Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Bomu lilirushwa likaangukia hapa

Hebu tungejaribu kuzikusanya hizi picha za baada,kabla na wakati wa tukio lenyewe toka kwa wadau mbalimbali waliokuwepo eneo la tukio si ajabu inaweza kutupatia mwanga juu ya kummbaini muhusika hasa wa hili tukio. Siasa za Tanzania zinatisha sana kwa kweli na huku tunapoelekea tunaiweka amani rehani wallahi!!

Kwa nini uko humu badala ya usalama?(joke). Yaani haya ndiyo waliyopaswa kufanya badala ya kukimbilia kutangaza dau!
 
Mtu anafika mbele ya huo umati na ulinzi wote, tena mbele ya Jukwaa halafu anarusha bomu, hivi hao jamaa waliokuwa wamevaa gwanda hapo mbele walikua wamelala? Na kwanini asirushe juu ya jukwaa? hapa kuna harufu ya mkono wa Lwaka.
 
Jamani tuzungumze ukweli kupitia Picha ile hata asiyejua kusoma ataangalia picha, bomu linaonekana kuelekezwa katika gari la matangazo ambapo walikuwa Viongozi mbali mbali .

aliyerusha bomu inaonekana alikuwa nyuma katika umati wa watu hii ni kwa mtazamo wangu niliosoma hii picha, sasa swali langu kama mpigaji alilenga wananchi angerusha kati kati ya umati wa watu ili kuuwa watu waliokuwepo hapo/ lakini inaonekana mrushaji alilenga viongozi . matokeo yake sasa ndio hayo mauaji yaliyotokea.

mungu walaze mahali pema peponi waliopoteza maisha katika tukio hilo
 
the first time i heard about this , my mind was trigered with thoughts of our arrogant neighbours..i wonder why would my fellow country men think that we are enemies just because of our political differences, the answer to that question was that, may be it is because our enemy saw that weakness and utilized it effectively, let us not point fingers at each other but instead work closely together to know who is realy our enemy of which i am sure it might be one among those arrogant neighbours
 
Mrusha bomu alionekana mkuu, watu walitaka kumkamata lakini polisi waliingilia kwa kurusha risasi na mabomu.

Aah! Halafu akapelekwa wapi mkuu?!
Inasikitisha sana kwa hili tukio
 
R.I.P walokufa wooote Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi.
 
hii ni prpaganda mpya kabisa,yaani unajiua ili upate huruma,sijui utaionaje huruma hiyo wakati umeshakufa? wanasema nae Nasari alijipiga na kujiumiza vibaya ili huruma ipatikane.
narudia tena
CDM hawaitaji huruma Arusha,ni kama CUF pemba hawahitaji huruma kwa kujiripua mambomu.
ile ilikuwa ni mbinu ya kuogopesha watu wasifanye maamuzi sahihi.
 
oh my God!!! hivi mtu anataka kuua umati wote huu? mimi nina imani wanaohusika ni wale wale waliotuma bomu kule olasiti... lengo ni kuwachonganisha chadema na ccm... serikali fanyeni home work yenu sawa sawa.
 
Mkuu Crashwise hakika tukio lile halitokaa linitoke. Na kwako Mungi, Mungu ni mkubwa sana kwani tulipoondoa miguu yetu pale pakarushwa lile bomu! Humu JF huenda kungekuwa na thread ya RIP Arushaone na Mungi.
Allah is great,poleni sana makamanda kwa kuepuka kifo hiki....kuna kamanda hapo kwenye picha anaitwa Noor Hassan na dogo wake mwenye combat jamani wamenusurika!!!Nina hasira sana na manyang'au masisiem...Cc to Arushaone & Mungi
 
Last edited by a moderator:
Mtu anafika mbele ya huo umati na ulinzi wote, tena mbele ya Jukwaa halafu anarusha bomu, hivi hao jamaa waliokuwa wamevaa gwanda hapo mbele walikua wamelala? Na kwanini asirushe juu ya jukwaa? hapa kuna harufu ya mkono wa Lwaka.
Nilipo anza kusoma post yako nikajua una kitu unataka kueleweshwa lakini mwisho nikagundua kuwa wewe ni kati ya vijana wa Mwigulu Nchemba..
 
Jamani tuzungumze ukweli kupitia Picha ile hata asiyejua kusoma ataangalia picha, bomu linaonekana kuelekezwa katika gari la matangazo ambapo walikuwa Viongozi mbali mbali .

aliyerusha bomu inaonekana alikuwa nyuma katika umati wa watu hii ni kwa mtazamo wangu niliosoma hii picha, sasa swali langu kama mpigaji alilenga wananchi angerusha kati kati ya umati wa watu ili kuuwa watu waliokuwepo hapo/ lakini inaonekana mrushaji alilenga viongozi . matokeo yake sasa ndio hayo mauaji yaliyotokea.

mungu walaze mahali pema peponi waliopoteza maisha katika tukio hilo
Mkuu, ni kweli unayosema kwani wakati bomu lina rushwa viongozi walikuwa wameshuka chini na kuchukua mabox ili kwenda kukusanya michango ya kukiwezesha chama hasa wakiwa wamelenga mawakala hapo walipo watoto viongozi hawakuwa mbali nao yaani Lema na Mbowe.......
 
