Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,568
Hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii na watu wake, hatuna uthubutu. The Boss, ni chama kipi kingine kimewahi kukamata madaraka ya nchi hii hadi useme hakuna replacement inayoaminika? Unatumia vigezo gani? Yaani unataka kuwaambia Watanzania waendelee kuongozwa na dead man walking kuliko kuwapa wengine ambao angalau wanajitutumua? What kind of thinking is this? Comments kama hizi huwa zinanikera kweli kweli kwani ni kama vile hivi tumelogwa, taifa limejaa dead men walking! Fikiria tunao watu wanaosema, hapana imetosha, hatuwezi kuendelea na watu wale wale, ni heri tufanye mabadiliko halafu anakuja mwingine anadai haoni mbadala, heri tuendelee na wale wale!
I understand, change can be scary. Doing anything for the first time or stepping into the unknown can at times be frightening and so requires courage and resolve, two ingredients most of us Tanzanians lack. But when one has hit rock bottom like we have, the only way out is up. It is insane to expect the same minds that led us into the pit to take us out of it hence the need for change; complete overhaul and complete about turn.
Nashangaa watu wanaopinga kuwapa nafasi nyingine upinzani. Sioni sababu ya maana wanayotoa zaidi ya kuongea tu ilimradi.
Ila nilichogundua, hawa watu wanaopinga upinzani kuingia madarakani ni wale watu waliozoea au wapo ndani ya system corrupt. Wananeemeka nayo.
Ila wanasahau kuna multiplier effect ya hiko wanachokitetea. Wanasahau kupitia hiyo CCM wanayoitetea kuna wazazi au ndugu zao wapo huko vijijini hawana maji safi ya kunywa, hawana madawa hospitali, hawana uhakika wa masoko ya mazao yao. Yani matatizo chungu nzima kiasi kwamba ananeemeka yeye pekee hapa mjini kwa ufisadi ila lundo la watu nyuma yake hawana uhakika wa kesho.
Mabadiliko katika jamii yeyote ni muhimu ili tupige hatua kubwa ya maendeleo. Kutokuwa na mabadiliko inamaanisha kuwa tunakubali fikra zile zile zilizotufikisha hapa tulipo.
Ndo maana watanzania wengi tunabaki masikini kwasababu hatuna hulka ya kufanya maamuzi magumu kwenye maisha yetu.
Sisi ni waoga na wasahaulifu sana.