BSS wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutoa lugha za kejeli na maudhi na wakasahau kabisa kuwa jukumu kubwa ni kuibua kipaji cha mshiriki katika muziki. Tangu kipindi hiki kianze hakuna mshiriki (aliyeshinda) ambaye ameweza kwenda sambamba na kina AY, Banana Zoro, Stara T etc. Angalia vipindi kama American Idol, You got talent etc product zinazotoka ni za uhakika (acha tuhuma za hivi karibuni dhidi ya AI). Majaji wako objective hata kama comment zao ni za maudhi lakini utaona jinsi mwisho wa siku mshindi anavyoweza kutamba nje ya AI kwa kupata recording contracts na kutoa nyimbo maridhawa. Nafikiri ni ufahamu mdogo wa majaji katika dhima nzima ya BSS