MKWEAMINAZI
JF-Expert Member
- May 28, 2023
- 930
- 1,299
Nimepitia katiba ya nchi yetu Katiba ambayo hata Rais anapochaguliwa lazima aiape kwanza ndio awe Rais na pia aseme atailinda ataihifadhi na kuiheshimu.
Pia Katiba hiyo hiyo imeeleza Spika anavyopatikana na kuala kuwa atailinda kuitetea na kuihifadhi. Katiba hiyo hiyo imeeleza jinsi Wabunge watakavyopatikana na sifa zao na pia imeeleza jinsi ubunge wao utakavyokoma ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama na chama kilichomdhamini.
Katiba hiyo hiyo nimeisoma mwanzo mpaka mwisho sijaona kifungu chochote kinachomlinda mbunge aliyefukuzwa uanachama kuendelea kuwa mbunge kama ilivyo kwa Halima Mdee na wenzake 18.
Suala la kupinga kufukuzwa uanachama ni suala binafsi la aliyefukuzwa na hulifanya mara baada ya kuvuliwa ubunge kama katiba inavyoelekeza lakini imekuwa kinyume kwa suala la wabunge 19 waliofukuzwa uanachama wao serikali na bunge vimeamua kwa makusudi kukiuka katiba kwa kutowavua ubunge kama ilivyowahi kufanya kwa wabunge wa CUF na CCM mara tu baada ya kupata barua ya kufukuzwa uanachama wao kutoka kwenye vyama vyao na bunge halikusubiri mahakama itoe maelekezo, lakini kwa hawa 19 bunge na serikali wamewaruhusu kuendelea kuwa wabunge bila kuwa wanachama wa chama cha siasa kinyume na katiba na kuwataka wapinge kufukuzwa kwao wakiwa Wabunge.
Swali gumu: Je, kwanini Halima Mdee na wenzake 18 bado ni wabunge ili hali sio wanachama wa chama cha siasa kwa mujibu wa katiba ya nchi?