Bongo Star Search 2009: Burudani kweli!?

p funk zamani ilisemekana unatumia kilevi aina ya bangi sikuamini lakini kwa sasa naanza kuamini kwamba unatumia kilevi hicho..... kwanini unafanya hivyo lakini? sijakupenda hata kidogo mkubwa jirekebishe plz!!

kama ulifuatilia kipindi kwa umakini ilifikia mahali baadhi ya matusi aliyokuwa akiropoka yakawa 'yanafichwa' kwa manufaa ya watazamaji.hata tukisema abadilike, na kweli akabadilika, itakuwa ni baadae kwenye final kwa kuwa hivyo vioja tunavyovishuhudia vilijiri wakati wa preliminaries huko mikoani. kwahiyo tutegemee kuendelea kushuhudia maoni ya bangi. Na mimi kwa mtazamo wangu inaonekana jamaa bado anakula msuba, kwa mtu mwenye akili zake kamili hawezi kudhalilisha wadogo zetu kiasi kile, isipokuwa mwenye kutumia sigara kubwa!!!!!
 
Kwa kweli inawavunja moyo washiriki. Kwani ukimwambia mshiriki umejaribu kaongeze juhudi itakuwaje? kwa lugha zenu chafu majaji mnaua vipaji badala ya kuvikuza. Hivi Tanzania hakuna majaji wazuri zaidi ya hao vichaa wawili Master J. na huyo P-Funk sijui nani mzee wa majani?
Madame Ritha waondoe kabisa hao jamaa wawili wanapunguza umaarufu wa kipindi . John Kitine yuko wapi?
 
Kwa kweli inawavunja moyo washiriki. Kwani ukimwambia mshiriki umejaribu kaongeze juhudi itakuwaje? kwa lugha zenu chafu majaji mnaua vipaji badala ya kuvikuza. Hivi Tanzania hakuna majaji wazuri zaidi ya hao vichaa wawili Master J. na huyo P-Funk sijui nani mzee wa majani?
Madame Ritha waondoe kabisa hao jamaa wawili wanapunguza umaarufu wa kipindi . John Kitine yuko wapi?[/QUOTE]

Bora ajipumzikie tu kama ni uamuzi wake. na hata kama kapigwa chini ni sawa tu. Nasema hivyo kutokana na jinsi ambavyo watanzania walivyokuwa wakimuamini kwakuwa ni mwanamuziki nguli lakini naye akaishia kufuata mkumbo akawa anaburuzwa na salama utadhani hajui muziki!!!Kama ritha angekuwa anasikiliza ushauri, master J asingekuwa jaji kwa miaka yote hii, na wala huyo mvuta bangi hangekuwa jaji. Lakinin huwezi kujua bana labda master J ana hisa kwenye hiyo 'project' kwahiyo lazima ashiriki kikamilifu mwanzo mwisho.
 
Niliangalia kipindi cha bongo star search cha j4 usiku,jaji p funk majani alipomuambia yule mshiriki akatafute mashuga mummy kwakuwa hajui kuimba,tv ilipomuonyesha jaji rita paulsen alionyesha kujikausha huku akichezea simu yake( kwa mara ya kwanza toka kipindi kuanza alikuwa serious), inaonyesha hiyo hoja ilimgusa yeye direct na huyo mtoa hoja alikusudia kumfikishia ujumbe yeye.
Rita ana umbo zuri,kuna mtu mwenye kujua age yake anijulishe?
 
Niliangalia kipindi cha bongo star search cha j4 usiku,jaji p funk majani alipomuambia yule mshiriki akatafute mashuga mummy kwakuwa hajui kuimba,tv ilipomuonyesha jaji rita paulsen alionyesha kujikausha huku akichezea simu yake( kwa mara ya kwanza toka kipindi kuanza alikuwa serious), inaonyesha hiyo hoja ilimgusa yeye direct na huyo mtoa hoja alikusudia kumfikishia ujumbe yeye.
Rita ana umbo zuri,kuna mtu mwenye kujua age yake anijulishe?


