Bungeni: Mayenga (Mbunge wa CCM) amsimanga Halima Mdee na wenzake 18 bila huruma

Inasikitisha. Hao 19 wanaongea point sana bungeni lakini hoja zao hazina maana kwenye bunge la CCM. Zinakuwa na mashiko zikitokea anga za upinzani halisi hasa CHADEMA. Na Halima ana DNA ya CHADEMA haswa...
Wakati mwingine simlaumu sana Halima Mdee.

Hivi kati yetu ni nani alitegemea Magufuli atakufa?

Huenda Halima alipiga mahesabu ktk uraisi wa maisha wa Magufuli.

Kweli inasikitisha alipoangukia Halima Mdee.
 
..wakati mwingine simlaumu sana Halima Mdee.

..hivi kati yetu ni nani alitegemea Magufuli atakufa...
Mimi nahisi sababu zilizomfanya afanye alioyafanya mpaka sasa hatuzijui. Kuna njia nyingi tu za kumshurutisha mtu afqnye ambalo hapendezwi nalo. Halima hakuwa mwenyewe tangu wakati wa kampeni. Hakuwa na moto wa kawaida.

Tusisahau pia kuwa hawa wakina mama toka wamefanya walichofanya hawajasema au kutenda lolote baya dhidi ya Chadema au uongozi wake pamoja matusi mengi wanayoporomoshewa kila kukicha. Hawa sio kama wakina Mollel, Silinde, Lijualikali au wale wakina dada waliohamia CUF. Kama ni suala ni la pesa au madaraka tu, zamani angeisha mkaanga Mbowe na wenzake.

Watu inabidi wapunguze munkari dhidi yao na wakumbuke kuwa hawa walikipigia chama chao kuliko wengi wanao watupia madongo waliweza kupigania.

Hii tamthilia bado inaandikwa. Tuwe wavumilivu.

Amandla...
 
Halima anapopolewa utazani kala nyama mbichi, hivi niwangapi wameunga juhudi jamani? Au kwasababu ni wanawake? Wengi waliotoka huko nakwenda upande wa pili na baadaye kurudi tena kuunga juhudi mbona hawachambwi hivyo?
 
Mimi nahisi sababu zilizomfanya afanye alioyafanya mpaka sasa hatuzijui. Kuna njia nyingi tu za kumshurutisha mtu afqnye ambalo hapendezwi nalo. Halima hakuwa mwenyewe tangu wakati wa kampeni. Hakuwa na moto wa kawaida...
Kweli kabisa mfano gari nyeupe isimame hapo utajitia kiburi kweli?
 
Wanajua kabisa siku zao zinahesabika mule bungeni. Wakiamka jambo la kwanza kabla hajaosha masaburi lazima aangalie habari isijekuwa mkeka umechanika😃😃😃

Wanaishi kama kunguru.
Hii naivulia kofia, kuishi Kama kunguru😆😆
 
hata ungekuwa wewe,ungetoka ili iweje...??...ukale wapi?lol..mnamponda Mdee kwa vitu/msimamo ambao wengi wenu mngefanya hivyo hivyo..lol

Madam usisahau kwamba Halima sio “sisi”. Ameshaonyesha kipaji cha kipekee sana cha ujasiri na upambanaji kisiasa. She’s not just anybody; she’s an extraordinary young woman. Usingetarajia baada ya vipondo vyote vile alivyopitia na kudumu (persevere) kwa miaka yote ile, ghafla aje aachie ngazi kirahisi vile. Alishaonyesha sacrifice kubwa sana beyond usual human greed.

Ni kama kumshuhudia Usain Bolt akiongoza mbio za mita 100 kwa mbali halafu umuone ghafla akikaa chini baada ya mita 90 mstari wa ushindi ukiwa hatua moja tu mbele yake.
 
Tulisha maliza maombi ,KWA kuendelea kuiba kodi za walipa kodi na wakijua hawastaili kuwa Bungeni ,mengi yaja juu yao wasipo ondoka Bungeni,ni mwanzo tu
Haya masimango yanahitaji akili zikuruke kwanza ndiyo uendelee kubaki bungeni na kuongea. Ningekuwa mimi ningebaki nifunge mdomo nisubiri mshahara na matokeo yake kwa sababu ndicho nilichokitaka.

Au wangejivua gamba kisha waunge mkono juhudi teuzi zingewapitia wawe na sauti sasa hivi chupi zimewabana vibaya mnoooo bungeni anayewapenda ni huyu kibushuti anaewapigania wenzao wanawaponda huku chadema wamebaki wameshika tama wanasikitika na kushangaa kwa walichokifanya wao wenyewe hatima ya rufaa yao bado hawaifahamu ingawa wana uhakika hata kama watashindwa watabaki bungeni kwa sababu nchi haiendeshwi tena na sheria ila matakwa ya kikundi cha wahuni wachache
 
..wakati mwingine simlaumu sana Halima Mdee...

Mkuu hata mimi sina jibu la uhakika. Ninachojua ni kuwa wale walochagua njia ngumu ya kisiasa hasa kule CHADEMA lazima wawe wamekamilisha hesabu zao. Wajue wamejitoa muhanga. Mbowe alishasema kuwa mpinzani wa kweli Tanzania ni maumivu makubwa.

Ni kweli Tanzania hata CCM yenyewe inategemea uwepo wa wapinzani wanaotikisa ili kusaidia kurejesha mambo yakienda mrama kupita kiasi. Lakini, nchi hii kwa ujumla bado haiko sympathetic sana na adha wanazopata wapinzani. Kiwango cha unafiki na “greed” kiko juu sana kwa wengi. Kujikomba ndio njia kuu ya kujipatia riziki ya haja.

Majuzi , Mch. Msigwa alizungumzia “defining moment” ya mpinzani wa kweli. Hata kama Magufuli angefanikiwa kuwa Rais wa maisha, isingetarajiwa mtu kama Halima afuate kauli ya “if you can’t beat them …”. Alishajipambanua sana kuwa tofauti na falsafa hiyo. Ilikuwa ni ama aendeleze mapambano kwa njia nyingine au aachane kabisa na siasa za ushindani atafute career nyingine.

The real Halima Mdee hawezi kuwa subservient kwa Magufuli au utawala wa CCM. Huyo hatakuwa Halima Mdee wala kivuli chake. Sivyo tulivyomfahamu. We have lost her. I’m just wondering if she’s going to rise from the dust. Kwa kweli Magufuli alishusha pigo kubwa huko CHADEMA. Kama kawaida yake hicho Chama ni kama phoenix; kimesurvive; lakini baadhi ya makamanda wameungua sana.
 
Back
Top Bottom