Wapumbavu wachache wanazidi kuvuruga Amani ya nchi,
Nivyema kuwadhibiti angali mapema!
Hii ndio Tanzania.
 
Mkuu Arushaone usinikumbushe, maana yake kama siyo wewe kufika pale tusingeondoka.

Labda kwa faida ya wanajf ni hivi:
Mimi nilikuwa sehemu ya mbele, ambapo bomu lilidondokea, Arushaone naye akaja pale akaniuliza Crashwise yuko wapi, nikamwambia twende nikupeleke mahali anapo zi upload picha, ndiyo kuondoka kwetu pale ambapo hata dakika moja haikuisha mlipuko ukatokea. Mkuu ukiangalia picha hapo juu utaona mahali niliposimama mara ya kwanza.
Pengine nisema Mungu alikuleta pale ili tuondoke zetu. Lakini pia mahali risasi zilipoingia kwenye gari ni sehemu alipokuwa crash amekaa kwa ndani. Ni Mungu tu mkuu!

Mkuu,poleni sana! Hapa nilipo machozi yananidondoka,lakini Mungu ni mkuu anajua matatizo yetu na hakika hawa madhalimu mwisho wao umefika. Narudia tena Poleni sana!
Na Mungu awapumzishe mahala pema peponi marehemu wote Amina!
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli mkuu, baada ya kuiona hiyo picha nilishtuka mpaka mwili unasisimka halafu napata hasira ya ajabu sana!
Tutapambana kwa haki na ukweli mpaka nchi hii itakapopata ukombozi!

Hakika Mwanajeshi harudi nyuma ktk uwanja wa mapambano na hakika ukombozi waja!
 
Kama ni kufunga na kuomba kwa dini zetu na imani zetu zote kuweza kufichua njama hizi za CCM na serikali yake. Inafaa nasi wananchi tujiandae ipasavyo kupambana na hili genge la CCM kwa kuwa serikali ni dhaifu na viongozi wake mpaka wanafikia mahali wa kutojali uhai wa watu. Kama Mungu alituumba kwa sura na mfano wake na akatupa utashi was kuishi kwa amani lakini madaraka yanageuza mioyo ya watu kuwa viumbe vya sayari nyingine. Kwa mtu mwenye moyo lazima aumizwe na kejezi za wana CCM ni fedheha kubwa sana kwa taifa letu Masikini. Wametuibia, wanatunyanyasa, wanauza nchi vipande vipande, wakapandikiza udini, ukanda, wakaona kete zao zinaishia shimoni wanaanza kutumia mabomu na risasi kuzidi kuangamiza. Yaani inauma sana. Sumu wamelishwa viongozi wachapa kazi na kwa unafiki wao wakameza kwa kupewa uwaziri, sasa tueleweje hichi CHAMA cha CCM? Nasema na natamka tena Kuwa CCM ni KANSA. Na ni ADUI kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu na mpenda nchi yake. CCM na washirika wake ni magaidi waliokubukhu kwa kila ovu.
Tuwalaani na kuwakataa.
 
Vichwa vyote ndani ya serikali ya CCM wameona Lukuvi ndiye mwenye akili timamu then wakamwachia atoe kauli ya serikali yenye maudhi,uchonganishi na upuuzi mkubwa wa kudharau roho za Watanzania, hivi angekufa mwanae katika mkutano wa CCM angejiropokea hivyo? Uroho huu wa madaraka unaopuuza thamani ya utu,ukweli na huruma ya kibinadamu haustahili kuvumiliwa!
 
Kama ni kufunga na kuomba kwa dini zetu na imani zetu zote kuweza kufichua njama hizi za CCM na serikali yake. Inafaa nasi wananchi tujiandae ipasavyo kupambana na hili genge la CCM kwa kuwa serikali ni dhaifu na viongozi wake mpaka wanafikia mahali wa kutojali uhai wa watu. Kama Mungu alituumba kwa sura na mfano wake na akatupa utashi was kuishi kwa amani lakini madaraka yanageuza mioyo ya watu kuwa viumbe vya sayari nyingine. Kwa mtu mwenye moyo lazima aumizwe na kejezi za wana CCM ni fedheha kubwa sana kwa taifa letu Masikini. Wametuibia, wanatunyanyasa, wanauza nchi vipande vipande, wakapandikiza udini, ukanda, wakaona kete zao zinaishia shimoni wanaanza kutumia mabomu na risasi kuzidi kuangamiza. Yaani inauma sana. Sumu wamelishwa viongozi wachapa kazi na kwa unafiki wao wakameza kwa kupewa uwaziri, sasa tueleweje hichi CHAMA cha CCM? Nasema na natamka tena Kuwa CCM ni KANSA. Na ni ADUI kwa kila Mtanzania mwenye akili timamu na mpenda nchi yake. CCM na washirika wake ni magaidi waliokubukhu kwa kila ovu.
Tuwalaani na kuwakataa.

Hakika mkuu,inanishangaza sana kuona vijana bado wanaendelea kushabikia CCM jamani! Akil gani hizo. Nina imani matatizo yakizidi basi ushindi unakaribia,basi jamii yote ya watanzania tujenge imani ushindi uko karibu!
 
Back
Top Bottom