CCK yaingia Arusha kwa kishindo

Mchambuzi,
Mkuu wangu kusema kweli hapo ndio umenipeleka nje kabisa maana nijuavyo mimi ni kwamba Dunia hii na hasa ktk tawala tulikuwa tukitawaliwa na sheria za DINI au MILA ambazo ndizo zilizotujenga ktk makundi ya Utaifa au jamii fulani. Na Uliberali ni mtazamo ulokuja kupingana na dhana ya kwamba binadamu anatakiwa kufuata AMRI ya imani fulani au mila fulani ambazo baadhi yake zinapuuza haki za binadamu na kwamba sisi binadamu wote sawa and we can govern ourselves ktk ku exercise freedom and rights of individuals..Na sisi Conservative tunaamini ktk sheria na amri tangulizi ambazo ndizo zilizotujenga sisi kama binadamu wa Kimataifa na hizi imani za dini, Mila na Tamaduni ndizo mwongozo wetu ni lazima kuenziwa japokuwa zipo sheria na mila mbaya zilizopitwa na wakati zinaweza kuondolewa lakini sio zile zilizotutambulisha sisi ni watu gani...

Sasa unaposema Uliberali unahusiana na Ufisadi kusema kweli kidogo inanipa shida maana ktk ushindani baina ya Uliberali na Uhafidhina tunafungwa wote na Ubepari kama ndio njia pekee ya kujiendeleza kiuchumi, mfumo ambao ndio shina la Ufisadi na wote tumeshindwa kuja na njia mbadala ambazo zinaweza kuendesha Ubepari bila kuathiri uchumi wenyewe ama maisha ya wananchi wanaotumikia Ubepari huo. Hivyo, ukinambia Ubepari ndio hukaribisha Ufisadi nitakuelewa lakini hii ya Liberali kusema kweli nimegota, pengine mimi ndio sijui hasa maana ya Uliberali hutumia tu neno hili bila uelewa maana yake na ndio maana nimetoka mtupu..

Mkuu Mkandara,

Kimsingi nakubaliana na wewe. Tunapopishana ni sehemu ndogo sana. Wewe unaongelea suala hili ‘in content', mimi naliongelea 'in context' – kwa maana ya kwamba, pamoja na kwamba ni kweli msingi wa Maendeleo katika jamii yoyote lazima ufuate CONTENT ya uliberali na ubepari, lakini mafanikio hutegemea mazingira - CONTEXT. Katika mazingira yetu, uliberali umezaa ufisadi kwa sababu, tofauti na nchi matajiri (USA, Canada, UK, n.k), nchini Tanzania, uliberali umekuwa unaendeshwa katika misingi ya Ubepari wa Kienyeji. Nitafafanua baadae kidogo. Kwanza tuangalie asili ya uliberali na uhafidhiana.

Uliberali katika nchi zilizoendelea haukupatikana kirahisi, bali ulitokana na harakati za muda mrefu za kupingana na utawala dhalimu wa kifalme. Lakini cha ajabu ni kwamba, hao hao waliofanikiwa kuutokomeza utawala dhalimu usio heshimu haki za wananchi za kijamii, kisiasa na kiuchumi, baadae wakaenda nchi za mbali na kutumia njia za uonevu uliopindukia kujinufaisha (utumwa, na baadae ukoloni). Hawa watu hawakutakiwa kufanya waliyofanya kwani - asili ya ulibearli ilikuwa ni harakati za kupigania haki za wananchi kutoka katika himaya za kifalme katika karne za nyuma kwenye nchi za ulaya. John Locke ndiye alikuwa moja wa waasisi wa mapinduzi yale ambayo yalijengewa hoja kwamba – uhuru wa mwananchi ndio msingi wa jamii iliyo imara na yenye kuishi kwa upendo kuvumiliana, na amani.

Hivyo, Serikali inatakiwa iwepo kuhakikisha tu kwamba haki hizi zinalindwa. Harakati hizi za uliberali zikahamia kwenye siasa na kuwa kiini cha demokrasia ya uwakilishi (representative democracy), na baadae pia kuhamia kwenye nyanja ya uchumi ambapo Adam Smith alikuja na itikadi kali iliyopinga serikali kuingilia katika shughuli za kiuchumi kwa hoja kwamba kufanya hivyo ni kukwaza ukuaji wa utajiri wa taifa. Kwahiyo ikahimizwa kwamba nguvu za soko ndio zitawale shughuli za kiuchumi, sio serikali.

