Bongo Star Search 2009: Burudani kweli!?

Son of Alaska,
Hebu na wewe tukana uone kama utasalimika. Ustaarabu ndiyo utamaduni na jadi yetu waTZ, lakini kwa staili hii mhh!!!
WE MZEE,mbona mnaishusha hadhi JF,naamini maadam wewe ni member humu unaweza tofautisha pumba na mchele.hiyo ni reality show na 90% ni STAGE MANAGED lengo ni watu kama wewe mpige kelele hili watu wakachungulie.people like you ndio mlikuwa mnamuona HULK HOGAN ni wrestler mkali wakati all along matokeo yako fixed
 
P funk ni mvuta bange jamani..
Hajui alitendalao,
wakati wa michuano ijayo kuweopo na screen ya hali ya juu ili majaji kama huyu mvuta bange wasiingie ili kunusuru heshima na utu wa mtu
 
Wanajamii,
Kuna mifano kama miwili iliyojitokeza juzi…..moja kwa mwanadada na wa pili kwa mwanakaka….. walilalilishwa kwa kweli.
Mwanadada: Aliimba kwa kadiri ya uwezo wake. Wakati wa majaji kutoa comments zao….mmoja alidiriki kumwambia huyu dada hawezi kuimba anachodhani anaweza “aende akazae tu” Hii maana yake nini? Ndio kujaji kweli? Halikadhalika;
Mwanakaka: kama alivyofanyiwa mwanadada naye kaambiwa akatafute “ma – sugar mummy” kwa vile alikuwa “smart” Mtanashati…..inatisha…
Sikuweza kujua kama kweli huyu Jamaa ana akili nzuri. Naomba nimtaje tu kwa sababu nia ni kumrekebisha na si kumsema vibaya. Ni kati ya wale majaji watatu anajiita P Funk. Mimi Binafsi na labda baadhi ya waliobahatika kutazama kipindi kile hafurahishi kwa comments zake. Anajaribu kuwe critique kama alivyokuwa Salama Jabir lakini si ki-hivyo. Ajaribu kuwa yeye asifanye vitu kwa kuiga…lazima ataharibu.
Naomba tujadili hili kwa busara kwa ajili ya kuboresha kipindi vinginevyo sijaona maana yake kama hali itaendelea kama hivi. Umaarufu usiwe kero….

labda anataka kumuiga simon cowell kwa wale wanaoangalia x-facrot uk or american idol watakuwa wanamfahamu

hiyo ni show tu kwa hiyo hayo ni mambo ya kawaida acheni kupenda kusifiwa
 
I think to them is another way of entertaining the viewers. Creativity ya kipindi Zero, Majaji mhh labda Dada Rita na Mzee Kitime lakini hao wala ndumu, mibangi inachemka kwa kichwa. Basata na MSI wamelala wapi au mpaka siku akashifiwe mtoto wa mnene ndio washituke? na wadanganyika wenzangu twapenda short-cuts na uvivu, kwani kazi lazima kuimba? na kama kuimba lazima kaimbe kwa church au hata kwenye kwaya za kisiasa tu. Wenye busara wamekaa mbalii na hiyo Bange Star Search.

Hiyo kali... teh teh..
 
P. Funk kama jina lake ni kichaa kabisa, mi nashangaa kwanini hajaonywa na mabosi wake. Najua jamaa anatafuta njia ya kukubalika kama ilivyokuwa kwa salama jabir lakini naona anatumia njia ya kihuni tena itampotezea heshima. Show za namna ile ziko kama mbili ambazo zinaendelea: Kuna ile ya wanafunzi wa sekondari pale TBC na hii ya Bongo star - ITV...wote wanamajaji watatu nafikiri. Kiukweli unaona kuwa wanalenga kuwasaidia wanafunzi kuelewa kitu fulani, lakini hii ya kumsaka nyota wa bongo mi nashindwa kuelewa imeegemea wapi. Yule ponjoro mweusi nafikiri hana akili sawa sawa na director wa kile kipindi inafaa afanye maamuzi magumu mapema ili kunusu heshima ya kile kipindi, P. Funk kakurupuka na mibange yake. Nina uhakika hajui anapaswa kufanya nini....anafikiri yuko studio kwake ambapo huwatia masingi akina juma nature na kuwatukana matusi ya nguoni. BENCHMARK MLIANZA VIZURI LAKINI MTAMALIZA VIBAYA.
 
Hivi hawa majaji ni wazawa kweli? Watanzania hatuna ukatili wa hivyo. These are not attitudes of typical Tanzanians. Mbona nchi hii kuna mashindano mengi tuu lakini watu wana judge kistarabu tu! HAWA SI WENZETU!!
 
Muda mchache nimetoka kuona wimbo wa mshiriki mmoja wa BSS enzi za j4, anaitwa mrisho wa kigoma, alikuwa konda. Wimbo mtam sana na utashika chati. Hofu yangu, mbona BSS inatoa wasanii wazuri sana lakini wanapotea? Wapi roja, misoji, yule jamaa mwenye sauti nyembamba na tam. Wako wengi tu. Wanakwamia wapi? Faida ya BSS iko wapi? Wanashindwa wapi? Hoja iko mezani, wadau
 
Yule judge wa mwaka jana sijui yuko wapi this time John Kitime.

kitime kaona anajidhalilisha tu. Yuko zake diaspora anapiga music na bendi yake. Nami unknowingly nimetuma thread inayohusu hii hii Bss ila kimtazamo tofauti kidogo
 
noma hivyo washkaji, yani mnachabo tu then hamcomment? em leteni mawazo yenu, au somo ni gumu?
 
kama wadau hatuna hoja ujue ndo ivo tena.
tumebobea kujadili ufisadi na kujiexpress mkuu.
ila kama unataka komenti yangu ni hii hapo.

BSS hakuna jipya, ni chariot chasser tu wala hakuna sustainability. Kwa mimi ambaye nina uzoefu na programme za utamaduni naweza kusema kwamba hizi prog za BSS, Kili Awards, Cheza Tanzania na zingiezo ni ulaji wa wachache na kutafuta umaarufu ambao hapo baadae utatumika ktk siasa za bongo.

Jumanne alishindishwa ingawa mkali halisi alikuwa yule jamaa wa mwanza. na tuseme nimjuavyo misoji angeweza kutoka sana tu ktk miezi sita ya kwanza baada ya ushindi ila wapi hakuna kitu. Rojas alipaswa kushinda ila alipata upinzani mkali kutoka kwa misoji lakini pia angewezeshwa kutoka pia. Ila ninachoona hapa ni endapo mikataba baina ya wanaoingia kumi bora na kampuni ya benchi la alama ingepitiwa na wanaofahamu mikataba ya kisanii (cosota) kungekuwa namwendelezo fulani chanya.

Umetaka mchango??? ndo huo sasa
 
Muda mchache nimetoka kuona wimbo wa mshiriki mmoja wa BSS enzi za j4, anaitwa mrisho wa kigoma, alikuwa konda. Wimbo mtam sana na utashika chati. Hofu yangu, mbona BSS inatoa wasanii wazuri sana lakini wanapotea? Wapi roja, misoji, yule jamaa mwenye sauti nyembamba na tam. Wako wengi tu. Wanakwamia wapi? Faida ya BSS iko wapi? Wanashindwa wapi? Hoja iko mezani, wadau

Tatizo mi naona liko kwenye usimamizi wanachofanya ni kuwaacha kama watoto yatima. muziki wa bongo sasa hivi hata ukiwa na nyimbo kumi lakini kama huna mshiko wa kupromoti nyimbo yako unaishia kurekodi tu na kusikika hewani mara moja. so mtaji pia unahitajika kwenye muziki ndio maana unaona kina dudu baya wanapewa air time ya kufa mtu na nyimbo zao zisizo na kichwa (kwa mfano wimbo wa we ni kenge tu).
 
kama wadau hatuna hoja ujue ndo ivo tena.
tumebobea kujadili ufisadi na kujiexpress mkuu.
ila kama unataka komenti yangu ni hii hapo.

BSS hakuna jipya, ni chariot chasser tu wala hakuna sustainability. Kwa mimi ambaye nina uzoefu na programme za utamaduni naweza kusema kwamba hizi prog za BSS, Kili Awards, Cheza Tanzania na zingiezo ni ulaji wa wachache na kutafuta umaarufu ambao hapo baadae utatumika ktk siasa za bongo.

Jumanne alishindishwa ingawa mkali halisi alikuwa yule jamaa wa mwanza. na tuseme nimjuavyo misoji angeweza kutoka sana tu ktk miezi sita ya kwanza baada ya ushindi ila wapi hakuna kitu. Rojas alipaswa kushinda ila alipata upinzani mkali kutoka kwa misoji lakini pia angewezeshwa kutoka pia. Ila ninachoona hapa ni endapo mikataba baina ya wanaoingia kumi bora na kampuni ya benchi la alama ingepitiwa na wanaofahamu mikataba ya kisanii (cosota) kungekuwa namwendelezo fulani chanya.

Umetaka mchango??? ndo huo sasa

nimekupata, mkuu na maoni yako, ila siasa zisifanye tukasahau upande wa 2 wa sumni kwani life is more than politics
 
Nadhani Kiwanda cha sanaa ndiyo moja ya sehemu ambayo haina zengwe la kututoa kama madini, sijui teknolojia, mafuta na vinginevyo vinavyoleta vita kila mahala. Kinachohitajika kweli ni sapoti ya wale wenye vipato vikubwa na hawajui wafanyie nini. Fungueni basi hata vyuo ili wasanii wetu wawe professional. Naamini kuna watu wengi wenye vipaji vya kuwafanya hawa vijana hata wawe bora zaidi lakini bado imekaa kushotokushoto. Yaani bora nikamfanyie kazi bepari jioni niingie kny kapremio kangu home nikacheki hollywood highlights. Lakini potentio moyoni zimo, madirectors, producers na kadhalika ila hailipi mazee! Sijui ni nani anatakiwa afanye nini
 
nakubaliana na wadau , mi nafikiri kinachokosekana hapa ni malengo ya muda mrefu. Ninaamini kabisa madame rita na Benchmark yake hawana malengo ya muda mrefu na hawa wasanii, naamini baada ya kumpata mshindi na kumsaidia kurekodi album moja humuacha kama kifaranga cha kuku wa kienyeji baada tu ya kuota manyoya huachwa kikajiangaikie. Lakini nilisikia misoji ameunda bendi yake na ina perform hata kule kigoma kwenye BSS walikuwepo, Rodgers mara ya mwisho nilisikia alipata deal la show za Ujerumani na nchi za scandinavia! J4 chaliiiiiiii sijui alilewa umaarufu! Mnajua kupanda kileleni sio tabu, tabu ni kubakia huko, sasa Benchmark inapandisha hawa wadogo kileleni kisha inawaacha huko, mwisho sababu hawawezi jishika ni kuporomoka tu.
 
kama wadau hatuna hoja ujue ndo ivo tena.
tumebobea kujadili ufisadi na kujiexpress mkuu.
ila kama unataka komenti yangu ni hii hapo.

BSS hakuna jipya, ni chariot chasser tu wala hakuna sustainability. Kwa mimi ambaye nina uzoefu na programme za utamaduni naweza kusema kwamba hizi prog za BSS, Kili Awards, Cheza Tanzania na zingiezo ni ulaji wa wachache na kutafuta umaarufu ambao hapo baadae utatumika ktk siasa za bongo.

Jumanne alishindishwa ingawa mkali halisi alikuwa yule jamaa wa mwanza. na tuseme nimjuavyo misoji angeweza kutoka sana tu ktk miezi sita ya kwanza baada ya ushindi ila wapi hakuna kitu. Rojas alipaswa kushinda ila alipata upinzani mkali kutoka kwa misoji lakini pia angewezeshwa kutoka pia. Ila ninachoona hapa ni endapo mikataba baina ya wanaoingia kumi bora na kampuni ya benchi la alama ingepitiwa na wanaofahamu mikataba ya kisanii (cosota) kungekuwa namwendelezo fulani chanya.

Umetaka mchango??? ndo huo sasa

Nasikia yule mwimba Taarab alichukulwia na Mzee Yusuf, ni kweli?
 
Nasikia yule mwimba Taarab alichukulwia na Mzee Yusuf, ni kweli?
Mkuu kuna kuchukuliwa kwa aina nyingi hebu elezea hapa. Isije akawa amechukuliwa na huyo shabibi na sasa anamlelea mtoto wao wa ndoa teh teh teh
 
nimekupata, mkuu na maoni yako, ila siasa zisifanye tukasahau upande wa 2 wa sumni kwani life is more than politics
...and politics is more than LIFE (angalizo: Kolimba, Moringe, Mwaikambo, Chifupa et all)
 
Hamna kinachonikera kama jinsi ma judge wanavyowabeza hawa washiriki.
Mtu amepiga mstari masaa kibao na kupoteza muda wake pamoja na kutaka kuwania hizo zawadi lakini ingebidi wawashukuru kwa kuja kwao pale hata kama mtu ameimba(perform )zero.
Utakuta wanamwambia mtu,nenda kapike-hapa si kwako,nenda kaolewe na matusi mengine makubwa zaidi na kejejeli nyingi.Kama wengine hamjayaona hayo niwiweni radhi labda nimeona vibaya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom