Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

Bunge Lisionyeshwe LIVE - Wabunge!

ITAWANUFAISHA NYINYIEMU A.K.A MAGAMBA, make hapo wakina wasila watakuwa wanaingia na mashuka pamoja na zile net za OBAMA ndani ya ukimbi wa Bunge na kuchapa Usingizi bila wasiwasi
 
ndio maana hawarushi bunge lte kwenye tbc radio inayosikika nchi nzima, wanaishia kwenye maswali tu maana wanajua kuwa kama wakiruhusu tbc redio irushe bunge muda wote basi hata wanakijiji wasio na tv wanawasikiliza pumba zao wanapokuwa wanabwabwaja bungeni.
 
Hii si habari tena. Ungesoma the Guardian ya juzi Anne Makinda amesema kwamba huwezi kufungia section moja ya media halafu ukaacha nyingine. Hivyo, hakuna hoja ya kukataza TV.

Wanaoropoka na kusinzia bungeni imekula kwao.
 
Wakati nchi za wenzetu kuna Parliament Channels ambazo zinaonyesha mambo ya bungeni tu, kwetu hata kicho kidogo tulichonacho tunanyang'anywa!
 
Kwanza kama kamati ya matumizi inayopitia vifungu huonyshwa live, kwa nini tusionyeshwe hata kamati zingine zinapokaa ili tuone kama huko nako kuna viroja.
 
Ina maana hawataki tupime utendaji wao wananadhan wamejiweka wenyewe hapo. Huyu nadhan atakuwa lukuvi au wasira.
 
ukiona hivyo pata jibu kuwa kuna watu waliomba ubunge ili waweze kujinufaisha mambo yao ya binafsi, so wachotaka kukifanya ni kwamba wanataka kukamilisha matarajio yao,
But for now ni kitu ambacho sidhani kama kitatokea tena, kwani naamini hatuwezi kurudi tulipotoka.
 
Naona sasa wameanza kulifanyia kazi wazo hili!
Bunge halionyeshwi tena!
 
hata ujio wa huyo jamaa yenu Lema umechangia sana, I hate Lema kwasababu amesababisha tukose kipindi cha Bunge live...
Mkuu, ni wewe kweli, au ID yako inatumika kwa siri kubwa na mfanyakazi mwenzio!

images
 


hahahaha! hujasoma vizuri mkuu, hawa TBCCM wanaogopa lakini wanamuogopa sana kamanda Lema, wewe unadhani kwanini wamezima mitambo? ni huyu Lema anayeitikisa nchi aisee, loh! Lukuvi na Pinda ndo wametoa amri mitambo isiwashwe,
 
"....Kama Zitto anaogopa kuwataja walioficha fedha Uswis, anipe mimi List yote, nitawataja dakika hiyohiyo!"
Godbless Lema.
 
Asiyetaka kuonekana live na ajitoe ubunge simple. Unajua hoja yao hii ni kujijengea mazingira ya kukwepa kipindi cha mchakato majimboni when it comes to 2015? Wengi wao hawana hoja ila vijisenti walivyopata kwa njia zisizo halali. kwahiyo chochote kikija live hawataki. Wataumbuka
 
Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?

Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.

.......
Hata mimi ntaandamana, hata wakiweka vifaru.
 
Uwiiii Lema umesababisha tusione bunge live

.......
LEMA NI MWANAZUONI HURU! Wakati ule alipokwenda gerezani kwa hiari watu presha ziliwapanda, na akaja na facts ambazo zilitikisa!

Sasa hivi amekaa kijiweni kwa almost mwaka mzima, akipiga M4C, wanajua kuwa akija lazima ataondoka na mtu! Dawa ni kutoonyesha Bunge Live!
Akili za Abunuwas!
 
Huu ndio utakuwa mwisho wa CCM. Cha kufanya ni kuandaa maandamano ya nchi nzima yakishirikisha watu wa makundi mbalimbali!!! Mimi niko tayari kuingia mtaani. Kinachoonekana CCM ni kushindwa na upinzani kwa hoja kila kona na 2015 ndio hiyooo imewadia. Kila wanapogusa ni moto!!!. Kenya, Uganda na nchi nyingine nyingi wanaonyesha bunge live. Sisi tutakuwa ni kituko cha mwaka. Kwa jinsi ninanyomfahamu Makinda na uwezo wake wa kuamua na kutenda, hili swala laweza kuletwa Bungeni na kupita kwa kura za ndio za wabunge goigoi wa CCM bila tatizo ila kwa hakika madhara yake yatakuwa ni sumu kali zaidi kwa CCM.
 
Back
Top Bottom