CCK yaingia Arusha kwa kishindo

CCK yaingia Arusha kwa kishindo

Soma hapa nadhani umekosea tu ulitaka kusema Ubepari au sio? Lakini maadam unasisitiza kuwa ufisadi umetokana na Uliberali naomba somo hapo kidogo..

Hivyo ndivyo nilimaanisha mkuu - ufisadi ni zao la uliberali/uliberali ndio chanzo kikuu cha ufisadi. Uliberali unakuja na vitu vikuu vitatu, hakuna kingine kikubwa nje ya hivi, na humo ndiko ufisadi revolves:
  1. Liberalization (ulegezaji wa masharti ya biashara ambao uliharibia viwanda vyetu soko la ndani, na ulianzia na mzee "RUKSA.")
  2. Marketization (ujio wa soko huria la kiholela lisilo na sheria za kulinda maslahi ya maskini.)
  3. Privatization (ubinaifisishaji wa mashirika yaliyojengwa kwa fedha za walipa kodi chini ya Mwl Nyerere).
I would call these kwa kifupi 'LIMP', each letter standing for each of the three enemies of maendeleo ya watanzania walio wengi. And as we know, LIMP means kiungo chenye ulemavu, ukosefu wa nguvu au something similar to that. Na kweli, vitu hivi vitatu vimetuletea janga la namna hiyo kiuchumi, kijamii na kisiasa. ​Nitarudi muda si mrefu kumalizia hoja yangu ya ufafanuzi.
 
Ni sawa na kuuliza, hivi Chadema ni zao la Mtei mwana Tanu na Mwana CCM aliyemkimbia nyerere na azimio la arusha na kwenda washington kujipanga akiwa mtumishi wa IMF na kuja kuanzisha Chadema? Chadema ni zao la CCM zaidi ya CCK kwa maana ya kwamba vijana wa CCK hawakuwahi kuwa wanachama watiiifu wa CCM kama Mzee Mtei, Bob Makani, Dr. Slaa, na pengine vijaa wengi wa CCK hata hawajawahi kuwa wanachama wa CCM. Nia yangu hapa ni kukuonyesha kwamba hoja yako haina mashiko kwani kama ni suala la original sin i.e. CCM, basi hakuna upinzani Tanzania.
Hapana Mchambuzi, hapo unakosea. Tulikuwapo wengi ambao tukiwa vijana, tuliamini kweli kweli katika harakati zilizotuwezesha kupata uhuru zilizoongozwa na Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere kupitia chama cha TANU. Tofauti yangu na vijana wa wakati huo ni kuwa nilikuwa na mawazo ya demokrasia iliyopanuka zaidi na niliamini katika ile philosophy ya uhuru wa mawazo. Huo uhuru ulitufanya wengi tuishi kama watoto yatima ndani ya nchi huru, hasa baada ya tarehe 10 Julai mwaka 1965, ila tuliishi kwa tumaini kuwa iko siku milango itafunguliwa.

Hadi sasa naamini kuwa watu hata kama wanashirikiana pamoja hawawezi kuwa na mawazo yanayofanana muda wote na lazima waizoee ile hali ya kutofautiana kwa kupingana bila kupigana. Huo msimamo wangu ulinifanya nisijiunge na TANU ingawaje sikuweza kufikia hatua ya kuitwa mpinzani ila niliamini nisingeweza kuwa huru nikiwa mwanachama mwenye kadi. Siku zilivyosogea ndivyo moyo wangu ulivyozidi kuwa mgumu kwa sababu hali ilijengeka ambayo iliiminya kwa kiasi fulani nafasi ya uvumilivu kwa mawazo pingamizi ndani ya chama tawala.

