Mkuu wangu nadhani wewe unatazam picha hii ukiwa ndani ya chama chako na kufanya mzaha ktk swala ambalo linatumaliza Watanzania wengi. Hizi habari za CCM sio mama yangu naweza kuachana nayo ni hadithi za Buricheka maana walioweza kuondoka wameondoka, lakini kama bado umo ndani basi una maslahi yako maana hakuna sifa yoyote ambayo inaweza kumwekla mwanaharakati ndani ya CCM.. Utanisamehe mkuu wangu ktk hilo..
Halafu kama wewe mwanachama wa CCM huwezi kuyaona nayozungumza kwa picha ile ile zaidi ya klutumia hiyo katiba ambayo mnaipanga wenyewe bila kumhusisha mwananchi hadi pale mtakapo taka NYIE ahusishwe. Na nazungumza haya yote sii kwa sababu ni Mwana Chadema bali mwanaharakati ambaye naitafuta haki ya wananchi kupitia vyombo hivi, hivyo sitazami hiyo katiba kitu ambacho hakipo leo nielndelee kutegemea labda kesho itakuwa bora zaidi.
Wazee wetu walipopigania Uhuru walikuwa ahadi nyingi tu, wakaahidiwa kupelekwa Ulaya na kupewa elimu, nyumba utadhani shetani alojmjaribu Yesu, lakini haikuweza badilisha nia zao. Wazee wetu waliambiwa tena ya kwamba - Watanzania bado hatupo tayari kuwa Huru na wakoloni walituwekea sera za kila aina kutonyesha wao wana nia nzuri na sisi lakini wazee wetu wakikataa katu na kusema - Tupeni nchini yetu na tutajikongoja vivyo hivyo.. Ndivyo navyoitazama Tanzania ya leo hatuhitaji maamuzi ya CCM hata kidogo bali sisi wananchi ndio wa kuwaambia CCM tunataka nini..
Chadema na CUF hawana sababu kabisa ya kuendelea kugombea chaguzi ndogo kama hizi wakati kuna chaguzi nyingi za nyuma wamepigwa chini, sasa waendelee tu kushiriki wakisubiri katiba?..Na kuna ushahidi gani hiyo katiba itawaletea mwongozo bora ambao utawawezesha wao kushinda. Mkuu wangu kupitia chama chako HAIWEZEKANI kabisa Chadema au chama kingine chochote kushinda kupitia sanduku la kura ikiwa katiba hiyo itaandikwa na wana CCM - HAIWEZEKANI labda kitafutwe chombo cha kimataifa kuifanya kazi hiyo maana najua fika majibu yake. Nasema sioni sababu kabisa ya vyama vya Upinzani kuendelea kugombea uchaguzi mdogo wakati wanatakiwa kuandaa mazingira ya uchaguzi wa 2015..Bora hata hao madktari waliogoma wameonyesha watu waliopania kuipata haki yao wenyewe.
Unapozungumzia CCM na kuharibu vyama vya Upinzani hii ni kawaida yake wala hawana wasiwasi maana waliweza kukivuruga NCCR lakini watu mnafikiria kwamba ni chama hicho kilichokuwa na matatizo.. Wameweza pia kukivuruga CUF na sasa hivi wanaitafuta Chadema hii inajulikana wazi wala haina ubishi kwani ktk mbinu zake mojawapo na kubwa ilotumika sana ni kuvunja nguvu ya chama mbadala cha ushindani. Na kwa bahati mbaya hawa vijana wa CCK mnaowasifia wameingia msikitini na mguu wa shoto. Haraka ya nini uda bado upo sana kufikia 2015, onyesheni uanaharakati wenu kwanza mpate kusifiwa na wananchi.
Na pengine huelewi maana ya Bad publicity is Good Publicy ni kama tunavyomsema Lowassa au Zitto. Ni kaa uweke tangazo baya linalouddhi watu lakini watu huitana kulitazama ili kesho libakie kichwani mwao na pengine hata waende KUNUNUA.. haina maana nje ya hiyo kama wanavyotaka CCK kujtangaza kana kwamba chama ni chao WAO na wao ni kina So and SO, heee! imekuwa bendi ya kizaire?.
Chama ni WANACHAMA unakitangaza chama ili upate wanachama wengi na through them ndipo chama kinajinadi kirahisi kutokana na mvuto huo. Kwenda kugombea Ubunge Arumeru haina kujitangaza bali unaingia ktk mashindano bila wachezaji afadhali hata wangekuwa miguu peku lakini wamekamilika.
Mkuu wangu kwa dalili hii inatuonyesha wazi kwamba CCK haikujiandaa kuchukua NCHI bali inadandia majimbo hapa na pale wapate KULA.. mabadiliko huanza na kuonyesha kivitendo yale unayoyalaani.. Kujenga UANAHARAKATI na kuzivuta mioyo ya watu washiriki nawe ktk vita dhidi ya utawala au vitu unavyopigania hata iwe UFISADI..lakini kuingia uchaguzi huku umebeba bango la Itikadi na sera mkuu wangu hii nisawa kabisa na kujidanganywa wao wenyewe.
Hata hivyo nawatakia kila la kheri ingawaje najua fika wameanza vibaya na pengine ndio utakuwa fundisho kwa vijana wadogo wanakurupukia siasa bila kujianda na vita nje ya sanduku la kura.
