Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Inasikitisha kudhani kwamba damu ya huyo mama itaimaliza CCM.
Tafakuri jadidi inatosha kukujulisha kuwa CCM kamwe haihusiki na haiwezi kuhusika na upuuzi huo wa kurusha mabomu.
Jiangalieni ndani ya CDM mtajua nani kafanya hivyo na nini madhumuni yake.
Pia mjiulize kwa nini Kaloleni na kwa nini isiwe kata zingine tatu zilizobaki za Arusha au mikoa mingine.
Nataka kuwahakikishia tu kuwa what goes around comes also around. Kwani mwisho wa siku mtajua nani kawafanyia hivyo.

Daaaaah!!!!!!!!!!!! pole sana kwa giza lililotanda ubongo wako mithili ya diaphrum, si kosa lako
 
Labda Mungu anaruhusu matukio haya kuwaonyesha Watanzania aina ya mashetani yaliyopo madarakani
Poleni sana WanaArusha na familia zilizopoteza ndugu na kujeruhiwa poleni pia Arushaone Mungi na Crashwise. Mungu ni mwema naamini ipo siku tutaona kuwa damu hii haijaenda bure

Nakubaliana na wewe, nadhani tunahitaji kumtegemea mungu sana muda wote.Maana ametualika kupitia isaya: ''Niiteni maana ni karibu nitafuteni maana ninapatikana''
 
Inashangaza sana,hv kwenye umati wote ule mtu anaweza rusha bomu na asionekane?polis walikuwepo kulinda usalama na kama mrushaji alifanya vile nini kazi ya polisi katika kulinda amani?Halafu wanatuambia kuwa mpaka sasa hakuna mtu anaeshikiliwa na polis kama hawana uwezo au wameshindwa kazi si waseme tu wananchi tujilinge wenyewe?
 
Dr slaa Tulianza na Mungu ,tunaendelea kuwa na Mungu na tutaishia kuwa na mungu.Amen
 
Kweli vijana wa Arusha hawajitambui!

Hivi hawana kazi za kufanya? eti maisha magumu, wakati wanapoteza muda kusimama simama kwenye mikutano ya wapiga deal hao.
nilisha kuambia, kutumika kinyume na maumbile ni chukizo kwa MUNGU na wanadamu pia. Na afanyaye hayo huwa analaaniwa. Kujua kuwa mtu kalaaniwa sio lazima atembee bila nguo ila aweza kutenda au kunena mambo ya hovyo yasiyo stahili binadamu mwenye staha kuyatamka.
mimi Chama cha Mapinduzi sikipendi kwa sera zake,ila nikisikia mtu katupa hata jiwe katika mkutano wao na likajeruhi mtu nitamlaani mtupaji hata kama ni Mhe Mbowe. Na bila kuogopa nitasema hafai kuwa kiongozi. Wewe una laana.
 
Kwa maana hiyo Mh. Lukuvi anataka kutuaminisha kuwa CDM ilitaka viongozi wake wote wajiuwe ili wapate kura za huruma kutoka kwa wananchi. Naona dalili zote za nchi hii kuingizwa kwenye machafuko kwa kulazimishwa. Dhamana ya hii nchi bado ipo mikononi kwa watawala wenye dola halali kikatiba. Sasa sisi wananchi IMANI yetu tuifukize wapi?
Huwa nashindwa kuelewa inakuaje kiongozi kama huyu kutoa kauli zenye maudhi . Hivi ni lazima kusema kama hujisikii kusema si unaweza kukaa kimya tu. Nadhani angekua kapoteza wa damu yake kwenye hili sokomoko angeongea kwa busara zaidi. Unamwambia nini aliyepoteza mama yake , mkewe , mtoto n.k. Watawala wetu ifikie wakati mtuhurumie sisi mnaotutawala jamani. Hawa wanaoumia, kuuawa ni ndugu zetu hata kama ninyi mna tofauti za kisiasa jaribuni kuongea kwa busara, kumbukeni mnaoongoza hamuongozi chama bali mnaongoza nchi yenye vyama vingi na mitazamo tofauti. Turudishe ule upendo wetu wa kale chukulieni mfano simba na yanga mbona ni watani wa jadi na hatujawahi sikia wakiwa na upinzani hata wa kuumizana.
 
Kwa umati huu mkubwa kiasi hiki na viongozi walikuwa juu ya jukwaa na bomu linaonesha kabisa kuelekea walipokuwa viongozi!!! kwa hiho kina Chama na Ritz kwa mchoro huu mnataka kutuambia kuwa Lema na Mbowe walitaka wajiue? Si jambo rahisi!! Mchawi anajulikana!!! Ila hii hali haipaswi kuachwa na wananchi wanatakia waelimishwe wafanye kweli 2015 na miaka ijayo.
 
Serikali inakosaje huruma na kupofushwa na uadui wa kisiasa jamani? Hawa watu wana kosa gani kuisikiliza CHADEMA ilhali mfumo wa vyama vingi umeruhusiwa kisheria? Waufute basi kama hawataki kushindwa
nakuunga mkono mkuu,leo wamehaki akaunti nyingi sana
 
Mkuu TUMBIRI leo asubuhi nilikuwa natazama TBC1 mahojiano live toka Dodoma Waziri Wassira na James Mbatia walizungumzia tukio la Arusha.Bwana Wassira katika hali ya mshangao alimshambulia Mbowe kwamba alipata kura 600,000 katika uchaguzi wa mwaka 2005 hivyo si tishio na kwamba serekali haiwezi kumshambulia.

Huo ndiyo mtazamo wa serekali na hiyo ndiyo kauli ya waziri wa nchi OR uratibu na uhusiano.Hivi kweli kuna haja ya kuendelea na wizara na waziri wa jinsi hii ?.
 
Last edited by a moderator:
Waheshimiwa watanzania wenzaangu. ni siku nyingi sijafika hapa jamvini kuweka taarifa mbalimbali. Lakini muda si mrefu, nitapatikana zaidi hii ni kwa sababu nilipata safari iliyonikeep busy bila access.

Nimesikitishwa na matukio ya serikali ya CCM ya kuendeleza mauaji nchini. Hivi kweli hii hali ya mauaji, utekaji, utesaji, milipuko, kesi za kubambikiana... zitaifikisha wapi CCM? Maana wananchi nao wana akili ya kujua jema na Baya maana Mungu amewapa hilo.

Nawaomba watanzania tuendelee kuungana ili tuikomboe nchi yetu.

Quality
 
Kwa umati huu mkubwa kiasi hiki na viongozi walikuwa juu ya jukwaa na bomu linaonesha kabisa kuelekea walipokuwa viongozi!!! kwa hiho kina Chama na Ritz kwa mchoro huu mnataka kutuambia kuwa Lema na Mbowe walitaka wajiue? Si jambo rahisi!! Mchawi anajulikana!!! Ila hii hali haipaswi kuachwa na wananchi wanatakia waelimishwe wafanye kweli 2015 na miaka ijayo.
Mkuu, viongozi walikuwa wameshuka jukwaani kama dakika mbili wakikusanya pesa kutoka kwa wanachama/wapenzi wa chadema kwaajiri ya mawakala na hapo walipo watoto viongozi walikuwa kama hata mbili kutoka hapo..
 
Mkuu TUMBIRI leo asubuhi nilikuwa natazama TBC1 mahojiano live toka Dodoma Waziri Wassira na James Mbatia walizungumzia tukio la Arusha.Bwana Wassira katika hali ya mshangao alimshambulia Mbowe kwamba alipata kura 600,000 katika uchaguzi wa mwaka 2005 hivyo si tishio na kwamba serekali haiwezi kumshambulia.

Huo ndiyo mtazamo wa serekali na hiyo ndiyo kauli ya waziri wa nchi OR uratibu na uhusiano.Hivi kweli kuna haja ya kuendelea na wizara na waziri wa jinsi hii ?.
Wamelewa madaraka mkuu....
 
Aah! Halafu akapelekwa wapi mkuu?!
Inasikitisha sana kwa hili tukio
huko aliko pelekwa hatujui lakini alichukuliwa na gari la polisi...siku si nyingi video itawekwa mitandaoni..
 
Karibu tena mkuu labda kupitia kwako roho mt. anaweza kuwapa uelewa hawa watawala wa CCM walioamua kuharibu amani yetu na kuingiza ugaidi nchini mwetu
 
HAWA NDIO TAIFA LA KESHO..
Tunapoijadili Tanzania ya kesho na hatima yake lazima fikra zetu zifikirie zaidi juu ya watoto hawa,ni lazima tufikirie namna ya kuandaa akili pamoja na afya zao ili baadae walitumikie taifa kwa umakini na uzalendo wa hali ya juu.Hawa ndio Madaktari,waalimu,wanasheria na ndio viongozi wakubwa wa taifa letu hapo baadae.Kama tutacheza na kizazi hiki ni dhahiri tunaangamiza taifa kwa makusudi na uzembe wa hali ya juu na kwa hili taifa halitapona kamwe.



KWA PAMOJA TUIPENDE TANZANIA




 
Back
Top Bottom