Bungeni: Mayenga (Mbunge wa CCM) amsimanga Halima Mdee na wenzake 18 bila huruma

Mnataka watoke huko alafu wakafanye kazi gani!?
Watu wanapigania matumbo yao

Ova
 
Nakweli patamu, ma professor wanakimbia lecture huko nakukimbilia bungeni itakuwa kina Halima jamani? Watu wanasema tu mama Tanzania aliteuliwaga na Mzee wa msoga kisha msimu uliofuata akagombea jimbo, wawaache jamani!
Bora umeliona hilo mkuu
 
Ukiwa na bei huwezi kuwa na heshima
Maneno saba (7) uliyoyatumia hapa, yenye maana nzito kwelikweli; lakini kwa bahati mbaya sana kwa Tanzania hii ya sasa.

Hebu nionyeshe "asiye na bei" kwenye jengo hilo la mipasho!

Angekuwemo humo Mchungaji Msigwa, labda ningesema usemalo ni kweli..., hawa wote uwemo wao humo bungeni ni kwa sababu bei ilitosha kuwapeleka huko.
 
Mbona mnamshambulia sana
Halima ?
Miaka ya karibuni, tumeshuhudia wanachama wengi wa Upinzani wakihamia CCM, hata iwe kwa kuhongwa, au hiari sasa limekuwa Jambo la kawaida kabisa.
Wengine wametunukiwa vyeo katika muda wote huo na wengine bado wanaendelea kulamba vyeo hadi sasa.
Halima ana nini cha maana kutofautisha na hao waliokimbilia CCM ?
Hao wabunge hawawezi kuachishwa hadhi ya Ubunge na Spika hili liko wazi.
Mwacheni Halima amalize muda wake wa miaka mitano ya awamu ya Sita.
Yeye hajawa wa kwanza kutofautiana na Chama chake.
Shida inajulikana, shida ni Njaa ndugu zanguni, kinachotafutwa ni Chakula.
Hivi nchi hii kuna mpinzani Mzalendo kweli. Angekuwepo CCM ingeisha angushwa.
Mi naona wazi kabisa, anayebaki Upinzani basi ana Cheo fulani, cheo kikiisha na akateuliwa mpinzani mwingine basi inatafutwa fursa nyingine.
Mwacheni Halima ale kama wanavyokula Wapinzani wengine wanaomaliza muda wao wa madaraka hali wakiwa vijana.

Kungekuwepo na Uzalendo kwenye upinzani basi CHADEMA wangeisha chukua Dola zamani sana.

Acheni Janja Janja, mwacheni Halima ale. Hakuna cha upinzani wala cha nini ni NJAA tu.
Wamwache miaka elfu, au kwasababu ni wanawake ndiyo maana wanasakamwa kiasi hicho?

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Shame upon them, aibu sana sana lakini madhali kodi zetu zinatafunwa hakuna tabu...!
HELA WANAYOWALIPA HAWA INGEPELEKWA HATA KATIKA DARAJA LA BUSISI.
 
Halima Mdee nje na ndani ya ukumbi unasutwa. Hata uongee point vipi ni pointless.
Kusutwa na mwanamke mwenzio ni aibu.

Ushauri wangu Jiuzulu Ubunge, kaombe msamaha kwenye chama chako.

Ndugai 2025 ni mstaafu, nani atakukingia.

Mh LUCY MAYENGA Hongera sana kwa kusema ukweli na kuonyesha wazi kuwa kitendo cha Uviko 19 hawana sifa yakumsema Magufuli huku wakijua kuwa ndiye aliyewaingiza.
ASANTE MAYENGA.SPIKA akikuita kama alivyofanya kwa NAPE sema unaumwa
CHADEMA wakifanya makosa ya kuwaondoa hawa wabunge bungeni, watakuwa wamejikaanga kwa mafuta yao wenyewe. Hawa watu wako Bungeni kama wabunge ndiyo lakini kwa upande mwingine, ni kama undercover ya chama wanaoweza ku-capture taarifa za kiintelijenisa za kisiasa kutokea Bungeni na possibly, mahali kwinginekko tofuati na Bungeni, zinazoweza kuwasaidia CHADEMA kuendelea kujiimarisha kisiasa au kama siyo kujiimarisha, basi kuendana sawia na upepo wa kisiasa. Tangu CHADEMA ianzishwe, hawajawahi kukosa wawakilishi Bungeni na hivyo hali ya wao kutokuwa na wawakilishi Bungeni hawaelewi madhara yake yanaweza kuwa ni nini kwa sasa, isipokuwa watakuja kuyaelewa pale tu watakapopelekea wabunge hawa kufukuzwa Bungeni.

Mimi nawashauri wawaache wabunge hawa wafanye kazi, after all sisi wanachi ambao ndiyo tunaowakilishwa na wabunge pasipo kujali itikadi za chama, hatujalalamika kuhusiana na wabunge hao, wanaolalamika ni wana siasa, tena wa CHADEMA tu. CCM au chama kingine siajsikia mtu analamikana kuhusiana na watu hawa

CHADEMA waacheni wabunge hao waendelee kuwemo bungeni, ni intelijensia yenu ya kisiasa kwenye system ya nchi. Mkiwatoa hao come 2025 watakuwa wameshahama chama na watgombea kwenye majimbo yao kwa tiketi ya vyama vingine na watashinda. Watarudi tena Bungeni wakiwa siyo CHADEMA, na CHADEMA inaweza kufa hata hiyo 2030 anayoiangalai Mbowe hamtafanya kitu.

Lakini pia kwa upande mwingine, Ubunge nao pia ni ajira. Watanzania wenyewe tunalalamika kila siku hatuna ajira; kuna watu ambao wako mahali fulani na wanafanya kazi halali, halafu mnataka tena muwafukuze, wakose tena ajira wakati kila siku tunalalamika hatuna ajira?
Tuwaacheni wabunge wafanya kazi waliyotumwa na umma wa watanzania, wakifanya makosa bungeni ndyo hapo inabidi tuwalalamike. Hizi marginals zingine zinazotu-keep busy kwenye mitandao kwa ajli yao hazitusaidii kitu. Tuwaacheni wafanye kazi ya kuisimamia vizuri Serikali ili mama aweze kutanya vizuri kwenye vipindi vyake vyote
 
Back
Top Bottom