Mkuu Mchambuzi naomba nisikuchoshe kwa hadithi ndefu ila ni kwamba hadi dakika ya leo sijawahi kujiunga rasmi na chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania. Mwaka 1992 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa, kidogo nivutiwe na chama cha NCCR-Mageuzi hadi siku ilee, ilipompokea Lyatonga Mrema kutoka CCM na kumkabidhi uongozi wa chama! Nilihuzunika, nililia na nilikata tamaa na kugundua kwamba kumbe nchi hii watu wanalilia mfumo wa vyama vingi lakini hawako tayari kusota na kujitoa mhanga kupanda, kupalilia na kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Mkuu Mchambuzi, bado tupo, tunaoielewa sana siasa ya nchi hii tulikotoka, tulipo na tunapoelekea kama tutazidi kuulea mfumo ule ule na watu wale wale! Tutapiga hatua pale tu Chama kile kile kilichotufikisha hapa, kitakapowekwa benchi na chenyewe kiwe mtazamaji wakati timu mpya inaingia uwanjani. Nina hakika ni hapo tu CCM itakapoweza kuona makosa yake na kujifunza mengi kama itabahatika kwa mara nyingine ya kukamata madaraka. Kwa sasa CCM ni mahututi na ni wakati muafaka itolewe nje na mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake.
Kama hadi dakika hii bado uko CCM, wewe ni kisiki katika harakati za kujikwamua kitaifa.
 
Soma hapa nadhani umekosea tu ulitaka kusema Ubepari au sio? Lakini maadam unasisitiza kuwa ufisadi umetokana na Uliberali naomba somo hapo kidogo..

Maadam hapo awali nimeshakueleza kwamba uliberali una vitu vikuu vitatu ambavyo ni Liberalization, Marketisation na Privatization, na pia nikaelezea kidogo uhusiano wa vitu hivi na ufisadi, nitajikita zaidi kwenye mifano kadhaa kuboresha hoja yangu kuhusu uhusiano baina ya ulibepari na ufisadi. Kabla sijaenda mbali, ni muhimu niseme kwamba, pamoja na umhimu wa vitu hivi katika Maendeleo ya uchumi, viongozi wetu wamechangia sana kufanya uwepo am ujio wa uliberali kuwa na madhara kuliko faida kwa wananchi walio wengi. Uliberali umekuwa ni chaka kubwa la viongozi wetu kujinufaisha binafsi kwa njia za ten percent na pia kuruhusu mikataba isiyokuwa na maslahi kwa watanzania walio wengi. Viongozi wetu walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuhakikisha uliberali unaleta faida kuliko hasara, hasa kwa kusimamia maslahi ya taifa wakati wa majadiliano/mashauriano mbalimbali na wawekezaji n.k.

Wakati tunapata uhuru (1961), mataifa makubwa yaliyotutawala walituambia kuwa sisi ni maskini kwa sababu tuna ardhi, rasilimali na nguvu kazi, lakini hatuna tekinolojia na mtaji. Hivyo, ili tuendelee, tunahitaji mitaji na tekinolojia kutoka nje, na pia mikopo ili serikali yetu iweze kuendesha shughuli mbalimbali, hasa kilimo. Lakini lengo walitaka tuendelee kuzalish mazao kwa ajili yao. Mwalimu alifuata maagizao haya kwa kuwa hakuwa na jinsi, kwani taifa lilikuwa bado changa na liliwahitaji wakubwa hawa. Lakini baadae (1967), Mwalimu akaona bila ya sisi kujitambua kama taifa, tutabakia kuwa taifa tegemezi. Hivyo akaja na mkakati wa kujenga viwanda, ili visaidiane na kilimo kujenga uchumi. Wakubwa wan je hawakupenda hili. Lakini ilibidi wampe sifa Nyerere kwa kujenga viwanda vingi muhimu, hasa vya ngozi, food processing, nguo, na sekta ya mafuta (TPDC), kwa kutumia zaidi rasilimali za ndani (fedha za walipa kodi), kuliko misaada/mikopo kutoka nje.

Uchumi ulipotetereka miaka ya mwisho ya sabini-mwanzo ya themanini, Mwalimu alichotaka toka kwa IMF ni bail out ili kuokoa viwanda vytetu na pia kilimo, bail out kama ile ya Ureno, Ugiriki, Marekani, n.k miaka ya sasa. Nyerere alijitahidi sana kujenga hoja kwamba tunachohitaji ni bail out, lakini Mzee Mtei (mwasisi wa Chadema), ambae aliegemea upande wa IMF, akapingana na hoja hiyo. Badala yake, IMF wakaja na kauli mbiu ile ile ya wakati wa uhuru - mna ardhi, rasilimali, na nguvu kazi lakini hamna mitaji na tekinolojia, hivyo fungueni uchumi wenu ili mpate mambo haya. Na mbaya zaidi ni kwamba, hata nchi wahisani nao wakaegemea kwa IMF na kuanzia wakati ule mpaka sasa, hawatoi mkopo/misaada wowote bila ya IMF na WorldBank kutoa ruksa. Hivyo, ili kupata misaada ya nje, IMF na WorldBank wakatupa masharti kama vile serikali kuachana na viwanda, na badala yake, kurudi kwenye kilimo cha enzi ya mkoloni.

Uliberali umepelekea viwanda vyetu vingi kufa au kuuzwa, hata vile vilivyokuwa vinatengeneza faida kubwa, vinalipa kodi, vinatoa ajira kwa watanzania – vya nguo, ngozi, oil sector (TPDC), food processing n.k, tena hivi vikawa vya kwanza kuathirika. Kuna makala moja ya profesa Shivji inaeleza kwa mfano kwamba, mashamba ya mikonge yaliuzwa kwa bei ya chini ya senti hamsini za dollar kwa heka moja katika miaka ya tisini! Leo, hii ni sawa na shillingi 750 za kitanzania kwa heka. Haya yote ni zao la uliberali. Badala ya uliberali kuleta faida kwa taifa, viongozi wameutumia kupata faida zao binafsi kupitia ten percent.

Bado serikali yetu, kupitia Tanzania Investment Centre inazidi kukumbatia ulibepari na masharti yake, ambayo yanachochea ufisadi na wizi wa mali za watanzania. TIC inaruhusu wawekezaji waje kutengeneza faida za haraka, tena kwa dhuluma, huku ubepari katika nchi yetu ukiendelea kuwa juu ya sheria za nchi. Wawekezaji hawa wanalenga zaidi rasilimali na ecology yetu ambayo bado ni ‘virgin', ambayo Nyerere alihimiza iachwe mpaka watanzania wenyewe watakapokuwa tayari kuitumia kwa faida yao wenyewe. Kwa mfano, chini ya ulinzi wa TIC, wawekezaji wanaingia kwenye sekta ya madini na kupewa umiliki wa asilimia mia moja na hawalipi kodi; wanapewa vibali vya kuiba ndege na wanyama wetu; wanapewa vibali vya kukata miti ovyo na kusafirisha magogo kwenda nje. Serikali haiweki mkazo kwa wawekezaji kwenda kuwekeza kwenye sekta muhimu kwa taifa, kama viwanda, ambavyo vingesaidia kutoa ajira kwa vijana na pia kuwapatia wakulima masoko - malighafi kama vile ngozi, mazao ya kilimo, n.k ambayo yangehitajika kwa ajili ya uzalishaji viwandani.

Mwekezaji anapata Baraka za TIC kwenda kupora ardhi kwa ndugu zetu wa kimaasai chini ya uwekezaji wa ‘ranch'. Anaweka ulinzi katika ardhi ile, na kutulia na bunduki zake kusubiria kuua watanzania watakapia eneo lile na mifugo yao, kwani watanzania hawa wanamvurugia shughuli yake ya kusubiria wanyama wetu wa porini wapite katika maeneo yale wakati wa misimu husika, kisha yeye na washirika wake kuwapiga risasi ovyo ovyo tu, kwa ajili ya kuwasafirisha nje kama nyama na ngozi.
Misituni nako, mbali ya kukata magogo na kupelekea nje kwa ridhaa ya serikali chini ya TIC, wawekezaji wanatumia nafasi hiyo pia to exploit bio diversity yetu - wanabeba ‘our exotic plants' na mbegu, halafu wanaenda kuzifanyia genetic engineering na kisha kuziwekea patent. Vizazi vyetu vya baadae vikija hitaji mbegu hizo, inabidi walipie patent, kwa mimea ambayo kwa asili ilikuwa ni mimea yao.

Pia suala la fedha chafu – tunashuhudia jinsi gani TIC inavyotoa vibali kwa makasino yanayoshamiri kila kona ya majiji yetu. Pia tunashuhudia jinsi gani maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yanavyoshamiri katika miji yetu kupitia mlango wa kulegeza masharti ya biashara kwenye sekta ya fedha. Shughuli hizi ndio vichaka vikubwa vya ufisadi, ambapo majizi ya mali ya umma na pia wawekezaji majizi ambao hawalipi kodi ndio wanaowapa faida kubwa wamiliki hawa wa hizi kasino, faida ambazo nyingi hutoroshwa nje ya nchi.

Matatizo yote haya ni matokeo wa uliberali ambao umeachiwa na serikali ufanye utakavyo, na uishi juu ya sheria. Ubepari sasa upo juu ya sheria na umechafuliwa na ufiadi, na kupelekea watanzania wengi kuuchukia kwa makosa, kwani mafisadi ndio hujificha humo, huku serikali ikijikita zaidi kusafisha ufisadi badala ya kusafisha ubepari uliochafuliwa na ufisadi. Uliberali ni janga kubwa sana kwa taifa letu kiuchumi na kijamii, na vyama vyote vinavyo unga mkono uliberali ki-itikadi – CCM, Chadema, na CUF, vina wajibu mkubwa sana wa kuwaeleza wananchi kulikoni?
 
Hapana Mchambuzi, hapo unakosea. Tulikuwapo wengi ambao tukiwa vijana, tuliamini kweli kweli katika harakati zilizotuwezesha kupata uhuru zilizoongozwa na Baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere kupitia chama cha TANU. Tofauti yangu na vijana wa wakati huo ni kuwa nilikuwa na mawazo ya demokrasia iliyopanuka zaidi na niliamini katika ile philosophy ya uhuru wa mawazo. Huo uhuru ulitufanya wengi tuishi kama watoto yatima ndani ya nchi huru, hasa baada ya tarehe 10 Julai mwaka 1965, ila tuliishi kwa tumaini kuwa iko siku milango itafunguliwa.

Hadi sasa naamini kuwa watu hata kama wanashirikiana pamoja hawawezi kuwa na mawazo yanayofanana muda wote na lazima waizoee ile hali ya kutofautiana kwa kupingana bila kupigana. Huo msimamo wangu ulinifanya nisijiunge na TANU ingawaje sikuweza kufikia hatua ya kuitwa mpinzani ila niliamini nisingeweza kuwa huru nikiwa mwanachama mwenye kadi. Siku zilivyosogea ndivyo moyo wangu ulivyozidi kuwa mgumu kwa sababu hali ilijengeka ambayo iliiminya kwa kiasi fulani nafasi ya uvumilivu kwa mawazo pingamizi ndani ya chama tawala.

Mkuu Mchambuzi naomba nisikuchoshe kwa hadithi ndefu ila ni kwamba hadi dakika ya leo sijawahi kujiunga rasmi na chama chochote cha kisiasa hapa Tanzania. Mwaka 1992 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa, kidogo nivutiwe na chama cha NCCR-Mageuzi hadi siku ilee, ilipompokea Lyatonga Mrema kutoka CCM na kumkabidhi uongozi wa chama! Nilihuzunika, nililia na nilikata tamaa na kugundua kwamba kumbe nchi hii watu wanalilia mfumo wa vyama vingi lakini hawako tayari kusota na kujitoa mhanga kupanda, kupalilia na kukuza demokrasia ya vyama vingi.

Mkuu Mchambuzi, bado tupo, tunaoielewa sana siasa ya nchi hii tulikotoka, tulipo na tunapoelekea kama tutazidi kuulea mfumo ule ule na watu wale wale! Tutapiga hatua pale tu Chama kile kile kilichotufikisha hapa, kitakapowekwa benchi na chenyewe kiwe mtazamaji wakati timu mpya inaingia uwanjani. Nina hakika ni hapo tu CCM itakapoweza kuona makosa yake na kujifunza mengi kama itabahatika kwa mara nyingine ya kukamata madaraka. Kwa sasa CCM ni mahututi na ni wakati muafaka itolewe nje na mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake.
Kama hadi dakika hii bado uko CCM, wewe ni kisiki katika harakati za kujikwamua kitaifa.