Movement yenu nyinyi wahafidhiana (conservatives) asili yake ni harakati za kupinga mapinduzi ya kung'oa ufalme wa ufaransa. Kama jina lenu linavyoelezea, ‘conserving' maana yake preserving/hifadhi. Kwahiyo upo sahihi kama ulivyoelezea kwamba mna thamini sana mambo ya kale na hamkubali kirahisi mambo hayo, hasa kama yamejengwa kitaasisi yabomoke hivi hivi tu. Wanaharakati wale wa ufaransa walipinga kubomolewa kwa fikra, dhana na imani zilizojengwa kwa muda mrefu katika misingi ya kidini, kiutamaduni, na autocracy (mfumo wa kisiasa/utawala ambao haukuwa unawapa watawala kikomo cha kutawala). Wahafidhiana wale walitaka haya yote yabakie kama yalivyo.

Wahafidhiana mna tofauti kubwa sana na waliberali, lakini mnafanana katika suala moja la msingi sana, nalo ni – wote kupinga serikali kuingilia katika shughuli za uchumi kwa mfano kutoa huduma za kijamii, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya umma n.k, kwa madai kwamba vitendo hivi vinachochea uvivu, na ni sumu kwa ustawi wa jamii kwani vinapelekea uwepo wa taifa la watu wavivu wanaosubiri ‘government handout', inapunguza motisha ya watu kuwa wabunifu na wachapa kazi ili na wao wajitajirishe kwa kutumia jasho lao n.k.

Sasa tukirudi katika uhusiano baina ya ubepari na uliberali:
Ili Uliberali uweze kutekelezeka, lazima pawe na mazingira ya ubepari; na ili Ubepari ushamiri na kustawi, lazima jamii ifuate kanuni za kiliberali. Swali linalofuata ni, JE: Katika mazingira ya ubepari, je kuna kanuni yoyote nyingine nje ya uliberali ambayo inaweza kusaidia ubepari kustawi na kushamiri? Sina majibu yatakayojitosheleza lakini, ukweli usiopingika ni kwamba Maendeleo ya kiuchumi duniani, utajiri duniani, na kukua kwa vipato (economic growth, wealth creation and income growth) yametokana na mfumo wa ubepari, sio vinginevyo. Lakini ni muhimu tukaugawa ubepari katika maeneo mawili makuu: Ubepari wa kienyeji (uliopelekea primitive accumulation of capital) na Ubepari wa kisasa (modern capitalism ambao sasa umetungiwa sheria ingawa sheria hizo zinaheshikima katika nchi tajiri tu).

Ubepari wa kienyeji (primitive accumulation of capital) ndio chanzo cha utajiri wa mataifa makubwa ya leo. Hata takwimu zinaonyesha kwamba nchi hizi zilianza kuwa na mafanikio makubwa baada ya zile safari za Vasco Dagama na wengineo. Hatuna haja ya kwenda kwa undani juu ya suala hili lakini bila ya utumwa, ukoloni, ubaguzi wa rangi n.k, ‘ubepari per se' usingezifanya nchi hizi kuwa na mafanikio waliokuwa nayo leo. Hata Walter Rodney aliuliwa kwa kuelezea siri hi katika kitabu chake cha: How Europe UnderDeveloped Africa. Aina ya pili ya ubepari ni ule wa kisasa – ambao baada ya wakubwa kunufaika kupitia vita vya wenyewe kwa wenywe na kutosheka, sasa wamewekeana taratibu za kuishi kwa amani na kufaidi kwa mijira ile ile. Wamejiundia madudu kama vile G8 na Development Assistance Committee (DAC) – ambao ndio wanahisa wa WorldBank na IMF, na hawa ndio mawakala wao wa kuendeleza ubepari wa kienyeji katika nchi zetu. n.k.

Leo hii, ubepari wa kienyeji bado unatekelezwa chini ya kanuni za uliberali ambao zinahimiza – Liberalization, Marketization na Privatization. Sina haja ya kwenda ndani sana juu ya hili kwani sote tunaelewa nini kinaendelea. Pia tunaelewa kwanini Mwl Nyerere alipingana na ubepari na uliberali wa kuamrishwa. Mwalimu hakuchukia ubepari per se bali hakupenda ubepari usiotutendea haki. Na sote tunaelewa kwanini leo hii baada ya miaka 26 ya kuruhusu ubepari wa kienyeji, unatotekelezwa chini ya kanuni ya uliberali, Tanzania tumebaki kuwa watumwa na wanyonge kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni, tofauti ikiwa tuna uhuru wa kisiasa, lakini mbaya zaidi ni kwamba, baada ya Nyerere kung'atuka, watawala waliofuatia wamekuwa ni kama magavana wale wale wakati wa ukoloni, tofauti ikiwa hawa wa sasa, ngozi zao ni nyeusi.

