PreGE2025 Camillus Wambura: Jeshi la Polisi halipo tayari kumvumilia yeyote atakayeleta uvunjifu wa amani

PreGE2025 Camillus Wambura: Jeshi la Polisi halipo tayari kumvumilia yeyote atakayeleta uvunjifu wa amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Wambura, amesema Jeshi halipo tayari kumvumilia yeyote atakayeleta uvunjifu wa amani. Amesema hayo leo Juni 9, Jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kufunga kozi ya maafisa na wakaguzi wa Jeshi la Polisi.

"Sote tunatambua kuwa mwaka huu 2025 nchi yetu inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu huo Jeshi la Polisi limejipanga vyema katika kuhakikisha kwamba Uchaguzi huu unafanyika kwa Amani na Utulivu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi huo"

"Mheshimiwa Rais tunakuahidi Nchi hii ni salama, Nchi hii ina Amani. Jeshi hili la polisi haliko tayari kumvumilia yeyote atakayeleta uvunjifu wa Amani kwa sababu yoyote ile"


Jeshi la Polisi halina hadhi Wala halina uhalali wowote ule wa kuweza kukemea au kupambana na uhalifu kwa sababu wao wenyewe Mapolisi ndio Wahalifu wenyewe.
 
Back
Top Bottom