Diagnosis imeeleweka, sasa tunapata vipi tiba? Na je, mwanachama yoyote wa CCM, wa mjini na wa kijijini ni wa kulaumiwa kwa matatizo haya? Maana "nyie nyie" zimekuwa nyingi sana katika hoja zako. Je, wanachama wenye matumaini na CCM unawapa nafasi gani? Au ni malofa as long as wanabakia CCM? Usisahau kauli yako sahihi kwamba chama ni watu, sio mtu mmoja mmoja.
Una hoja nyingi za msingi lakini ile ya NCCR kwamba wameharibiwa na CCM sio kweli hata kidogo. NCCR ilimvuta hadi Wassira ambae isingekuwa awamu ya nne kumpitisha JK, wasira angekuwa NCCR mpaka kesho, kama sio kuhamia Chadema na kundi lote kama ilivyo ripotiwa. kwanini? alikuwa anatafuta madaraka. Na hiyo ndio sababu kuu ya wanasiasa wengine wote hata vyama vya siasa - kukamata madaraka, halafu ndio wajipange kutatua matatizo ya nchi. Mambo hayaendi hivyo kwani unaweza kujikuta unaingia ikulu kwa siasa za kubahatisha bahatisha na usikae madarakani kwa zaidi ya miaka mitano.
Kilichoiua NCCR ni haraka haraka, ambayo hata wewe unaizungumzia katika moja ya hoja zako kuu. NCCR waliwekeza kwenda Ikulu na wakaona Mrema ndio kete yao. Sababu unazotoa wewe za kuanguka wa NCCR zipo lakini ni secondary, vinginevyo ni jambo lisilokuwa na ubishi kwamba the primary reason to why NCCR ilianguka ni NCCR yenyewe - waliwekeza kwenye vitu vya muda mfupi kama vile personalities na vuvuzela la ufisadi, bila ya kujijenga ki-itikadi, ndio maana baada ya kushindwa uchaguzi, wakaishiwa hoja. Hili ni tatizo katika chama chako cha Chadema pia kwani hata Slaa miezi michache iliyopita, kwenye TV alitoa tamko la ajabu kidogo pale aliposema kazi yetu kubwa chadema ni kuikosoa serikali, na ikitokea ikajirekebisha, tutaishiwa hoja. Matamshi haya sio ya kutolewa na chama cha siasa, hasa chama kikuu cha upinzani, hizi ni hoja za pressure groups kama akina Mtikilia na wengineo, sio chama kikubwa cha siasa kama Chadema. Ndio maana Chadema pamoja na mafanikio yenu kadhaa, bado inawapa shida watu wengi kuona kwamba Chadema ndio mbadala wa kweli. Ni jambo lililo wazi kwamba hata miongoni ma vijana wasomi, wamegawanyika kuhusu Chadema. Msiendeshe siasa kama za pressure groups, endesheni siasa programmed, vinginevyo mtaishia kuilamu CCM kwa makosa mengine ambayo ni ya kwenu wenyewe.
Nikiwa bado kwenye suala la kuanguka kwa NCCR, haaingii akilini kwamba eti wasomi wote wale, kwa pamoja warubuniwe na wachotwe akili na CCM, how? Haijawahi kutokea wasomi wakubwa wa namna hii, kwa umoja wao, kushindwa na CCM na serikali yake katika mazingira ya siasa, kwani historia ya nchi yetu inatuelezea suala tofauti kabisa na hili.
Again, umetoa diagnosis nzuri lakini sijaona solution zaidi ya ile kwamba "CCM haiwezi angushwa kupitia sanduku la kura, unless waje international observers". Pia bado sioni kwanini CCK wasishiriki katika uchaguzi Arumeru, kwa dhana ile ile ya any publicity is good publicity. Inawezekana kabisa wasishinde lakini ni muhimu wakatumia haki yao chini ya sheria zilizopo, kwenda kujipatia uzoefu katika chaguzi zozote kabla ya mwaka 2015. Binafsi, sioni dhana ya haraka haraka katika hili kwani publicity na kuuza sera ni part ya kujijenga, na chaguzi hizi ndogo ndogo ndio the best platoform kufanikisha lengo hilo. Mimi nadhani hilo ndo lengo lao kuu, kwenda kuuza sera zao kwani matukio ya kampeni za wagombea wa Arumeru yata trickle down the whole nation.
Na je, Mwaka 2010, mtu angewaambia Chadema mna haraka sana msigombee Urais, jipangeni zaidi kwenye majimbo, kwa mtazamo wako hoja hiyo ingekuwa sahih? Kwani 2005, CCM ilishinda urais kwa 82%, na je bila ya kujaribu/kujipima mwaka 2010 mngeweza kweli kubaini nguvu yenu? Msiwaogope CCK, waacheni wafanya vitu vyao kwa jinsi wanavyojisikia wao ili mradi hawavunji sheria na taratibu zilizopo. Una hoja nyingi sana nzuri Mkuu Mkandara ambazo ungezipanga katika mazingira ya kuleta mjadala wa kisera na ki-itikadi kwa kuangalia je, vyama vya CCK, Chadema, CCM, CUF, NCCR, vinawapa watanzania varieties gani na nani yupo tofauti na kivipi n.k, hakika tungejifunza mengi sana. Pia nikuulize mkuu, leo hii ukienda kijijini kwenu na ukapata wasaa wa kuzungumza na vijana ambao hawana ufahamu wowote wa siasa lakini wangependa wachagua chama cha kujiunga au kukipigia kura, ungeitumiaje nafasi hiyo kuiuza Chadema/ungeiuzaje Chadema?