Bongo ukiwa na PhD lazima uchukiwe

Bongo ukiwa na PhD lazima uchukiwe

Tatizo ni wao wenyewe huwa na show off za kubore outomati watu hujiweka mbali nao
 
Inategemea na PhD ni ya nani.
Kuna ya Mwakyembe ambayo haimsaidii.
Kuna ya gwajiboy ya kiuno feni.
Kuna ya baraza la uchaguzi ambayo hata akiongea kukitetea chama unajua Ina walakini.
Kuna ya Lipumba ni Kali na safi Ila haitumii imeovatekiwa na njaa.
Kuna ya Amour ya miezi tisa Kama mimba.
Zipo mpaka zinazopatikana gesti haus.
Wewe yako ikoje?
 
Waliochafua PhD ni Mwakyembe, Kabudi na lijamaa fulani hivi lilikuwaga likuu la mkoa wa Morogoro.
 
Wenye mamlaka wanakauli zaidi ya wenye utaalamu, kwetu sisi JPM ndiyo jaji, mganga mkuu, mtunga sharia, injinia mkuu , n.k kila kitu hata chenye kuitaji wataalam wenye mamlaka wanaingilia.. Hivyo hata uwe na PhD ukichangamana na siasa lazima jamii yetu ikuone kituko

wazee wa upembuzi yakinifu.

injinia anafanya upembuzi miezi sita ya utanuzi wa barabara,kwanini mwanaisasa asikuingilie akuoshee mbele za wananchi!!!!

angalia bweni la shule limewaka limeondoka na vijana wetu huko arusha,kumbe walikuwa wanalala wanne kila double deker!!!!,wataalam wamelala usingizi wa pono.
 
Unachokizungumzia sijawahi kukiona. Nilichokiona ni wenye hizo PhD wengi wao hawajui kutangamana na binadamu wenzao ndani ya jamii.

Mara nyingi kwa sehemu ya elimu waliyoipata huwa wanawadharau wale wengine ambao hawajapata sehemu ya elimu kama waliyopata wao. Wanakuwa na viburi na dharau.

Matokeo yake yanakuwa huo uzi uliyouleta wewe. Hawachukiwi kwa sababu ya elimu yao, wanachukiwa kwa sababu ya mienendo yao ya kutangamana na watu ndani ya jamii.
Mkuu, habari yako kaka.

Bila shaka upo mzima wa afya.

Kaka mkubwa, ninaomba kutofautiana na wewe kidogo katika hii hoja yajo ya kutangamana na watu katika jamii.

Mkuu, mimi sina Phd lakini watu wanasemaga sijui kutangamana na watu katika jamii ninamoishi lakini mimi huwa siwajali maneno yangu bali ninakuwa nipo busy na shughuli zangu.

Mkuu, watu wameumbwa tofauti sana. Kila mmoja na namna alivyo. Kuna watu wameumbwa ni waongeaji ila wengine ni wakimya sana.

Sasa tatizo linakuja unapokuwa mkimya alafu una Phd. Watu watakusema mpaka basi.
 
PhD sio intelligence don't confuse Education and intelligence
 
Hii imekaaje? Yaani tukimbie umande wenyewe wakati wenzetu wamekakomaa mpaka kapata PhD halafu tunanuna?

Tuache ghilba na chuki dhidi ya wasomi wetu. Kama hatukupata nafasi ya kusoma mpaka PhD tusiendekeze chuki itazidi kutuumiza sisi Kiwango Duni (KIWADU).
Ungefafanua zaidi ukatoa na mifano nafikiri ingekaa vizuri na madam yako ingetoa fundisho na hamasa hatimaye wengi wangezitatuta hizo PhD ahsante.
 
Back
Top Bottom