Mchango juu ya kilimo cha mahindi kwa uzoefu wangu

Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,371
1,041
Wakuu heri na amani na iwe kwenu ni matumaini yangu kuwa hamjambo kama mimi.

Kabla sijaenda kwenye mada nikiri wazi kabisa kipaji cha kuandika sina ila ninauwezo wa juu wa kusikiliza na kuongea tena bila kipaza sauti,kwa kipaza sauti huwa nashindwa kuongea kwa kiwango nilicho nacho.

Baada ya hayo naomba nianze kutoa mchango wangu wa kimawazo juu ya kilimo cha mahindi kutokana na uzoefu nilionao.

Jambo la kwanza kabisa kilimo kinamuhitaji kwa asilimia kubwa mtu mwenye hobi ya kulima na kwa asilimia ndogo mtu mwenye dhamiri ya kupata pesa kupitia kilimo. Kwanini hivi? Ni kwasababu mtu mwenye hobi ya kilimo hana bajeti ya muda wala pesa katika kilimo chake yeye furaha yake ni kuona mwili wake umechoka kutokana na kufanya shughuli za kilimo/shamba anatofautiana na huyu wa pili yeye ndio anakihitaji kilimo kimkwamue sio kwamba hatafanikiwa ila njia yake haitalingana na huyu wa kwanza (power and concentration zitawazawadia kwa viwango vyao).

Jambo la pili ni kwamba unapoamua kuingia kwenye kilimo cha mahindi vitu ambavyo nakusisitiza sana kwa uzoefu wangu ni viwili tu. Moja eneo mbili palizi ya kwanza. Kwanini? Unapochagua eneo angalia jiografia yake kama inakubali kilimo cha mahindi.

Mapendekezo yangu kutokana na uzoefu wangu, eneo ambalo walau linapata mvua ya 1800mm kwa wiki na kwa muda usiopungua miezi miwili na nusu mfululizo, eneo ambalo ni bonde na linastawisha nyasi ndefu (bonde hupokea mbolea za asili kutoka kwenye miinuko,kukaa na unyevu kwa muda mrefu,kustawisha nyasi ndefu ni kiashiria kikubwa cha aina ya udongo kustawisha mahindi both are monocoty plants).

Palizi ya kwanza ifanyike kwa muda usiozidi siku thelathini na tano 35 ili kutoruhusu mgawanyo wa chakula cha mimea kuwa mkubwa mfano upatikanaji wa nitrogen, mwanga wa juu na madini mengine yaliyomo ndani ya udongo (ki binadamu mtoto mchanga huangaliwa kwa ukaribu sana tofauti na mwenye umri wa kutumwa). Na ukizingatia mwanzo mpaka hapa nilipofikia shamba lako litakuwa linaanza kukuvutia kulitembelea mara kwa mara.

Nyongeza katika uzoefu wangu wa kilimo hiki cha mahindi ni uchaguzi wa mbegu,upandaji na uwekaji wa mbolea ya ziada(ya kiwandani). Katika kuchagua mbegu kwa ajiri ya mapato mazuri mbegu yoyote ya HYBRID hairudiwi mara mbili inapotoka kiwandani huwa ni kwa msimu mmoja tu. Hivyo usinunue kwa mtu ambaye anakuuzia kama sehemu ya mavuno yake. Kuna mbegu fupi na ndefu. Kwa faida ya ziada usije ukapanda mbegu ndefu kwenye eneo ambalo nyasi hazirefuki sana vizuri uzingatie nilichoeleza kwenye upande wa eneo.

Upandaji mstari kwa mstari pima sm 90 na mche kwa mche pima sm 60 panda mbegu mbili mbili itakupunguzia kurudishia kama punje moja haijaota na ikitokea ukaweka mbolea ya ziada kifuniko kimoja cha soda kitatumika kwenye hiyo miche miwili. Uwekaji wa mbolea ya ziada ufanyike nwiki ya tano tangu mche kuota,mapendekezo yangu chukua mbolea ya DAP nyeusi changanya na can kwa kipimo sawa weka kwa pamoja. Kama utatumia UREA weka wiki ya nne tangu mmea kuota ila ili urudi kunishukuru tumia mchanganyiko wa DAP na CAN.

