Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012

wakina mrema, komba na msabaha wanaogopa kuonekana wakiota ndoto za mchana bungeni, wakipitisha hiyo hoja 2015 hakuna watakaorudi wote tupige chini. tuanze kuwafanyia kampeni
 
masikini hawa wabunge....
hivi wanadhani watakuwa wabunge milele eeeh?
Hawa binadamu wamefungwa ufahamu kabisa na kuna mambo ya ajabu zaidi ya haya watayafanya, naamini Mungu ndivyo alivyowaandalia destiny yao!
 
Jambo hili ni la kupingwa kwa nguvu zote. Hili wazo ni baya kuliko wizi wa wanyama hai au wizi wa EPA/Richmond.
Wanataka kuturudisha enzi zile za zama za giza. Huu ni wakati wa mapinduzi ya habari... Ibara ya 18 ya katiba inalinda uhuru wa habari, wanataka kukiuka katiba...kurusha vikao moja kwa moja kunasaidia wananchi kuwajua na kurekodi tabia za wabunge wao, wananchi ndio mabosi wanatakiwa waone watumishi wao wanavyowajibika ili nao waweze kuwawajibisha!!
 
'Ukila nyama ya mtu hutaacha', walianza na JF, wakaja mwanahalisi sasa wanataka giza kabisa!
Wanaogopa kwasababu wananchi wanawafuatilia, sasa wasio na hoja wanajiuliza watarudi vipi Dodoma

Nanyi JF mnawatisha, yaani akibofoa haipiti dakika keshapandishwa jukwaani, ha ha ha ha, yaani hamtoi hata muda wa kujipanga mtu, ni faulu na kiki hapo hapo, hakuna kujenga ukuta!
Tena siku hizi mbunge akitoa pumba Jf mnaanza na CV halafu anageuzwa upside down, mnawatesa wenzenu. Haha ha ha

Wanatudharau sana wananchi, sidhani kuna muda tena wa kulumbana nao. Tunawaambi wabunge mlioko Dodoma, tumeshapata formula kutoka Mbeya! Mkileta hoja hii ya kipuuzi hatuna jinsi mnatulazimisha tuwageuze maembe kama kiranja mkuu alivyotendwa mbeya.

Kigwangalla, Mdee, Zitto, Mnyika, Dr Faustine Ndungulile, Filiku njombe, Mbatia, Wenje, Mh Mbowe na wengine mliopo hapa jamvini, tunawatuma muwaeleze wenzenu kuwa wananchi tupo frustrated na hali mbaya sana ya maisha, hali mbaya ya kisiasa liuchumi na kijamii. Tumekata tamaa na tunasubiri jua kuchomoza na kuzama.
Hatuna cha kupoteza kwasababu tumepoteza sana Umoja wetu ni wa kuchimba makaburi na kuzikana, leo kwa J kesho kwa K.

Tuna kitu kimoja tulicho nacho, kwamba katika hasira, ghadhabu na mkanganyiko huu tunatafuta sababu.
Tunatafuta sababu ili tutoe hasira zetu, kama mumeamua kutuletea sababu basi jaribuni kuleta huu mswaada.

Narudia, we have nothing to lose, you have lot to lose!
The situation is tense and volatile, we need alittle bit of spark you will see!
 
Hilo halitafanikiwa kamwe.
Uzuri ni kuwa wanapitia sn JF na kila tukiwarushia kombora wanapashana habari.
Nadhani kwa advertise hii ya leo watajiuliza umakini wa hoja yao na kujipanga upya!
 
Kweli tunayo safari ngefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli!
Hivi wanataka kuficha nini hasa!!?

Maandamano yako lini na yanaanzia wapi wajameni!
 
Naomba Mungu iyo ipelekwe bungeni na Nina amini itapitishwa na hapo Ndio ukombozi wa kweli wa taifa hili utapatikana maana Sidhani Kama patatosha uwanja wa taifa au jangwani wadau tusiwapinge kwanza tuwapeni support ili tupate njia baada ya wao kubweteka wakapitisha....Ndio tutafute tahariri squire yetu na madai hayatakuwa hoja tu Bali ni hatuitaki serikali nzima na hapo tutaikomboa Tanzania yetu kutoka kwa mkoloni mweusi
 
Kweli tunayo safari ngefu kuelekea kwenye demokrasia ya kweli!
Hivi wanataka kuficha nini hasa!!?

Maandamano yako lini na yanaanzia wapi wajameni!
sasa hivi letu bunge likipata msukumo wa chama fulani, linaingia rasmi kwenye siasa kandamizi na za kibeberu. Bunge letu linawaacha rasmi wananchi na kuingia kwenye udikteta.
Hakika tunazidi kupata point na vipengele vya kubadili ktk katiba yetu hasa kuhusu mfumo wa Bunge.
 
Wabunge wa CCM wanateswa sana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja kama Chama ndio maana ndani ya bunge wengi huwa upande wa serikali hata kama ni kuunga mkono hoja za kipuuzi, lakini wakienda kwenye vikao vyao vya wabunge wa CCM huwa wanacharuka sana na kuambiana ukweli kwani wanaelewa kwamba sehemu kubwa ya umma inaunga mkono hoja wa wapinzani karibia katika kila kitu na hii sio salama kwao kuelekea uchaguzi mkuu ujao (2015); Hivyo moja ya njia za kujaribu kujiokoa na tatizo hili ni kujaribu kujenga hoja ya namna hiyo kama wabunge wa CCM, hoping kwamba itapitishwa kirahisi kwani wabunge wa CCM ndio majority wa "NDIYOOOOO"

Mchambuzi,
Bado hujanibu ni kitu kinachokufanya utuhumu kuwa ni wabunge wa CCM wanataka mijadala isionyeshwe live; kuhusu hawa wabunge wote wanafanana kwa matendo ni makada tu wabunge kama wapo hawazidi 20%

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Sijatuhumu bali nimetoa hisia zangu kama nilivoelezea na binafsi sioni kwanini wabunge wa upinzani waje na hoja kama hiyo wakati ukweli uliopo ni kwamba live coverage ya bunge kwenye TV imekuwa na manufaa kwa Chadema kuliko CCM in terms of upinzani kuikosoa serikali na kufanikiwa ku convince the electorate kwamba udhaifu wa serikali ya CCM unachangia sana ugumu wa watanzania walio wengi;

Hoja juu ya wabunge na ukada na pia juu ya udhaifu wa wabunge wengi bila kujali vyama ina mashiko lakini suala la msingi hapa ni kwamba:

*Je ikiwa ni kweli kuna baadhi ya wabunge wanaandaa kuwasilisha hoja kama hii, je watakuwa ni wabunge wa upande gani?

Maoni yangu ndiyo hayo kwamba kama hizi ni taarifa za kweli, itakuwa ni baadhi ya wabunge wa CCM ambao wameshagundua kwamba hoja wanazozitetea hazina maslahi kwa umma na umma umeshaona hilo, sasa given ushindani unavyozidi kujengeka majimboni as we head towards 2015, tatizo hili lazima liwe arrested mapema or else majimbo yenye wabunge wa namna hii yataenda upinzani. It is as simple as that.
 
Sijatuhumu bali nimetoa hisia zangu kama nilivoelezea na binafsi sioni kwanini wabunge wa upinzani waje na hoja kama hiyo wakati ukweli uliopo ni kwamba live coverage ya bunge kwenye TV imekuwa na manufaa kwa Chadema kuliko CCM in terms of upinzani kuikosoa serikali na kufanikiwa ku convince the electorate kwamba udhaifu wa serikali ya CCM unachangia sana ugumu wa watanzania walio wengi;

Lakini unfahamu hisia zako zinaweza zisiwe sahihi; kama unakumbuka zilipotoka za wabunge wala rushwa wengi hisia zenu zililenga ni wabunge wa CCM kumbe hata wa Chadema wamo; labda nikuulize umeshawahi kwenda Dodoma kujumuika na hawa waheshimiwa baada ya shughuli zao za bunge?

Inawezekana hisia zangu hazipo sahihi na ndio msingi wa mijadala kama hii kueleweshana kwa hoja; vinginevyo nimejitahidi to support my position kwa hoja nilizotoa;
Kuhusu kwenda dodoma, nimewahi mara kadhaa na kushuhudia jinsi gani wabunge wengi wakiwa na mahusiano tofauti kabisa in a non-partisan way tofauti na tunavyowaona kwenye TV; lakini hoja ya msingi hapa sio social life outside shughuli za bunge, tunazungumzia suala linalohusu shughuli zao za bunge zinazofuatiliwa na jicho la jamii LIVE;
 
Kwasababu bado ni hisia haziwezi kuwa nguvu kwasababu zimesimamiwa na udhanifu kwa mantiki hiyo hakuna haja ya kuwajengea watu hukumu kwa misingi ya udhanifu

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Kwasababu bado ni hisia haziwezi kuwa nguvu kwasababu zimesimamiwa na udhanifu kwa mantiki hiyo hakuna haja ya kuwajengea watu hukumu kwa misingi ya udhanifu

Chama
Gongo la mboto DSM

Sawa mkuu. Vinginevyo baada ya kusoma taarifa hiyo, that was my personal belief/judgement and all along kama umenisoma vizuri, its simply an opinion that is not founded on proof or certainty;

Kumbuka: I am entitled to my own opinion, but not my own facts; and so are you;
 
Itakuwa magwanda hao, hawataki waonekane wanaposusa.
 
Back
Top Bottom