hakuna chama chochote hata UKAWA kina nguvu ya kuondoa CCM madarakani kwa sababu kiukweli kabisa tena ukweli mchungu, kwa Tanzania bado hatuna mbadala wa CCM!, mnaobisha bisheni tuu ili kujifurahisha na kujifariji lakini ukweli ndio huo!.

Tanzania bara hatuna anye credible opposition yenye uwezo wa kuishinda CCM, not Chadema not UKAWA, hivyo wale wote wenye matumaini kuwa UKAWA wanaweza kuishinda CCM na kuingia ikulu keshokutwa, wote ni wishful thinkers and day dreamers!. The only hope kwa opposition kushinda nchi hii ni kama CCM itameguka!, na ili CCM imeguke ni endapo itamkataa Lowassa, kisha huyo Lowassa amege kundi lake na kuhamia nalo opposition, then agombee urais, hapo ndio the only chance kwa opposition kukanyaga ikulu yetu ya Magogoni chini ya hapo hakuna kitu!.

Chadema kama Chadema, hakuna kitu kabisa mule!. Kwa wale wenye nafasi, hebu pitieni uzi huu wa Mkuu Mchambuzi
muusome kwa makini uliandikwa lini?, nini kilisemwa?, leo ni lini?, na nini kimefanywa?!, halafu tukiwaambia humu Chadema ni empty, watu mnaishia kutunyooshea vidole kuwa sisi ni magamba!.
Tangu 2010 sisi tumesema humu,
CCM Imechokwa: CHADEMA Haijajipanga!,

CHADEMA: Hamkujipanga, hamjajipanga, hamjipangi na Hamtajipanga!.

CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015!.

Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!...Only if

Tubishane kwa hoja na sio kwa wishful thinking only!.

Pasco.
Pasco, hujawahi kuwa "realist" kama unavyojigamba! badala yake wewe ni "oppurtunist" mkubwa uliyekosa aibu. Hujawahi kuandika chochote ambacho ni "realistic" zaidi ya kujikomba kwa watawala na vibaraka wao. Ushahidi ni hiki ulichokiandika hapa. Hoja ya Mwanakijiji ni CCM kuvunjika na wala hajasema upinzani kuchukua nchi, wewe ulivyompuuzi unakuja na hoja zako na kuzipandikiza kwa mtoa hoja. Wapi Mwanakijiji kazungumzia CHADEMA? Ni waandishi wa habari ya kariba yenu ndio mnayeiabisha taaluma ya wanahabari kwa mawazo fyongo na duni kama haya. Najua unajipendekeza ili usogee sebuleni kwa watalawala. Na bado hujapewa tenda ya kuwachafua wagombea wengine kwa kalamu yako.
 
Sidhani kama itameguka! Wakati mmoja akina Mwakyembe, Sitta et al walisema kama gamba halivuki wao wataondoka. Gamba likakwama kiunoni. Hawakuondoka. Ilipokuja katiba wakaungana, mpaka Mwayembe akamwita Chenge mtemi! Sasa unajiuliza hawa watu wanasimamia nini? Jibu ni hakuna, ndio maana liwalo na liwe, maadam mkono unakwenda kinywani, basi sisi ni CCM damu.

Weka Lowassa, Chenge upande mmoja kisha weka Sitta, Mwakyembe upande mwingine. Jiulize kati ya makundi haya ni kitu gani wanachoshabihiana. Ni kimoja tu - ufisadi! Chukua makundi mengine - kama yapo - fanya hivyo hivyo. Utagundua kinachowaunganisha CCM sasa hivi ni ufisadi. Kwamba kila mmoja kesha-fisidi hivyo kilicho bora ni mmoja wao kuwa Rais aendelee kulinda maslahi yao - ufisadi. Kwa hiyo, pamoja na sarakasi zote wanazocheza sasa hivi utafika wakati watakumbatiana na kutuongopea kuwa wamekomaa kisiasa kumbe wapi - wamekubaliana ufisadi kwa kwenda mbele. Sidhani kama CCM itavunjika kwa hiari - natofautisha na KANU kwa sababu Kenya kuna wanasiasa waliokuwa na nguvu za kiuchumi hata nje ya siasa hivyo ilikuwa rahisi kwao kutoka KANU. Tanzania kuna wanasiasa matajiri uchwara-wanaotegemea ufisadi kuishi kibiashara - hawatathubutu kutoka CCM. Hivyo sioni CCM ikiwa kama KANU.

CCM itaondolewa madarakani kwa nguvu ya umma, si kwa hiari yake yenyewe.
Bravo!
 
Barbarossa wewe unaamini katika kutishia watu. Amin usiamini CCM inaendakuvunjika. Utakuja kubaini baada ya 12 July 2015. Wakina Mkama walituharibia Chama na operation zao za kijinga ambazo hazikufua dafu.

CHADEMA nako kuna shida ni mkusanyiko wa watu kutoka kanda Fulani. Hawa watakuwa wabaya kuliko CCM. Hawa wana ishara za siri hata watia nia katika jumbo au kata waCDM ni hao hao kwa wingi wao. Wameshahamasishana wajianfikishe lengo likiwa moja tu................inchi.

Kwa kila kitu,,..............

Maadamu Mwenyekiti wa CCM ndiye Raisi wa JMT basi hakuna mwenye jeuri yya kuivunja CCM, kumbuka CCM ni Chama Dola kila chombo cha Usalama nchini kiko chini yake kupitia Raisi wa Nchi ambaye ndiye Mkuu wa CCM!
 
Back
Top Bottom