MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 9,646
- 13,827
Waache tu waijadili hiyo hoja ili tuwajue wabaya wetu.
Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?
Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.
Mara nyingi utawala unao anguka huwa unaviasharia vingi. Naamini wabunge waliotoa wazo hilo watakuwa ni wabunge ambao hakika niwa chama chenye dola inayo anguka ambayo imekuwa inakimbilia kujificha kwenye mahakama, leo hii inataka kuficha uovu kwa kuminya habari.
Hili tusikubaliane nalo maana linapingana na ibara ya 18 ya katiba yetu. Wanataka kutuficha ukweli ili watumie wing wao kuzidi kuichuuza nchi yetu.
Wabunge wengi wa CCM ambao kazi yao ni kuunga mkono hoja za kipuuzi ili kuilinda serikali, hata kama hoja hizo zinamuumiza mwananchi wamegundua kwamba wapiga kura wao wanaona mchezo wote na kwamba mwaka 2015 patachimbika huko majimboni kwao. Nadhani hii ndio sababu ya msingi ya hao wabunge kuja na hoja hizi kwani hata mimi katika pita pita zangu, nimeshuhudia hata wanachama wa CCM katika majimbo mbalimbali wenye nia ya kugombea ubunge kupitia CCM 2015 wanakwenda kwenye majimbo ya wabunge wa "NDIYOOOO" na kuwaonyesha mara nyingine video clips jinsi gani wabunge waliowachagua wasivyokuwa in touch na maisha ya wapiga kura; Sitashangaa kama hoja hii itapitishwa kwa vigezo kwamba bunge limekuwa la kihuni na lililokosa maadili kwahiyo wabunge wajirekebishe kwanza n.k;
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!
CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
all the nonsenses that have been taking place with this crucial institution were the 'beginning of the end' but by this move, it's obvious "the end of the end"!Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!
CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!
CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
Spika wa Bunge amesema kuwa baadhi ya wabunge wanaandaa hoja ya kuzuia vipindi vya Bunge kuonyeshwa LIVE kwa wananchi!
Ninavyochukulia: Huku ni kulewa Madaraka!...Wanataka wachape usingizi bila kuhojiwa na wapiga kura hawa!
CHANZO: Gazeti la Mtanzania leo 13/08/2012
Spika hana lolote,hiyo hoja lazima kaianzisha yeyemwenyewe! ashindweee!!
Na hotuba ya Mr.White aka Dhaifu isionyeshwe live... Kazi ya TV ya serikali ni Wedding showz au ze comedy?
Ni kitu gani kinachokufanya utuhumu kuwa ni wabunge wa ccm? Bunge lote hilo si wa CCM wala Chadema ni wababishaji tu huo ndio ukweli wenyewe na ndio sababu zaidi ubishani hakuna kinachofanyika; kimsingi hao si wabunge ni makada wa vyama wabunge karibu 90% ni vituko tu hata kuchambua bajeti hawajui hata hao wa upinzani kusoma bajeti yao wenyewe iliwashinda sasa tutasema tuna wabunge?
Chama
Gongo la mboto DSM
hivi mgonjwa wa nyonga karudi?? lazma atakuwa kwenye list ya wanaopinga! atakesha saa ngapi na vibinti?? MUNGU ATUNUSURU!
Lazima wabunge wa chama cha mabwepande 2 ndo waasisi wa hoja hii.
Kwenye red hapo weka KIFAFA