Nimeielewa vizuri sana hoja yako na kimsingi kukubaliana na wewe. Jibu langu kwa "smartboy" lililenga suala hilo hilo unalolizungumza - kwamba sio kila mtu ambae amewahi kuwa mwanachama wa CCM au kitu kinachokaribiana na hilo, basi mtu huyo akihamia chama kingine au akianzisha chama chake, basi ni mamluki wa CCM. Akitanda wa CCK na Dr. Slaa kwa mfano wana utofauti gani? Wote ni wapinzani, na Dr. Slaa ilitakiwa aonekane ni mamluki zaidi kwani alikuwa ni Mbunge wa CCM na alipishana na CCM pale tu alipohujumiwa kwenye kura za maoni. Lakini kuhama kwake pengine ilikuwa ndio wakati muafaka wa yeye kuamua kusonga mbele baada ya kuvumilia siasa uchwara za CCM. Hivyo ndivyo inatakuwa Dr. Slaa aheshimiwe, na hata Akitanda na mtu yeyote mwingine ambae alikuwa na mahusiano na watu wa CCM. Vinginevyo tukiruhusu hoja za ovyo ovyo kuhusu chama hiki kuwa mamluki wa chama kile, sana sana anaefaidika ni CCM. Hoja kama hizi hazitakiwi kupewa nafasi. Vyama vishindane kwa hoja zinazotokana na itikadi. Hivyo ndivyo kwa pamoja tutajenga upinzani wa kweli na wenye manufaa kwa watanzania.

Na kuhusu kauli yako hii:

"Kama hadi dakika hii bado uko CCM, wewe ni kisiki katika harakati za kujikwamua kitaifa."

Sijakupata sawa sawa licha ya kujaribu kufanya hivyo lakini pengine niseme tu kwamba mimi sio kiongozi wa aina yoyote wa CCM ni mwanachama tu ambae nina amini kwamba kokosoana na kukosolewa ni silaha ya mapinduzi. Na kama umekuwa unanifuatilia, nimekuwa natoa mawazo yangu mengi tu kama raia aliye na uhuru wa kufanya hivyo, yanayoelezea kusumbuliwa kwangu na hali mbaya ya nchi yetu katika nyakati hizi, hasa udhaifu wa kisera, ki uongozi n.k. Unless maana yako ni kwamba sitakiwi kukosoa chama changu bali nibakie kuwa sehemu ya tatizo? Au kuikosoa CCM haina maana kama bado nipo humo kama mwanachama na kwamba kuna maana zaidi kuikosoa ccm ukiwa nje ya chama, hasa ukiwa mwanachama wa chama kingine? Kwa kweli sijakuelewa, unless kwa ufahamu wako, mimi ni kiongozi ndani ya CCM.
 
<<<<<<<<ala! hata wewe! hivi nimekutisha mkuu? kama ni nia njema fanya kazi ya kuwakomboa waTanzania na utaungwa mkono tu, hata mimi niliyeumia moyo nisipowakubali mtajitahidi kutenda mema na mtapata wengine wengi tu na huenda siku moja majeruhi akapona akashika japo kisu kama hatakuwa na uwezo wa kushika AK 47.

Tunajituma na tutaendelea kujituma kwa moyo mmoja! si vyema kuweka maneno mengi matamu humu! Lakini Nawahakikishieni ya kwamba CCK imeanza kazi ya kujenga chama na kukipeleka kwa wananchi, hilo ndilo muhimu kwetu, haijalishi tunaingia bungeni leo au kesho, muhimu kwetu ni kuweka misingi mizuri itakayowezesha taifa kwenda mbele huku Watanzania wakiifurahia nchi yao
 
tumeichoka CDM,issue ya katiba ndo ilonifanya nikate tamaa na hawa wafanyabiashara wa siasa wa CDM,kwenda ikulu wakahongwa na kurudi bungeni kupitisha madudu yale waloyapinga mwanzo???? nini hii?? afadhali CCK ije arusha

Haujambo lakini ......?
 
Watu wa CDM wangekuwa wanachangamka kujenga ushiriiano na chama hicho kidogo...
wewe umewasahau kwa vizungu vyao "who are they by the way?". CDM mara nyingi wanajiona kuwa wao ndiyo King makers, Play makers na ndiyo Play masters wa mchezo wa upinzani Tanzania. Kuwashauri inatakiwa kuwa na moyo wa chuma na uvumilivu unaozidi chungu kwenye moto!!
CDM ni chama kinachopanuka (siyo kukua) kwa kasi sana lakini kinakosa Oganaizesheni makini kwa wakati sahihi. Sasa hivi vurugu kubwa ni nani atakuwa nani baada ya 2015. Hivi Sekretarieti ya CDM inafanya uchambuzi wa kina muelekeo wa chama dhidi ya vyama vingine!!
 
Umeongea jambo la msingi sana maana Akitanda anajua niliumizwa na nilipambana sana, na anajua sina tatizo naye lakini ameingia nyumbani kwa mpambanaji mwenzake bila hata kumtaarifu, si hata angenisms kama kweli anajua mchango wangu mzuri?
Aje na safu ya wapambanaji tumpe saport, unajua ukitaka kufanikiwa usidharau mchango wa mtu aliowahi kuutoa hata kama ni kidogo, hasa ukiwa eneo la nyumbani kwake maana anaweza kufikiri una ajenda ya siri..:A S 465:

Paul Mafie, na wadau wote wa JF, nawahakikishieni kuwa sina tatizo lolote na Paul Mafie, ni bahati mbaya sana Naibu Katibu Mkuu wetu Bara ndiye aliyeshughulikia suala la uongozi mp[ya mkoani arusha alikuwa hukom kwa muda wa wiki moja. sina tatizo na Paul na alinikaribisha vizuri sana enzi za CCJ, namkubali ni mpambanaje mzuri, ila Paul alitukimbia wakati mambo yakiwa magumu, katika siasa tegemea milima na mabonde, simlaumu maana ni mimi niliyewaelekeza wafuasi wa CCj kote nchini kuelekeza nguvu CDM kwa ajili ya uchaguzi wa 2010, ila nashangaa leo mashambulizi mazito dhidi ya CCk yatoke kwa watu tuliokuwa nao. Ninakwenda Arusha wiki ijayo nitazungumza na wana Arusha kazi yetu kubwa ni kujenga siyo kubomoa. Tumesajili CCk katika mazingira magumu sana labda ni Mungu pekee anajua, nilinusurika kufa kwenye ajali ya Spice Icelanders nikiwa naelekea Pemba kufanya uhakiki wa CCK, inaniuma sana, kama kweli ningekuwa nimetumwa na magamba kama wengine wanavyojinasibu nadhani wangenipandisha ndege! Lakini yote namwachia Mungu.

Ninachokiona ni kwamba watanzania wanahitaji mabadiliko ya haraka wamechoshwa na CCm kama mimi na wanachama wa CCK kote tulikopita, suala la kuelekeza lawama kwetu kwanini tumesajili chama kipya hiyo si hoja tena, walipaswa watuhoji tukiwa na usajili wa kudumu. naomba ifahamike kwamba CCK ni chama halali kwa mujibu wa sheria na sasa kinaanza rasmi kutoa mchango kwenye taifa letu, usipotuunga wewe mwana JF wako wanaotuelewa.

Paul ni rafiki yangu, sitamsahau, sitamsahau pia Kandoro aliyekuwa mwanafunzi wa High school lakini alijitoa mstari wa mbele. Mimi Akitanda, sina ubaya na chama chochote cha upinzani pia hata CCK hatuna ubaya na chama chiochote, tumesema wazi wazi kwamba mbaya wetu ni CCM, chama hiki kimeendelea kutesa Watanzania kwa kuwapiga mijeledi ya hadharani pasipo sababu za msingi, tunasema hapana, kuna matatizo makubwa sana hii leo, hayajazungumzwa na kama hatuchukui hatuia madhubuti nchi inaingia kwenye matatizo makubwa mno, si kiuchumi tu, bali hata kisiasa na kijamii. Mashambulizi tuliyoyaona humu JF dhidi yetu hayakustahili kabisa sisi ni Watanzania. Hatuombi huruma kwenu bali tunataka mtuelewe, lakini si lazima mtuelewe polepole mtajua tunasimamia nini. Safu ya uongozi wa kitaifa wiki ijayo itakuwa hadharani na tunaahidi kazi moja tu, nayo ukombozi..

