Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Nahisi komba na wasira ndio wataoandaa mpango wa kutafuta kura za wabunge wanaounga mkono hoja mfu namna hii. Only in tanzania
 
komba lazima atakuwepo kwenye list.

Na Steven Wassira!!! Halafu for sure hii hoja ni lazima iletwe na wabunge wa Mwabwepande na wale mapandikizi waliotuma vyama vya upinzani. CDM msikubali. Mbona CDM na CUF hawalali japo CUF ndo plan B yenu? Mizee imejaa huko inakuwa Dom inakesha kulewa na nyama halafu kesho yake digestion inagoma ndo kulala mtindo mmoja!!! Aibu, we need Transparency. Ambaye anataka kulala asihudhurie bunge siku hiyo?
 
Asiyewajibika na asiyejiamini ndiye anaogopa Wananchi kumuona alivyowadanganya au kutaka wasifahamu ni kiongozi wa namna gani kulinganisha anayojitangaza au kudai kusimamia.

Mimi ningependa iwe sehemu ya kanuni zetu, kila Mbunge awe na column ktk website ya Bunge ikiorodhesha yote aliyoahidi Mbunge na taarifa ya utekelezaji wake in real time.

Kila Halmashauri inatakiwa kuchapisha taarifa zake za robo mwaka na kuzisambaza bure kwa wananchi wa maeneo yao wakionyesha waziwazi mapato na matumizi ya fedha pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mendeleo iliyopangwa ndani ya mwaka wa fedha na hatua iliyofikiwa kwa wakati huo.

Hata Usalama wa Taifa (UwT) unatakiwa sasa uwe na tovuti (for public consumption) na kuweka wazi yale yote yanayotakiwa kuwa wazi (makusudi ya jumla, idara na vitengo, nafasi wazi, jaribio la AWALI la binafsi (preliminary self-appraisal) kutathmini kama una sifa za awali za kujiunga na UwT, Tafiti na Machapisho yao mbalimbali na rangi kama ishara za hali ya Usalama wa nchi yetu, link ambapo mtu anaweza kutoa credible info zinazohusu hatari ya usalama wetu na ufisadi mkubwa nchini na usiri wa mtoa habari ukahakikishwa n.k.

Huu ni muda wa uwazi na ukweli.
 
Hoja ya hawa MPs wetu haina mashiko kabisa! Wanataka wapitishe mambo yao kule mjengoni sie bila kujua. Nonsense!
Kwa kweli hii haikubaliki tunataka tuone ili tujue udhaifu wa wabunge wetu !!


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Dah! wanataka kuuficha uchafu wao mbali mbali wanaofanya wakiwa Bungeni ikiwemo kutukana, kuingia Bungeni huku wamelewa, kuchapa usingizi, kuomba rushwa n.k. Kama hawataki waliowachagua waone jinsi Wabunge wanavyowawakilisha Bungeni basi hakuna haja ya kuwepo na Bunge ni bora lifutwe tu ili tupunguze gharama kubwa za kuwa na hili Bunge lenye wabunge wengi haramu toka Magamba.

Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
 
masikini hawa wabunge....
hivi wanadhani watakuwa wabunge milele eeeh?
 
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012

Haimezeki kirahisi, what!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Hii inakinzana na uhuru wa habari

Parliamentary members wasifikiri bunge ni private property, ni la wananchi na wao ni wawakilishi. Kama wanafanya madudu wanataka yafichwe. Respect cannot be bought but it can be built. Wasitake kuficha uchafu for the sake of cheap respect.
 
Yes, kwa jinsi wanavyobehave kama watoto wa chekechea na wanavyolala fofofo bungeni, lazima wachukie kuonyeshwa LIVE. Hata mimi nisingekubali.
 
Hakika kabisa, hao uliotaja wanahusika moja kwa moja, na amini usiamini lazima ni wa CCM wote!
Hakika hoja hiyo ikifanyiwa kazi wananchi tunapaswa kuonyesha live kuwa hatukubali upopompo huo!...


Kwanza waache kuchukuwa posho ambazo ni kodi zetu
 
Wanaogopa kivuli chao wenyewe!inachekesha sana ,huwezi pata sehemu ingine yeyote duniani zaidi ya Tanzania!wakizima hizo TV wanaenda mashuka na dawa za mbu kabisa!!
 
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!

CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012

Hahahhaha sasa si bora waongee na wazee wa TANESCO tu kuwa wakati bunge linaendelea wahakikishe umeme unakwata nchi nzima ili watu wasione ***** wao badala ya kukataa kuoneshwa?,hahahahah mtakoma mwaka huu mlikuwa mnatoa hela ili muitwe waheshimiwa kwa ku sign posho na kuuchapa usingizi imekula kwenu sasa
 
Nadhani wanaogopa nguvu ya wananchi na wamebaini kwamba tunawafuatilia kwa karibu especially kwenye mahudhurio na kuongea pumba LIVE.
 
Ufisadi umepiga hodi ndani ya Bunge, badala ya kujadili jinsi ya kuwaadhibu wanaoondosha heshima ya Bunge wanawaza kuondoa live broadcasting!
Huu ndio mwisho wa akili za wabunge wa Tanzania?
Au hivyo viti vya kuzunguka vinadumaza?
Wale tunaowaiga oneni Bunge lao lilivyo simpo!
4238_lg.jpg
 
Jini likishatoka kwenye chupa huwezi kulirudisha.

Hii ni alama ya totalitarianism.

Wananchi waliowachagua wana haki ya kuona utendaji wao uko vipi bila kusubiri.
 
Back
Top Bottom