Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Hebu tungejaribu kuzikusanya hizi picha za baada,kabla na wakati wa tukio lenyewe toka kwa wadau mbalimbali waliokuwepo eneo la tukio si ajabu inaweza kutupatia mwanga juu ya kummbaini muhusika hasa wa hili tukio. Siasa za Tanzania zinatisha sana kwa kweli na huku tunapoelekea tunaiweka amani rehani wallahi!!

Exactly unaweza kukuta mrusha bomu akaonekana hapo hapo kwenye picha!

Wenye picha wazipeleke vyombo husika.
 
Crashwise, Arushaone na Mungi poleni sana kwa tukio hili na Crashwise asante kwa picha hii. Hili ni tukio baya sana ambapo watu wameamua kuwapa majonzi wanaarusha bila sababu maalum zaidi ya kusaka vyeo na kushibisha matumbo yao. Watoto walioumizwa hawakuwa wanajua lolote na walikuwa pale wakijua watarudi nyumbani salama wakaungane na wazazi na ndugu zao ila tukio la mtu mmoja limepoteza ndoto zao nyingi kwa wale waliopotez amaisha na wale walioumizwa wengine ni vilema na maumivu na kumbukumbu isiyosahaulika. Poleni sana wakuu
 
Last edited by a moderator:
Hapa walilengwa viongozi wa CHADEMA. Kama lingekuwa tukio la kushambulia tu mkutano na kuua watu, bomu lingerushwa katikati ya umati wa watu.
 
"Tutaona, tuko Arusha kwa kazi maalumu kuhakikisha CCM ina shinda hata kama wananchi hawata tuchagua, na tutahakikisha wanaingia gharama kubwa ya kuishabikia CHADEMA." Mtela Mwampamba siku 2 kabla

Hii ishu ina watu wengi kuna gody mwalusamba,kuna jumanne mjusi,kun mmoja.huyu gody anawatumia hawa majambazi kufanya vurugu kweanye mikutano ya cdm.
 
Mkuu Crashwise hakika tukio lile halitokaa linitoke. Na kwako Mungi, Mungu ni mkubwa sana kwani tulipoondoa miguu yetu pale pakarushwa lile bomu! Humu JF huenda kungekuwa na thread ya RIP Arushaone na Mungi.
God Forbid....
Poleni sana ndugu zetu...
hata hivyo inasikitisha sana kuwapoteza hao wengine, inasikitisha sana nchi yetu imefikia hapa, I wish........
 
Lengo hasa la kurushwa hilo bomu lilikuwa ni lipi? Kutisha watu wasipige kura au ni chuki kwa Cdm?
 
Mungu azilaze mahali pema roho za waliotutangulia, hii serikali dhalimu ya Kikwete ipo siku italipwa kwa mabaya yake pamoja na viongozi waliopo bungeni wasiokuwa na adabu kwa watanzania.

Wabunge wa CCM hawana heshima kwa wananchi wanachojali wao ni kuuwa na maslai binafsi
 
Aliyerusha alitokea kwa wapi mbele ya huo umati au? na kwanini alirusha upande wa wa wananchi hakurusha jukwaa kuu au alilenga kurusha jukwaa kuu lakini bomu halikufika?

Wenzetu wakichunguza wanaenda sambamba na kuangalia MOTIVE.

Mrushaji alikuwa na lengo la kulipua jukwaani....kuna mawili, ama bomu halikufika kwa walengwa au hakutaka kutimiza kile ambacho aliagizwa na mashetani akikafanye....Anaweza kuwa alipewa Amri ya kuwalipua kina Lema na Mbowe lakini dhamira yake ilikuwa haimtumi kufanya hivo..lakini vile vile kukwepa lawama akaamua kurusha tu kwa raia wa akwaida,,,,,,
 
na ni bora wangekaa kimya tungeelewa lakini wanakuja na kauli zenye kejeli bila hata ya kutoa pole kwa wafiwa.
Haki haikuwahi kushindwa na udhalimu labla kama historia ya binadamu inaundwa upya!
 
Kweli vijana wa Arusha hawajitambui!

Hivi hawana kazi za kufanya? eti maisha magumu, wakati wanapoteza muda kusimama simama kwenye mikutano ya wapiga deal hao.
 
si mshangai lukuvuvi wakuu na mshangaa aliempa dhamsna ya kuwa kiongozi sababu inaeleweka wazi elimu ina walakini sasa mwenyewe kathibisha kuwa hatumii akili ila anatumia ushabiki, na ukiangalia wengi walio kama lukuvi wso kutumia akili ni ngumu bali hutumia ushabiki na nguvu nyingi zisizo na tija mfano ni kikwete, mwigulu,nape, lowasa, wasira,juma nkamia, issa michuzi na wengine wengi, wao hushabiki ndo uko kwenye damu kama juma nkamia na issa michuzi waliwahi kukaririwa wakisema JF ifungiwe et inachoche fujo sasa swali kati ya jf na mwigulu+nape nani anachochea fujo? Tena wao husema hadharani pia lowasa hutumia nguvu katka mambo yake mf ni nguvu aliotumia kuwapiga viongoz wa chadema makuyuni kama nasari na wenzie ili ccm ishinde, wasira ns kikwete wao hufuata mkumbo na ushabiki, hawana maamuzi binafsi
 
Dah! poleni sana wakuu hii nchi sijui imekuwaje sasa hivi...walilazimisha kuwepo na vyama vingi sasa wanavipinga kwa juhudi mbadala.

Mkuu Crashwise hakika tukio lile halitokaa linitoke. Na kwako Mungi, Mungu ni mkubwa sana kwani tulipoondoa miguu yetu pale pakarushwa lile bomu! Humu JF huenda kungekuwa na thread ya RIP Arushaone na Mungi.
 
Acheni Mungu Aitwe Mungu!
Macho yaliyofumbwa sasa yamefunguliwa, kila kilichokuwa gizani sasa kipo nuruni.
Uongozi huu wa kidhalimu na njama zake zote zinawekwa hadharani mchana mweupe...
Tazama, hata picha zipo kuonyesha nani alikuwa wapi, nadhani waliopanga udhalimu huu walifikiri njia za giza walizozoea kutumia kufanikisha udhalimu wao zitabaki gizani milele!
Hatuhitaji kutafuta mchawi, hatuhitaji kuundiwa tume, hatuhitaji kuwa wataalamu wa 'nuclear science' kujua nani alikuwa anawindwa na bomu hilo, na kujua aliyelirusha alikuwa na dhamira gani.
Roho inaniuma sana kuona tumepoteza wapiganaji wetu kwa uroho wa kubaki madarakani wa watu wachache na serikali yao ya kidhalimu.
Lakini kama Andiko linavyosema, Hakika Neno la Mungu Litasimama!
Damu iliyomwagika pale Soweto itakuwa chachu ya mabadiliko.
Na sijui kwa nini siku hiyo mkutano mkubwa ulifanyika mahali panapoitwa Soweto.

Tujaribu kujikumbusha historia ya SOWETO kwenye mapambano ya kuwaondoa madarakani makaburu wa Afrika ya Kusini!

Mungu Awalaze Pema makamanda wetu waliopoteza maisha, na Awape nguvu ya uponyaji wote waliojeruhiwa!

Aluta Continua!
 
Mrushaji alikuwa na lengo la kulipua jukwaani....kuna mawili, ama bomu halikufika kwa walengwa au hakutaka kutimiza kile ambacho aliagizwa na mashetani akikafanye....Anaweza kuwa alipewa Amri ya kuwalipua kina Lema na Mbowe lakini dhamira yake ilikuwa haimtumi kufanya hivo..lakini vile vile kukwepa lawama akaamua kurusha tu kwa raia wa akwaida,,,,,,

Nawashauri kuanzia sasa hawa wanaofanya mikusanyiko wawe wanafanya sweep kuhakikisha kwamba maeneo yapo salama. Na vile vile CCTV Camera ziwe zinatumika ijapokuwa na matukio ya muda mfupi. Kungekuwa na camera huyo jamaa angeonekana na angekamatwa.
 
Exactly unaweza kukuta mrusha bomu akaonekana hapo hapo kwenye picha!

Wenye picha wazipeleke vyombo husika.

Mrusha bomu alionekana mkuu, watu walitaka kumkamata lakini polisi waliingilia kwa kurusha risasi na mabomu.
 
I feel for hao watoto masikini ambao walikuwa hata hawajui why wapo hapo labda walifuata mdundo wa muziki na shangwe.
 
Acheni Mungu Aitwe Mungu!
Macho yaliyofumbwa sasa yamefunguliwa, kila kilichokuwa gizani sasa kipo nuruni.
Uongozi huu wa kidhalimu na njama zake zote zinawekwa hadharani mchana mweupe...
Tazama, hata picha zipo kuonyesha nani alikuwa wapi, nadhani waliopanga udhalimu huu walifikiri njia za giza walizozoea kutumia kufanikisha udhalimu wao zitabaki gizani milele!
Hatuhitaji kutafuta mchawi, hatuhitaji kuundiwa tume, hatuhitaji kuwa wataalamu wa 'nuclear science' kujua nani alikuwa anawindwa na bomu hilo, na kujua aliyelirusha alikuwa na dhamira gani.
Roho inaniuma sana kuona tumepoteza wapiganaji wetu kwa uroho wa kubaki madarakani wa watu wachache na serikali yao ya kidhalimu.
Lakini kama Andiko linavyosema, Hakika Neno la Mungu Litasimama!
Damu iliyomwagika pale Soweto itakuwa chachu ya mabadiliko.
Na sijui kwa nini siku hiyo mkutano mkubwa ulifanyika mahali panapoitwa Soweto.

Tujaribu kujikumbusha historia ya SOWETO kwenye mapambano ya kuwaondoa madarakani makaburu wa Afrika ya Kusini!

Mungu Awalaze Pema makamanda wetu waliopoteza maisha, na Awape nguvu ya uponyaji wote waliojeruhiwa!

Aluta Continua!

Labda Mungu anaruhusu matukio haya kuwaonyesha Watanzania aina ya mashetani yaliyopo madarakani
Poleni sana WanaArusha na familia zilizopoteza ndugu na kujeruhiwa poleni pia Arushaone Mungi na Crashwise. Mungu ni mwema naamini ipo siku tutaona kuwa damu hii haijaenda bure
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom