Bongo Star Search 2009: Burudani kweli!?

mkuu hivi timu ya Bongo star search unaiangaliaje? ile ni project ya watu,lakini sio kusaidia wasanii watoke,unajua hata biashara ukiendesha uwezi fanya running cost zizidi mpaka faida isionekana mambo hayo ni kwa wanaojitolea tu,lakini sio mjasiriamali ritta,jaribu angalia star search za wenzetu,ukisikia winner ujue basi ni winner kweli,na hata aki release song inakua hott,nadhani haitoshi kumpa contract ya album winner,lazima na viambatanishi vingine vya lazima ili huyo msanii aweze toka atimiziwe, ila kwa ajili imekaa kijasiriamali zaidi na walianza na wadhamini wadogo tunapoelekea income ikiwa kubwa(vodacom,labda tusker na kampuni zitakazovutiwa na kipindi kurusha matangazo),basi yatafanyika yanayofanyika nchi zingine ili msanii atoke na mjasiriamali abaki na profit,huo ni mtazamo wangu juu ya bongo star search
 
Nadhani Kiwanda cha sanaa ndiyo moja ya sehemu ambayo haina zengwe la kututoa kama madini, sijui teknolojia, mafuta na vinginevyo vinavyoleta vita kila mahala. Kinachohitajika kweli ni sapoti ya wale wenye vipato vikubwa na hawajui wafanyie nini. Fungueni basi hata vyuo ili wasanii wetu wawe professional. Naamini kuna watu wengi wenye vipaji vya kuwafanya hawa vijana hata wawe bora zaidi lakini bado imekaa kushotokushoto. Yaani bora nikamfanyie kazi bepari jioni niingie kny kapremio kangu home nikacheki hollywood highlights. Lakini potentio moyoni zimo, madirectors, producers na kadhalika ila hailipi mazee! Sijui ni nani anatakiwa afanye nini
kwenye bold najibu hoja zako mkuu

    1. Umesema kiwanda cha sanaa ambapo labda ulimaanisha cultural Industry ambapo kwa kiswahili tunaita Tasnia ya Utamaduni ambapo sanaa inapitia hatua zote muhimu za uzalishaji kabla ya kufika kwa walaji. Hapa ninaongelea mass production ya arts ambapo kwa kiasi fulani sanaa ya muziki imejaribu kujinyumbulisha vizuri ingawa wahusika hawafaidiki ki hivyo. Hawa kina Benchmark wanapozalisha wasanii kwa kuwashindanisha na kuwatrain ili waje kuzalisha vipande vya nyimbo zao, wanakuwa wamewafanyia kazi njema wasambazaji (wahindi) ambao watawadaka hewani hawa vijana baada ya search kuisha na kuwagharimia kuingia studio kisha wanawalima mbele kwa mbele. Pia Kwa kuwa wasanii wa muziki wachanga wanaingia kwenye game wakiwa hawajui lolote na wala hawatoi nafasi kujifunza lolote basi wamekuwa ni victim wa walafi wachache ambao ni prodyuzas, wasambazaji na mameneja wao (redio presenters). Ninaamini elimu na usimamizi mzuri wa tasnia hii ndiyo mkombozi wa wasanii kudhalilika kivile
    2. Umesema kuhusu vyuo. Naweza kusemakwamba hilo nalo ni utata mtupu kwani bado kuna ombwe la waalimu na mitaala ambapo since sehemu kubwa ya sanaa imekuwa ni sehemu ya utamaduni basi watawala wetu wameipiga teke. Kuna kitengo cha sanaa na maonesho pale chuo kikuu ambapo mahala kilipo ni eneo la gereji I I mean it. Na hata admission ya pale imekuwa as if ni escaping route kwa wanaoshindwa kuingia vitivo vingine. Ndo maana tuna wasomi wengi wamegraduate sanaa pale ila hakuna lolote linaloonekana. Sana sana wasanii makini wanabaki ni wale ambapo hawakupata elimu rasmi ya pale. Nasema hivyo nina ushahidi kwani mimi nimekuwa victim wa mda mrefu kunyimwa kupata nafasi ya kusoma pale UDSM kitengo cha sanaa kusoma. Niliwahi kudokezwa kwamba malekcha wa pale wanaogopa candidates ambao wapo practicals kwa kuwa watatishia nafasi zao pale chuoni. Lakini sisi tulio mtaani tunajitahidi kupunguzwa ombwe kwa kutoa ujuzi na elimu kwa wasanii wachanga wenye nia. Na suala la ufunguaji vyuo bado ni tata kwani process zake ni balaa n asana sana watakwambia nenda VETA ukaombe vibali. Hatuna art thinkers wa kutosha nchini, hata critical hawapo na huwezi ukaniambia kwamba mtu kama Salama au Master J nao ni art critics.

    Ni budi ziwepo sera za wazi kuweza kuibua maswali na majibu ktk kuboresha sanaa yetu nchini. Tutaishia kuingia ktk nominations za kimataifa lakini hatutafika mbali.
 
Ni kweli ukiangalia vipindi vya Bongo Star Search utasikitika sana - yaani maneno wanayoambiwa yanaumiza sana - hata kama mtu hawezi - sio kumkebehi, kumtukana na kumdharau - kuna judge mmoja kaingia safari hii - amechora chora mikono yake - kwa kweli I HATE THE WAY HE IS TREATING OUR YOUNG TANZANIANS TRYING TO WIN SOMETHING FOR THEIR LIVES - SOMEONE CHECK IS HE A TANZANIAN REAL???????? Kama kuna mtu anaweza kuwafikishia ujumbe hao judges ni kuwa WAWE WASTAARABU, NA WAJUE HAO VIJANA WAMEJIPANGA HIVYO WAWATENDEE HAKI -
 
...and politics is more than LIFE (angalizo: Kolimba, Moringe, Mwaikambo, Chifupa et all)

kaaz kwel kwel. Ila kama alivyosema mdau mmoja, hawa benchmark hawana mikakati ya muda mrefu na hawa wasanii. Kuna kitu wanakipata hapa ktkt na ndo inakuwa mwisho wa mchezo. Congo uchumi wa raia (micro level) unategemea muziki. Sasa hapa siasa hatumo, madini, kilimo, utalii, etc. Hata muziki ambao vijana wanapikwa na kina rita unashindwa kututoa? Bora kina THT na wasanii wao ambao wana mikakati
 
Hamna kinachonikera kama jinsi ma judge wanavyowabeza hawa washiriki.
Mtu amepiga mstari masaa kibao na kupoteza muda wake pamoja na kutaka kuwania hizo zawadi lakini ingebidi wawashukuru kwa kuja kwao pale hata kama mtu ameimba(perform )zero.
Utakuta wanamwambia mtu,nenda kapike-hapa si kwako,nenda kaolewe na matusi mengine makubwa zaidi na kejejeli nyingi.Kama wengine hamjayaona hayo niwiweni radhi labda nimeona vibaya.

mwakani wakitangaza BSS then asitokee mshiriki hata mmoja ndio watajiju na matusi yao. Sijui watamjaji nani
 
Serikali yaishukia Bongo Star Search
• Wapewa onyo, wakikaidi kufutiwa kibal

na John Joseph


amka2.gif

SERIKALI imesikitishwa na kulaani vikali udhalilishwaji unaofanywa na majaji wa programu ya kusaka vipaji vya wasanii, ‘Bongo Star Search’ (BSS), kwani wamekuwa wakitumia lugha chafu isiyostahili kutumika mbele ya jamii iliyostaarabika.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Ghonche Materego, alisema wakiwa wasimamizi wakuu wa shughuli za sanaa, wanalaani vikali kilichofanywa na Bongo Star Search chini ya Kampuni ya Benchmark Production.
Materego alisema, kadiri siku zinavyosonga mbele, majaji wa programu hiyo ambao ni Rita Paulsen, Master Jay na P. Funk, wamekuwa wakivuka mipaka, kwa kuwadhalilisha washiriki, kitu ambacho ni kinyume cha maudhui ya programu hiyo, kwa mujibu wa maombi ya Benchmark Production.
Alisema, kwa muda mrefu majaji hao wamekuwa wakilalamikiwa, ingawa si kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa, lakini wameshindwa kubadilika, hivyo wanatoa onyo kali dhidi ya majaji, programu na BSS kwa ujumla.
“Tunashukuru Watanzania kuonyesha wanajali vitu vya kwao, hii si mara ya kwanza majaji wa BSS kulalamikiwa, kwani hata mwaka jana yalikuwepo, lakini safari hii hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema Materego huku akionyesha kukerwa na kitendo hicho, Materego alisema majaji wanapaswa kujua vijana (wasanii) ni binadamu kama wao (majaji) na kuwataka kuwa na moyo wa kibinadamu badala ya kuudhalilisha utu wa vijana hao.
“Kama ni njia ya kunogesha kipindi, wahusika wanapaswa kutafuta nyingine, si kuwadhalilisha vijana wenye nia ya kutaka kujikwamua kimaisha kupitia tasnia ya sanaa ya uimbaji, kitu ambacho kinaungwa mkono na Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
“Rais Kikwete aliahidi kutoa ajira milioni moja, kwa jinsi BSS walivyoleta maombi yao, ilikuwa ni lazima mwisho wa siku vijana wanufaike na ajira. Sasa kama ajira zenyewe zinapatikana kwa manyanyaso kiasi hiki, sidhani kama ni sahihi,” alisema Materego.
Aliongeza kuwa, anaamini majaji hao ni watu wenye taaluma, ni imani yake kwamba, watajisahihisha, yaani kuwapa heshima washiriki hao ambao ni Watanzania wenzao, badala ya kuwachukulia kama wadudu.
“Naelewa majaji wanapata changamoto kubwa ya kukutana na vijana wengi katika muda mfupi, lakini hiyo isiwe sababu ya wao kuwatukana na kuwatolea lugha chafu washiriki,” alisema na kuongeza:
“Master J na P. Funk ni wafanyabiashara, kwani wanamiliki studio za kurekodia, siamini kama huko kwenye studio zao wanawafanya kama wanavyowafanya kwenye BSS,” alisema Materego.
Alisema, itakachofanya BASATA ni kukutana na uongozi wa Benchmark Production haraka iwezekanavyo kujadili suala hilo na kama wahusika wataendelea na udhalilishaji, watasimamisha au kuifuta kabisa programu hiyo. Hii ni mara ya tatu kufanyika kwa shindano hilo ambalo hurushwa na kituo cha ITV. Mshindi wa mwaka 2007, alikuwa ni Jumanne Iddy kabla ya Misoji Nkwabi kushinda mwaka jana. Mei 17, Gazeti la Tanzania Daima Jumapili (gazeti dada na hili), lilikuwa na makala iliyozungumzia namna vijana wenye fikra na nia ya kujikwamua kimaisha kupitia sauti zao (achilia mbali kama wana vipaji au la), wanavyoishia kuvuliwa thamani ya utu wao na majaji wa BSS.
 
Ndio bwana angalau serikali imenena. Nadhani mwenye shida hapo ni P-funk tu. Wengine wako poa. P-Funk anadhalilisha watu.
 
Good serikali,huyo P-Funk labda haongozwi na akili peke yake anachanganya na vitu vingine. Vibaya kuwakatisha watu tamaa kwa kejeli.
 
afadhali serikali imeliona hilo,cjui wanavuta bange wale majaji au maana maneno wanayowapa washiriki cyo mazuri lakini majani na masster j wamezidi,wamesahau kwamba hata wao walihangaika kutafuta ila kama wangekuwa wanapewa maneno machafu kama wanavyowapa hao vijana wasingefika hapo walipo wakumbuke kuwa hata mbuyu ulianza kama mchicha,si waangalie wenzao wa tusker project fame walivyokuwa wanafanya?ila majani acha kuvuta jani ndo maaana unatoa majibu ya kipumbavu.ni hayo tu
 
BASATA nawashkuru sana mmeona hilo. Ninachefuka sana na programme yao hii. Ni jambo zuri kwa vijana wanaochipukia mziki ila wanavyoiendesha ni sanii na matusi tu, hakuna heshima kabisa. Na mbaya zaidi kudharau washiriki wanapokosea. Ingekwa ni waalimu wa madarasani basi nina hakika darasa hilo lingekuwa zero lote. Yaani utafikiri ni lugha za kule mitaa shimoni kariakoo. It is not worth hasa kwa madam Ritta!
 
