Bongo ukiwa na PhD lazima uchukiwe

Bongo ukiwa na PhD lazima uchukiwe

Wabongo wanataka mwenye PhD awe na mawazo kama yake wa darasa la saba.

Yaani wanataka wafanane mawazo, bila hivyo mara ni msaliti, mara PhD fake au elimu haija msaidia.

Mtu unalazimisha wa PhD awe na mtazamo kama wako wa darasa la 7.
You nailed it. Yaani chuki dhidi ya PhD
 
Hii imekaaje? Yaani ukimbie umande mwenyewe wakati mwenzako kakomaa mpaka kapata PhD halafu unanuna?

Tuache ghilba na chuki dhidi ya wasomi wetu. Kama hatukupata nafasi ya kusoma mpaka PhD tusiendekeze chuki itazidi kutuumiza sisi Kiwango Duni (KIWADU).
Ukweli ni kwamba, wabongo wengine wenye Ph.D wana ulimbukeni.

Wanaona kama kuwa na Ph.D ndiyo mwisho wa mjadala.

Wakati si kweli.

Sasa mtu kama Mwakyembe anabishana na Roma, si kwa hoja, bali kwa kulinganisha namba za degree.

Mpaka hapo namuona Mwakyembe ni limbukeni wa elimu.

Kwa sababu mtu aliyeelimika anajua kwamba hata mwalimu hufundishwa na wanafunzi wake.

Ulimbukeni wa Ph.D unachangia sana watu kuona kwamba hao wenye Ph.D hawana lolote.

Sehemu ambazo wameendelea kielimu huwezi kusikia Dr. Condoleezza Rice, Dr. Susan Rice, Dr. Robert Gates anabishana na mtu kwa kusema yeye ana Ph.D. Atabishana kwa hoja tu.

Ukianza kubishana na mtu kwa kusema "mimi nina Ph.D" una invoke authority badala ya ku invoke reason. Unalazimisha kwamba Ph.D yako itakufanya uwe sawa kila mara, kitu ambacho si kweli. Fundi wa gari aliyeishia darasa la saba anaweza kujua mambo mengi zaidi kuhusu injini ya gari kuliko mwanasheria mwenye Ph.D.

Bob Marley hana hata degree moja. Lakini nyimbo zake zinajadiliwa mpaka leo. Watu wanazitumia kwenye kupata Ph.D.

Shakespeare hakuwa na Ph.D, lakini tungo zake mpaka leo zinatumika na watu wanaopata Ph.D.

Tunaheshimu usomi. Sitaki kusomeka kama watu wa Cambodia ya Pol Pot waliochukia usomi. Lakini usomi halisi ni zaidi ya degree. Tusifupishe kwamba usomi ni namba za degree. Kuna watu wengine wana Ph.D, lakini ukiwasikiliza wanaongea mpaka uambiwe huyu ana Ph.D ndiyo utajua. Kwa sababu hawana gravitas ya Ph.D katika kujieleza.

Kufupisha habari kwamba usomi ni namba ya degree ni ulimbukeni katika usomi.

Mtu anayesema hivyo anaonekana kama ni wa kwanza kwao kusoma, bado analimbuka tu.
 
Hii imekaaje? Yaani ukimbie umande mwenyewe wakati mwenzako kakomaa mpaka kapata PhD halafu unanuna?

Tuache ghilba na chuki dhidi ya wasomi wetu. Kama hatukupata nafasi ya kusoma mpaka PhD tusiendekeze chuki itazidi kutuumiza sisi Kiwango Duni (KIWADU).
Mwakyembe umeyataka mwenyewe lakini
 
Ukweli ni kwamba, wabongo wengine wenye Ph.D wana ulimbukeni.

Wanaona kama kuwa na Ph.D ndiyo mwisho wa mjadala.

Wakati si kweli.

Sasa mtu kama Mwakyembe anabishana na Roma, si kwa hoja, bali kwa kulinganisha namba za degree.

Mpaka hapo namuona Mwakyembe ni limbukeni wa elimu.

Kwa sababu mtu aliyeelimika anajua kwamba hata mwalimu hufundishwa na wanafunzi wake.

Ulimbukeni wa Ph.D unachangia sana watu kuona kwamba hao wenye Ph.D hawana lolote.

Sehemu ambazo wameendelea kielimu huwezi kusikia Dr. Condoleezza Rice, Dr. Susan Rice, Dr. Robert Gates anabishana na mtu kwa kusema yeye ana Ph.D. Atabishana kwa hoja tu.

Ukianza kubishana na mtu kwa kusema "mimi nina Ph.D" una invoke authority badala ya ku invoke reason. Unalazimisha kwamba Ph.D yako itakufanya uwe sawa kila mara, kitu ambacho si kweli. Fundi wa gari aliyeishia darasa la saba anaweza kujua mambo mengi zaidi kuhusu injini ya gari kuliko mwanasheria mwenye Ph.D.

Bob Marley hana hata degree moja. Lakini nyimbo zake zinajadiliwa mpaka leo. Watu wanazitumia kwenye kupata Ph.D.

Shakespeare hakuwa na Ph.D, lakini tungo zake mpaka leo zinatumika na watu wanaopata Ph.D.

Tunaheshimu usomi. Sitaki kusomeka kama watu wa Cambodia ya Pol Pot waliochukia usomi. Lakini usomi halisi ni zaidi ya degree. Tusifupishe kwamba usomi ni namba za degree. Kuna watu wengine wana Ph.D, lakini ukiwasikiliza wanaongea mpaka uambiwe hiyu ana Ph.D ndiyo utajua. Kwa sababu hawana gravitas ya Ph.D katika kujieleza.

Kufupisha habari kwamba usomi ni namba ya degree ni ulimbukeni katika usomi.

Mtu anayesema hivyo anaonekana kama ni wa kwanza kwao kusoma, bado analimbuka tu.
Usihaingaishe kichwa mkuu,Mwakyembe ana Ph.D ya unafiki hakuna kingine
 
Cha ajabu bunge letu PhD na Profesa za kumwaga lakini watu wanaoishi karibu na Ziwa Victoria wananunua maji ya dumu, mniwie radhi kama sijaeleweka.
Si kazi ya PhD kusolve matatizo yote ya jamii. Maana ya PhD ni mtu ambaye ana jifunze kila wakati kutoka kwa msomi hata na ambaye hajawahi kuingia darasa! Hivyo tunategemea mwenye Phd asiukwaze uongozi kwa kuropoka bali kutumia hekima za kujenga hoja kutegemea na nani anawasiliana naye. Vijana jiongezeni Mpate Phd.
 
Hiyo PhD imeleta manufaa gani tofauti na dili za wizi kwa kushirikiana na wazungu
Hii imekaaje? Yaani ukimbie umande mwenyewe wakati mwenzako kakomaa mpaka kapata PhD halafu unanuna?

Tuache ghilba na chuki dhidi ya wasomi wetu. Kama hatukupata nafasi ya kusoma mpaka PhD tusiendekeze chuki itazidi kutuumiza sisi Kiwango Duni (KIWADU).
 
Ngoja nifikiri kipihedii "mtu hawezi kuwa na utalaamu na uwezo wa kuoa hadi awe na cheti cha kuzaliwa"Kwa hiyo ni vizuri ikawekwa sheria
Kuna jamaa kasema hapo juu, tatizo la wabongo tunataka wa PhD wafikiri kama 'nyie' wa darasa la saba, wakifikiri kiPhD ndio comment kama yako mkuu zinakuja.
Kukimbia umande ni chaguo.
 
Wasomi ni rahisi kuwaona.Mkuu ijapo sikujui lakini nakuheshimu kwani shule huwa haijifichi
Bibie Nina masters ya aquatic Science kutoka uholanzi GPA ya 4.3, ningekuwa sipo kwenye kujiwekeza na kufanya mambo ya biashara zaidi sasa hivi ningekuwa na PhD na full scholarships zipo na nazipata daily. Kwahiyo nilichokiandika nakiamini na kukikubali. Mwakyembe ana PhD ya ujinga hawezi kukana somo thesis take kwasababu ya tumbo
 
Wabongo bana inatakiwa ata mwenye Degree 4 akibaka asihukumiwe miaka 30
Na isiitwe kubaka itafutwe definition nyingine isiitwe kubaka!!
Mnaonaje ijulikane kama kushindwa kuzuwia hisia!
 
Tz kweli wasomi wamekuwa watu wa ajabu sana. Tangu awamu ya tatu, maprofesa waliopata uwaziri ndio waliharibu kabisa.Unajiuliza hivi hiyo digrii yake ni feki au vipi? Hata sasa kwenye awamu hii ni wasomi wengi wamepewa vyeo lakini utekelezaji ni mpaka Rais apite alipo aagize ndipo uanze kumsikia huyo digrii holder akisema anatekeleza agizo la Rais. Maana yake ni kwamba hao wasomi wanashindwa kubuni chochote kupya kwa ajili ya maendeleo ya eneo lao. Hivi yule aliyesema watu wasipooa wachapwe vibokao ana digrii ?
 
Hii imekaaje? Yaani ukimbie umande mwenyewe wakati mwenzako kakomaa mpaka kapata PhD halafu unanuna?

Tuache ghilba na chuki dhidi ya wasomi wetu. Kama hatukupata nafasi ya kusoma mpaka PhD tusiendekeze chuki itazidi kutuumiza sisi Kiwango Duni (KIWADU).
Hawachukiwi kwa sababu ya Phd (Pull her/him down) zao, bali wanachukiwa kwa kwa dharau na matendo yao yasiyo lingana na elimu yao.
 
Kuna mkuu wa mkoa wa Moro(PHD) ya mambo ya food security wkt Magu anaingia alitengua uteuzi wake jamaa likaanza kulia lia eti ooh eti hata yohana alimezwa kwny tumbo la samaki sijui nini nisamehe baba.Matunda ya PHD hayo

PHD-Permanent Head Damage
PhD ni PhD tu kila fani inamtegemea mwenzake.Wewe lete dharau wenzako wanatengeneza Maisha
 
Back
Top Bottom