...ili ufanyeje, mwana! :rolleyes: :rolleyes:
 
Hata mimi nilikitazama lugha ya huyo jamaa haifai kabisa mimi nataraji kama wenyekuendesha kipindi hicho na mkurugenzi wa station hiyo ya TV ni wastaarabu basi watamuondoa katika ujaji.vinginevyo mamlaka husika kama zinajali majukumu yao wachukue hatua.
 
nikusahihishe bangi sio kilevi ni kiburudisho.......
....bangi inafanya uwe na akili ya ziada na mawazo mbadala sio kama ya p funky....tafadhalini sana msihukumu bangi


We Yo Yo nani kakwambia bangi inakufanya uwe na akili!!? Bangi inakufanya uwe na Hasira nyingi na Nguvu kidogo. Sasa Jaza mwenyewe wacha kupotosha watu
 
We Yo Yo nani kakwambia bangi inakufanya uwe na akili!!? Bangi inakufanya uwe na Hasira nyingi na Nguvu kidogo. Sasa Jaza mwenyewe wacha kupotosha watu
inaelekea wewe unaikosea, unatakiwa uwe na chakula tumboni kabla!
 
nyie watu ni washamba sana.. tafadhalini mgoogle simon cowell!.. that is reality tv
 
Jamani.. hivi mapaka sasa hamjajua hii ni Reality show.. its meant for entrtainment.. producer wa show yeye ndo nataka vitu kama hivyo na anavi encourage kwasababu vina ongeza viewers.. ikiongeza viewers wao wana benefit though matangazo na njia nyengine.. ila the whole concept is to get u fired up vitu kama hivyo na hype..
Au hamkusika kua jaji alimjibu rudi mtoto mdogo kwenye show moja kama aina hiyo hiyo huko india. mtoto akajaribu kujiua.. akashindwa kwasababu ya remarks za jaji.. na jaji hakushtakiwa wala nini??
au aukusikia the famous show American idol ambapo Paula alimmaindi porducer kwa mui entertain a fan ambaye alikuwa stalker.. akaishia kujiua nje ya nyumba ya Abdula???
Ts for entertainment

Kwahiyo unatuambia nini? Wewe unafurahishwa nahaya? Au kuna haja gani ya kuiga upuuzi eti kwavile tu Wamarekani na Wahindi walifanya hivyo?
 
Wanajamii,
Leo kwa mara ya kwanza nashuka katika jamvi hili nikiwa na maswali ya kuuliza. Napenda kuuliza kwa kuwa sina uhakika kama ninafahamu maana ya neno la kingereza “celebrity” …yaa inaweza ikawa ni umaarufu au kusema ni mtu maarufu. Kama ndiyo hapa ndani ya nchi yetu nzuri Tanzania watakuwepo “celebrity” wengi sana. Lakini pamoja na kuwa nao kuna mambo yanafanywa na hao watu ninaowaita maarufu ambayo hayana maana kabisa katika jamii yetu. Hivi Juzi Jumapili ya tarehe 10 Mei, 2009 nilibahatika kutazama kipindi maarufu kwenye Luninga kinachokwenda kwa jina la “Bongo Star Search” kinachorushwa na Stesheni ya ITV. Kuna hawa watu maarufu…ni maarufu kweli na hata kipindi chenyewe ni maarufu lakini kwa sasa naona kama kimekwishapoteza umaarufu. Maswali yangu ni haya: Hivi nini maana ya kipindi Hiki? Kwa ajili ya nani? Je washiriki wale wanavyotendewa na hao majaji (Judges) au kwa lugha ya kawaida waamuzi ni sahihi? Iweje kutumia lugha chafu kwa washiriki? Kuna mifano kama miwili iliyojitokeza juzi…..moja kwa mwanadada na wa pili kwa mwanakaka….. walilalilishwa kwa kweli.
Mwanadada: Aliimba kwa kadiri ya uwezo wake. Wakati wa majaji kutoa comments zao….mmoja alidiriki kumwambia huyu dada hawezi kuimba anachodhani anaweza “aende akazae tu” Hii maana yake nini? Ndio kujaji kweli? Halikadhalika;
Mwanakaka: kama alivyofanyiwa mwanadada naye kaambiwa akatafute “ma – sugar mummy” kwa vile alikuwa “smart” Mtanashati…..inatisha…
Sikuweza kujua kama kweli huyu Jamaa ana akili nzuri. Naomba nimtaje tu kwa sababu nia ni kumrekebisha na si kumsema vibaya. Ni kati ya wale majaji watatu anajiita P Funk. Mimi Binafsi na labda baadhi ya waliobahatika kutazama kipindi kile hafurahishi kwa comments zake. Anajaribu kuwe critique kama alivyokuwa Salama Jabir lakini si ki-hivyo. Ajaribu kuwa yeye asifanye vitu kwa kuiga…lazima ataharibu.
Naomba tujadili hili kwa busara kwa ajili ya kuboresha kipindi vinginevyo sijaona maana yake kama hali itaendelea kama hivi. Umaarufu usiwe kero….
Hapo kwenye bold ni neno la kudhalilisha na nilidhani BASATA wangeuliza mantiki ya kutumia lugha dhalili kama ile.
Mnakumbuka ile big braza ya UK iliyofanyika uingereza miaka fulani nyuma, kuna mwanadada alifanya bulying kwa mshiriki kutoka India ambapo matata yake hayakuwa madogo.
Mimi nashauri vyombo vinavyohusika kumulika hivi vipindi kwa sana tu. kwa kuwa maadili siku hizi si ishu basi waangalie kama UTU unalindwa ktk hizi rialiti showz. Mimi nimeacha kabisa kuangalia hiki kipindi since mwaka jana na pia hata habari zake kwenye magazeti naziepuka.
 
Kweli majani anabowa amekifanya kile kipindi kipoteze maana halisi ya kutafuta vipaji. Wale wanaokwenda pale nikwa wanaamini kuwa wanaweza sasa zile kauli matusi,kejeli zinawakatisha tamaa.
Rita jaribu kuwashauri hao unaowaona kuwa ndio majaji kuwa kile kipindi kinaangali hakiangaliwi na wake zao ama wahuni wenzao kinaangaliwa na watu wengi marika tofuti hivyo wafuate maadaili sio kubwatuka mambo yasio faa.

Jambo jingine hivi kweli kabisa Rita ulikosa waalimu waliobobea ktk muziki wanaojua nini maana ya sauti mtu anawezaje kucheza na koo lake kama Mzee Kitime ukaenda kuwaokota hao viokote vyako wanao jiona kuwa wanajua muziki kumbe ni wizi mtupu.

Ushauri wa bure Rita wewe ni mtu mzima jaribu kuwakanya hao vijana wako kuhusu matumizi ya lugha na utafute waalimu halisi wanao jua muziki Tanzania ina waalimu wengi sana wanao jua muziki, ukiendelea na hao vibweka vyako hadi mwisho kipindi kitapoteza maana ya kuibuwa vipaji.
 
Madame Rita, waondoe hao majaji wako mara moja la sivyo project nzima itakosa maana na itaonekana kuwa ni ya kihuni. Mlianza vizuri lakini sasa mnakosa mwelekeo.

Hata kama ni ofisini mtu amekwenda kufanya interview, akifanya vibaya haambiwi maneno ya kejeli kama ya hao wahuni wanavyofanya. Hebu wawe wastaarabu na waache mara moja kuwadhalilisha wasanii vijana wetu, la sivyo tunaangalia namna nyingine ya kushughulika nao. Komeni nyie.
 
Son of Alaska,
Hebu na wewe tukana uone kama utasalimika. Ustaarabu ndiyo utamaduni na jadi yetu waTZ, lakini kwa staili hii mhh!!!
 
Ama hakika washiriki waliojibiwa majibu hayo ya kudhalilisha ya huyo anayejiita P.Funk... Kama hawatapata counselling wanaweza wakapata hali ya mfadhaiko wa akili...Haswa yule dada aliyeambiwa nina-nukuu "HUJUI KUIMBA...KAZAE HUKOO...TOOOKA ...MLANGO ULEEEE..." Mimi binafsi nilisikitishwa sana na kauli ile na zaidi pale alipomuambia yule aliyekuwa akiitwa Joachim...(Master J anaiitwa Joachim) Nina nukuu "Joachim wote ni vichaa..." Bora hata Salama Jabir huyu anayejiita P.Funk... Kazidi... Rita Paulsen... Kumbuka Coca-cola Pop star ilivyokuwa bomba... Ni hayo tu

aisee! imebidi nicheke aisee.. eti tokaa mlango ulee
 
Hawa majaji si P-Funk tu peke yake, bali na wengine wanatumia lugha ambayo haifurahishi wala kupromote vijana, wanaonekana wanaarrogance fulani na hata huo ujaji sijui walisomea na kujifunzia wapi. Kama wapo kwenye mtandao huu nawaomba wabadili kauli zao wazotumia kwa washiriki wa bongo star search
 
I think to them is another way of entertaining the viewers. Creativity ya kipindi Zero, Majaji mhh labda Dada Rita na Mzee Kitime lakini hao wala ndumu, mibangi inachemka kwa kichwa. Basata na MSI wamelala wapi au mpaka siku akashifiwe mtoto wa mnene ndio washituke? na wadanganyika wenzangu twapenda short-cuts na uvivu, kwani kazi lazima kuimba? na kama kuimba lazima kaimbe kwa church au hata kwenye kwaya za kisiasa tu. Wenye busara wamekaa mbalii na hiyo Bange Star Search.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom