Wanajamvi,
Wenyewe wanasema 'I stand to be corrected'.
Hoja ya thread ipo wazi na ni dhima yetu tuijadili kama ilivyo na si kama hoja ya PakaJimmy. Tutakuwa tunafanya makosa kwa kumshambulia PakaJimmy kwa hoja aliyosikia na kutuletea. Kwahiyo tuna wajibu wa kuishambulia hoja ima kwa kuitetea au kuikosoa tukiheshimu uhuru wa kila mmoja kutoa mawazo yake katika jukwa hili huru.
Binafsi nimeikataa hoja hii kwa sababu zifuatazo
1. Bunge ni eneo la uwakilishwi wa wananchi na ni mahali huru kwa wawakilishi na wawakilishwi kuwasiliana. Wabunge ni waajiriwa wa wananchi na ni haki ya mwajiri kujua mwajiriwa wake anafanya nini na kwa wakati gani. Hakuna mahali popote duniani bunge limefanya kazi kwa siri. In fact sisi tumechelewa sana katika teknolojia, wenzetu majirani wamekuwa na utaraibu wa kuwa na vyombo vya habari kama Radio na TV miaka dahari.
2. Kuna jambo gani ambalo wabunge wanadhani ni siri na halipaswi kuonekana na jamii wanayowakilisha?
3. Wakati wa kuomba ubunge, wawakilishi wetu walikuja kutushika mikono na hata kupiga hodi majumbani.
Walifanya hivyo kwa kuelewa kuwa tulihitaji kuwajua kwa mambo mengi:
Jinsi wanavyowasilian nasi (communication), wanavyojenga hoja (Argument), wanavotusikiliza na wanvyotujibu (communication tena), wanavyojistahi(behave), ucheshi wao (humour), weledi wao( intellect) n.k.
Hawakufanya hivyo kwa kutumia mikanda ya kaseti au kupitia radio au video, walikuja na kutushika mikono tena wakigonga nyumba zetu na kufunguliwa na mahausi geli.
Iweje leo wanapotuwakilisha wahisi kuwa hawana haki ya kuonekane wakitetea sifa hizo hapo juu zilizowapeleka Dodoma?
4. Teknolojia ya mawasiliano imemleta mwanadamu karibu na mazingira yake. Ilianza ya audio kama radio na hatukuwahi kusikia malalamiko, sasa TV ambayo inatufanya tuwe karibu na mwakilishi wetu kwanini ionekane kama ni chombo kinachojenga uadui kati ya mbunge na mwananchi?
5. Ni kwa kipengele gani cha maadilli ya kazi(ethics), haki za mfanyakazi (Labor laws), haki za binadamu (Human right), sheria za nchi (Laws and regulations) amabacho kinakiukwa (Infringed) kwa mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi kuonekana akifanya kazi?
Haya ni maoni yangu na si lazima yashabihiane au yapingane na mtu. Hakuna usahaihi au makosa kwa maoni binafsi ili mradi hayavunji haki za mwingine.
PakaJimmy ameuliza swali la uchokozi pengine kutak kujua nini mtazamo wa hoja ya Mwanakijiji kama ambavyo anaweza kuchagua hoja nilizozitaja na kuniuliza. Yaweza kuwa alitaka kufahamu au ku-provoke ili mtu afunguke zaidi.
Hakuna kosa katika hilo ni sehemu ya ku-moderate nyuzi yake na nampongeza.
Tatizo ni pale tunapoacha mada halisi kwa kuishambulia hasi au chanya na kuanza kushambulia watu (character assassination) au kushambulia wajihi ( personality attack).
Tumetoka nje ya mstari kwa kuacha hoja na yatokanyo na hoja na kuanza kushambuliana. It is very unfortunate!
Ningependa mtu azishambulie hoja zangu na si mimi kama Nguruvi3. Ubaya wa jina langu, uzito au wepesi wa hoja zangu usiwe sehemu ya mjadala.