Kama nilivyoeleza tangu awali kwenye uandishi sipo vizuri ila nimejitahidi kadri nilivyoweza.

Nawatakia Pasaka njema na mafanikio mema. Mwenye swali anaweza kuniuliza.
 
Sidhani kama wewe ni mzoefu wa hiki kilimo maana vyote humu ume copy na kupest

God save us
Mhh! Anyway hata nyumba nayoishi asilimia kama 95 ni kutokana na shughuli zangu za kilimo hiki cha mahindi na hivi nipo najiandaa kuvuna ya msimu huu. Ila sipo kubishana juu ya uzoefu wangu nafurahi tu kama mchango wangu umekufikia.Ila kama utakuwa kwa ajiri ya mabishano niletee ushahidi wa hoja yako. I swear nipigwe radi.
 
S
Mhh! Anyway hata nyumba nayoishi asilimia kama 95 ni kutokana na shughuli zangu za kilimo hiki cha mahindi na hivi nipo najiandaa kuvuna ya msimu huu. Ila sipo kubishana juu ya uzoefu wangu nafurahi tu kama mchango wangu umekufikia.Ila kama utakuwa kwa ajiri ya mabishano niletee ushahidi wa hoja yako. I swear nipigwe radi.
Sijapinga hoja yako, maana yangu ilikuwa kwamba; kwa wewe kuwa mzoefu katika hiki kilimo tungetegemea zaidi ya ulichokiamdika maana kiko very common.

Vipi unalimia wapi. Mi mkulima mwenzio.
 
NB: Kuna kitu nilikisahau katika uwekaji wa mbolea nikiwa Tabora kihome home tulikuwa tunatoboa na mtu pembeni ya mche kisha tunaweka mbolea na kuifukia nikasafiri baadhi ya mikoa nikakuta hali ni hiyo hiyo nilijua ndio namna yake mpaka msimu wa mwaka 2013/2014 nakumbuka tulikuwa tunasikiliza radio shutuma za Mh.Lowasa kuwafadhili wapinzani tulimuona mgeni mmoja yeye alikuwa anaweka mbolea bila kuchimba wala kufukia tukaona hii mpya nayo.

Hakuwa mchoyo wa maarifa alitufundisha kwanini inatupasa kufanya kama alivyofanya. Ipo hivi mbolea za ziada huwa zimeambatanishwa na NITROGEN na mmea huvuta hewa ya Nitrogen kupitia vinyweleo vyake (stomata) na mchanganyiko mwingine unatakiwa uyeyuke na kushuka taratibu ndani ya udongo kuifata mizizi iliko. Kwa hiyo nilichokisahau hapo juu ni namna nzuri ya uwekaji wa mbolea ya kiwandani ni juu ya udongo kwenye mche na sio kuifukia wala kutoboa shimo.

Asanteni.
 
S
Sijapinga hoja yako, maana yangu ilikuwa kwamba; kwa wewe kuwa mzoefu katika hiki kilimo tungetegemea zaidi ya ulichokiamdika maana kiko very common.

Vipi unalimia wapi. Mi mkulima mwenzio
Mimi sio mtaalamu wa kilimo nimechangia kwa uzoefu tu nilionao juu ya kilimo hiki na siamini kama kunauchawi mwingine wa mahindi zaidi ya huo. Ila nipo tayari kupokea maarifa zaidi tushushie mbinu mpya.
 
Nakadiria tu ktk kiganjani, alafu naweka ktk mashina mawili hadi matatu kwa kiganja kimoja

Sent using Jamii Forums mobile app
Kipimo kimezidi ila sio mbaya sana wakati wa mahindi kukomaa utakuta baadhi ya mabunzi yanabeba punje kubwa nyeusi na bunzi kuoza hutahitaji kulimenya ili uzione punje litajifumua lenyewe.ni kama asilimia kumi tu ya shamba zima. Chakuomba tu ni mvua
 
Binafsi kilimo, tena cha mahindi, tena mahindi ya kutegemea mvua? Huwa naona kama kucheza bahati nasibu sana.
Afadhali ya kumwagilia.
 
Back
Top Bottom