Halima Mdee na wenzake ni wanachama halali wa CHADEMA kwa mujibu wa mahakama, ila watagombea ubunge kupitia CCM 2025 kwa mujibu wa CCM

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,105
Mahakama ikisema wakina Mdee siyo wanachama wa CHADEMA na wala siyo wabunge wapo watu nimewasikia wakitafakari kuwafungulia mashtaka ya wizi wa mali za umma.

Maamuzi yakumweka Ndugai safe na kuisaidia CCM kupumua ni Mahakama kusema ni wabunge halali ila baadaye huko 2025 watapokelewa rasmi CCM kwa ajili ya kupewa mkate wa siku.

Hoja kubwa hapa itakuwa, case ya uchaguzi Tanzania inachukua muda gani kuamuliwa na mahakama ? Je, kuna umuhimu wowote wa wabunge kupewa ridhaa na chama au wanaweza kujiamulia tu kwenda bungeni na kuapishwa endapo wanaoapisha wanataka iwe hivyo? Kwanini tufanye kampeni na kuchagua wanasiasa kwa mamilioni wakati yupo mtu mmoja anayeweza kusema huyu ni mbunge wenu na wote msipinge?
 
Back
Top Bottom