Katika nchi za wenzetu, tunaona jinsi gani serikali zinapindisha kanuni za uliberali wakati wa shida. Kwa mfano ni kawaida kusikia ‘bail-outs' huko Ulaya na Marekani, ili kurekebisha mapungufu ya uliberali. Pia kama unakumbuka, Great Depression miaka ya 1920s, ilitokana na kosa la serikali kuachia uliberali utawale uchumi bila ya mipaka. Na bila ya serikali kuingilia kati kuokoa hali ile, mapinduzi yangeutokomeza ubepari. Hivi umebaini kwamba wakati wa shida na maafa, jamii za kibepari katika nchi kubwa kwa mfano Marekani huwa zina ‘adopt' maisha ya kijamaa, kidugu n.k, lakini hali inaporudi kuwa shwari, hali ya ubinafsi inajirudia? Umewahi kujiuliza kwanini inakuwa hivyo?

Kama serikali ina uhalali wa kuingilia kati wakati wa maafa kama yale ya great depression na global financial crisis, kwanini haitokeo hivyo Katika nchi zetu? Nadhani nitakua sahihi nikitamka kwamba – watanzania walio vijijini wamekuwa kwenye ‘great depression' tangia uhuru (kwa miaka 50). Kama utapingana na hili, nasimama kupingwa. Sasa kama serikali za waasisi wa uliberali huwa zinaingilia kurekesbisha uliberali unapoleta maafa, sasa kwanini huku kwetu uliberali unaachiwa utumalize? Kwanini WorldBank, IMF hawaruhusu serikali kuingilia kati na kuokoa watanzania? Tuna rasilimali zote muhimu za kutukomboa, lakini uliberali nchini kwetu ambao unahimiza - Liberalization, Marketization na Privatization, unatunyima haki hata kutumia maliasili zetu kwa jinsi tunavyotaka wenyewe, kwa faida yetu wenyewe. Eti tunaambiwa tatizo letu hatuna mitaji na tekinolojia.

Kwa mfano, Je, ni nchi gani inayofuata ubepari na uliberali imeendelea bila kutoza kodi? Kwanini wanatulazimisha tusitoze wawekezaji kodi? Katika nchi za wenzetu kama hapo ulipo – Canada n.k, ubepari ndio ulipelekea mapinduzi ya viwanda ambayo ndio yamesaidia jamii kuboresha hali zao za maisha kwa namna mbali mbali. Ubepari unapelekea ushindani ambao unazaa ufanisi, bidhaa na huduma bora zenye bei nafuu n.k, lakini pia serikali nayo ikishiriki kwa kikamilifu kurekebisha pale kanuni za uliberali zinapogonga mwamba. Kwenye nchi za waasisi wa ubepari, Uliberali umeleta kheri kuliko hasara, lakini kwetu sisi Tanzania na nchi maskini, uliberali na ubepari vimetuletea majanga makubwa sana, faida ni kama haipo. Mtu unabaki kujiuliza: Hivi, sera za kiliberali nia yake ni kunufaisha binadamu wote au binadamu wa aina fulani fulani?

Kama nilivyokwisha sema, serikali za nchi tajiri huwa zinawaokoa jamii wakati wa shida kwani bila ya kufanya hivyo, kutatokea mapinduzi dhidi ya ubepari. Sisi Tanzania na nchi maskini je? Serikali yetu ipo wapi tunapotimiza miaka 50 ya uhuru? Ni uhuru gani huu? Hizi ‘nguvu za soko' zina uhalali gani kwetu kubakia kama zilizvyo, wakati kwao haziachiwi ziote mapembe makubwa namna hii na kuzaa ufisadi? Tanzania, wanaofaidika kanuni za uliberali ni wachache sana, na hasa wawekezaji na mabepari uchwara ambao ni majizi na mafisadi ndani ya mfumo kilema wa uliberali katika nchi yetu. Hii ni kwa sababu ubepari uliopo kwetu ni ubepari wa kienyeji (primitive accumulation of capital), na hali hii ndio inawapa nafasi wanasiasa wa Tanzania na wao kuongeza kasi ya wizi na ufisadi.
Kwenye nchi za wenzetu, Uliberali na ubepari umezaa viwanda ambavyo vimeinua sana hali zao maisha kiuchumi na kijamii, lakini wewe haujiulizi kwamba: Inakuwaje Uliberali na Ubepari ambao msingi wake ni Maendeleo ya viwanda, ulipokuja kwetu ukaua viwanda?

