Bodaboda na Bajaji mnapaswa kulipa Kodi kwa Mujibu wa Sheria Mpya ya Kodi. Acheni kuleta Blah blah!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!.

Pesa za kuhonga huwa zinapatikana ila za kulipa Kodi mnaanza kuleta singeli za kipumbavu!.

Huwa mkisikia kulipa mapato(stahiki ya serikali) mnaanza ngonjera kibao kana kwamba ni dhambi kulipa mapato. Kama unafanya kazi kila siku na unapata faida kwanini usilipe kodi?

Huwa mnakenua meno mkiona Machinga na wafanyabiashara wengine wakibanwa kuhusu Kodi, mlidhani nyie ni spesho sana hampaswi kulipa kodi?

Mtake msitake kodi mtalipa na kama huwezi acha kuingia barabarani hupaki chombo chako,lakini kama unaingia barabarani kodi ni lazima ulipe.

Nikiwa kama muendesha Bodaboda nasema kwa Msisitizo ya kwamba "SERIKALI ILICHELEWA SANA"

UKITENGA BAJETI YA KUHONGA HAKIKISHA UMETENGA KODI YA SERIKALI

Ni hayo tu.
 
Kwan serikali inazifanyia nn hizo hela kama sio kupeleka huko huko kwa malaya? Si bora zipelekwe na bodaboda wenyew , kila siku wimbo wa umaskin wkt mapato tunayaona
Ukimaliza kuimba Si-Ngeli hakikisha unalipa kodi.
 
Kaka Umughaka hamna anaekataaa kulipa Kodi, binafsi sio boda boda lkn mazingira nayofanyia kazi hua npo tayar ninunue risiti (risiti zinauzwa)ili nitumie kama kizugio tu unajua kwann

Kwa sababu sioni msaada wa serikali kwenye baadhi ya huduma yaan umeme huku ni shida, maji ni changamoto, ulinzi nalipia sungu sungu sasa si bora nile Hela zangu kuliko nilipe kodi
 
Mkuu hata wenzio wanalalamika hivyo hivyo,nadhani baada kulipa kodi vijana wa Kitanzania watapata Akili
 
Kulipa kodi sio tatizo,tatizo ni pale unaposikia mjinga mmoja anataka kukarabati uwanja wa taifa kwa bilioni 31,hujakaa sawa unasikia kuna mjinga kapiga sjui bilioni ngapi huko kwenye mradi fulani na husikii wanashughulikiwa
 
Back
Top Bottom