CCK yaingia Arusha kwa kishindo

CCK yaingia Arusha kwa kishindo

@Mchambuzi

Hiyo haraka haraka na pupa kwa vyama vya upinzani ni kweli..

Wasomi wetu ni watu wenye kukataa tamaa mapema katika mapambano..mfano wale waliokuwa NCCR

Ndio maana mimi nawahusudu CUF kwani ni wavumilivu sana na wanaenda taratibu na kujenga taasisi yenye msimamo,

Sijui siku kina Lipumba wakikaa pembeni CUF itakuwaje? lakini hadi sasa ndio chama kinachojenga taasisi bila pupa

Sera zao ziko clear na wanasimamia hoja zinazoeleweka...chadema mmmm! (too much fantasy)
 
Mchambuzi,
Mkuu wangu hata Hitler alikuwa na wafuasi na alijenga kwanza wanachama wa NAZI na jeshi kubwa kisha ndio akaingia vitani. Kwa hiyo CCM kuwa na wanachama hilo ni given lazima wawepo na sisi sote tumetoka humo.. Lakini waliobakia bado wana mtazamo ule ule na ndio maana nimekwambia wewe unatazama ukiwa ndani ya chama huwezi yaona ya nje mkuu wangu.

Watu wote wanaotetea CCM wanafaidika kwa njia moja ama nyingine na wengine hawana jinsi kama utawala wa Julius Kaizali..Lakini kuwa ndani ya CCM halafu unazungumzia Uanaharakati hapo ndipo napowapinga kwa sababu huwezi ku serve two masters..Tuyaache haya na nakuomba tena samahani - Kuwepo kwako CCM pengine kunaweza wabadilisha chama au nchi lakini navyoamini mimi haiwezekani na ndio maana mnaona kwamba Ufisadi is not an issue!..

Nimeandika mengi sana hapo juu kama ushauri tu sema lugha yangu ndio huwa nzito kiasi kwamba hata mwenyewe naporudia kusoma wakati mwingine husema Duh mkandara punguza Jazba.. lakini ndio hivyo nina uchungu sana na nchi yangu na sioni mabadiliko wala ukombozi..
 
Nchi ngumu hii ukiwa na uchungu sana watakwambia unataka urais
 
Kuwepo kwako CCM pengine kunaweza wabadilisha chama au nchi lakini navyoamini mimi haiwezekani na ndio maana mnaona kwamba Ufisadi is not an issue!..

Ufisadi is an issue lakini utatuzi wake sio wa kukata matawi bali kuitoa mizizi. Sio Chadema, wala CCM wanaojitambulisha kama wapiganaji, wana mikakati ya kweli ya kutoa mizizi hii kwani wanasahau kwamba itikadi wanazotekeleza - uliberali ndio chanzo kikuu cha ufisadi. Utang'ang'aniaje kupigana na ufisadi wakati hata wewe kama chama unajiendesha kifisadi? Ruzuku za vyama vya siasa ni ufisadi mtupu, na wanaotoa hizo fedha ni hao hao wanao hubiri faida za ulibepari na upanuzi wa demokrasia. Hivi unajua kwamba vyama vikubwa vya siasa vinavyopata ruzuku havitaki kabisa habari ya CAG kwenda kukagua mahesabu yao kwani watagundulika kumbe na wao ni vinara wa ufisadi? Ufisadi ni tatizo kubwa lakini ni la kimfumo, sio la kulipinga majukwaani with a wrong diagnosis.

Vinginevyo uchungu wako kwa nchi yako huwa nauona siku zote, na nina amini kabisa una uzalendo mkubwa sana kwa nchi yako. Nadhani inapotokeaga kwamba tuna tofautiana, ni juu ya njia ya kufikia ukombozi.
 
Baada ya kukamilisha safu ya uongozi wa mkoa wa Arusha,CCK inatangaza rasmi kuwa tunaingia katika uchaguzi mdogo wa Arumeru kwa ajili ya kuchukua jimbo.
Mbona heading ya uzi wako haiendani na body?? nilidhani wamefanya mkutano mkubwa na kuzoa wanachama wengi kumbe ni maneno tu??
 