Pamoja na umuhimu wa ‘nguvu za soko' chini ya uliberali na ubepari katika kuleta ufanisi wa uchumi, mimi sidhani nchi maskini kama Tanzania inatakiwa iachwe itegemee ‘nguvu za soko' katika kugawanya rasilimali (resource allocation). Badala yake, ni muhimu serikali iwe na mkono mrefu kama ilivyotokea kwa nchi za South Korea, Malaysia na wengine wanaoitwa ‘The Tigers', kwani hawa waliendelea kutokana na ‘Guided Capitalism' chini ya marekani, uingereza na ufaransa ili waone ubepari una manufaa hivyo wasivutike na ukomunisti. Sijui kwanini watu wengi wanakuwa wavivu kuelewa hili na badala yake wanaimba nyimbo za kuiga Asian Tigers. Vinginevyo bila ya ubepari na uliberali kuwa guided/kupewa mwongozo na serikali hizi wakisaidiwa na nchi za kibepari, leo nchi hizi zingekuwa maskini kama Tanzania. Ni wakati muafaka sasa kwa nchi tajiri kutujengea mazingira kama yale ya Asian Tigers, badala ya kutudanganya kwamba tukifuata kanuni za kibepari na uliberali na sisi tutafika. Vinginevyo, chini ya mfumo wa sasa, hakuna lolote la maana litakalofanyika kuwaokoa watanzania waliopo vijijini ambao miaka 50 iliyopita walikuwa ni asilimia 85 ya idadi yote ya watanzania, leo hii ni asilimia 75. Lakini tusisahau kwamba mwaka 1961 asilimia 85 ilikuwa ni watanzania 750,000 (laki saba na hamsini) leo hii ni Watanzania zaidi ya milioni 33. Hata kama idadi hii itapungua na kuwa asilimia tuseme 50 mwaka 2020, hii ina maana itakuwa watanzania zaidi ya milioni 25.
 
Hakuna kitu, utapeli mtupu, wanaJF msidanganyike na hawa jamaa maana walipokuwa ccj tulifanya nao kazi nzuri sana na kutengeneza mtandao mzuri mno, na tukapata wanachama maelfu kwa gharama zetu bila hata shilingi kumi yao, tukahatarisha maisha yetu maana tulikuwa tunawindwa sana na ccm A maana hii ilikuwa ccmB kabla haijaporwa nafasi hiyo na cuf aka KAFU, tulitumia pesa zetu na gharama kubwa sana bila wao wenyewe kutuwezesha chochote, mwisho waanzilishi wakaamua kurudi kulamba viatu vya wakubwa!
Leo wanakuja na habari mpya, wala hawakumbuki utapeli wao! tuelewe CCK ni late CCJ, nashangaa sana M/kiti wake wa Taifa kipindi hicho na katibu wake walikuwa wanatupiga mizinga ya vocha, nauli, pesa ya kulipia guest house! mpaka leo hii nina sms zao kwenye cm yangu ya zamani ambayo sitataka kuitupa nimeiweka makumbusho maana ni aibu tupu. Ila mwenyekiti wake wa sasa Taifa sina sana tatizo naye japo alitakiwa aangalie walipoangukia na atubu. Enzi hizo alikuwa katibu mwenezi,.Mr Akitanda. Sidhani kama ni chama makini hiki.
A%20S%20embarassed.gif
Huu ni ubabaishaji mpya kwa mbinu mpya, Nimechoka nawaasa hakuna haja ya kuhangaika nacho maana ni walewale tu hawa. walikosa usajili wakaondoa J wakaweka K, kitu ni kilekile hata katiba nahisi ni ileile.
Najua watanishambulia lakini wakifanya hivyo nitaweka mambo yao yote hapa.

Ushamba ni sawa na mzigo wa kuni, siasa za bongo Chuki chuki chuki mtupu! kwa staili hii wakulaumiwa siyo wanasiasa bali ni jamii kwa kushindwa kuchuja na kupima kabla ya kumeza
 
mawazo mgando hayo! ni vyema ungeenda kukojoa kwanza alafu ukalale! umesahau kuwa slaa ana damu ya chama cha magamba? aliyekuwa mke wake? rose?? alikuwa diwani wa chama cha magamba! baregu je? katokea wapi? mbowe??? we vipi wewe nyambaf
haya subirini kiongozi wenu mmoja kashakuwa zeruzeru tehetehetehe
 
Back
Top Bottom