Ukweli ni kwamba, wabongo wengine wenye Ph.D wana ulimbukeni.
Wanaona kama kuwa na Ph.D ndiyo mwisho wa mjadala.
Wakati si kweli.
Sasa mtu kama Mwakyembe anabishana na Roma, si kwa hoja, bali kwa kulinganisha namba za degree.
Mpaka hapo namuona Mwakyembe ni limbukeni wa elimu.
Kwa sababu mtu aliyeelimika anajua kwamba hata mwalimu hufundishwa na wanafunzi wake.
Ulimbukeni wa Ph.D unachangia sana watu kuona kwamba hao wenye Ph.D hawana lolote.
Sehemu ambazo wameendelea kielimu huwezi kusikia Dr. Condoleezza Rice, Dr. Susan Rice, Dr. Robert Gates anabishana na mtu kwa kusema yeye ana Ph.D. Atabishana kwa hoja tu.
Ukianza kubishana na mtu kwa kusema "mimi nina Ph.D" una invoke authority badala ya ku invoke reason. Unalazimisha kwamba Ph.D yako itakufanya uwe sawa kila mara, kitu ambacho si kweli. Fundi wa gari aliyeishia darasa la saba anaweza kujua mambo mengi zaidi kuhusu injini ya gari kuliko mwanasheria mwenye Ph.D.
Bob Marley hana hata degree moja. Lakini nyimbo zake zinajadiliwa mpaka leo. Watu wanazitumia kwenye kupata Ph.D.
Shakespeare hakuwa na Ph.D, lakini tungo zake mpaka leo zinatumika na watu wanaopata Ph.D.
Tunaheshimu usomi. Sitaki kusomeka kama watu wa Cambodia ya Pol Pot waliochukia usomi. Lakini usomi halisi ni zaidi ya degree. Tusifupishe kwamba usomi ni namba za degree. Kuna watu wengine wana Ph.D, lakini ukiwasikiliza wanaongea mpaka uambiwe huyu ana Ph.D ndiyo utajua. Kwa sababu hawana gravitas ya Ph.D katika kujieleza.
Kufupisha habari kwamba usomi ni namba ya degree ni ulimbukeni katika usomi.
Mtu anayesema hivyo anaonekana kama ni wa kwanza kwao kusoma, bado analimbuka tu.