Good serikali,huyo P-Funk labda haongozwi na akili peke yake anachanganya na vitu vingine. Vibaya kuwakatisha watu tamaa kwa kejeli.

Duh, umenikumbusha Jaji wao wa mwaka jana aliyeitwa Salama. Nilikwa simwelewi yule dada na sidhani kama alikuwa na akili timamu au ndo kulewa mambo ya Majuu. Sijui yuko wapi siku hizi Dada Salama.
 
Inatia moyo kwamba Serikali imelitupia jicho hilo. Kweli majaji wamekuwa wakiwadhalilisha mno washiriki na pia kuwavunja moyo. Yaani mshiriki anafukuzwa kama mbwa na mbaya zaidi bila kuelezwa wapi anakosea, na hata akielezwa inakuwa si kistaarabu hata kidogo. Si P-Funk tu, hata Rita mwenyewe, pale wanapotizamana wote na kuangua kicheko, ni ishara ya kukosa ustaarabu. Bora hata Salama alikuwa anampa mtu sure. Lakini BSS ya sasa, haina mvuto kabisaaaaaa!
 
Serikali imechelewa sana kuchukuwa hatua kali kwa benchmark production na hawao wanaojiita majaji. P- funk na master J. Hawa majaji wana elimu gani ya music? Wote ni wababaishaji tu na sasa wameamua kutumia jukwaa la bongo star search kutukana vijana wa kitanzania.

Je benchmark production inania ya dhati ya kukuza vipaji vya vijana wa kitanzania au ni sehemu ya kupata pesa kutoka kwa wadhamini kama Vodacom? Swali rahisi je mshindi wa mwaka jana ametoa nyimbo ngapi na je zimekubalika? Ni bora Benchmark wajifunze kutoka THT (Tanzania House of talents).
 
Serikali sielewi inakemea nini wakati ime-prove failure na yenyewe ndio source ya yote haya. Serikali iliyopo madarakani pamoja na kushika hatamu kwa zaidi ya miaka 40, ndiyo imesababishia kilema wananchi kiasi cha kukosa matumaini na kusababisha vijana kuwa na mawazo ya mkatomkato..sasa hivi vijana mashuleni akili zao zipo kwenye miziki na kutoa singo. Hawana mawazo mapana .. kama wamerogwa.

Ukifungulia TV ndio hayo mambo ya BS (maybe its reaallly bull shyt) na miziki ya kuacha miili wazi huku wakijinyonganyonga viuno. Halafu mbele serikali hiyohiyo inakuja kulalamikia suala la mimba mashuleni na ongezeko la maambukizi ya HIV..oxymoronism. Wenye TV wanaacha kutilia mkazo kwenye fani zitakazochochea ubunifu utakaoleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii yetu wanaishia huku kwenye BS..
 
bhagosha,

P-Funk a.k.a MAJANI, ivi mwategemea nini?? naye baada ya kuchanganya hayo majani yake ndio ajifanya anamwigilizia Da Salama jamani, Huko ni kutotaka boresha vipaji vya wasaniii,

P-Funk a.k.a na Master J wote ni maproducer sasa hapo kweli me sijawaelewa wao nia yao thabiti kwa hao vijana? wanataka kuwasaidia au kuwanyongea kati?

maana vipaji vikiwa vingi na maproducer nao wanaongezeka ndani ya nchi kwa hiyo soko kwao linashuka, Tizameni hili jambo kwa jicho la 3

Leka nize
 
Hivi ngoja niulize, nani alichaugua P-Funcky na Rita kuwa majaji, na je waliwekwa kwenye mashindano na wakafanya interview na kufaulu au waliokota tu.Mimi nadhani BASATA ingechukuwa nafasi ya kufanya interview na kuchagua majaji wakuendesha kipindi.Naona kama hao wote wamechaguliwa kwa umaarufu wa kishamba walionao.Unajua wanaropoka wakidhani wao ni maarufu ao watu,si dhani kama ni maarufu, BASATA chagueni majaji wa kuendesha kipindi,vigezo vitumike, yaani wekeni qualifications na mtangaze watu wa apply, sio mchague kwasababu jamaa ana studio, anaweza kuwa na studio kumbe ni mfanyabiashara hana ujuzi wa hiyo fani.Ndio maana wanazungumza ovyo tu, hawajui maadili ya kazi hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom