Bundi analia juu ya mpapai wangu

Bundi analia juu ya mpapai wangu

Jamani uoga ni asili ya binadamu. Utafiti unaonesha kila binadamu ambaye hajafa ni muoga.

Hapa kwangu yamenikuta, Kuna bundi kavamia, yupo juu ya mpapai analia kwa sauti kama vile anatumia kipaza sauti. Nimemuuliza jirani yangu kwa simu kama hampigii kelele ikiwezekana akamfukuze lakini hajanijibu, nahisi anaogopa. Nimejaribu kuwasiliana na mwenyekiti wa serikali ya mtaa amesema nipambane na hali yangu.

Kuna mwanajeshi anakaa mtaa wa pili kanishauri nimpotezee ikiwezekana niweke head phone ili nisimsikie. Naombeni ushauri
dume zima unaogopa ndege kama bundi....shida kweli kweli...
 
Watu na imani zao za ajabu ajabu huyo ni ndege kama wengine tuu na usiku ndo mida yake anatembea anatafuta chakula... hasa mijusi wa kwenye taa..

Hao wanaokutisha wanaendekeza story za mababu zao za kutishana tishana tuu hii ni sawa na zile story ukichapwa na ufagio unakuwa mtembezi
 
Bundi hula wafu na mizoga na anauwezo wa kunusa mizogo na wafu waliopo kwa umbali mrefu. Watu humuhusisha kuwa anaeza tabiri kunamtu atakufa karibuni endapo atakuja nyumban kwako kulia kwani anauwezo wa kunusa kiumbe ambacho baadh ya sehem zake zimekufa kutokana na maradh hali itakayompelekea mgonjwa kufarik karibuni au asilimia ndogo sana kupona kama atapata matibabu stahiki. Ila hana madhara yoyote unaeza ukaenda mfukuza tu ni viumbe kama vile kunguru.
Au jiulize hapo mtaan nan mgonjwa kama hamna bas kuna msiba gan au kuna mzoga gan labda upo?
 
Huyo ni kiumbe kama kunguru tu...akilia Tausi anaimba..akilia bundi uchuro punguzeni imani potofu Congo huyo bundi watu wanamla na hawapatwi chochote....Tafuta manati mpige nyama yake nzuri ina protin nyingi
 
Ila kiwanja kina mgogoro. Mpapai niliukuta tu, sijui nani aliupanda. Ina maana atakufa?

Mkuu mbona unakwepa sana kuhusu upande alipo bundi? Umeanza kwa kukataa kuwa mpapai uko karibu sana na jirani yako japo mpapai ni wako, haya sasa unasema kiwanja kina mgogoro so unauliza kama aliyeupanda ndiye atakufa. Jibu ni no anayetafutwa hapo ni wewe. Kakope kwa wingi ili ukifa ache madeni yasiyolipika
Rip in advance (utani tu)
 
Back
Top Bottom