CCM ivunjike tu

CCM ivunjike tu

Hili ndilo tatizo kubwa la nchi hii na watu wake, hatuna uthubutu. The Boss, ni chama kipi kingine kimewahi kukamata madaraka ya nchi hii hadi useme hakuna replacement inayoaminika? Unatumia vigezo gani? Yaani unataka kuwaambia Watanzania waendelee kuongozwa na dead man walking kuliko kuwapa wengine ambao angalau wanajitutumua? What kind of thinking is this? Comments kama hizi huwa zinanikera kweli kweli kwani ni kama vile hivi tumelogwa, taifa limejaa dead men walking! Fikiria tunao watu wanaosema, hapana imetosha, hatuwezi kuendelea na watu wale wale, ni heri tufanye mabadiliko halafu anakuja mwingine anadai haoni mbadala, heri tuendelee na wale wale!

I understand, change can be scary. Doing anything for the first time or stepping into the unknown can at times be frightening and so requires courage and resolve, two ingredients most of us Tanzanians lack. But when one has hit rock bottom like we have, the only way out is up. It is insane to expect the same minds that led us into the pit to take us out of it hence the need for change; complete overhaul and complete about turn.

CCM itavunjika hilo halina shaka. Unachochangaya hapa ni matokeao ya kuvunjika huko. Huo mvunjiko upo kwa pande mbili. Upande wa kwanza utakuwa na NGUVU NA MAMLAKA kuliko CCM ya mwanzo. Upande wa pili utakuwa CCM iliyopitwa na wakati.

Awamu ya 5 iko mikononi mwa CCM yenye Nguvu na Mamlaka yaliyoirudishia Uasisi na Uasili Wake. Hali Halina UBISHI.
 
Wewe jazba inakufanya ushindwe kuelewa nilicho andika
umeelewa nilicho andika?
wapi nimesema tuendelee na hawa hawa?
huoni nimeuliza na tena nimemuuliza mtu mmoja kuwa je anaona replacement?
na swali ni je wananchi wanaiona replacement?
huelewi nini haswa?
kuuliza wananchi wanaona ndo sawa na kusema wananchi hawaoni?
na hata kama ningesema mimi sioni tabu ingekuwa wapi?
si ingekuwa msimamo wangu binafsi?

wewe kama kuna replacement iliyokushawishi na ukaiona na kuiamini
huna haki ya kuwalaumu ambao hawajashawishika na kuiona hiyo replacement...

The Boss nimemnyooshea concept yake. Na kumuonyesha UIMARA WA CCM ulipo.

Na kusema kweli UKAWA haiwezi kupuuzwa kwenye ujenzi wa Demokrasia Ya Taifa Tanzania. Naiheshimu UKAWA kwa pressure na ufuatiliaji ulioifanya CCM kuwa kwenye Sura mbili ambapo moja inachukua Uongozi wa Taifa Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Lowassa hawezi kuenguliwa na ndilo hofu na tumaini la wengi. Kama ataenguliwa basi CCM itapona japo sasa hivi ipo ICU watu hawajui tu ila wao wanajua hilo. Wala sio wasiwasi ya Lowassa kukihama chama bali vichwa haswa wamejiandaa kukihama chama kama Lowassa atapita uchaguzi CCM na hiki ndicho UKAWA wanakisubiri mwaka huu 2015 - kazi kwisha... Ya Mwanakijiji yametimia.

Uwezekano wa Wa Kutokea CCM moja nzito yaye Heshima na Mamlaka yenye Nguvu kuliko UKAWA na CCM Lowasa UPO. Na hiyo ndiyo ya kuchukua Uongozi.
 
Wewe jazba inakufanya ushindwe kuelewa nilicho andika
umeelewa nilicho andika?
wapi nimesema tuendelee na hawa hawa?
huoni nimeuliza na tena nimemuuliza mtu mmoja kuwa je anaona replacement?
na swali ni je wananchi wanaiona replacement?
huelewi nini haswa?
kuuliza wananchi wanaona ndo sawa na kusema wananchi hawaoni?
na hata kama ningesema mimi sioni tabu ingekuwa wapi?
si ingekuwa msimamo wangu binafsi?

wewe kama kuna replacement iliyokushawishi na ukaiona na kuiamini
huna haki ya kuwalaumu ambao hawajashawishika na kuiona hiyo replacement...
Typical statement from a dead man walking, at least this much I expected! Maybe you didn't say it in so many words, truth is you implied it and that is even worse; you don't even have the courage to do so plainly. Tatizo ni kwamba wanafiki mko wengi. Mara ngapi swali linajitokeza humu likiuliza hao wapinzani wamefanya nini, mbona wameshindwa kutimiza ahadi zao, kwa nini wanapenda kulia lia. Wakiandamana wakipinga, wakashambuliwa na polisi, wakapigwa wakaumizwa na hata wengine wakauawa, mpo watu mtakaowabeza mkidai wameyataka wenyewe. Shame on you people!
 
