CCM ivunjike tu

CCM ivunjike tu

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,131
Reaction score
43,696
2-en-1116938c9f89284a9bf4058caef47ad7.jpg


Kuvunjika kwake kumechelewa; kulipaswa kutokea tangu Kikao cha Butiama. Na labda ingevunjika hata kabla ya uchaguzi wa 2010. Ilichelewa kwa sababu bado hakukuwa na watu waliokuwa tayari kuimegua. Sasa hivi watu hao wapo, sababu zipo na inaonekana kuvunjika huku safari hii hakuepukiki - iwe kabla ya Uchaguzi au baada ya uchaguzi (itakapopoteza kiti cha Urais).

Ni vigumu kwa wote waliomo humo ndani kuweza kurithi yaliyomo ndani; wameshindwa kukaa kwa amani na sasa inaonekana wanaelekea kugongana. Wangeweza kuepusha mambo haya miaka kadhaa iliyopita ambapo wengine tulishauri mapema tu usalama wake ni kumeguka. Tofauti ambazo zimefunuliwa ndani ya chama hasa linapokuja suala la ufisadi ni kubwa mno kiasi kwamba ni vigumu kuona jinsi gani watu hawa wataweza kuwa wamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Na hili limesababishwa kwa kiasi kikubwa na udhaifu wa mifumo na taratibu za chama kushughulikia watu maarufu kiasi kwamba watu hao sasa wamepata nguvu kubwa kiasi cha kutishia uwepo wa chama na tishio hilo haliondoki kwa mikwara tena. Mikwara ingekuwa inaondoa watu basi "operesheni vua gamba" ingekuwa tosha kabisa. ILishindwa ile, zilishindwa hotuba za mikwara za mwenyekiti na hata maneno ya baadhi ya wana CCM yalishindwa kuwaondoa 'mafisadi'. Nina uhakika hata hili la "tuachieni chama chetu" litafeli. Wanaodai chama ni chao watajiuta hawana chao tena isipokuwa kuondoka.

Na kama watabakia itakuwa ni sababu tosha kwa Watanzania kufikiria kama kweli watu hawa wana ukweli ndani yao au yatakuwa yale yale ya ya kujikomba tena. Wataanza kutulisha maneno tena kuwa "hawakumaanisha yule" au "hawakumaanisha wale". Walimaanisha wengine wote isipokuwa "wale". Tusije kuona wale wale ambao wanasema "wale" ni mafisadi ndio hao hao wakawa wa kwanza kuimba "tuvunje makundi". Makundi CCM hayawajahi kuvunjwa yavunjwe leo kwanini?

Wakati mwingine utaona ni vizuri kwa CCM kuvunjika hata kupoteza Urais na kukaa pembeni ili labda akili zitawarudia. Na inaweza kuchukua muda kweli akili kuwarudia. KANU ya Kenya ilibidi akae pembeni na ikavunjika kweli lakini ilirudi kwa namna nyingine kabisa na kundi lililomeguka. CCM inabidi iende njia hiyo.

Ni kwa sababu hiyo naiombea sana wang'atane, waumane, wachubuane, na hata ikibidi wavunjane. Ili hatimaye wameguke na kutawanyika huku wakibebeshana lawama wakiwa nje ya madaraka.

Siombei wapatane hata kidogo. Maana wakipatana itakuwa shida nyingine ya miaka mitano. Sioni ni nani anayeweza kuwapatanisha sasa hivi maana walijaribu hata vikao vya mashauriano na madudu gani sijui walishindwa. Sasa wananchi wa kawaida wanafikiria watapatana kwa nini, ili kiwe nini, kwa nani na kwa nini?

Meguka!

MMM
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.
 
Kuna jamaa anapata wadhamini malaki kwa malaki. Ina maana;

1. Huyo jamaa ana pesa sana.?
2. Watanzania ni bei rahisi sana.?
3. Au anapendwa kweli?

Yangu macho
 
wizi,uoga, urafi wa madaraka,makundi yote hayo yanapelekea hali iliyopo...udhaifu wa mwenyekiti wa chama hicho ndio tatizo la msingi..amulea ugonjwa kwa mda wote..uwezo alikuwa nao...sasa anaelekea kubanwa kwenye kona..haakuwa na uwezo wa kufanya lolote.....mwenyekiti hana tofauti na miti ya ashoki
 
Imekuwa kama watoto wadogo,eti Lowasa anatishia wenzie akikatwa atamleta Dr.Balali,sasa hicho ni chama ama ni genge la wavuta bangi nibangue

hana uwezo wa kumleta balali labda kama anataka amfae aliko...tatizo la yote haya ni mwenyekiti wa chama..kawalea h hao miungu mtu..sasa watampanda kichwani....
 