Naomba kuwasilisha.

CCK-Mwenyekiti wa Muda
 
Kwa wana JF, mapokeo yetu humo JF kwa kifupi hayakuwa mazuri, wengi wametutusi, wengine kutukejeli na mambo mengi ya mzaha, lakini kumbukeni mzaha wenu ni mauti kwa wengi ambao hawapati fursa ya kuingia na kuona haya. Tunaelekea vijijini waliko wapiga kura na kuwaeleza kilichotkusajili chama. Kwa kifupi Tanzania mnayoifahamu si hii ya leo, nchi imeliwa na inakwisha, wakati wengi wenu mkitutukana, walaji wanashangilia lakini wazungu wanasema "END JUSTFIES THE MEANS" Kwaherini
 
Mchambuzi,
Mkuu wangu kusema kweli hapo ndio umenipeleka nje kabisa maana nijuavyo mimi ni kwamba Dunia hii na hasa ktk tawala tulikuwa tukitawaliwa na sheria za DINI au MILA ambazo ndizo zilizotujenga ktk makundi ya Utaifa au jamii fulani. Na Uliberali ni mtazamo ulokuja kupingana na dhana ya kwamba binadamu anatakiwa kufuata AMRI ya imani fulani au mila fulani ambazo baadhi yake zinapuuza haki za binadamu na kwamba sisi binadamu wote sawa and we can govern ourselves ktk ku exercise freedom and rights of individuals..Na sisi Conservative tunaamini ktk sheria na amri tangulizi ambazo ndizo zilizotujenga sisi kama binadamu wa Kimataifa na hizi imani za dini, Mila na Tamaduni ndizo mwongozo wetu ni lazima kuenziwa japokuwa zipo sheria na mila mbaya zilizopitwa na wakati zinaweza kuondolewa lakini sio zile zilizotutambulisha sisi ni watu gani...

Sasa unaposema Uliberali unahusiana na Ufisadi kusema kweli kidogo inanipa shida maana ktk ushindani baina ya Uliberali na Uhafidhina tunafungwa wote na Ubepari kama ndio njia pekee ya kujiendeleza kiuchumi, mfumo ambao ndio shina la Ufisadi na wote tumeshindwa kuja na njia mbadala ambazo zinaweza kuendesha Ubepari bila kuathiri uchumi wenyewe ama maisha ya wananchi wanaotumikia Ubepari huo. Hivyo, ukinambia Ubepari ndio hukaribisha Ufisadi nitakuelewa lakini hii ya Liberali kusema kweli nimegota, pengine mimi ndio sijui hasa maana ya Uliberali hutumia tu neno hili bila uelewa maana yake na ndio maana nimetoka mtupu..
 
Constantine, usikate tamaa hata kidogo. JF ni tanuru kali la moto ukipita hapa na kusalimika basi wewe imara. Angalia pm yako.
 
Mkuu,
Upo sahihi kabisa, tunapopishana ni sehemu ndogo sana, nipe masaa machache nitulie ili nifafanue zaidi nina maana gani ili unielewe.
 
Ndoto za alinacha,ni maneno ya kanga hayaumizi kichwa,mdomo mali yenu mnaweza kuongea sana bila kujua namna ya kutimiza...karibuni kwenye siasa.Nadhani kuna vigogo toka CCM mnawasubiri.
 
Hivi hawa CCK ni tofauti na CCJ ya akina Mpendazoe?

No differences,slightly difference we can observe in their name,instead of CCJ they just omit the letter J and then replace with K...but the founders are the same except Mpendazoe...again the issue of constitution is the same,policies and vision are the same.I think there are some people behind this movement,I guess Bro Nepi na mzee six.
 
Back
Top Bottom