@mkandara

Embu Tuache wananchi tupate burudani na mawazo mapya na CCK..

Unajua Chadema tumeshaanza kuchoka na wengine hata mtufanyeje hatuwaamini tena chadema??

Toka lini Topical akawa Chadema? halafu watu kama Topical wakiendelea kuchangia upande wa CCK wataharibu maana itaonekana ni ccmB. maana wanajulikana, acheni CCK wajieleze wamejipanga vipi?
 
Mkubwa mwenzao lakini wa huku mkoani Arusha, nawachukia watu wanaojaribu kina cha maji kwa kidole! watu wanaojiingiza kwenye siasa kwa madhumuni ya tumbo kwanza kabla ya kuangalia maslahi ya Taifa. :A S-confused1:

Huu ni unafiki mkubwa, maneno yako hayana msingi, wewe kama uliwasaidia hao waliokuwa viongozi wa ccj so what? CCK has nothing to do with CCJ, unaonekana hata ukilala na mwanamke ukagundua anakasoro au hukumpenda ndiyo lazima kesho ukamtangaze? tumia akili hao waliokubomu pesa unajuana nao wewe usitutishie!
 
Hivi hii cck ndo zao la ccj ile ya nape,sitta na mpendazoe?
 
Ni sawa na kuuliza, hivi Chadema ni zao la Mtei mwana Tanu na Mwana CCM aliyemkimbia nyerere na azimio la arusha na kwenda washington kujipanga akiwa mtumishi wa IMF na kuja kuanzisha Chadema? Chadema ni zao la CCM zaidi ya CCK kwa maana ya kwamba vijana wa CCK hawakuwahi kuwa wanachama watiiifu wa CCM kama Mzee Mtei, Bob Makani, Dr. Slaa, na pengine vijaa wengi wa CCK hata hawajawahi kuwa wanachama wa CCM. Nia yangu hapa ni kukuonyesha kwamba hoja yako haina mashiko kwani kama ni suala la original sin i.e. CCM, basi hakuna upinzani Tanzania.
 
Mchambuzi,
Nakubaliana nawe lakini mahala pamoja tu uliposema "Ubepari ni zao la Uliberali unaweza kunifafanulia hapo?"
 
Huu ni unafiki mkubwa, maneno yako hayana msingi, wewe kama uliwasaidia hao waliokuwa viongozi wa ccj so what? CCK has nothing to do with CCJ, unaonekana hata ukilala na mwanamke ukagundua anakasoro au hukumpenda ndiyo lazima kesho ukamtangaze? tumia akili hao waliokubomu pesa unajuana nao wewe usitutishie!

<<<<<<<<ala! hata wewe! hivi nimekutisha mkuu? kama ni nia njema fanya kazi ya kuwakomboa waTanzania na utaungwa mkono tu, hata mimi niliyeumia moyo nisipowakubali mtajitahidi kutenda mema na mtapata wengine wengi tu na huenda siku moja majeruhi akapona akashika japo kisu kama hatakuwa na uwezo wa kushika AK 47.
 
Constantine Akitanda na Mafie PM,

Sasa wakuu zangu mkianza nyie wenyewe kugombana hata chama hajifika mahala kweli kuna usalama. Kwa nini msikae mkayazungumzia yale yaliyopita, mkajifunza makosa kisha mkaendelea mbele maana navyomsoma mimi Mafie anaonyesha hana imani na baadhi ya watu na pengine hao watu wamo pia CCK..kutoka Chama cha Jamii kwenda chama cha Kijamii hakuna tofauti kwa mwenye kusoma alama za wakati.

La muhimu wekeni majina ya viongozi wenu wanachama ambao mnataka kuwanadi kwa wananchi baadaye. Kujificha ya nini kama kweli mnayo nia njema maana uchaguzi Tanzania jamani sii lelemama ni mchakato unaoanza na Wahusika hizi sera na Itikadi ni kachumbari tu kukoleza pilau. Tupeni list ya uongozi watu wengine wabebe ndizi wakijua kuna pilau la nguvu..
 
Mchambuzi,
Nakubaliana nawe lakini mahala pamoja tu uliposema "Ubepari ni zao la Uliberali unaweza kunifafanulia hapo?"

Sikumbuki kusema kwamba ubepari ni zao la uliberali kwani hii sio sahihi. Ili uliberali utekelezeke, ni lazima pawe na ubepari. Nilimaanisha ufisadi ni zao la uliberali. Je ulimaanisha kuuliza ufafanuzi kuhusu uhusiano wa uliberali na ufisadi?
 
Bwana mkubwa hawa watu kama kiongozi wao ni huyo Akitanda Constantine namfahamu sana na ni mtu makini sana labda kama kwa hizi siku chache kabadilika , nampenda ni kijana mpambanaji na mwadilifu sana, mgogoro wangu na wao uko kwa huko nyuma tulipotoka CCj tulikuwa na viongozi wa kitaifa matapeli ila yeye wakati huo alikuwa katibu mwenezi, alifanya kazi nzuri sana ila kuna uzembe mkubwa ulikuwepo awali, kama atakuwa na safu nzuri ya uongozi naamini baadaye chama chake baada ya Chadema kitafuatia. maana ccm,tlp,tadea,nccr,udp cuf aka KAFU na majina mengine yafananayo na hayo tutavisahau soon. ilmradi tu wasiwe ccmB. au wakawa wametumwa kuharibu, ila kama wako serious nina imani na Akitanda baada ya kukuta yupo. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Akitanda ni mtu makini sana iwapo ataungana na wapambanaji wenzake akina Willbrod Slaa,Mbowe,Lema ,Mdee,Mnyika,Kabwe, Ndessa na wengine kama hao ambao hupatikana Chadema.:welcome:
Sasa kuwa mkweli,kama alifanya kazi nzuri,mbona chama kilifia wodini?

Wewe unamsifu kama mpambanaji mzuri hebu tiumwagie CV yake humu ili tujuwe aina ya upambanaji wake ni upi tafadhali.
 
Constantine Akitanda na Mafie PM,

Sasa wakuu zangu mkianza nyie wenyewe kugombana hata chama hajifika mahala kweli kuna usalama. Kwa nini msikae mkayazungumzia yale yaliyopita, mkajifunza makosa kisha mkaendelea mbele maana navyomsoma mimi Mafie anaonyesha hana imani na baadhi ya watu na pengine hao watu wamo pia CCK..kutoka Chama cha Jamii kwenda chama cha Kijamii hakuna tofauti kwa mwenye kusoma alama za wakati.

La muhimu wekeni majina ya viongozi wenu wanachama ambao mnataka kuwanadi kwa wananchi baadaye. Kujificha ya nini kama kweli mnayo nia njema maana uchaguzi Tanzania jamani sii lelemama ni mchakato unaoanza na Wahusika hizi sera na Itikadi ni kachumbari tu kukoleza pilau. Tupeni list ya uongozi watu wengine wabebe ndizi wakijua kuna pilau la nguvu..

Umeongea jambo la msingi sana maana Akitanda anajua niliumizwa na nilipambana sana, na anajua sina tatizo naye lakini ameingia nyumbani kwa mpambanaji mwenzake bila hata kumtaarifu, si hata angenisms kama kweli anajua mchango wangu mzuri?
Aje na safu ya wapambanaji tumpe saport, unajua ukitaka kufanikiwa usidharau mchango wa mtu aliowahi kuutoa hata kama ni kidogo, hasa ukiwa eneo la nyumbani kwake maana anaweza kufikiri una ajenda ya siri..:A S 465:
 
Sikumbuki kusema kwamba ubepari ni zao la uliberali kwani hii sio sahihi. Ili uliberali utekelezeke, ni lazima pawe na ubepari. Nilimaanisha ufisadi ni zao la uliberali. Je ulimaanisha kuuliza ufafanuzi kuhusu uhusiano wa uliberali na ufisadi?
Soma hapa nadhani umekosea tu ulitaka kusema Ubepari au sio? Lakini maadam unasisitiza kuwa ufisadi umetokana na Uliberali naomba somo hapo kidogo..

Back
Top Bottom