T
Sidhani kama itameguka! Wakati mmoja akina Mwakyembe, Sitta et al walisema kama gamba halivuki wao wataondoka. Gamba likakwama kiunoni. Hawakuondoka. Ilipokuja katiba wakaungana, mpaka Mwayembe akamwita Chenge mtemi! Sasa unajiuliza hawa watu wanasimamia nini? Jibu ni hakuna, ndio maana liwalo na liwe, maadam mkono unakwenda kinywani, basi sisi ni CCM damu.

Weka Lowassa, Chenge upande mmoja kisha weka Sitta, Mwakyembe upande mwingine. Jiulize kati ya makundi haya ni kitu gani wanachoshabihiana. Ni kimoja tu - ufisadi! Chukua makundi mengine - kama yapo - fanya hivyo hivyo. Utagundua kinachowaunganisha CCM sasa hivi ni ufisadi. Kwamba kila mmoja kesha-fisidi hivyo kilicho bora ni mmoja wao kuwa Rais aendelee kulinda maslahi yao - ufisadi. Kwa hiyo, pamoja na sarakasi zote wanazocheza sasa hivi utafika wakati watakumbatiana na kutuongopea kuwa wamekomaa kisiasa kumbe wapi - wamekubaliana ufisadi kwa kwenda mbele. Sidhani kama CCM itavunjika kwa hiari - natofautisha na KANU kwa sababu Kenya kuna wanasiasa waliokuwa na nguvu za kiuchumi hata nje ya siasa hivyo ilikuwa rahisi kwao kutoka KANU. Tanzania kuna wanasiasa matajiri uchwara-wanaotegemea ufisadi kuishi kibiashara - hawatathubutu kutoka CCM. Hivyo sioni CCM ikiwa kama KANU.

CCM itaondolewa madarakani kwa nguvu ya umma, si kwa hiari yake yenyewe.
Analysis yako ni sahihi. Wote wameamua kukomalia humo humo iwe kwa woga au kiburi. Tatizo hata wakikubaliana baadaya uteuzi wa wagombea bado kutabaki makundi. Chama kitaendelea kuwa na matatizo makubwa zaidi maana ni afadhali adui aliyeko nje kuliko adui wa ndani. Makundi yaliyoko ndani na ya kisiri yanasumbua aidi kuliko yaliyoko nje na dhairi. Kwa vyovyote vile ni shida, wampitishe Lowassa au wasimptishe!
 
Kumeguka kwa CCM ni dhahiri. Lowassa amekusanya kundi kubwa la viongozi na wanachama kiasi kwamba asipopitishwa vikao vya NEC na Mkutano Mkuu vitakuwa na vurugu na havitafanyika. Naamin Kikwete hapendi jamaa apitishwe na chama kugombea, lakini bahati mbaya au nzuri hana kawaida ya kuchukua 'unpopular' decision. Ndiyo maana anapenda kuwatumia watu wengine kama Nape, Mangula na Makonda. Japo hampendi jamaa hana uwezo wa kutamka wazi kuwa hana vigezo. Tena Lowassa anatishia kujiondoa CCM kwa kauli zake alizorudia mara kibao ya kuhusu mabadiliko kupatikana ndani au nje ya CCM.

Mkuu kama nchi yetu HAIITWI Tanzania basi maandishi mekundu yana ukweli. Lakini kama inaitwa Tanzania basi umepotoka kabisa. Nakuuliza.. hao viongozi na wanachama wenye uwezo na uthubutu wa kufanya vurugu ni kina nani?
 
Natabili katika picha hizi hapa chini ndio jinsi itakavyokuwa siku ya mkutano mkuu wa CCM kuteua jina moja la kugombea urais
Vua Gamba.JPG
ngumi_ccm.jpeg
 
Mzee Mwanakijiji wewe ni team mdmu tunakujua ila kwa taarfa yako na uweke kwenye diary yako 1995 Abdulrahman Kinana na Anna Makinda walitoa machozi lowasa alipowatangazia kua ameamua kujitoa kugombea urais na kumuunga mkono kikwete wakiamini lowasa amekosea ebu mwanakijiji na midimu wenzako jiulize machozi ya kinana yalifutika lini mpaka amchukie lowassa mnacheza ngoma msiyoijua na kna nape bahati nzuri mangula anaijua ndio maana anachoma na kupuliza ila.si kikwete wala.mangula wenye uwezo wa kumzuia lowasa kugombea urais take it from me.
 
Last edited by a moderator:
CCM itavunjika hilo halina shaka. Unachochangaya hapa ni matokeao ya kuvunjika huko. Huo mvunjiko upo kwa pande mbili. Upande wa kwanza utakuwa na NGUVU NA MAMLAKA kuliko CCM ya mwanzo. Upande wa pili utakuwa CCM iliyopitwa na wakati.

Awamu ya 5 iko mikononi mwa CCM yenye Nguvu na Mamlaka yaliyoirudishia Uasisi na Uasili Wake. Hali Halina UBISHI.
Uwezekano wa Wa Kutokea CCM moja nzito yaye Heshima na Mamlaka yenye Nguvu kuliko UKAWA na CCM Lowasa UPO. Na hiyo ndiyo ya kuchukua Uongozi.
Na wewe The President, tatizo lako ni kwamba unadhani unaielewa CCM lakini kulingana na post yako naona huielewi na huijui CCM. CCM wameweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu moja, umoja wao na uwezo wao katika kulindana na kuteteana pale wanapokabiliwa na utata. Kama unafuatilia malumbano ambayo mara nyingi yangehatarisha umoja wao, huwa wanaitana na kuwekana sawa na kutoka hapo wakiwa wamoja.

Uchafu hufagiliwa hadi mvunguni kwa sababu kila moja anatoka hapo akijua mapungufu ya mwenzie na hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake hadi pale litakapozuka tafrani nyingine. Unakumbuka walivyoenda kumtafuta Mang'ula kule kijijini alipokuwa analima nyanya? CCM ilikuwa inachungulia kaburi, magamba yamekwama kiunoni huku Nape akipita huko na huko akiropoka...waliyamaliza kwa maazimio, maazimio ya kufunika kombe.

Maazimio ya kulindana ndio dawa kwa CCM na leo hii akipita Lowassa, tofauti zote ndani ya CCM zitaisha na ataungwa mkono na wale wale wanaomtupia madongo. Hiyo ndiyo CCM, chama kinachoishi kwa ulaghai na nguvu za dola; watamtoa wapi huyo msafi asiye na doa? Jaribu kukaa chini ufikirie huyo atakayeteuliwa na CCM halafu, Mungu atupishilie mbali, awe Raisi wa awamu ya tano, atapambana vipi na wenziye ndani ya CCM?
 
Mzee Mwanakijiji

Tatizo kubwa sana nilionalo mimi Watz wengi sana mnafananisha CCM na KANU na kwamba kilichotokea kwa KANU basi kitatokea CCM hilo haliwezekani!
CCM SIYO KANU!
Mazingira ni tofauti kabisa, Kenya na TZ tuko tofauti sana na sababu kubwa ni hii!
Kenya siasa ni Mtu na ndio maana KANU ilivunjika kwa maana Wananchi wanafwata Mtu, hapa kwetu siyo hivyo Siasa siyo Mtu bali ni Chama hivyo leo hii Mtu yoyote yule maarufu CCM pmj na Lowasa mwenyewe kama akitoka CCM hakuna atakayemfwata na huo ndio utakuwa mwisho wake!

Na hii ni kwa sababu hakuna kitu ambacho kitamfanya Mtz awe tayari kufa kwa ajili ya binadamu mwingine tofauti na Kenya au nchi nyingine wana siasa za Ukabila hivyo kama kwa mf. Raila akiwa KANU basi wajaluo wanaona wana muwakilishi KANU hivyo kama akitoka ni rahisi kufanya propaganda na kuwadanganya Wajaluo kwamba anaonewa na Wakikuyu na hivyo Wajaluo wote wanafwata kwa maana wanaona kama wanatea Kabila lao vivyo hivyo kwa Wakikuyu au sijui Kalenjili sasa hilo TZ halipo hivyo Lowasa akitoka kesho CCM ambacho ni chama Dola watamtumia TAKUKURU watamtafungulia mashitaka na watamfunga kabla ya Uchaguzi na HAKUNA kitu yeye (Lowasa) au wafuasi wake watafanya sana sana wataingia brn. mara moja Serikali watapiga risasi wawili watatu na wengine hawataona umuhimu wa kufa kwa ajili yake kwa maana hakuna bond ya aidha Ukabila au udini zaidi ya siasa hivyo hakuna aliye tayari kufa kwa ajili tu ya siasa hiyo ndiyo tofauti!

Ukitaka kuielewa CCM angalia Chama cha kikomunisti cha Uchina au Komunisti ya Urusi hivyo ndivyo vyama ambavyo CCM imefwata muundo wake na siyo KANU, hivyo na Urusi hakuna mwenye uwezo wa kuitoa Chama cha Putini madarakani hata iweje labda ije Vita Kubwa sana lkn siyo kwa Kura na sababu ni moja tu kama ilivyo CCM ni Chama Dola!

Kumbuka ukubwa wa madaraka ya Raisi wa JMT ambaye ndiye Mkubwa wa CCM, Kikwete ana uwezo wa kuahirisha uchaguzi na hakuna kitu Mtz yoyote yule anaweza kufanya, anaweza kubuni tu kwa kutumia Usalama wa Taifa hali ya hatari na kila kitu kwisha, anaweza kukifuta CHADEMA kesho na hakuna kitu CHADEMA watafanya zaidi ya kwenda kulia kwa Wazungu ili waikemee CCM, hivyo yoyote yule kwenye makundi ya CCM analijua hilo, kwani Amrani kombe yuko wapi si alipigwa risasi live na hakuna kitu Mtu alifanya?

Haya ndio mambo (Katiba Mpya) ambayo Upinzani walipaswa kupigania kwenye katiba Mpya, Madaraka ya raisi, kofia mbili lkn wapi walikuwa busy kudai haki ya Mtz Bara kuishi Zanzibar akina Tundu Lisu wakaishi kumtukana Nyerere na kusifiwa kwenye Majukwaa lkn mambo ya muhimu wakayapuuzia, hivyo CCM itabakia Madarakani hata Miaka 50 ijayo labda nguvu za nje ziingilie na hilo kutokea ni lazima Wazungu waone maslahi yao yako hatarini!
 
Last edited by a moderator:
Typical statement from a dead man walking, at least this much I expected! Maybe you didn't say it in so many words, truth is you implied it and that is even worse; you don't even have the courage to do so plainly. Tatizo ni kwamba wanafiki mko wengi. Mara ngapi swali linajitokeza humu likiuliza hao wapinzani wamefanya nini, mbona wameshindwa kutimiza ahadi zao, kwa nini wanapenda kulia lia. Wakiandamana wakipinga, wakashambuliwa na polisi, wakapigwa wakaumizwa na hata wengine wakauawa, mpo watu mtakaowabeza mkidai wameyataka wenyewe. Shame on you people!

mkuu Mag3, watu nchi hii bado sana kwenye eneo la ukombozi wa kifikra....what's even more dismaying ni kuona kuwa ukombozi huu wa fikra kumbe bado unahitajika hata kwa watu "wenye vidato" vyao ambao tulitegemea wawe ndiwo crusaders. pathetic.

kuna mchangiaji mmoja kwenye uzi huu hapo juu amemjibu huyu bwana kuwa afadhali ya pengo kuliko jino bovu...a sobering answer to a slumbering retard!

anyways, historia inatufundisha kuwa watu wa aina hii watakuwepo daima...kama ilivyokuwa wakati Mwl Nyerere alipokuwa anigania uhuru - kuna wasomi wa wakati ule walitaka mkoloni ang'olewe lakini bado walitia shaka kuhusu mbadala (huku wakijua fika kuwa Mwalimu was already there at the helm of it all)
 
Kama fisadi ni moja tu ndani ya CCM, kama mikwara yote ya watangazania 42 inasababibishwa na mtu moja tu, kama katika idadi ya wananchama wanaodaiwa kuwa milioni tano (sic!) fisadi na mwizi ni mtu moja tu, kama kwa watangazania wote 42 ni mtu moja tu anayedhani chama ni cha kwake na kama, kama...duh! Heri hiki chama kivunjike vipande vipande kila moja abebe fito zake.

Fikiria mtu moja...EPA yeye, Richmond yeye, Kagoda yeye, Meremeta yeye, mauaji ya tembo yeye, kutoroshwa kwa twiga yeye, Escrow yeye, utawala dhaifu yeye, mauaji ya Albino yeye, ufujaji kwenye halmashauri yeye, madawa ya kulevya yeye, Katiba mbovu yeye, kero za Muungano yeye, ukosefu wa madawa hospitalini yeye, uhaba wa madawati yeye, kufeli katika masomo yeye, polisi kuua watu yeye, TISS kuwang'oa wananchi kucha na meno yeye, wanajeshi kuwapiga raia yeye, kuzurura nje kwa Raisi yeye na, na...

Bavaria, je unakubaliana na Mzee Mwanakijiji kuwa kama ni kuvunjika ni heri CCM ivunjike haraka taifa lipate nafuu kwa kuondokana na yote niliyoyataja hapo juu?

CCM ife hata leo, tuanze upya. Shida kubwa ya matatizo tunayokumbana nayo tanzania ni mfumo ambao CCM wameutengeneza.
 
Kifo cha nyani miti yote huteleza ndivyo ilivyo kwa utawala hakuna njia za kuzuia kuondoka madarakani.
-wakimpitisha Lowasa kuwa mgombea uraisi kupitia ccm UKAWA tunashinda asubuhi kabisa
-wasipompitisha Lowasa kugombea lazima ccm ipasuke vipande vipande kutokana na makundi .
CCM imeshavunja siku nyingi sana sema itamalizikia rasmi 12.07.2015
 
Lowasa hatiishi ccm kama unavyodai, ila amejua wezi wapo wengi wamejifa kwenye jina lake wakitaka kumtoa kafara, kama ccm ni chama makini kwanini lowasa hakufukuzwa uanachama?

CCM wote ni wezi, wanatafuta mtu wa kulinda wizi wao. Sitegemei kiongozi imara toka CCM kwasababu hakuna kiongozi anayeweza kuongoza system ambayo ni corrupt kutoka levels za juu hadi chini.
 
lowassa hawezi kuhama ccm...akienguliwa atakaa kimya....tatizo kubwa ni huyo mweyekiti wao..

CCM ambayo viongozi/wanachama matajiri walikuwa hawahami ni ile ya kabla ya 95-ile iliyomdhibiti Kolimba. CCM ya sasa inapungua nguvu, ndio maana viongozi wanaanzisha chama(CCJ) wakiwa bado ndani ya CCM. CCM ya zamani iliyokuwa na ubavu, Lowassa asingeanza 'kampeni' mapema kama anavyofanya, maana wanahitajika wadhamin 450, yeye ana laki 8, na anaendelea kuwakusanya. Ni kweli anawatishia CCM kuwa ana kundi kubwa nyuma yake, wasiwasi wangu ni kuwa ameshaanza kuamini kuwa kweli atashinda hata nje ya CCM. Vurugu zinaweza kutokea kwasababu kila mwanachama sasa ana sharubu kama ukoo wa Kambale. Heshima ya Mwenyekiti iliyokuwepo zamani, haipo tena. Naamini, bila kuwa na FFU nje ya ukumbi wa mikutano, si NEC wala Mkutano Mkuu utakaofanyika.
 
CCM usalama wao upo katika kuvua Gamba baada ya hapo watakua lmara sana kuwahi kutokea,

Tatizo liko kwa UKAWA kushindwa kutengeneza MoU mpaka sasa jinsi watakavyo gombea Urais na Ubunge na jinsi watakavyo gawana hicho watakachopata.

Replacement inatakiwa UKAWA watuthibitishie kama wako tayari siyo kukaa kimya kungoja CCM wamkate Lowasa na Mzee wa Makengeza.

Ukitazama katikati ya kauli ya Kinana wako tayari sasa kuvuana Magamba hilo halina shaka.
 
Nafunga na kuomba jina la Lowassa likatwe tuone mikwara yake itaishia wapi. Mtu mmoja fisadi na mwizi hawezi kutishia watu wazima kana kwamba chama ni chake.

Hatuwezi kuongozwa na rais fisadi.

Ccm kwa lowasa wanalo mwaka huu wakimkimbia mshale wakimchukua mkuki yaani wana boonge la soo waamue kukumbatia moto uwachome au wauzime upepo uueneze kwingine sijui watauzimaje.
 
Back
Top Bottom