Hakuna kitu, utapeli mtupu, wanaJF msidanganyike na hawa jamaa maana walipokuwa ccj tulifanya nao kazi nzuri sana na kutengeneza mtandao mzuri mno, na tukapata wanachama maelfu kwa gharama zetu bila hata shilingi kumi yao, tukahatarisha maisha yetu maana tulikuwa tunawindwa sana na ccm A maana hii
ilikuwa ccmB kabla haijaporwa nafasi hiyo na cuf aka KAFU, tulitumia pesa zetu na gharama kubwa sana bila wao wenyewe kutuwezesha chochote, mwisho waanzilishi wakaamua kurudi kulamba viatu vya wakubwa!
Leo wanakuja na habari mpya, wala hawakumbuki utapeli wao! tuelewe CCK ni late CCJ, nashangaa sana M/kiti wake wa Taifa kipindi hicho na katibu wake walikuwa wanatupiga mizinga ya vocha, nauli, pesa ya kulipia guest house! mpaka leo hii nina sms zao kwenye cm yangu ya zamani ambayo sitataka kuitupa nimeiweka makumbusho maana ni aibu tupu. Ila mwenyekiti wake wa sasa Taifa sina sana tatizo naye japo alitakiwa aangalie walipoangukia na atubu. Enzi hizo alikuwa katibu mwenezi,.Mr Akitanda. Sidhani kama ni chama makini hiki.
Huu ni ubabaishaji mpya kwa mbinu mpya, Nimechoka nawaasa hakuna haja ya kuhangaika nacho maana ni walewale tu hawa. walikosa usajili wakaondoa J wakaweka K, kitu ni kilekile hata katiba nahisi ni ileile.
Najua watanishambulia lakini wakifanya hivyo
nitaweka mambo yao yote hapa.