CCM ivunjike tu

CCM ivunjike tu

Kumeguka kwa CCM ni dhahiri. Lowassa amekusanya kundi kubwa la viongozi na wanachama kiasi kwamba asipopitishwa vikao vya NEC na Mkutano Mkuu vitakuwa na vurugu na havitafanyika. Naamin Kikwete hapendi jamaa apitishwe na chama kugombea, lakini bahati mbaya au nzuri hana kawaida ya kuchukua 'unpopular' decision. Ndiyo maana anapenda kuwatumia watu wengine kama Nape, Mangula na Makonda. Japo hampendi jamaa hana uwezo wa kutamka wazi kuwa hana vigezo. Tena Lowassa anatishia kujiondoa CCM kwa kauli zake alizorudia mara kibao ya kuhusu mabadiliko kupatikana ndani au nje ya CCM.

lowassa hawezi kuhama ccm...akienguliwa atakaa kimya....tatizo kubwa ni huyo mweyekiti wao..
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.

Lowasa hatiishi ccm kama unavyodai, ila amejua wezi wapo wengi wamejifa kwenye jina lake wakitaka kumtoa kafara, kama ccm ni chama makini kwanini lowasa hakufukuzwa uanachama?
 
Wakati mwingine utaona ni vizuri kwa CCM kuvunjika hata kupoteza Urais na kukaa pembeni ili labda akili zitawarudia. Na inaweza kuchukua muda kweli akili kuwarudia. KANU ya Kenya ilibidi akae pembeni na ikavunjika kweli lakini ilirudi kwa namna nyingine kabisa na kundi lililomeguka. CCM inabidi iende njia hiyo.

Sio tu wakati mwingine. Ni wakati wote!

CCM kikiwa chama cha upinzani nchi yetu itafaidika, na itafika mbali sana. Kwa hiyo, sababu si tu kwamba Ruswa na Ufisadi umekidhiri huko CCM ndio maana ni lazima kiondoke. Ila pia, muhimu zaidi, kinahitajika ili kiwe ni chama cha Upinzani.

Muda wa CCM kuwa kwenye kambi ya upinzani ndio huu.
 
Naona huu uzi umevamiwa na Bavicha mnatiana moyo,CCM wapo vizuri hakuna makundi wala nini subirini tumpitishe mamvi ndo mtaona moto wake,mamvi atakuwa Rais wa kwanza kupita bila kupigwa
 
Dua la Kuku kamwe halimpati Mwewe!!! ... Ila naomba kwa Maanani iwe hivyo pengine akina mama wataacha kujifungulia sakafuni, mikataba ya kisenge haitafungwa tena kwenye rasilimali zetu...
 
Shida sio CCM kufa kabisa
CCM now ni kama 'dead man walking'
shida ipo kwenye replacement tukishaizika CCM
je wananchi wanaiona na kuiamin replacement?
we umeiiona?
Lowassa hawezi kuenguliwa na ndilo hofu na tumaini la wengi. Kama ataenguliwa basi CCM itapona japo sasa hivi ipo ICU watu hawajui tu ila wao wanajua hilo. Wala sio wasiwasi ya Lowassa kukihama chama bali vichwa haswa wamejiandaa kukihama chama kama Lowassa atapita uchaguzi CCM na hiki ndicho UKAWA wanakisubiri mwaka huu 2015 - kazi kwisha... Ya Mwanakijiji yametimia.
 
Kuna jamaa anapata wadhamini malaki kwa malaki. Ina maana;

1. Huyo jamaa ana pesa sana.?
2. Watanzania ni bei rahisi sana.?
3. Au anapendwa kweli?
Yangu macho

Mkuu watu wamepigika na maisha pesa ni ngumu, kwahiyo nahisi watu wakisikia Lowasa anakuja wanakimbia kujiandikisha kumdhamini kwa maelfu ili wapate hata ya kilo kadhaa za unga. Lowasa hafai hata kuwa mwenyekiti wa nyumba kumi
 
Shida sio CCM kufa kabisa
CCM now ni kama 'dead man walking'
shida ipo kwenye replacement tukishaizika CCM
je wananchi wanaiona na kuiamin replacement?
we umeiiona?

Hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii na watu wake, hatuna uthubutu. The Boss, ni chama kipi kingine kimewahi kukamata madaraka ya nchi hii hadi useme hakuna replacement inayoaminika? Unatumia vigezo gani? Yaani unataka kuwaambia Watanzania waendelee kuongozwa na dead man walking kuliko kuwapa wengine ambao angalau wanajitutumua? What kind of thinking is this? Comments kama hizi huwa zinanikera kweli kweli kwani ni kama vile hivi tumelogwa, taifa limejaa dead men walking! Fikiria tunao watu wanaosema, hapana imetosha, hatuwezi kuendelea na watu wale wale, ni heri tufanye mabadiliko halafu anakuja mwingine anadai haoni mbadala, heri tuendelee na wale wale!

I understand, change can be scary. Doing anything for the first time or stepping into the unknown can at times be frightening and so requires courage and resolve, two ingredients most of us Tanzanians lack. But when one has hit rock bottom like we have, the only way out is up. It is insane to expect the same minds that led us into the pit to take us out of it hence the need for change; complete overhaul and complete about turn.
 
Kwa undani kabisa CCM imevunjika na kuna Roho Mbili Tayari.

Roho Ya Ufisadi na Roho ya Uadilifu ulio msingi wa uasisi wa Chama.

Kwa nje haraka haraka utaiona ccm moja lakini ukitulia na kutumia darubini ya kuvuta na kukuza tukio. Utaiona CCM yenye makundi mawili tu.

Conservative CCM and Liberal CCM.

Msitie SHAKA. Watia nia wamegawanyika kihivo. Makundi ndani ya CCM sio mengi ni mawili tu. Na Rais wa awamu ya 5 anatokea Conservative CCM. Ambapo kwa Vyote vvyote vile Mtu mwenye nywele nyeupe hawezi kuwepo.

Conservative CCM Hoyee. Watuachie Chama Chetu Cha Wafanyakazi na Wakulima KIPINDUE ufisadi na kurejea Misingi.

Eewe Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania ASILI.
 
Hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii na watu wake, hatuna uthubutu. The Boss, ni chama kipi kingine kimewahi kukamata madaraka ya nchi hii hadi useme hakuna replacement inayoaminika? Unatumia vigezo gani? Yaani unataka kuwaambia Watanzania waendelee kuongozwa na dead man walking kuliko kuwapa wengine ambao angalau wanajitutumua? What kind of thinking is this? Comments kama hizi huwa zinanikera kweli kweli kwani ni kama vile hivi tumelogwa, taifa limejaa dead men walking! Fikiria tunao watu wanaosema, hapana imetosha, hatuwezi kuendelea na watu wale wale, ni heri tufanye mabadiliko halafu anakuja mwingine anadai haoni mbadala, heri tuendelee na wale wale!

I understand, change can be scary. Doing anything for the first time or stepping into the unknown can at times be frightening and so requires courage and resolve, two ingredients most of us Tanzanians lack. But when one has hit rock bottom like we have, the only way out is up. It is insane to expect the same minds that led us into the pit to take us out of it hence the need for change; complete overhaul and complete about turn.

Wewe jazba inakufanya ushindwe kuelewa nilicho andika
umeelewa nilicho andika?
wapi nimesema tuendelee na hawa hawa?
huoni nimeuliza na tena nimemuuliza mtu mmoja kuwa je anaona replacement?
na swali ni je wananchi wanaiona replacement?
huelewi nini haswa?
kuuliza wananchi wanaona ndo sawa na kusema wananchi hawaoni?
na hata kama ningesema mimi sioni tabu ingekuwa wapi?
si ingekuwa msimamo wangu binafsi?

wewe kama kuna replacement iliyokushawishi na ukaiona na kuiamini
huna haki ya kuwalaumu ambao hawajashawishika na kuiona hiyo replacement...
 
Back
Top Bottom