Siombei wapatane hata kidogo. Maana wakipatana itakuwa shida nyingine ya miaka mitano. Sioni ni nani anayeweza kuwapatanisha sasa hivi maana walijaribu hata vikao vya mashauriano na madudu gani sijui walishindwa. Sasa wananchi wa kawaida wanafikiria watapana kwa nini?

Meguka!

MMM


maombi yangu usiju na mchana ni chama hichi cha kijani kiondoke kwa uso wa ulimwengu
 
Sidhani kama itameguka! Wakati mmoja akina Mwakyembe, Sitta et al walisema kama gamba halivuki wao wataondoka. Gamba likakwama kiunoni. Hawakuondoka. Ilipokuja katiba wakaungana, mpaka Mwayembe akamwita Chenge mtemi! Sasa unajiuliza hawa watu wanasimamia nini? Jibu ni hakuna, ndio maana liwalo na liwe, maadam mkono unakwenda kinywani, basi sisi ni CCM damu.

Weka Lowassa, Chenge upande mmoja kisha weka Sitta, Mwakyembe upande mwingine. Jiulize kati ya makundi haya ni kitu gani wanachoshabihiana. Ni kimoja tu - ufisadi! Chukua makundi mengine - kama yapo - fanya hivyo hivyo. Utagundua kinachowaunganisha CCM sasa hivi ni ufisadi. Kwamba kila mmoja kesha-fisidi hivyo kilicho bora ni mmoja wao kuwa Rais aendelee kulinda maslahi yao - ufisadi. Kwa hiyo, pamoja na sarakasi zote wanazocheza sasa hivi utafika wakati watakumbatiana na kutuongopea kuwa wamekomaa kisiasa kumbe wapi - wamekubaliana ufisadi kwa kwenda mbele. Sidhani kama CCM itavunjika kwa hiari - natofautisha na KANU kwa sababu Kenya kuna wanasiasa waliokuwa na nguvu za kiuchumi hata nje ya siasa hivyo ilikuwa rahisi kwao kutoka KANU. Tanzania kuna wanasiasa matajiri uchwara-wanaotegemea ufisadi kuishi kibiashara - hawatathubutu kutoka CCM. Hivyo sioni CCM ikiwa kama KANU.

CCM itaondolewa madarakani kwa nguvu ya umma, si kwa hiari yake yenyewe.
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.
Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.
Kama fisadi ni moja tu ndani ya CCM, kama mikwara yote ya watangazania 42 inasababibishwa na mtu moja tu, kama katika idadi ya wananchama wanaodaiwa kuwa milioni tano (sic!) fisadi na mwizi ni mtu moja tu, kama kwa watangazania wote 42 ni mtu moja tu anayedhani chama ni cha kwake na kama, kama...duh! Heri hiki chama kivunjike vipande vipande kila moja abebe fito zake.

Fikiria mtu moja...EPA yeye, Richmond yeye, Kagoda yeye, Meremeta yeye, mauaji ya tembo yeye, kutoroshwa kwa twiga yeye, Escrow yeye, utawala dhaifu yeye, mauaji ya Albino yeye, ufujaji kwenye halmashauri yeye, madawa ya kulevya yeye, Katiba mbovu yeye, kero za Muungano yeye, ukosefu wa madawa hospitalini yeye, uhaba wa madawati yeye, kufeli katika masomo yeye, polisi kuua watu yeye, TISS kuwang'oa wananchi kucha na meno yeye, wanajeshi kuwapiga raia yeye, kuzurura nje kwa Raisi yeye na, na...

Bavaria, je unakubaliana na Mzee Mwanakijiji kuwa kama ni kuvunjika ni heri CCM ivunjike haraka taifa lipate nafuu kwa kuondokana na yote niliyoyataja hapo juu?
 
Hakuna mwenye ubavu wa kuondoka CCM na kuimega CCM
Lowassa afya yake tu itam keep busy enough hata akiondoka CCM..
waliosalia ndo kabisa watajikunyata na kumpigia kampeni mgombea atakae tangazwa..
CCM bado ni jini litakalo isumbua Tanzania kwamuda
 
Kumeguka kwa CCM ni dhahiri. Lowassa amekusanya kundi kubwa la viongozi na wanachama kiasi kwamba asipopitishwa vikao vya NEC na Mkutano Mkuu vitakuwa na vurugu na havitafanyika. Naamin Kikwete hapendi jamaa apitishwe na chama kugombea, lakini bahati mbaya au nzuri hana kawaida ya kuchukua 'unpopular' decision. Ndiyo maana anapenda kuwatumia watu wengine kama Nape, Mangula na Makonda. Japo hampendi jamaa hana uwezo wa kutamka wazi kuwa hana vigezo. Tena Lowassa anatishia kujiondoa CCM kwa kauli zake alizorudia mara kibao ya kuhusu mabadiliko kupatikana ndani au nje ya CCM.
 
Back
Top Bottom